Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itakavyozuia Mgawanyiko wa Kimadhehebu

Ni Uislamu, thaqafa yake, historia yake na turathi yake ambazo ndizo viunganishi vya kimaumbile vinavyo wafungamanisha Waislamu kote katika Ulimwengu wa Kiislamu, wawe Sunni au Shia, huku nidhamu ya kisekula ya Kimagharibi iliyo lazimishwa juu yao ikipatiliza ikhtilafu zao kwa malengo ya kisiasa. Imani ya Kiislamu inayo waunganisha ni kubwa zaidi kuliko ikhtilafu fulani za kimadhehebu zilizopo baina ya madhehebu tofauti tofauti. Wote wanakubali misingi ya itikadi ya Kiislamu na Qur’an na Sunnah ndio chimbuko la sharia ya Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَطِيعُواْ اللّهَ وَأَطِيعُواْ الرَّسُولَ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً)

“Enyi mlio amini! Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora na yenye mwisho mwema.” [An-Nisa: 59]

Ni Uislamu na utawala wa Kiislamu pekee ambao unarekodi ya kushuhudiwa ya kuangamiza umadhehebu na ukabila na kuwaunganisha watu wa usuli, makabila na imani tofauti tofauti kuwa Ummah mmoja na dola moja. Kabla ya Uislamu, makabila ya Aws na Khazraj yalipigana vita vingi dhidi ya wao kwa wao, lakini pindi walipoukubali Uislamu, walikuwa ndugu na kwa pamoja walijulikana kama Answar. Mwenyezi Mungu (swt) asema,   

(وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ لَوْ أَنفَقْتَ مَا فِي الأَرْضِ جَمِيعاً مَّا أَلَّفَتْ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَـكِنَّ اللّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ)

“Na akaziunga nyoyo zao (waumini). Na lau wewe ungelitoa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunganisha nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ni Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye hekima.” [Al-Anfal: 63]

Waislamu Masunni na Mashia nchini Yemen, Iraq na kwengineko waliishi sako kwa bako kwa amani katika mtaa mmoja kwa karne nyingi chini ya utawala wa Kiislamu wa Khilafah. Walioana, waliswali katika msikiti mmoja na kupigana pamoja dhidi ya maadui wa dola.

Khilafah si dola ya Masunni wala Mashia au dola iliyojengwa juu ya Madhhab yoyote. Bali, ni nidhamu ya kisiasa iliyojengwa juu ya Uislamu kwa Waislamu wote na wanadamu wote, bila ya kujali itikadi, kabila wala utaifa.

Kinyume na serikali na nidhamu zisizokuwa za Kiislamu katika ardhi za Waislamu ambazo hupatiliza tofauti zilizoko baina ya watu kwa malengo ya kisiasa, Khilafah hutazama umoja wa kisiasa baina ya raia wote kwa umuhimu mno. Sera zake za ndani humulika njia ya kipekee katika kuwafinyanga watu tofauti tofauti kuwa mujtama mmoja tulivu unao heshimu tofauti za kidini. Wanaunganishwa pamoja ndani ya Khilafah kwa msingi wa uraia, na haki, dori na majukumu yaliyomo. Khilafah pia itang’oa uangiliaji wowote wa wakoloni katika ardhi za Waislamu, ikiwemo utumizi wa taasubi ya kimadhehebu kuugawanya Ummah. 

Raia wote wa Khilafah hufurahia haki sawa za uraia – katika siasa, uchumi, elimu, matibabu na nyanja nyenginezo za kimaisha – bila ya kujali itikadi zao, kabila, jinsi au chochote chengine. Hii ni kwa sababu Uislamu una haramisha ubaguzi baina ya watu katika utoaji haki za uraia. Mtume (saw) asema,

«ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى التَّحَوُّلِ مِنْ دَارِهِمْ إِلَى دَارِ الْمُهَاجِرِينَ، وَأَخْبِرْهُمْ أَنَّهُمْ إِنْ فَعَلُوا ذَلِكَ فَلَهُمْ مَا لِلْمُهَاجِرِينَ وَعَلَيْهِمْ مَا عَلَى الْمُهَاجِرِينَ»

“Kisha waite kuhama kutoka katika ardhi yao kuja katika ardhi ya Muhajirin na uwape habari kuwa hakika wakifanya hivyo watakuwa na haki sawa na Muhajirin na juu yao watakuwa na majukumu sawa na Muhajirin.”

“Raia wote wa Dola ya Kiislamu wanastahiki kufurahia haki na majukumu ya Kisheria.” (Kifungu cha 5 – Kielelezo cha Katiba ya Khilafah cha Hizb ut Tahrir)

Nidhamu ya kisiasa ya Khilafah haikujengwa juu ya uwakilishi kwa misingi ya ukabila, rangi, au madhehebu ambayo yaweza kuchochea mgawanyiko, uhasama na ushindani baina ya sekta tofauti tofauti za mujtama kwa ajili ya rasilimali na mamlaka. Bali Khalifah (kiongozi wa dola) anawajibika Kiislamu kuwa msimamizi juu ya mahitaji na maslahi ya raia wake wote bila ya kujali itikadi zao, kabila wala asili. Hii ina jumuisha kuhakikisha kila raia wa dola – Sunni au Shia, Muislamu au asiyekuwa Muislamu – mahitaji yao msingi ya chakula, mavazi, makao na elimu yanashibishwa, na kiwango chenye hadhi cha maisha pamoja na kudhamini ulinzi wa damu, imani, heshima, na mali zao. 

“Raia wote wa Dola wataamiliwa kwa usawa bila ya kujali dini, jinsi, rangi au jambo lolote jengine. Dola ina haramishwa kubagua miongoni mwa raia wake katika mambo yote, iwe katika utawala au mahakama, au uchungaji wa mambo.” (Kifungu cha 6 – Kielelezo cha Katiba ya Khilafah cha Hizb ut Tahrir)

Wale watakao chaguliwa kuwa sehemu ya Baraza la Ummah (Majlis al-Ummah) ambacho ni chombo cha ushauri kinachomhisabu Khalifah kuhusiana na majukumu yake kwa watu na kuwakilisha maslahi ya wote katika jamii zao badala ya maslahi ya vikundi maalumu vya watu ndani ya mujtama.

Khilafah haitatabanni sheria katika kadhia za kiimani au za kiibada katika Uislamu isipokuwa zikiwa na athari ya kijamii kama vile Zakah, na itawaacha Waislamu kufuata dhehebu lolote wanaloliona kuwa na nguvu zaidi katika maeneo hayo. Hii ni kwa sababu kutabanni katika mambo kama haya kwaweza kusababisha uzito na bughdha miongoni mwa wale Waislamu walio na ikhtilafu za rai juu ya kadhia hizi, ambayo nidhamu ya Kiislamu ina kusudia kuzuia. Bali Khilafah itatabanni tu juu ya zile kadhia zinazohitajika kwa ajili ya umoja wa kisiasa na uendeshaji imara wa mambo ya dola pekee. Fauka ya hayo, Khalifah huenda akatabanni kutoka katika dhehebu lolote katika mambo ya dola, iwe la Kisunni au la Kishia, kwa msingi wa rai atakayoiona kuwa yenye nguvu zaidi katika Uislamu.  

“Khalifah hatabanni huukmu za kiShari'ah kuhusiana na ibada, isipokuwa zinazohusu Zakah na vita (Jihad). Pia, hatabanni fikra yoyote kuhusiana na Itikadi ya Kiislamu.” (Kifungu cha 4 – Kielelezo cha Katiba ya Khilafah cha Hizb ut Tahrir)

Nidhamu ya Elimu ya Khilafah itakuza maadili na ufahamu sahihi wa Kiislamu. Itafanya bidii kujenga fungamano imara la udugu wa Kiislamu baina ya wanafunzi wa Kiislamu ili kutibu na kuzuia migawanyiko yoyote baina ya nyoyo za waumini, ikiwemo kufanya bidii kuondoa fahamu zozote kama taasubi ya kimadhehebu, utaifa na ukabila zinazo sababisha mgawanyiko. Pia itajenga miongoni mwa wanafunzi wake, hisia imara ya uchungaji na majukumu kwa wengine, na haki, mahitaji na maslahi yao, ambayo yatahakikisha mshikamano wa mujtama tulivu.  

Nidhamu za mahakama na kuadhibu wahalifu zitapambana vikali na wale wanaotaka kueneza taasubi ya kimadhehebu au kuwagawanya Waislamu kwa njia yoyote ile. Dola haitakuwa na uvumilivu hata kidogo kwa aina yoyote ya mgawanyiko wa kimadhehebu au ghasia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake Katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:56

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu