Jumatatu, 11 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dori ya Wanawake Katika Vyombo vya Habari vya Kiislamu Ndani ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Wakati sisi Waislamu tunapofikiria kuhusu dori ya wanawake katika vyombo vya habari, kuna uhalisia wa aina unaojitokeza akilini. Wa kwanza  umeegemea juu ya uhalisia uliopo tunaouona kote duniani ambapo wanawake na wasichana mara nyingi huwa ndio wanaolengwa na kudhulumiwa katika vyombo mbali mbali vya habari, kwa kuwekwa utupu, wakitumika kama chombo cha anasa kuliko kuwa mtu kamili na ambapo michoro iliosanifiwa ya wanawake na mvuto wao wa kijinsia hutumika kwa manufaa ya kifedha. Wa pili ni ule mpangilio wa kuhilikisha unaoonyeshwa kwetu na vyombo vya habari vya kilimwengu vya sasa kuwa wanawake wametengwa kabisa katika vyombo vya habari kama tuonavyo katika nchi za Kiislamu. Je, haya ndio machaguo mawili tu walionayo wanawake katika vyombo vya habari; ima kufanywa kama vyombo vya ngono au kufanywa wasionekane kabisa?

Tunahitajika kufafanua vyombo vya habari ni nini ili tuweze kujibu hili swali. Vyombo vya habari vyenyewe ni njia huru za mawasiliano ya umma. Hivi leo inajumuisha televisheni, intaneti, sinema, magazeti, radio na majarida. Watazamaji wanaweza kuona baadhi ya jumbe za picha kupitia aina maalum za matangazo na matangazo ya biashara. Lengo ni kuwashawishi wengine. Japokuwa vyombo vya habari ni zana ilio huru, lakini mara zote vinaelekezwa kwenye kichujio maalum kutegemeana na mitazamo katika jamii. Serikali huvitumia kushawishi maoni ya kifikra na kisiasa na kupitia vipindi vya vyombo vya habari, maoni haya husukumwa kwenye jamii.

Kulingana na jamii za kiliberali, vyombo vya habari vitakuza uhuru wa kiliberali na malengo ya kirasilimali kupitia njia zake mfano uhuru usio na mipaka wa kijinsia, ikiwemo kubadilisha muelekeo wa kijinsia, kukosekana kwa maadili imara ya familia, na watoto kuwa wanaongeza mzigo na kizuizi cha matumizi ya mtu binafsi, kukosekana kwa uwajibikaji wa kifedha na maisha ya kutegemea mikopo. Wakati huo huo, itakitenga kila kitu chenye kutafautiana na muundo huo kama udini na alama za kidini.

Pia jukumu la wanawake litatokana na uoni huu wa maisha na hii ndio sababu ujanajike wake unatumika kama njia ya starehe au namna ya kukuza hadhi yake ya kijamii na kifedha na ya wengine.

Katika hali kama hiyo, vyombo vya habari katika jamii ya Kiislamu itakuwa ni zana yenye nguvu katika kukuza maadili ya Kiislamu na fikra na kujenga uoni maalum wa maisha unaoegemea itikadi ya Kiislamu. “Chini ya Khilafah Chombo cha Upashaji habari ni afisi inayotawala, kuweka na kutekeleza siasa ya upashaji habari ya Dola ili kuhudumia maslahi ya Uislamu na Waislamu.-- Kwa ndani: Ili kubuni mujtamaa wa Kiislamu unaoshikamana, mujtamaa unaofukuza uovu na kukuza wema.” (Kifungu 103: Kielelezo cha Katiba ya Dola ya Khilafah ya Hizb ut Tahrir)

Kwa sababu hii, vyombo vya habari vya Kiislamu vitatafautiana kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari viliopo sasa duniani.

Kila kitakachotolewa kitakuwa ni chenye manufaa kwa mtu binafsi na jamii kwa jumla. Kila chenye kusababisha madhara kwa Uislamu na Waislamu kitazuiliwa. Habari, filamu za matukio, maonyesho ya mijadala na programu nyengine zitakuwa kwa mujibu wa hukmu za sharia, hazitohusisha mchanganyiko baina ya wanaume na wanawake, kudhihirisha uchi (Awrah) na matendo ya Haram, na vitu vyote visivyo na manufaa.

Dori ya wanawake katika vyombo vya habari vya Kiislamu vitaegemea juu ya uoni wa Uislamu na haki zao. “Mwanamke anapewa haki na majukumu yale yale anayopewa mwanamume ila kwa yale Uislamu ulimhusu mmoja wao kupitia dalili za kiSharia. Kwa hivyo ana haki kusimamia biashara, ukulima, viwanda, kusimamia mikataba na mu’amala, kumiliki kila sampuli ya mali na kuizidisha kibinafsi au pamoja na wengine. Na anaweza kusimamia mambo yote ya maisha kibinafsi.” (Kifungu 114: Kielelezo cha Katiba ya Khilafah ya Hizb ut Tahrir)

Dori yake itaonyeshwa kwa heshima ya juu, kuihifadhi heshima yake muda wote kama ilivyotajwa katika dalili za Kiislamu.

Mtume (saw) amesema:

«إِنَّمَا النِّسَاءُ شَقَائِقُ الرِّجَالِ، مَا أَكْرَمَهُنَّ إِلَّا كَرِيمٌ وَمَا أَهَانَهُنَّ إِلَّا لَئِيمٌ» 

“Wanawake ni mapacha wa wanaume. Hakuna anayewakirimu isipokuwa mkarimu, na hakuna anayewatweza isipokuwa mjinga” [Abu Dawuud]

Mtume (saw) pia amesema:

«اسْتَوْصُوا بِالنِّسَاءِ خَيْرًا» 

“Watendeeni wema wanawake.” [Bukhari na Muslim]. Kwa hivyo, Khilafah itaweka ulinzi wa heshima ya wanawake na usalama kuwa ni nguzo ya sera ya dola, ikiwemo ndani ya kitengo chake cha upashaji habari. “Yeye (Mwanamke) ni heshima (ird) ambayo lazima ihifadhiwe.” (Kifungu 112, cha Kielelezo cha Katiba ya Khilafah ya Hizb ut Tahrir)

Pia kutafuta elimu ni wajibu juu ya kila Muislamu awe mwanamume au mwanamke, kwa kuwa anabeba da’wah ya Kiislamu na kufikisha maarifa ya Kiislamu ili aelimishe, alee na kupandikiza shakhsia ya Kiislamu ndani ya wanajamii. Chombo cha Habari ni zana muhimu ya kufikia ummah na kwa sababu hiyo wanawake wanachukua dori muhimu katika vyombo vya habari kujenga jamii imara za Kiislamu kwa kukuza maarifa ya Kiislamu na kuamrisha Al Ma’rouf (mema) na kukataza Al Munkar (uovu) na hasa  kuwavutia wanawake wengine kuwa vigezo wakiwa ni mama, wake, wanazuoni na wabebaji da’wah na hatimaye kujenga heshima na imani inayoegemea juu ya fikra sahihi za Kiislamu. 

Tunaomba kuwa karibuni tuweze kuhisi athari za moja kwa moja za vyombo vya Habari vya Kiislamu ambavyo vitacheza dori muhimu mno katika kuiokoa jamii kutoka kwenye mmiminiko wa kuendelea wa sumu tunaouruhusu ndani ya majumbani mwetu, chombo cha habari ambacho wanaume pamoja na wanawake watafanya kazi kwa bidii kubadilisha uoni na fikra za jamii kwa kiwango kikubwa kuelekea kwenye Uongofu uliotukuka wa Muumba wao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Yasmin Malik

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

 #YenidenHilafet         #ReturnTheKhilafah     #TurudisheniKhilafah        الخلافة_101  #أقيموا_الخلافة#    

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu