Jumatatu, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Shariah ndio Suluhisho Pekee la Kuwahifadhi Wanawake wa Kiislamu Kutokana na Unyanyasaji wa Kijinsia

(Imetafsiriwa)

Ubakaji na aina nyengine za udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wanawake wa Kiislamu ni jambo lililoenea katika ardhi za Waislamu tokea kuanguka kwa Khilafah. Wakoloni wametumia udhalilishaji wa kijinsia kuwafedhehesha na kuwatiisha wanawake na familia zao. Mataifa ya Kimagharibi yaliochukua ardhi za Waislamu hivi leo kupitia watawala wao vibaraka bado wanatumia maonevu ya kijinsia, kunajisi, ubakaji, ubakaji wa kimakundi, na mateso ya kijinsia kuwa si tu njia ya kuingiza hofu kwa wanawake na wanaume na kutia makovu ya aibu kwa wanawake, bali pia kuvunja kiunzi cha jamii ya familia. Ubakaji wa kupangwa kwa dada zetu huko Srebrenica, Darfur, Sierra Leone, na maeneo mengine mengi yalimalizwa kwa machozi ya mamba tu ya viongozi wa dunia na kutowajibishwa kwa wakosaji wa uovu huo kwa sababu wao ni sehemu ya hali ya sasa ilivyo.

Licha ya CEDAW, licha ya Jukwaa la Utendaji la Beijing, licha ya kauli za mara kwa mara, sheria, na maazimio ya UN kupitishwa kwa kipindi cha miongo kadhaa, suala la ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake limeenea kama lilivyokuwa. Maovu haya bado yanafanyika dhidi ya ndugu zetu wa kike katika Myanmar, ambako watoto wetu na dada zetu wanabakwa kutokea umri wa miezi 4 hadi miaka 80, nchini Afghanistan ambako dada zetu wanashurutishwa kufanya ngono kwa lengo la kupatiwa upendeleo ili wahifadhi ajira zao kwa kusaidia familia zao, nchini Syria, ambako dada zetu wanapata mateso ya kijinsia ya ajabu. Wakati dada zetu wanapojaribu kuomba hifadhi katika nchi nyengine za Waislamu, au nchi za Ulaya, wanakutana na hali ya kinyaa na isiyo na usalama, unyanyasaji zaidi wa kijinsia, na kitisho cha usafirishaji haramu wa binaadamu. Haya yote yanatokea kutokana na sheria za kisekula, za kirasilimali na utamaduni unaodhihirisha kwa uwazi ujinsia, na kutumika wanawake kukuza ajenda zao za kubomoa familia na jamii tunayolazimika kuishi nayo. Hakuna kilichobadilika na hakuna kitachobadilika, kama historia inavyotuthibitishia muda baada ya muda chini ya nidhamu ya ukandamizaji na ufisadi. Dada zetu wanalilia msaada, lakini hakuna serikali au jeshi la kuja kuwasaidia.

Fikiria namna gani maisha yatakuwa kwetu sisi, kama wanawake Waislamu, kote duniani pindi Khilafah itaposimamishwa na kutabikisha Shariah. Tutapata heshima katika jamii na kuhifadhiwa wakati wa vita na wakati wa amani (Kifungu 112). Wanawake wa Kiislamu hawatoishi kwa wasiwasi kutokana na kunyanyaswa kijinsia, au mbakaji wake kutembea huru mitaani bila hofu ya kuadhibiwa. Wanawake hawatatazamwa kama ni vyombo vya kutumiwa na wakati wowote mwanamume anapotaka ili kupata elimu au kazi (Kifungu 113 na 118). Dola ya Khilafah itatekeleza nidhamu ya elimu itakayozingatia juu ya kujenga kitambulisho cha Kiislamu katika fikra na matendo kulingana na Aqida ya Kiislamu (Kifungu 171), ambayo itahakikisha kuwa wanawake wanaamiliwa kwa heshima na hadhi muda wote, na sio kama Aqida potofu ya Wamagharibi.

Hatuwezi kuendelea kuzitazamia serikali zile zile za Kimagharibi na mabwana wa vibaraka kuja na kuhifadhi ardhi ya Waislamu kwani hao ndio hasa wanaosababisha machafuko na kukosekana usalama. Sisi kama Waislamu, tunahitaji kuangalia Dini yetu kwa ajili ya suluhisho. Tunahitaji kukimbilia kusimamisha Khilafah na kutabikisha nidhamu ya Kisharia tulioletewa na Muumba wetu.

InshaAllah, wanawake wataishi kwa amani na usalama, kama tulivyowahi kuishi chini ya Khilafah, ambapo machafuko ya kila aina yalikuwa machache kutokana na utabikishaji wa Shariah na nidhamu ya kiadilifu ambayo ilimuadhibu vikali kila aliyetenda uovu dhidi ya wanawake. Nidhamu ambayo tutakuwa na Khalifah atakayepeleka jeshi kumuokoa kila mwanamke Muislamu atakayelilia msaada. Nidhamu itakayokuwa ni mwangaza kwa wanawake kutokana na Magharibi kuja kuishi chini ya kivuli chake na hifadhi, kwani nao wanateseka pia kutokana na idadi kubwa sana ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na huku wakiwa na matumaini madogo kwa waovu kuhukumiwa kwa makosa yao.

Hii ndio dunia tutakayokuwa nayo, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt), tutakapoichukua Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuitabikisha chini ya Nidhamu Yake kwa namna ambayo Mtume wetu kipenzi Muhammad (saw) alivyofanya mjini Madina.

#YenidenHilafet    #ReturnTheKhilafah     #أقيموا_الخلافة#

  #TurudisheniKhilafah 

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sarah Mohammed – Amerika

 

Kutoka Kielelezo cha Katiba ya Khilafah cha Hizb ut Tahrir:

Kifungu 112 – Kimsingi mwanamke ni mama na msimamizi wa nyumba. Na yeye ni heshima ambayo ni wajibu kuhifadhiwa.

Kifungu 113 – Kimsingi hutenganishwa baina ya wanaume na wanawake wala hawajumuiki pamoja ila kwa haja ambayo Sharia imeikiri, na kukiri kujumuika kwao kwa ajili yake mfano hajj na biashara.

Kifungu 118 – Kuketi kifaragha (khalwa) baina ya mwanamume na mwanamke wa kando (ajnabi) huzuiliwa kama hakuna mahram, na kadhalika tabarruj na kuonyesha tupu huzuiliwa mbele ya ajnabi.

Kifungu 171 – Lengo la elimu ni kuunda shakhsiya ya Kiislamu na kuwapa watu elimu na maarifa yanaohusu mambo ya maisha. Njia (twariqa) za elimu hupangwa kwa njia inayohakikisha lengo hili, na kila twarika inaofikisha kwa lengo tofauti na hili huzuiliwa.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu