Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuiweka Wazi Hali ya Palestina

(Imetafsiriwa)

Tokea siku za mwisho za Ramadhan wakati watu wengi kote duniani wakitazama picha za kuogofya huku vikosi vya Kizayuni vikivamia eneo la al-Aqsa na walowezi wa Kizayuni wakijaribu kuwafurusha wakaazi katika Sheikh Jarrah, mambo sasa yamepamba moto na kuwa mzozo kamili wakati umbile la Kiyahudi sasa likiivamia Gaza. Wakati Mazayuni wakitekeleza uhalifu wao, vyombo vingi vya habari vilitilia umuhimu mchache na vilianza kuripoti matukio baada tu ya makombora yalipoanza kurushwa. Waungaji mkono wa Wazayuni wa Magharibi na waungaji mkono wao katika vyombo vya habari walianzisha taarifa zao za vita kugeuza mazingatio ya watu dhidi ya maovu yao halisi. Kiini cha mgogoro wa sasa kikiwa ni juu ya maeneo ya Shaikh Jarrah katika Mashariki ya Jerusalem. 

Tokea mwaka 2009, vyama vya walowezi wa Kizayuni vimekuwa vikifanyia kazi lengo lao wanalolieleza la kuwafukuza na kuwatimua Wapalestina wote kutoka Sheikh Jarrah. Eneo hilo limeshuhudia walowezi wakivamia majumba na kuwafukuza wakaazi na kujimilikisha mali. Hii imekuwa ni sera thabiti ya utawala huu wa Wazayuni katika eneo lote la Palestina wanalolishikilia kwa kuyasaidia makundi ya walowezi katika kuiba ardhi kutoka kwa Wapalestina wanaoishi katika maeneo kama Sheikh Jarrah kwa miongo mingi. Wapalestina hawana haki kwa mujibu wa mfumo wa kisheria wa ‘Israeli’. Chini ya sheria za Kimataifa, Sheikh Jarrah na Jerusalem ya Mashariki iko katika maeneo ya Wapalestina. Lakini Wazayuni wanaendelea kuikalia kimabavu tokea Vita vya 1967.

Kama walivyo wakaazi wengi wa Palestina iliokaliwa kimabavu, wakaazi wa Sheikh Jarrah wamejielekeza kutegemea mfumo wa kisheria kwa ulinzi lakini mahakama za ‘Israeli’ zimeendelea kushikilia msimamo wa ubwana wa Wazayuni. Mahakama kuu ina historia ya kuwaunga mkono walowezi wa Kizayuni. Walowezi wa Kizayuni wamekwisha pora majumba katika Sheikh Jarrah miongoni mwa maeneo mengine kupitia ufanikishaji wa mfumo wa kibaguzi. Wakaazi wa Sheikh Jarrah wamejielekeza kwenye maandamano ya amani huku watu wengi wakiungana nao wakisaidia familia zilizopangwa kufukuzwa. Haya hayakuwa maandamano ya vurugu ambayo yakihusisha nyimbo na kwamba ilikuwa ni mwezi wa Ramadhan, waandamanaji wakila futari kwa pamoja na kuswali pamoja. Walowezi wa Kiyahudi, huku wakiona mamia ya waandamanaji nje ya majumba yao waliyopora karibuni, waliwaelekea polisi wa ‘Israeli’ ili kulindwa. Polisi wakaanza kurusha maji ya kunuka kwa waandamanaji, ambayo ni maji machafu yalioongezwa kemikali. Video zilirushwa katika mitandao ya kijamii zikionyesha polisi wakitumia nguvu kwa raia walioenea na kuvunja majumba katika Sheikh Jarrah na kuwakamata watu.

Kisha, katika siku 10 za mwishoni mwa Ramadhan, vikosi vya Wazayuni vikiwa na zana nzito viliingia kwa vishindo ndani ya Al-Aqsa wakati waumini wakiabudu. Wakaendelea katika kutumia maguruneti ya kushtua na kuanza kufyatua risasi za vyuma zilizotiwa mipira. Wakalazimisha kufungwa milango ili watu wasiweze kutoka. Hali hii ilisababisha majeruhi wasio na hesabu hasa katika maeneo ya macho na vichwa vyao.

Utawala wa Kizayuni kwa muda mrefu umeitumia al-Aqsa kuwadhibiti Wapalestina. Kuna historia ndefu ya maandamano na uasi katika maeneo yote ya kihistoria ya Palestina na utawala wa Wazayuni hujibu kwa kuishambulia al-Aqsa. Mkakati ukiwa kwamba kwa kuwa Jerusalem iko chini ya udhibiti wa Wazayuni, itachukuliwa kutoka kwenu pindi mkipinga au kuasi. Ujumbe kwa watu ni kuwa utawala wa Wazayuni unawaruhusu nyinyi kuswali kwenye eneo lenu takatifu. Huu umekuwa ni mkakati tokea 1967 – chombo cha kuwadhibiti watu katika eneo hilo.

Sheikh Jarrah, kama yalivyo maeneo mengi ya kihistoria ya Palestina, ni eneo lililokaliwa kimabavu na umbile la Kiyahudi linawalazimisha Wapalestina kuliwacha ili walowezi wa Kizayuni waweze kuingia. Hii ilikuwa ni sababu kwa nini malalamiko yaliongezeka ya kuihami Sheikh Jarrah na kuwalinda watu wanaotakiwa kufurushwa kutoka majumba yao. Utawala wa Wazayuni ulijibu kwa namna ile wanayofanya kikawaida kwa kuishambulia al-Aqsa. Al-Aqsa ilivamiwa na polisi wa Kizayuni kutokana na malalamiko yaliyotokea katika Sheikh Jarrah.

Vyombo vya habari vingi vilianza kuzungumzia habari hii wakati umbile la Kiyahudi liliposhambuliwa. Huu haukuwa ni mvutano au mapambano baina ya nguvu mbili zinazolingana. Silaha zao Wapalestina dhidi ya vikosi vya polisi vilivyojizatiti ni mawe na changarawe. Lakini picha hizi zimeleta ukuaji wa rai jumla dhidi ya watawala wa Waislamu na majeshi waliowazunguka kuingilia kati kwa niaba ya Waislamu. Watawala hawa wamekwama baina ya kuwaridhisha Wamagharibi na udumishaji usawazishaji wa mahusiano na umbile la Kiyahudi. Baada ya miongo mingi ya kutoa wito kwa ajili ya maazimio ya Umoja wa Mataifa na msaada wa kimataifa, sasa ummah unataka majeshi ya Waislamu kuikomboa Palestina.

       #الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#Aqsa_calls_armies

#OrdularAksaya

#AqsaCallsArmies

#AqsaYawaitaMajeshi

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na
Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu