Alhamisi, 09 Rajab 1446 | 2025/01/09
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itakavyo Andaa Jeshi Lenye Nguvu Duniani Litakalo Pambana kwa Ajili ya Uislamu

• Tangu kuvunjwa kwa Khilafah 1924, usalama umekosekana ndani ya ulimwengu wa Waislamu, na kuwapelekea Waislamu kukosa mlinzi dhidi ya uvamizi wa madola ya kiulimwengu na kimaeneo, mapambano baina ya Waislamu yaliyo dhaminiwa kutoka nje na mabomu ya droni na kupelekea damu za Waislamu kukosa thamani. Fauka ya hayo, kuwepo kwa mashirika ya kiusalama ndani ya ardhi za Waislamu na matumizi ya majeshi ndani ya ardhi za Waislamu kupambana na watu wao inaonyesha wazi namna watawala walioko mamlakani hivi sasa ndani ya ulimwengu wa Waislamu walivyo telekeza jukumu la kulinda maisha ya watu wao wa kawaida.

• Mtume (saw) – alimuita Khalifah "ngao" na ni kurudi kwa ngao hii pekee ndiko kutakako pelekea kupatikana kwa amani na usalama ndani ya mipaka yake na kuwa lengo kuu la dola kwa mara nyingine.

 “Siasa ni kusimamia mambo ya Ummah kindani na nje. Hutekelezwa na Dola na Ummah. Dola ndiyo husimamia mambo ya Ummah kivitendo moja kwa moja na Ummah unaihesabu Dola." (Kifungu 181, Kielelezo cha Katiba, Hizb ut Tahrir)

• Usimamizi wa mambo ya Ummah kindani na kinje unatekelezwa kupitia utabikishaji wa mfumo (Uislamu). Kusimamia mambo ya Ummah kinje kunajumuisha mahusiano yake na dola nyingine, watu na Ummah nyingine na ulinganizi wa mfumo wa Kiislamu kwa ulimwengu hii ikiwa ndiyo sera ya kigeni ya dola ya Khilafah. Msingi wa sera ya kigeni ya Kiislamu umefungwa juu ya fikra isiyobadilika na inajumuisha kulingania ujumbe wa Uislamu kwa kila mtu na kila Ummah. Kwani Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

(يَا أَيُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ)

“Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake.” [Al-Ma'idah: 67]

“Mwenyezi Mungu (swt) amewapa utukufu Waislamu kwa kuwafanya kuwa ndio walinganizi wa Ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu wote na Yeye (swt) na amewawekea njia ya kuubeba ulinganizi huo kwa Da'wah na Jihadi.” (‘Jeshi', Nidhamu ya Utawala ya Kiislamu, Taqiuddin an-Nabhani, Hizb ut Tahrir)

• Ummah wa Kiislamu ni Ummah wa Jihadi na umefaradhishiwa kuulingania Uislamu kwa wanadamu wote. Umepewa sifa ya Ummah ambao unaondosha udhalimu na ukandamizaji kutoka shingoni mwa watu.

• Kuulingania Uislamu duniani ni kitendo msingi cha kisiasa, lakini nguvu za kijeshi huchangia katika mchakato huo. Hivyo basi, Khilafah italenga kuwa na jeshi bora duniani ili kuiwezesha Khilafah kudumisha amani na usalama ndani ya Dar ul-Islam na kufungua ardhi za Ukafiri na kuwa za Kiislamu.

• Khalifah ndiye aliye na mamlaka ya kisiasa na kijeshi. Hivyo basi, ataliandaa jeshi kuwa imara ili kuweza kutimiza jukumu lake la Jihadi na kuulinda Ummah kutokana na uadui wa dola zisizokuwa za Kiislamu.

“Khalifah ndiye Amiri Jeshi na humchagua kiongozi wa maafisa wakuu, jemedari wa kila bendera kubwa na kiongozi wa kila kikosi.” (Kifungu 65, Kielelezo cha Katiba, Hizb ut Tahrir)

• Ujenzi wa sera ya kigeni ya Khilafah itatilia maanani dhurufu zote za hali ya kimataifa. Uislamu umeweka muongozo katika hili na vipi kuendesha mahusiano yake na dola zilizopo duniani na kwa msingi huo Khilafah itachora mipango yake ya kisiasa ili kufikia malengo yake. La muhimu ni kwamba “njia muhimu zaidi ya kisiasa ni kudhihirisha utukufu wa fikra za Kiislamu katika kusimamia mambo ya watu binafsi, Ummah na dola.” (Kifungu 186, Kielelezo cha Katiba, Hizb ut Tahrir).

• Punde tu itakaposimama Khilafah, Khalifah atafanya kazi ya kusitisha mipaka baina ya Waislamu, kuziunganisha ardhi za Waislamu kuwa dola moja na kusimamisha jeshi moja. Miongoni mwa vipaombele itakuwa ni kuliboresha jeshi kwa thaqafa ya Kiislamu na kulipa dori yake ya kutumikia Uislamu na Waislamu.

• Khalifah binafsi atasimamia masuala ya jeshi na kubuni uhusiano baina ya ruwaza ya kisiasa na mipango ya kijeshi. Fauka ya hayo, kwa kuwa ni mwanasiasa na kiongozi wa kisiasa, Khalifah hafungwi na mtizamo finyu wa fikra za kijeshi na atabuni mbinu za kisiasa kushabiana na uwezo wa kijeshi ili kufikia malengo.

• Mafunzo ya kijeshi yataliboresha jeshi kwa ujuzi muhimu ili kutekeleza majukumu yake na kulipekea kuwa na taaluma ya kijeshi na ufahamu wa Kiislamu. Ufahamu wa Kiislamu ni muhimu mno katika kushajiisha vitani na kuimarisha ushindi kwa kuwavutia watu ambao ardhi zao zimefunguliwa upya ili waingie katika Uislamu na haki zake.

 “Ni lazima jeshi lipewe elimu ya kijeshi ya ustawi wa juu zaidi inayowezekana, na kunyanyuliwa ustawi wake wa kifikra kadri inavyowezekana. Kila mtu katika jeshi lazima apewe  thaqafa ya Kiislamu inayo muwezesha kuwa na busara ya kijumla kuhusu Uislamu.” (Kifungu 67, Kielelezo cha Katiba, Hizb ut Tahrir)

• Ni faradhi kulikabidhi Jeshi silaha, zana, vifaa na kila ambacho ni muhimu na kinachohitajika ili kuliwezesha kutekeleza majukumu yake kama jeshi la Kiislamu.

(وَأَعِدُّوا لَهُمْ مَا اسْتَطَعْتُمْ مِنْ قُوَّةٍ وَمِنْ رِبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّآُمْ وَآخَرِينَ مِنْ دُونِهِمْ لاَ تَعْلَمُونَهُمُ اللَّهُ يَعْلَمُهُمْ)

“Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamuwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawaju.” [Al-Anfal: 60]

• Ni faradhi kwa kila kambi iwe na idadi ya kutosha ya maafisa wa ngazi za juu walio na taaluma ya kijeshi na tajriba ya kuchora mipango na kuendesha vita. Jeshi kwa ujumla lazima liwe na maafisa wengi iwezekanavyo.

• Kila mwanamume Muislamu ambaye ametimia umri wa miaka 15 ni faradhi kupata mafunzo ya kijeshi ili kuandaliwa kwa Jihadi.

• Mshahara wa jeshi lazima uendane na thamani iliyowekwa juu yake na Uislamu kwa kuwa na jeshi lenye uwezo na taaluma ya kijeshi. Mchakato wa kuchagua maafisa na wanajeshi lazima uhakikishe ni kwa watu bora walio na uwezo wa kazi hiyo. Mapendeleo hayato ruhusiwa kudhoofisha jeshi la Dola ya Kiislamu.

• Jeshi halito husishwa na siasa, biashara au chochote kuhusiana na idara za Serikali ambacho italipelekea kutotimiza majumu yake.

“Jeshi ni sehemu mbili: Sehemu ya Akiba nao ni Waislamu wote wanaoweza kubeba silaha, na Sehemu ya Daima wanaolipwa mishahara kutoka katika bajeti ya Dola kama wafanyikazi.” (Kifungu 63, Kielelezo cha Katiba, Hizb ut Tahrir) Kando na kubuni kuwa na jeshi lenye nguvu la Kiislamu lililopata thaqafa, sera ya kigeni itahakikisha kuna kuweko maumbile huru ya Khilafah na jeshi lake kwa:

• Kusitisha utegemezi wote wa kiteknolojia kutoka kwa dola adui kwa kubuni mpangilio kabambe na wakasi wa kiviwanda ili kufikia ubora wa kijeshi unaodhaminiwa na nidhamu bora ya kiuchumi inayozalisha mapato makubwa ili kuweza kutekeleza majukumu yote ya serikali ya Khilafah.

• Kusitisha mafunzo yote yanayo tegemea dola adui kwa kubuni taasisi za dola za kutoa mafunzo na mipango ya kijeshi na ufahamu wa Kiislamu.

• Kusitisha mahusiano yote na maafisa wa dola adui na yote yanayotokana na mahusiano hayo mfano mafunzo ya kijeshi kutoka ng'ambo, kubadilishana ujasusi na mahusiano ya jeshi kwa jeshi.

• Kuzitizama dola zote zisizokuwa za Kiislamu kwa mtizamo wa kivita. Haya ni mataifa ambayo yanakalia Ardhi za Waislamu au zimefanya vitendo vya kimabavu. Khilafah itazifunga rasilimali za Ummah kukomboa Ardhi zilizo vamiwa mfano Kashmir na Palestina.

• Kuondosha vitisho kutoka kwa dola adui kwa kusitisha kambi zao zote, balozi zao zote na watu wao wote ndani ya Ardhi za Waislamu.

• Kufutilia mbali mawasiliano yote ya kisiasa na kijeshi na dola adui ambazo zinatumia mawasiliano hayo kutoa maagizo na kuwakanya vibaraka wao ndani ya uongozi wa kijeshi na kisiasa na kisha kutafuta wapya. Yote haya yataiwezesha Khilafah kulinda ardhi zake, raia wake na wale Waumini ambao wanakandamizwa pamoja na kueneza haki na huruma ya Uislamu kwa mataifa duniani.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلاَّ رَحْمَةً لِلْعَالَمِينَ)

“Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.” [Al-Anbiya: 107]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:52

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu