Jumatatu, 19 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ufahamu wa Kina (Basira) na Mtazamo wa Mbele (Firasa) Unataka Ulinganizi wa Khilafah

(Imetafsiriwa

Mwezi wa Rajab ni kipindi pekee cha wakati unaovuma katika miezi mitatu mitukufu, unaowasha tafakkur (kutafakari) na tadabbur (kuzingatia) na kusababisha muanga wakati wa mwezi wa Ramadhan na Laylat-ul Qadr. Hii ni awamu ya kukumbuka, kuhakiki na kuhesabu mwaka mzima, zaidi ya hayo kipindi chote ambacho Wahyi ulikuwa umehakikisha izza na maendeleo kwa wanadamu, hivyo kufanya mipango, kubuni mikakati mipya na ya makusudi ili kumridhisha Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Walimwengu. Mwezi wa Rajab ni kipindi cha kuwa, kushikana na kuongeza ufahamu.

Ni kweli, kwamba sisi Waislamu tunafahamu mambo na hali. Kwa hakika, si Waislamu pekee, bali wanadamu wote wanafahamu orodha isiyo na kikomo ya maovu, na ukweli kwamba ulimwengu na wanadamu vinapeperuka kuelekea shimoni. Hata hivyo, kuwa na ufahamu kama watu wengine haitoshi kwa “Ummah bora ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameutoa kutoka miongoni mwa wanadamu” ili kuwa mwongozo na shahidi kwa wanadamu.

Ufahamu ni hali au uwezo wa kutambua, kuhisi, au kuwa na utambuzi wa matukio, vitu, au mipangilio ya hisia. Inamaanisha "kuwa na ufahamu wa kitu". Hata hivyo, kama ilivyo katika kila suala linalohusiana na maisha, Uislamu umefafanua "ufahamu" kwa njia inayozingatia suluhisho la kweli kwa wanadamu na umeweka katika fomula yenye fahamu ya "ufahamu wa kina na mtazamo wa mbele" na kuziunda kama "mradi" ambazo ni lazima utekelezwe.

Ufahamu wa kina (Basira - البصيرة) umetumika katika Qur'an kwa maana ya jumla ya "kuona" na vile vile kwa maana ya "uwezo wa kugundua haki, kutambua njia sahihi, kutenganisha haki na batili" na katika suala hili inachukuliwa kuwa ni kinyume cha upofu wa kiroho au upotofu (Al-An'am 50, 104; Hud 24; Al-Isra 72; An-Naml 81). Ufahamu wa kina ni uwezo wa kupata ufahamu sahihi na wa kina wa mtu au kitu fulani, kukijua kutoka katika kila nyanja, asili yake na ukweli wake. Kinyume chake ni uzembe na upofu.

Mtazamo wa mbele (Firasa - الفراسة), ambayo inamaanisha "uchunguzi, utambuzi, mtazamo wa mbele" katika kamusi, ni kutathmini hali ya sasa au maoni kwa usahihi, kuchukua hatua sahihi za siku zijazo kupitia nuru ya Uislamu, uwezo wa kuhukumu kwa usahihi na haraka na kuchukua hatua sahihi. Kuona mbele ni njia ya kimkakati ya kufikiri ili kufanya maamuzi sahihi kwa kujilinda kwa Mwenyezi Mungu (swt).

[وَمَا يَسْتَوِى ٱلْأَعْمَىٰ وَٱلْبَصِيرُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَلَا ٱلْمُسِىٓءُ ۚ قَلِيلًا مَّا تَتَذَكَّرُونَ]

Na kipofu na mwenye kuona hawalingani; na walio amini na watendao mema hawalingani na muovu. Ni machache mnayo yakumbuka.[Al-Ghaafir: 58]

[يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۗ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ]

Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo, na atakufutieni makosa, na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.” [Al-Anfal: 29]

Ili mtu awe na muono wa mbele, ni sharti ausafishe moyo wake kutokana na nia mbovu na chuki, na akili yake kutokana na kila aina ya uchafuzi usio wa Kiislamu. Muumini mwenye utambuzi wa kina na muono wa mbele ameegemeza akili yake, hisia na matendo yake juu ya dalili na hukmu za Sharia pekee.

Ufahamu wetu wa kina na muono wa mbele unatuonyesha kwamba tulikuwa na hadhi na maendeleo tu wakati wa utawala wa Dola ya Khilafah. Kwani Uislamu ulitabikishwa pekee kama mfumo mpana chini ya Dola ya Khilafah. Na tunaona kwamba tulipoteza hadhi hii na maendeleo haya katika mwezi wa Rajab mwaka 1924, pale Khilafah ilipo ondolewa na Magharibi kafiri na vibaraka wake. Kutokana na hasara hii kubwa, tunaona kwamba sisi wenyewe pamoja na wanadamu tumetumbukia katika mazingira ya kukua na kuenea kwa machafuko.

Ufahamu wa kina na kuona mbele yanatuonyesha njia pekee ya kutoka katika machafuko: ambayo ni kurudi kwenye Maisha ya Kiislamu! Kwani Aqida ya Kiislamu sio tu ya kiroho pekee, bali ni itikadi ya kiroho na ya kisiasa, kila Muislamu kimaumbile ni mwanasiasa. Muumini mwenye ufahamu wa kina ni mwanasiasa ambaye anafanya kazi ya kuuasisi Uislamu kama mamlaka yanayotawala kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt), ili Waislamu waishi maisha ambayo wanaweza kumtumikia Mwenyezi Mungu pekee kwa njia salama na amani.

Mtazamo wetu wa kina na muono wa mbele unatuonyesha kwamba Mola wetu hakutuamrisha tu kuufanya Uislamu utawale, bali pia aliweka njia ya namna ya kutekeleza amri hii. Njia hii ndiyo njia ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliifuata wakati alipokuwa Makka. Ambayo ni kujenga rai jumla kuhusu lengo na masuluhisho ya Uislamu ili kuyafanya maisha ya Kiislamu yatawale tena, ambayo ni kazi ya kisiasa na kifikra bila ya kuogopa chochote na bila ya shaka kuwa Mwenyezi Mungu ndiye atakayejaalia mafanikio. Hili linahitaji kuwaeleza watu kwamba haki na batili (Haqq na Batil) vimetenganishwa waziwazi. Ni lazima tuone na kufichua uozo wa mawazo ya Kimagharibi, fahamu, masuluhisho na ajenda zisizo za Kiislamu za Magharibi. Kwa ufupi: Ulinganizi wetu kwa Uislamu ni ulinganizi juu ya Njia ya Utume wa utawala wa Khilafah Rashida, ambao utaregesha maisha kamili ya Kiislamu, kuzima mashambulizi yoyote dhidi ya Aqida ya Kiislamu kwenye chanzo chake yanapoanzia, na ambao utawaongoza wanadamu kutoka katika machafuko ya giza hadi ndani ya nuru ya Uislamu, ambapo inahakikisha maisha ya amani kwa wanadamu. Kwani njia pekee ya kuutabikisha Uislamu ni Khilafah Rashida pekee.

Mtume wetu (saw) amesema: «اتَّقُوا فِرَاسَةَ الْمُؤْمِنِ فَإِنَّهُ يَنْظُرُ بِنُورِ اللَّهِ» “Uogopeni mtazamo wa mbele wa muumini, kwani yeye hutazama kwa nuru ya Mwenyezi Mungu.” Kuanzia hapo na kuendelea, muumini aliye na ufahamu wa kina na kuona mbele hatakuwa na wasiwasi tena juu ya mustakabali wake, kwa sababu amechukua tahadhari zote muhimu kwa ajili ya mustakabali.

[قُلْ هَٰذِهِۦ سَبِيلِىٓ أَدْعُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا۠ وَمَنِ ٱتَّبَعَنِى ۖ وَسُبْحَٰنَ ٱللَّهِ وَمَآ أَنَا۠ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ]

Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina.[Yusuf: 108]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu