Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Muungano wa Kijeshi AFRICOM: Mabwana na Sio Marafiki

Katika mkutano wa karibuni baina ya Raisi Bukhari na Waziri wa Kigeni wa Amerika Anthony Blinken, ambapo Raisi alimtaka Waziri kuisaidia Nigeria na eneo la Afrika la kusini mwa Sahara kwa changamoto za kiusalama kwa kuiondoa AFRICOM kutoka Stuttgart, Ujerumani na kuiweka kwenye bara muwafaka. Katika uwezekano wote ni kwamba hiyo ni fikra mbaya Mheshimiwa Raisi, na hii ndio sababu. AFRICOM, ufupisho wa Africa Command, ni moja ya kombaini 6 za wapiganaji zilizounganishwa kijiografia zilizo chini ya mfumo wa komandi za Idara ya Ulinzi ya Amerika. Ni moja ya muundo wa komandi za karibuni zilizoundwa mwaka 2007 hadi mwaka uliopita 2020 Komandi ya Anga ilizinduliwa rasmi. Nyengine ni US Europe Command (EUCOM mwaka 1947) inayoshughulikia Ulaya na Urusi, US Pacific Command (PACOM mwaka 1947, ikaitwa baadaye INDOPACOM mwaka 2018), inayoshughulikia Eneo la Pasifiki, US Southern Command (SOUTHCOM mwaka 1963) kwa ajili ya Amerika Kusini, US Central Command (CENTCOM mwaka 1983) kwa ajili ya Mashariki ya Kati na Misri, US Northern Command (NORTHCOM mwaka 2002) baada ya mashambulizi ya Septemba 11.

Ukweli wa AFRICOM ‘kupambana na vitisho vinavyovuka mipaka na wenye madhara, kuimarisha vikosi vya usalama na kupambana na mizozo ili kuendeleza maslahi ya kitaifa ya Amerika na kueneza usalama wa kieneo, utulivu na ustawi’ kwa mujibu wa kauli ya dira yao kwenye africom.mil. Kilichomo kwa ufupi. Nini dhumuni halisi la AFRICOM? Baada ya Vita vya Pili vya Dunia, kuanguka kwa Uingereza kama taifa kuu iliruhusu Amerika kuibuka na kuchukuwa nafasi yake ya muenezaji mkuu wa mfumo wa Urasilimali wa kiulimwengu. Kisha baada ya kuanguka kwa Ukomunisti na Umoja wa Kisovieti mwaka 1989 sera ya kigeni ya Amerika ilibadilika kutoka mapambano ya kimfumo na mara moja kuwa ni ukoloni wa rasilimali za duniani kote. Ili kudumisha udhibiti huu wa kiulimwengu, Amerika imekuwa na zaidi ya kambi 800 za kijeshi zilizoenea kote duniani kuelekeza nguvu na kuhifadhi na kumiliki rasilimali za nishati. Kama CENTCOM ilivyotumika kuweka umiliki kwa vyanzo vya nishati ya Mashariki ya Kati kwa ajili ya Amerika kupitia Vita vya Ghuba, AFRICOM hivyo hivyo ililengwa kuhifadhi akiba ya nishati ya Afrika miongoni mwa malengo mengine. Taarifa nyingi mwanzoni mwa miaka ya 2000 zimeashiria umuhimu wa rasilimali za nishati ya Afrika. Kutoka kwenye Ripoti ya Sera ya Taifa ya Nishati iliyotolewa na Afisi ya aliyekuwa Makamu wa Raisi Richard Cheney mnamo 16 Mei 2001, hadi kwenye ripoti ya Jopo Kazi la Kituo cha Mafunzo ya Mikakati na Kimataifa ya 2005, juu ya Usalama wa Ghuba ya Guinea, Amerika imeshikilia msimamo endelevu wa sera yake ya Afrika – kulinda na kudhibiti rasilimali za nishati za Afrika.

Lengo ziada la AFRICOM ni kukabiliana na sera ya China kwa Afrika. AFRICOM imeibuka kama matokeo ya moja kwa moja ya kuongezeka kwa uwepo wa China katika bara hilo. Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulioandaliwa na China mnamo Oktoba 2006 umeamsha hatari kwa Washington wakati Raisi wa China wakati huo, Hu Jintao, alipokuwa mwenyeji wa mkutano wa Beijing uliowaleta takriban maraisi na mawaziri hamsini wa mataifa ya Afrika katika mji mkuu huo wa China. Tokea wakati huo China imekuwa ikifanya uingiliaji wa kisiasa na kiuchumi Afrika huku Amerika ikijaribu kukinzana nayo. Biashara baina ya Afrika na China imekuwa kwa zaidi ya mara tatu tokea 2006, ikipita US$200 bilioni mwaka 2011. Hivi sasa ikisimama kwenye $187 bilioni kwa 2020 (baada ya kufikia kiwango cha juu cha $200 bilioni katika 2019). Kama walivyokuwa watangulizi wake kabla yake – Hillary Clinton mwaka 2012 na Pompeo – Blinken aliwafunza Waafrika kuwa na hadhari na sera ya China kwa Afrika kwenye mkutano kupitia mtandao mnamo Jumanne tarehe 27 Aprili.

Bukhari atanabahi kuwa wengi ya Waafrika hawakupendelea juu ya fikra ya AFRICOM kuweka kambi kwenye bara hilo wakati Amerika ilipoanza kuhangaika huku na huko kwa ajili ya nchi itayokubali. Mnamo 2007 wakuu wa serikali wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), wanachama wake wakiwa ni Angola, Botswana, Msumbiji, Afrika Kusini, Tanzania, na Zimbabwe, waliijadili AFRICOM na kumalizia wazi wazi ‘kuwa ni bora kama Amerika ingejihusisha na Afrika ikiwa mbali kuliko kuwa ndani ya bara’. Jumuiya ya nchi ishirini na tano za Mataifa ya Sahara ya Sahel (Cen-Sad) imesisitiza kuwa ‘kukataa wazi wazi uwekaji wa komandi yoyote ya kijeshi au uwepo wa jeshi lolote la kigeni la nchi yoyote kwenye sehemu yoyote katika Afrika, kutokana na sababu yoyote na uhalali wowote’. Nigeria ilitupilia mbali na kukataa wazo hilo chini ya Yar’adua mwaka 2007 na kurudia Novemba 2009. Hata hivyo, uhasama mwingi zaidi unaoelekezwa kwa AFRICOM ni kutokana na ushawishi wa mabwana wa zamani wa mataifa haya kama Uingereza na Ufaransa, ambapo maslahi ya mabeberu yamekita mizizi. Ushawishi huu umedhihirika na kuelezewa wazi na waziri wa Uingereza kwa Afrika, James Duddridge akizungumza siku hiyo hiyo ya mkutano wa Blinken. Akizungumza na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria, Geoffrey Onyeama, mjini Abuja, alisema “Hali ni tete sana na hakuna ushirikiano unaoweza kutatua ongezeko kubwa la matatizo.” Aliongeza kuwa “Kwa upande wa Uingereza mna mshirika madhubuti katika upeo mpana wa mambo, hivyo sio tu katika ujasusi na usalama ulio mgumu na masuala ya kijeshi; ni kuhusiana na jamii, ni kuhusiana na msaada wa kibinaadamu, ni kuhusiana na elimu na ushirika wa maendeleo.” Kwa kuyatafsiri ni kuwa: hamutaki muungano wa kijeshi na Wamarekani!

Mwishowe ni kuwa kila nchi inasukumwa na maslahi yake binafsi. Madhali Amerika inahubiri usalama wa kieneo, utulivu na neema au Uingereza ikihubiri juu ya msaada wa kibinaadamu na maendeleo ya kijamii au kwamba China inatowa mikopo mikubwa yenye tahafifu, haitoficha ukweli kuwa Amerika itatumia tu nguvu za kijeshi itakapoona inafaa juu ya msukumo wake wa kikoloni, au kuwa Uingereza itatumia tu nguvu hafifu ya kidiplomasia katika kukabiliana na ushindani mkubwa wa Amerika au ukarimu wa China unaopelekea ukoloni mambo leo wa ‘diplomasia ya madeni’.

Kuingia kwenye miungano ya kijeshi na nchi kama Marekani ni kutabiri mwisho wenye madhara tu. Hawatokuwa kama ni washirika bali ni mabwana, wakiweka vifungu na masharti yasiyofaa. Amerika itaitumia AFRICOM kufikia maslahi yake kwa gharama kubwa upande wetu. Watatumia vikosi vyetu vya kijeshi, kwanza kwa jina la kupigana na ugaidi, kisha kuiwezesha Amerika kufikia eneo la kusini mwa sahara ya Afrika, kwenye maeneo ambayo kabla haikuweza kutanua ushawishi wake. Kuiweka Uturuki ndani ya NATO kuwa ni kinga ya eneo la kusini ya Ulaya dhidi ya kujipanua kwa Usovieti – na sasa Urusi – na kutumia nguvu kubwa za kijeshi za Pakistan kuiingiza Amerika ndani ya uvamizi wake Afghanistan na kutanua ufikaji wa Amerika ndani ya bara dogo la India ni mifano michache ya kile inachoweza kukitegemea kutokana na muungano huo. Miungano inatumiwa kuipa nguvu zaidi dola ilio na nguvu, kwa gharama ya dola dhaifu. Hivyo, ni kipi cha dola ilio na nguvu zaidi, kama katika hali hii ya muungano wa Amerika na Nigeria? Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amekataza miungano kama hii. Ahmad na An-Nisai amepokea kutoka kwa Anas (ra) amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «لَا تَسْتَضِيئُوا بِنَارِ الْمُشْرِكِينَ» “Msitake mwangaza kwa moto wa washirikina.” Yaani msiufanye moto wa washirikina ni mwangaza kwenu. Imekuja katika hadith ya Adh-Dhahak (ra),

أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ ﷺ خَرَجَ يَوْمَ أُحُدٍ، فَإِذَا كَتِيبَةٌ حَسْنَاءُ، أَوْ قَالَ: خَشْنَاءُ، فَقَالَ: «مَنْ هَؤُلَاءِ؟» قَالُوا: يَهُودُ كَذَا وَكَذَا، فَقَالَ: «لَا نَسْتَعِينُ بِالْكُفَّارِ»

“Kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitoka siku ya Uhud, ghafla akaona kikosi kizuri cha kijeshi au kikali, basi akasema: ‘Ni nani hawa?’ Wakasema: ‘Mayahudi wa kadha na kadha.’ Akasema: ‘Hatutaki msaada wa Makafiri.’”

Zaidi ya hayo, je, kwani Amerika sio tishio kubwa zaidi kwa Waislamu kila sehemu, wachochezi na wahalifu wa vita na kukosekana utulivu katika ulimwengu wa Kiislamu? Kutatua changamoto nyingi za usalama zinazoisumbua Nigeria, ni lazima iunde uoni unaokwenda mbali zaidi ya kutegemea mahusiano yasioaminika na maadui wa Uislamu na Ummah wa Kiislamu.

 [إِن يَنصُرْكُمُ اللّهُ فَلاَ غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللّهِ فَلْيَتَوَكِّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani basi baada yake yeye atayekunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.” [Surah Aali-Imran, 3:160]

Hakuna shaka kuwa njia ya kupata nguvu ni mradi wa Khilafah na sio miungano na maadui wa Uislamu na Waislamu. Muda umefika sasa tuwe mabwana sisi wenyewe. Ni muda wa Khilafah, na sio miungano.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Salihu Mahmud

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu