Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Serikali ya Kyrgyz kwa Kutapatapa Inajaribu Kulinda Maadili ya Kisekula

Kupitia Kuwapiga Vita wale wote Wanaoeneza Fikra za Kiislam

(Imefasiriwa)

Japokuwa wengi wa watu wake ni Waislam (80%), serikali ya Kyrgyz imekuwa ikisisitiza juu ya kuwa na mfumo wa serikali ya kisekula na kuendelea kushikamana nao. Katika jibu lake juu ya utata uliotokea kuhusiana na utambulisho wa nchi mwaka 2014 kufuatia kutangazwa Bishkek mji mkuu wa Kyrgyzstan kuwa mji mkuu wa thaqafa ya Kiislamu katika eneo la Asia, serikali imehakikisha kuwa hilo halitoathiri usekula wa dola, na haya ni mambo ya kitamaduni ambayo hayaipotoi dola kutoka katika njia yake ya kisekula.

Njia ambayo inapelekea – kama ilivyo nchi nyengine za kisekula zinazouangalia Uislamu na ibada zake kuwa ni kitisho kwa uhai wao – kuwa na aina tofauti na kuchukua vigezo viwili vyenye kugongana; inadai kuhifadhi ibada za kidini kwa upande mmoja, na kwa upande mwengine kumnyanyasa kila anayefanya kazi kueneza fikra za Uislamu na kunyanyua bendera yake. Inaeleza kuwa inahakikisha haki za binaadamu na uhuru, hivyo inaendesha mikutano kuzungumzia hatua zinazolenga kuimarisha mfumo kwa lengo la kuhifadhi haki hizi na uhuru, na baadaye kugeuza maamuzi yao na kuwakamata na kuwanyanyasa vijana wengi wa Kiislamu wake kwa waume.

Mwaka 2009, Raisi wa Kyrgyzstan alipiga marufuku uvaaji wa shungi katika shule za umma, akidai kuwa anahifadhi maadli ya kisekula na kutoyumba katika njia ya umma ambayo inapambana na “ugaidi” na kila kitu kinachoashiria! Hakusita kuelezea kukataa kwake na msimamo wa kupinga hijab na kuingilia juu ya uhuru wa wanawake Waislamu wa kuvaa kwa kusema, “Uislamu hauko katika nguo lakini uko katika nyoyo na tabia”, na alidai kuwa “Quran haikuelezea kuhusu uvaaji wa Kiislamu, na kuwa Uislamu umesisitiza juu ya usafi wa nguo tu”, (Alukah.net). Mgongano wa wazi katika sera yake, wakati akidai kuwa nchi yake inawakilisha thaqafa ya Kiislamu, lakini kwa upande mwengine, amezuia wasichana waliojihifadhi kuingia katika shule na vyuo vikuu, achilia mbali ukiukaji wa serikali yake juu ya haki na uhuru wa wanawake Waislamu watwahirifu ikiendeleza ukamataji na kuwasukumiza korokoroni kwa mashtaka dhaifu ya kutungwa na kutoa vitisho kwao na kwa watoto wao na familia zao, kwa sababu tu ya kueneza fikra za Uislamu na kujifunga na maadili yake.

Serikali ya Kyrgyz inafuata njia ya mfumo wa kisekula, kuonyesha uaminifu wake na utiifu kwa India, ambayo inaipatia msaada wa kifedha na huku nyuma yake ikitekeleza mipango yake kuushambulia Uislamu “Mkali” na Waislamu. Nia mbaya na chuki ya India kwa Uislamu na vitendo vyake viovu dhidi ya ndugu zetu Waislamu haifichiki, hivyo serikali ya Kyrgyz inasumbuliwa na umasikini unaoisukuma kukumbatia fedha kutoka kwa muabudia ng'ombe, Waziri Mkuu wa India!

Kukosekana kwa hisia za kiroho na umasikini wa vitu ambavyo nchi za kikafiri zinavitumia kwa manufaa yao wenyewe: zinalazimisha hali na mbinyo kwa serikali ya Kyrgyz kutekeleza mipango yao ili kudhoofisha, kuwakandamiza na kuwanyanyasa Waislamu.

Mnamo 30/06/2015, Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan alifanya mkutano ambapo alimpatia Waziri wa Ndani, Usalama wa Taifa na Idara Kuu ya Usalama kufanya kazi ili kuhakikisha na kuchunguza taasisi zote za Kiislamu nchini. Sera iliochukuliwa na serikali kudhoofisha Waislamu chini ya anwani “ugaidi” imeanzishwa na mfumo wa kiulimwengu wa kisekula wa kirasilimali katika vita vyake vya hadhara ya kifikra dhidi ya Uislamu.

Serikali hii, kama serikali nyengine za kisekula, zinahitaji kubakisha ufisadi wa mfumo wake, kunyanyua wito na madaha ili kudanganya kuwa ni walinzi wa maslahi na wenye kuhifadhi haki na uhuru, lakini kwa hakika umejifunua, kuwacha wazi uovu wake, na udhalilishaji wake na kukiuka haki hizi na uhuru kumeonekana: wanatenda kinyume na kile wanachokisema.

Mnamo Februari 7, 2020, Raisi wa Kyrgyzstan alimpokea Mchunguzi wa Malalamiko ya wananchi (Ombudsman), aliyempatia taarifa na habari kuthibitisha ukweli na matakwa ya wananchi kuhusiana na ukiukwaji wa haki zao na uhuru, na kusaidia kuwaregeshea.

Ripoti ya mwaka ya Ombudsman “Juu ya suala la haki za kibinadamu na kiraia na uhuru katika Jamhuri ya Kyrgyz” ilitayarishwa na kutolewa kwa Baraza Kuu la Kyrgyz. Taasisi ya Ombudsman ina jukumu maalum katika kuchukua hatua muafaka kuhifadhi haki za kibinaadamu, kuzuia aina yoyote ya ubaguzi katika haki za kiraia na uhuru, na kuonyesha haja ya hatua za haraka kwa mambo yote ya ukiukwaji wa heshima na uhuru wa raia.

Hivyo, iko wapi hii taasisi ya Ombudsman kwa kile kinachotokea kwa Waislamu na wasichana wao, wanawake na watoto?! Iko wapi wakati wanajeshi wakivamia na kupekua makumi ya majumba ya Waislamu?!

Ziko wapi hatua muafaka zinazochukuliwa na taasisi hii kuhifadhi haki za wanafunzi watatu wa kike, wenye miaka kati ya 18 na 20 waliowekwa ndani mwaka 2013 kwa makosa ya kueneza thaqafa ya Kiislamu na kumiliki baadhi ya matoleo, ambapo ni kinyume na uhuru wa kujieleza wa kisekula wanaojisifia nao?!

Iko wapi taasisi hii, ambayo italinda kila aina ya ubaguzi wa haki, kwa yale yaliowatokea dada zetu Zulfiya Amanova, aliyekamatwa kwa jaribio lake, miaka 14 baada ya vikosi maalum vya Uzbek kumteka baba yake, kuanzisha uchunguzi kuhusu mazingira ya kuuliwa kwake jela?!

Yako wapi mateso na uovu unaotokea kwa wasichana Waislamu walio jela?!...

Machafuko na ukamataji unaendelea dhidi ya wanawake watwahirifu nchini Kyrgyzstan, wakati taasisi hii na taasisi nyengine zinazodai kulinda haki za wanaadamu kutowajali, hivyo kufichua vita vinavyo ongozwa na mataifa ya Kikafiri na kuungwa mkono na serikali vibaraka ambazo zinaendesha masuala ya Waislamu na kuwaongoza kwa fikra za Kimagharibi ambazo ni ngeni na dini yao. Maovu ya serikali ya Kyrgyz yanaendelea, wakivamia nyumba za Waislamu wa kike katika siku chache zilizopita na kuwakamata kwa mashtaka ya kuhusika na taasisi iliopigwa marufu bila kuwajali walio wagonjwa katika wao, au wenye kuwatunza wazee wao, au kuwalea watoto wao: inagonga kila kitu kwenye ukuta na kutupa chini miito yake yote ya kifahari ili kuonyesha kujitolea kwao ili kutekeleza maagizo na utiifu wake kwa maadili ya kisekula.

Mateso ya dada zetu katika Kyrgyzstan yatakwisha tu kupitia serikali ambayo Imam atahukumu kwa Uislamu, ambayo haitaruhusu heshima kuvunjwa, wala kumwagwa damu ya Muislamu, hivyo ataweza kuhamasisha majeshi na kuwalinda raia wa dola na kuwahifadhi. Mateso yao na mateso ya Waislamu wa kike kila mahala hayatokwisha isipokuwa kwa kusimamishwa Dola ya Khilafah, ambapo wataishi maisha ya utulivu na amani.    

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aiharakishe, afute maumivu na aponye majeraha.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Zeinah As-Samit

                                                                                                                                                                                                                                                                                                                        #مسلمات_قرغيزستان

#KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük

#FreeMuslimahsKyrgyzstan

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 29 Agosti 2020 13:10

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu