Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mfumo wa Kiulimwengu wa Khilafah

 (Imetafsiriwa)

Kuna mfadhaiko ulio halali kwa Waislamu wa Pakistan kwa upuuziaji wa watawala wao kuhusiana na uchumi na usalama. Upuuziaji huu wa watawala sio kwa sababu ya kutoweza, bali ni kutokana na ufuasi ulio madhubuti kwa mfumo wa dunia uliotengenezwa na mataifa ya kikoloni ya Kimagharibi.

Kuhusiana na uchumi, watawala wa Pakistan wamejitolea kulipa malipo ya riba ya rupia trilioni tatu, wakati makadirio jumla ya kodi ni rupia trilioni sita. Licha ya kukiri suala la kuwa Uislamu umekataza riba na kusimamisha malipo yote ya riba, watawala wataziba pengo la nakisi ya bajeti ya rupia trilioni 3.5 kwa mikopo zaidi ya riba. Kwa kufanya hivyo wanashikamana na mfumo wa kiulimwengu wa kiuchumi ambao wakoloni wameuhakikisha kwa kila muongo unaopita, (wa kuwa) Pakistan inazama ndani zaidi ya janga la deni lenye msingi wa riba. Mwaka 1971, deni la Pakistan lilikuwa rupia bilioni 30, lakini hivi sasa linakaribia rupia trilioni 40, ambalo ni ongezeko la zaidi ya mara elfu.

Kwa kufuata kwake mfumo wa sasa wa uchumi, watawala wa Pakistan wanaiangamiza nchi hiyo kwenye madeni zaidi, malipo zaidi ya riba na mizigo ya kodi inayopaa kwa kasi ili kukidhi malipo ya riba. Mfumo wa sasa wa uchumi kwa muundo wake ni muendelezo wa ukoloni wa moja kwa moja, pamoja na uvamizi wa kijeshi. Ni ukoloni mamboleo ambapo ubwana wa Wamagharibi unahifadhiwa kupitia utumwa wa kiuchumi.

Kuhusiana na usalama, watawala wa Pakistan kwa masikitiko wamepuuza matukufu ya Uislamu. Wameitelekeza Kashmir Iliokaliwa Kimabavu kwa Modi, wameikubali hofu kwa vikwazo vya Ulaya kuzuwia matakwa ya kumfukuza balozi wa Ufaransa juu ya suala la heshima ya Mtume (saw). Kwa kuliwacha suala la heshima ya Mtume (saw), wamekiri kizuizi cha kujiweka mbali na haja ya kupeleka Jeshi la Pakistan kuikomboa Masjid Al-Aqsa.

Kupuuza kwao ni kutokana na kushikamana barabara na mfumo wa kimataifa wa Kimagharibi ambao ni urithi wa mapambano ya makruseda na Khilafah. Kutokana na muundo huo, mpango wa kimataifa wa usalama ni kuhakikisha ubwana wa Wamagharibi, kuhakikisha kuwa Waislamu wanayatelekeza matukufu yao. Hii ndio sababu ya watawala wa Pakistan kutekeleza kujizuia huku Kashmir Iliokaliwa Kimabavu ikichukuliwa na Modi, lakini wanajitahidi hivi sasa kuisaidia Amerika kudhibiti umakinifu wa usalama katika eneo, baada ya kujiondoa kwa udhalili. Hii ndio sababu watawala wa Pakistan hukiri kizuizi cha masafa na mipaka ya kieneo katika suala la Msikiti wa Al-Alqsa, wakati ukombozi wa Kashmir Iliokaliwa Kimabavu iko wazi kufikiwa, katika madai yote, ya kieneo, masafa, uwezo na fursa.

Waislamu wanaweza tu kutarajia udhalilifu na maafa pekee huku wakilemewa na watawala ambao wanatekeleza sheria zisizo za haki za wakoloni wa Kimagharibi. Hali yao itakuwa bora mara tu baada ya kuwaweka watawala ambao watawatawala kwa Dini yao. Ni Khilafah pekee ndiyo itakayokataa malipo ya riba, yanayotokana na mtego wa madeni ya wakoloni ili kuweka mikondo ya mapato iliyoiwezesha Khilafah kuhakikisha kuwa Uislamu ulibakia juu kwa karne nyingi. Khilafah ndiyo itakayoyaachia huru majeshi ya Waislamu kutokana na pingu za sheria ya kimataifa, kuregelea Da’wah na Jihad ili kueneza Uislamu duniani kote.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na

Musab Umair – Wilaya ya Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu