- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Saudi Arabia na Qatar – Sarakasi ya Kisiasa Katika Ghuba
Katika Mkutano wa 41 wa Wakuu wa nchi za Ghuba GCC, Saudi Arabia na Qatar zimerejesha mahusiano zikihitimisha “ugomvi” wa miaka mitatu baina ya nchi mbili hizi. Viongozi wa Ghuba wametia saini tamko katika mkutano uliofanyika Saudi Arabia masaa kadhaa baada ya Riyadh kutangaza kuwa imeondosha vikwazo vya angani, ardhini na baharini kwa Qatar. Qatar pia ilitengwa na Misri, Imarati na Bahrain zinazotegemewa kufuata mkondo wa Saudia mwaka huu kwa kurejesha mahusiano yao ya kisiasa.
Mshikamano wa Kidugu una matokeo magumu ya kisiasa
Sisi sio Ummah wa kusimamisha biashara, kufunga mipaka au kukata mahusiano baina ya nchi za Waislamu kwa ajili ya kiburi cha kisiasa. Sisi pia sio Ummah ambao ni tiifu kwa sera za kigeni za Amerika au wa kuambiwa lini tupigane vita au kuweka vikwazo dhidi ya Waislamu. Kwa hakika sisi ni Ummah ambao unamuabudu Muumba mmoja, matatizo yetu ni mamoja, Dini yetu ni moja, ardhi yetu ni moja na ujumbe wetu ni mmoja. Dini yetu inatuunganisha, na kutawala kwa Ukafiri na kuwa watiifu kwa mataifa ya Kimagharibi kunatugawa na kutusambaratisha.
[إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]
“Kwa hakika huu Ummah wenu ni Ummah mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [TMQ 21:92].
Badala ya kufanya na kuvunja mshikamano wa kisiasa na mikataba baina ya nchi za kitaifa zilizobuniwa kuugawa Ummah, Waislamu wanapaswa kuwa na lengo la kuungana juu ya msingi wa Uislamu. Mwenyezi Mungu (swt) anatutambulisha sisi kama Waislamu na hajatutambulisha kwa msingi wa mahala tulipozaliwa au rangi za ngozi zetu.
Uislamu umekuja kubadilisha mahusiano yaliotabiriwa juu ya fikra finyu ya utaifa na maslahi kwa fungamano la udugu miongoni mwa Waislamu. Fungamano la udugu katika Uislamu sio tu ni fungamano imara zaidi linaloweza kuuleta Ummah pamoja na kuunganisha lakini pia ni fungamano ambalo Uislamu unatuongoza kwalo kujengea mahusiano yetu. Fungamano hili lina matokeo mazito ya kisiasa, ukweli ambao watawala katika ulimwengu wa Kiislamu wanashindwa kufahamu.
Sarakasi ya kisiasa katika eneo la Ghuba imefichuwa vipaumbele vya watawala katika nchi hizo. Kuanzia kuwa wenyeji wa vituo vya kijeshi vya Amerika vinavyotumika kama ni sehemu za ugavi wa mahitaji dhidi ya Ummah katika kuongoza mipango inayopelekea kuwauwa Waislamu Yemen na Palestina. Yote haya yanafanyika kama ni matokeo ya fikra ya “kila nchi kivyake” ambayo inawagawa Waislamu na kuwaunganisha tu kwa msingi wa maslahi ya muda ya kisiasa kwa kipindi maalum.
Ni Khilafah pekee ndiyo itakayowaunganisha Waislamu, kuwahifadhi na kufanya kazi kwa ajili yake badala ya kuwagawa kwa kutumia mipaka, bendera na utambulisho wa kitaifa ambao huvunjika yanapopatikana maslahi ya muda. Khilafah itaiangalia mipaka iliopo baina ya nchi za Waislamu kama ni njia tu ya kuwagawa Waislamu na itatupilia mbali maoni yoyote kutoka nje ya kuiwekea kizuizi au kikwazo Nchi jirani ya Waislamu.
[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ]
“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu pamoja wala msifarikiane” [TMQ 3:103]
Utiifu wa Kisiasa
Kwa mshangao, tawala za sasa zinaruhusu kubadilika tu kwa uongozi nchini Amerika, kuanzisha au kumaliza miaka mitatu ya mtengano wa kisiasa baina ya Qatar na Saudi Arabia. Kwa kuzingatia kuwa Trump ndio anaondoka sasa, watawala watayawacha maamuzi ya kisiasa kufanywa na mabwana zao katika Magharibi na watakimbilia kujiweka katika kurasa nzuri za raisi mpya.
Na hivi sasa utawala mpya wa Amerika unajitayarisha kuingia Ikulu na Raisi Mteule Joe Biden ameweka wazi kuwa atachukua msimamo mkali zaidi ya mtangulizi wake katika baadhi ya misimamo ya Saudia.
Jengine la kushangaza kama hili, tumekuwa hatutarajia chochote hata kwa uchache kutoka tawala za kitumwa katika ulimwengu wa Kiislamu. Tawala ambazo zinatekeleza maagizo ya kisiasa na mikakati ilioundwa na Magharibi kudhoofisha Waislamu, tawala ambazo huwa na furaha kuvunja mahusiano na nchi jirani za Waislamu lakini ilhali zina mahusiano mazuri na umbile la Kizayuni.
Suala linaloleta mshangao zaidi ni kuwa watawala wa sasa katika ulimwengu wa Kiislamu sio tu ni watiifu kwa kisichokuwa Uislamu lakini ni watiifu hasa kwa mataifa ya Kimagharibi yanaotawala kwa fikra zilizoooza za kidemokrasia, usekula na Ubepari. Watawala katika nchi za Waislamu ni watumwa kwa ile ile Amerika ya waandamanaji waliovamia jengo la Serikali (Capitol), raisi ambaye amekataa kutoka na ameligawa vibaya taifa. Raisi mteule Joe Biden ameliita tukio la uvamizi la Jumatano la US Capitol “moja ya siku ngumu zaidi katika historia,”
Karata ya “Msimamo Mkali”
Licha ya watawala katika ulimwengu wa Kiislamu kujaribu kuhalalisha maamuzi yao ya kisiasa na utiifu wao kwa Wamagharibi kwa kueleza kuwa haya ni kwa kuboresha mahusiano ya kidiplomasia, hawaelekei kufahamu kuwa mataifa ya Magharibi kamwe hayawaangalii zaidi ya kuwa ni zana za kutekeleza mipango yao katika maeneo.
Karata ya “kugharamia, kuunga mkono au kusaidia msimamo mkali” mara nyingi hutumiwa na Amerika ima kwa kuzifuta baadhi ya nchi au kwa kuzitambulisha kwa kuzitoa kwenye orodha hiyo “ya nchi zenye msimamo mkali”. Qatar haina tofauti na Sudan, wakati mwengine, karata hiyo hiyo ilitumiwa kuiagiza Saudia na nchi nyengine kuiondoa Qatar.
Kuwa mbele katika kutandaza sera za kigeni za Amerika kama “kupambana na msimamo mkali” ni kama kucheza na moto. Utaishia kujidhuru mwenyewe kutokana na ujinga kwani sera hiyo hiyo itatumiwa dhidi yako katika kipindi muwafaka kwa Amerika.
Jinamizi la mataifa ya Magharibi ni kuibuka kwa Uislamu. Kuibuka kwa dola itakayounganisha Ummah, kuunganisha rasilimali zake na ardhi, ikiongozwa kwa Quran na Sunnah na kuueneza Uislamu kwa Da’wah na Jihad. Kwa hivyo wao hufanya kazi mchana na usiku, kupanga, kutumia muda na fedha, kuzipindisha siasa zao na kutumia vibaraka katika ulimwengu wa Kiislamu muda wote kusimamisha kuibuka huku kusitokee. Hata hivyo, fedha hizo zote, muda huo, na mipango hiyo punde itaisha na Khilafah kwa njia ya Utume itasimamishwa tena hata kama Washirikina watachukia. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:
[وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللّهُ وَاللّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ]
“Wakapanga mipango yao na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.” [TMQ 8:30].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ghassan Ibn Kamal