Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Raisi Mpya Mteule Hatokuwa Tofauti

“Tarajio Lililosubiriwa Limekwisha Huku Biden Akishinda nchini Amerika Iliyogawanyika Vibaya.

https://epaper.dawn.com/DetailNews.php?StoryText=08_11_2020_001_006

Baada ya ushindani uliokaribiana mno kuliko walivyotegemea watafiti wa maoni, uendelezaji wa kuhisabu kura na madai ya Trump na Chama cha Republican; mwana democrat Joe Biden ameongoza kura za electoral college zinazohitajika ili kuwa raisi mteule.

Hata hivyo wakati kura zikihesabiwa ilikuwa sio kawaida kuona taifa linagawanyika kwa namna isiotarajiwa baina ya jozi ya wazee weupe wawili. Wote wakiwa wenye sifa zisizoweza kutetewa, sio kusifiwa kwa uwezo wao mzuri wa kimaamuzi wala kisiasa, na wote wakiwa mbali na kuwa waonyeshaji wa kupiga hatua mbele na maendeleo – lakini kwa sasa wao ndio wabora zaidi ambao taifa linaloongoza duniani limewatoa.

Hata hivyo eneo la kisiasa la Amerika ndio liko hivyo. Ima wapiga kura wawe wanajiita waliberali au wahafidhina, uhalisia wa mfumo wa kirasilimali ni kuwa unaenea katika kila eneo la fikra ya kisiasa kwa kuunda kila mjadala kwa maadili ya kisekula na kiliberali kwa kiwango cha kukaribia kutokuwepo mpaka wa uhuru wa kibinafsi na wa kifedha.

Kwa kuwepo Joe Biden kama raisi wa Amerika, Waislamu kote duniani huenda wakahisi kuwa Waislamu nchini Amerika watapata uhuru kuufanyia kazi na kuutekeleza Uislamu na kuwa sera ya kigeni ya Amerika haitokuwa dhidi ya Uislamu. Waislamu huenda wakadanganyika na baadhi ya kauli za Raisi mteule.

“Raisi mteule ameahidi kusitisha vizuizi vilivyowekwa na utawala wa Trump kwa zaidi ya darzeni ya mataifa.”

“Jumbe katika mitandao ya kijamii zinadai kuwa mgombea uraisi wa Amerika Joe Biden anataka “Uislamu ufundishwe katika shule zetu”, wakidhania kuwa hili litakuwa ni kwa gharama ya ufundishaji wa Ukristo. Dai hili ni lenye kupotosha na lisilowakilisha kauli ya Biden.

“Raisi Mteule wa Amerika Joe Biden amemnukuu Mtume Muhammad…”

Kwa mtazamo mfupi wa urithi wa maraisi mtawalia wa democrat na wa republican, utawala wa Bill Clinton ulikuwa maarufu katika kufuatilia kinachoitwa mchakato wa amani wa Waarabu na ‘Wayahudi’. Clinton alitekeleza dhamira lake kwa mapatano ya Mkataba wa Oslo baina ya Yitzhak Rabin na Yasser Arafat mnamo 1993 ikiwa ni sehemu ya mradi unaoendelea wa Kizayuni na Kiamerika, ambao unatumika kuwanyang'anya Ummah wa Kiislamu haki yao ya kikanuni na kisharia kwa ardhi iliobarikiwa ya Palestina.

Kujihusisha kwa Clinton nchini Iraq baada ya uingiliaji kati wa George Bush Baba nchini Kuwait, umemsukuma kupeleka makombora ya masafa mafupi kwenye vituo vya Iraq na kuweka vikwazo kwa raia. Uingiliaji wake nchini Somalia na Sudan umetekeleza malengo ya jiografia ya kisiasa ya Amerika katika eneo; na kufeli kabisa kukabili mauwaji ya halaiki ya Rwanda yaliogharimu zaidi ya maisha ya watu 800,000. Jukumu lake la kuweka vikwazo vya silaha nchini Bosnia limewaacha Waislamu bila silaha, iliopelekea mauwaji Srebrenica, ambayo pengine ndio yanayoelezea zaidi kuhusu msukumo wa wana Democrat.

Akimfuata Clinton, George W Bush Mwana ni maarufu kwa kuchochea uvamizi wa Iraq na Afghanistan baada ya 9/11. Alitoa ufafanuzi wa vita vya kilimwengu dhidi ya ugaidi (WoT) ambapo vyombo vya habari vya serikali kwa haraka vimevitengezea silaha kwa kuweka msamiati 'Waislamu wenye misimamo mikali', kama propaganda yenye kuwapa sifa hii Waislamu wanaopinga ubeberu wa kimagharibi na sera ya kigeni.

Vita vya utawala wa Bush vimeshuhudia angalau watu milioni 5 wakikosa makao nchini Iraq, huku mamilioni wakiwa wajane na mayatima. Mtu moja kati ya kila watu wawili ameathirika na kubadilika kwa maisha yake au kutokana na athari za baada yake, huku ikikadiriwa vifo vya zaidi ya watu 1.2 milioni. Ukatili na udhalilishaji wa vikosi vya washirika wa uvamizi wa Iraq umewaweka raia wa Iraq katika mazingira ya udhalili kwenye magereza ya kijeshi, pamoja na makombora ya mabomu ya angani na fosforasi nyeupe, ambapo athari zake za kushtua zinadhihirika hadi leo.

Vivyo hivyo nchini Afghanistan, vikosi vya Amerika vimeuwa makumi ya maelfu katika juhudi za kuiwinda Al Qaida na kuiadhibu Taliban halisi kwa kusubutu kuunda fikra ya utawala wa Kiislamu. Askari waoga wa  Amerika wamefanya maovu ambayo mfano wake hayajashuhudiwa au kusikika kabla, ya kuwafunga jela bila hatia wanaume, wanawake na watoto, unyanyasaji wa kingono na kuzidhulumu nafsi safi na kudai kuleta demokrasia kwa wa-Afghani wanaokandamizwa.

Huku Vita dhidi ya Ugaidi vikiendelea wakati wa uraisi wa Barrack Obama, jina lenye lafdhi ya Kiislamu na ufasaha wa kuzungumzwa yaliupumbaza ulimwengu na Waislamu wengi walinaswa kwenye mvuto wake wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democrat. Wakiwa wepesi kumpatia msaada wa ukarimu huyu mbwa mwitu aliejivika ngozi ya kondoo, dunia ilitazama huku akiyapoteza mwelekeo Mapinduzi ya ya Kiarabu na akiutetea utawala dhalimu wa Syria. Obama ameuwa Waislamu wengi zaidi ya waliomtangulia kwa mashambulizi ya droni nchini Yemen na Libya, huku akiinajisi Iraq na Syria chini ya kivuli cha kupambana na waasi katika mapambano mengi.

Haya yakizungumzwa, chini ya maraisi hawa watatu tu tumeshuhudia kuongezeka kwa kasi udhibiti wa Amerika kupitia sera zake za utandawazi, uingiliaji kati, biashara na ushuru wa mauzo ya nje na uwepo wa mchakato wa amani wa Palestina kila mahali. Kueneza demokrasia kupitia mtutu wa bunduki, huku haki za kujitawala zikizuia, kuyaparaganya zaidi mataifa ya Waislamu kupitia kura za turufu, vikundi vya siri vinavyotekeleza operesheni za kijeshi, vita vya wakala na kupitia kusaidia na kuanzisha wanamgambo ili kuziba njia za umoja wa Waislamu.

Katika miaka ya 1980, Biden aliunga mkono sheria za uhamiaji na akapigia kura kuunga mkono miswada mingi ya sheria yenye kuwapendelea wahamiaji, lakini baada ya katikati ya miaka ya 1990, alikuwa akiendeleza kusaidia kupitisha sheria zilizodhoofisha haki za wahamiaji, zilizonakiliwa rasmi na zisizonakiliwa, huku zikizipa mamlaka nguvu na rasilimali zaidi, kwa ajili ya kuwatafuta watu wasiosajiliwa na kuwafukuza. Akiwa makamu wa aliyekuwa raisi – Barack Obama kutoka 2008 hadi 2016, Biden alikuwa mtetezi wa sera zilizodhamini ulindaji kijeshi wa mpaka na ufukuzaji wa wakimbizi ili kukabiliana na mzozo unaoongezeka wa uhamiaji, na uliomruhusu Obama kujiingiza kwa nguvu katika vita vya utumiaji wa droni kote Mashariki ya Kati, yakiuwa raia wa kawaida na raia wa Amerika.    

Ni wazi kuwa licha ya sura, wana democrat na wana republican wana ajenda sawa za siasa za kijiografia, hivyo hatuwezi kudai kitoto kuwa kuna muovu nafuu kati ya waovu hawa wawili wa dhahiri.

Njia pekee ya kuvunja duara hili ni kwa kuleta mabadiliko ya maana ya kimfumo kitu ambacho kitaipatia dunia usalama na amani ya kweli, ambayo itadhibiti hisia zao na mahitaji yao ya kighariza katika namna ya sawa; mfumo ambao unaweza kukabiliana na mfumo wa sasa wa kirasilimali kwa kuleta nidhamu tofauti kabisa ya kisiasa na kiuchumi ambao unatoa usalama, amani na haki kwa raia wote. Kwa hivyo, Uislamu ndio mfumo pekee unaoweza kufanikisha hili. Ukomunisti umo ndani ya kaburi la sahau na ubepari ndio tumaini pekee la watu japokuwa ni tumaini linalofifia. Kutokana na kuwa watu wengi duniani wamekuwa wanataka mabadiliko ya kihakika, hawawezi kuukwepa mfumo huu, isipokuwa kitu kilicho bora zaidi kije kichukue nafasi yake. Zaidi ya hayo, Uislamu pia unakaidi fikra ya mantiki ya mizani ya kijeshi kutokana na nguvu ya mfumo huu, umelizifurusha tawala za Waroma na Waajemi japokuwa eneo la kijiografia la Madina halikuwa kwa manufaa yake. Ni hakika! Uislamu utarudi tena na kuukomboa ulimwengu kwa namna ilivyofanya kwa miaka 1400 na unasubiri kuandikwa kama dola kuu ijayo katika vitabu vya historia. Iko karibu mno.

    [هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndie aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [TMQ 9:33].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohammad Adel

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 19 Novemba 2020 22:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu