Jumatatu, 23 Sha'aban 1445 | 2024/03/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mabadiliko kama Yalivyofafanuliwa katika Quran na Sunnah

(Imetafsiriwa)

Pindi mtu anapokuwa ameikubali Shahada na kujitolea kuwa mja wa Mwenyezi Mungu (swt), hakuna upinzani katika kusalimisha fikra na hisia zake zote kwa yale yaliyoamrishwa katika Quran na Sunnah.

Hakuwezi kuwa na udhuru wowote kuwa haiwezekani, kwani masuala yote ya mahitaji ya mwanadamu yamejibiwa na Mwenyezi Mungu (swt).

[الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينًا]

“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” [Al-Maida: 3]

Tunapoangalia maana ya “Mabadiliko” katika Uislamu, ni lazima basi tupate maana sahihi ya muundo wa Mwenyezi Mungu (swt), kwani chimbuko jengine lolote la tafsiri litakuwa dhaifu na lisilolingana na kitambulisho cha aqliya ya Muislamu. Aya ya maarufu inayotumika vibaya kuhusu mabadiliko ni Surah Ra’d aya ya 11. Mwenyezi Mungu (swt) asema yafuatayo

[لَهُ مُعَقِّبَاتٌ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ يَحْفَظُونَهُ مِنْ أَمْرِ اللَّهِ إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِقَوْمٍ سُوءًا فَلاَ مَرَدَّ لَهُ وَمَا لَهُمْ مِنْ دُونِهِ مِنْ وَالٍ]

“Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake.” [Ar-Raad: 11]

Wanamambo sasa na wapenda maendeleo hutumia hii kama dalili ya kuhalalisha maendeleo ya ndani ambayo hayana uhusiano na mabadiliko mapana ya kijamii na kisiasa. Aghlabu tunasikia mazungumzo, vipindi na matangazo ya vyombo vya habari yanayotoa wito wa kujiendeleza kibinafsi bila kuwahisabu watawala hata kidogo ambao kwa ukaidi wanafanya maovu na kuwanufaisha mabwana zao makafiri mwaka baada ya mwaka, utawala baada ya utawala.

Mamilioni mengi ya watu wamejielimisha katika Sharia, wamehifadhi Qur'an na wakafanya juhudi "kuikamilisha dini yao" (ambayo haiwezi kukamilishwa kwani tutalipwa kwa juhudi zetu za dhati). Yemen ina watoto wenye njaa kwa mamilioni. Vita vya 1 na 2 vya Ghuba vilitekelezwa bila kizuizi cha mauaji na kususia na kukamatwa kwa Waislamu wasio na hatia. Warohingya wanazurura duniani mwaka baada ya mwaka bila msaada wowote kutoka uhamishoni mwao. Palestina inakaliwa kimabavu kwa miongo kadhaa, huku vizazi vikizaliwa katika kambi za wakimbizi chini ya uvamizi wa adui. Orodha ya ugaidi na machafuko ambayo mataifa yetu ya Kiislamu yanakabiliwa nayo haina mwisho. Vijana wetu wanavurugwa akili kwa tamaduni za watu waliobadili jinsia na ubinafsi wa hali ya juu hadi kufikia nukta ambapo maadili ya familia hayana maana. Talaka ni mchezo wa kuchezwa mtu atakapo.

Hayo yote yanatokea huku Ummah ukiuliza "ni lini haya yatabadilika?!!"

Jibu lipo katika tafsiri ya aya hii ambapo maana sahihi inatolewa na wanavyuoni wasomi wa Kiislamu.

Ibn Kathir anaeleza haja ya kutabikisha kikamilifu maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt), kwani vyenginevyo hakuna anayeweza kukusaidia.

“Hii ni kuwaonya zaidi kwamba wasikae katika upotofu wowote kwamba mtu fulani mtakatifu au Malaika ana nguvu ya kuwaokoa na adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwani hakuna wa kuwatetea mbele ya Mwenyezi Mungu, ijapokuwa huenda walikuwa wakitoa heshima na kutoa sadaka kwa wale wanaoitwa wasimamizi na walinzi wao kwa kutaraji kuwa watawaokoa na adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama."

Tunapotazama Sunnah, tunaona kwamba Mtume (saw) alipopewa ruhusa ya kuswali, wakati aliadhibiwa na Maquraishi hapo mbeleni, bado aliwaamrisha Maswahaba kusimamisha utawala wa Kiislamu mjini Madina kama ya mamlaka Quran na Sunnah ili kuwepo katika nguvu yake kamili ya nje. Kwa hivyo wazo hili kwamba maendeleo ya ndani ndio tu tunayohitaji haliwezi kuwa sahihi. Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) adumishe njia iliyonyooka ya fikra safi na uongofu ili tukutane Naye (swt) kwa heshima tukipokea thawabu na radhi zake (swt), Ameen!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammed
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu