- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mfumo Huu Hautowalinda Waislamu wa Palestina
(Imetafsiriwa)
Mnamo Alkhamisi, ‘Israel’ na Palestina zilihakikisha kuwa zimekubaliana kwa kauli moja juu ya usitishaji wa mapigano, ambapo Raisi wa Amerika Joe Biden aliukaribisha kwa kuwa ni “fursa ya kweli ya kupiga hatua” kuelekea amani ya kudumu katika Mashariki ya Kati. (Chanzo) Siku iliyofuata, ‘Israel’ iliwashambulia Waislamu wa Palestina katika Al-Aqsa.
Msururu wa matukio yasitushangaze. Usitishaji wa mapigano hautosimamisha ukandamizaji unaowakumba Wapalestina - haukuwahi kabla, wala hautoweza sasa au siku za mbeleni. Mwaka 2014, makubaliano 9 ya kusimamisha vita yalikuja na kuondoka kabla mzozo kumalizika. (Chanzo) na msururu wa mashambulizi ya karibuni yanaonyesha kuwa makubaliano hayo yalikuwa ni masitisho ya muda tu.
Msighilibiwe na miito kwa ajili ya usimamishaji - watawala wa sasa hutegemea rai jumla iwe upande wao.
Watawala katika mfumo wa sasa hutegemea rai jumla iwe upande wao. Na shutuma kali za hivi karibuni dhidi ya ‘Israel’ zimekuwa sio za kawaida – kumekuwa na miito duniani kote, huku mitandao ya kijamii ikihanikiza taarifa zenye kueneza uelewa kuhusu hali katika Palestina. Pia wakivitaka vyombo vya habari vya kawaida kujitokeza kwa kuionyesha taswira potofu ya hali ilivyo au kwa vichwa vya habari ambavyo kwa makusudi vinatuondosha kutoka kiini cha tatizo – watu wa Palestina wanataabika, na ‘Israel’ inalindwa na mataifa duniani kote.
Kila siku zikipita, na dola kuanza kutoa matangazo ya kusitisha vita na kile kinachoitwa masuluhisho ya tatizo, ni muhimu kuwa tusiruhusu mazingatio yetu kufifia - usitishaji vita, hata ukiendelea kwa muda kiasi gani, hautobadilisha hali. Hautotatua tatizo, hautozuia Wapalestina kukandamizwa. Mabomu yanaweza kusita, lakini kuamiliwa kwao kuwa ni raia wa daraja la pili - na la tatu katika ardhi ambayo Mazayuni wanaikalia hakutobadilika.
‘Israel’ inaikalia ardhi ya Palestina- na wanawachukia watu wake
‘Israel’ imepewa ardhi ya Palestina mwaka 1948, kilele cha ahadi zilizotolewa na Uingereza (Pamoja na msaada wa dola nyengine) kwa Mazayuni katika Azimio la Balfour. Kwa kipindi kirefu, ‘Israel’ imekuwa ikitumia jeshi kueneza udhibiti wao, kukalia ardhi ya Palestina na kuwafanyia uadui mkubwa watu wa Palestina.
Viongozi wa ‘Israel’ hata hawalifichi hili.
Wapalestina ni kama Wanyama, sio binaadamu (MK Ben Dahan, Naibu Waziri wa Zamani wa Ulinzi)
“Wapigeni, sio mara moja, bali mara nyingi, wapigeni ili wapate maumivu sana, hadi isiweze kuvumilika” Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
Uongozi unazidi kusisitiza kuwa ‘Israel’ ni dola ya Kiyahudi, na makaazi ya Mayahudi kwenye ardhi ya Palestina ni “thamani kuu ya dola hiyo”. Na uzoefu wa Wapalestina (katika) “uhamishwaji kwa nguvu, upokonywaji wa ardhi, hadhi duni kisheria na vifungo ni hali halisi inayowakumba Wapalestina wote, ima wa ‘ndani’ ya ‘Israel’ au katika maeneo yaliyokaliwa kimabavu.” (Chanzo) Walowezi wa ‘Israel’ katika Ukingo wa Magharibi uliokaliwa wanaruhusiwa kubeba silaha, na mara nyingi wanawashambulia Wapalestina pamoja na majumba yao na mashamba. (Chanzo)
Upigaji mabomu unaweza kusita lakini hali ya maisha ya Wapalestina ni ya kuogofya
Mnamo 2012, Umoja wa Mataifa ulieleza kuwa Gaza inaweza isikalike, isipokuwa hali itengemae. Tokea muda huo, hali imekuwa mbaya- na sio nzuri. (Chanzo) Ukingo wa Gaza “umegeuzwa kuwa ni suala la ufadhili kwa maafa makubwa na utegemeaji misaada na uwezo wa uzalishaji wa Gaza umevurugwa na operesheni kubwa tatu na kudhoofishwa angani, baharini na kizuizi cha ardhini.” (Chanzo)
Ripoti ya 2018 imesema kuwa kuna “rasilimali chache kwa maendeleo na uchocheaji wa uchumi wa uzalishaji.” Mapato halisi ya sasa katika Gaza ni asilimia 30 chini zaidi ya ilivyokuwa mwanzoni mwa karne hii. Kwa wastani, familia zinapata masaa 2 tu ya umeme kwa siku. (Chanzo)
Ripoti ya karibuni ya BBC imefichua kuwa ufungaji wa ‘Israel’ umeathiri “nyendo za kuingia na kutoka kwenye Ukingo na uwezo wa kufanya biashara.” Watu wengi katika Gaza wanasumbuliwa na uhaba wa maji na zaidi ya watu milioni moja katika Gaza wanawekwa kuwa ni “waathirika wa wastani wasio na uhakika wa chakula” licha ya kuwa wengi hupokea aina fulani ya msaada wa chakula.
‘Israel’ inazuia upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo na uvuvi, ambapo hupunguza kiasi cha chakula ambacho watu wa Gaza huweza kuzalisha wenyewe. Hawaruhusiwi hata kulima katika “eneo la amani lililotangazwa na Israel”. ‘Israeli’ pia imeweka ukomo katika uvuvi, inayoathiri fursa za chakula na ajira ndani ya Gaza. Hata hivyo, mnamo wiki chache zilizopita, ‘Israel’ ilizuia uvuaji wa Samaki kutoka Ukingo wa Gaza moja kwa moja.
Huduma za afya ziliharibiwa au kuvurugwa, kutokana na mashambulizi ya ‘Israel’ ndani ya miaka kadhaa. Ndani ya Gaza, kwa upande mwengine ni “gereza huru la anga”, pindi wagonjwa wakihitaji matibabu katika Ukanda wa Magharibi au hospitali za Jerusalem ya Mashariki lazima kwanza watake maombi yanayohakikiwa na Mamlaka ya Palestina na kisha yapate ruhusa ya serikali ya ‘Israel’ – katika mwaka 2019, kiwango cha maombi ya wagonjwa waliotaka kuondoka Ukanda wa Gaza yaliokubaliwa yalikuwa ni 65% (Chanzo)
Hatuwezi kusahau shida zao- wala tusiruhusu nafsi zetu kuchanganyikiwa
Waislamu wa Palestina wanahangaika, wamekuwa katika mihangaiko kwa miongo kadhaa na wataendelea kuhangaika hadi hali itatuliwe.
Lakini vipi tunaweza kuuamini mfumo ambao umezalisha tatizo, kuleta suluhisho. Uwepo wa Israel ni kwa sababu Mfumo wa Kirasilimali wa Kiliberali umewapa ardhi, umewahalalishia mamlaka yao juu yake na kwa majivuno unailinda kutokana na kila aina ya matokeo halisi.
Dola ndani ya mfumo huu zitaendelea kufanya hivyo, hata kama ‘zitalaani’ namna wanavyo watendea watu wa Palestina wanaume, wanawake na watoto.
Na vipi tunaweza kutarajia tahafifu yoyote?
Wakati mfumo unawashajiisha watawala 'kusawazisha' mahusiano na ‘Israel’ hadi kufikia watawala hawa wanaoitwa wa Waislamu kuweka maslahi ya kibiashara na kisiasa mbele ya maisha ya wanaume, wanawake na watoto?
Wakati mfumo ukiruhusu kwa dhihaka orodha ndefu ya ukatili- nje na ndani ya Palestina? Orodha ya ukatili ambayo haipo tu katika historia bali inahisiwa na Waislamu duniani kote hivi leo, na katika dakika hii.
Kama tupo makini kuhusiana na kuwasaidia ndugu zetu wa kike na wa kiume na kutimiza Faradhi ya kuzihifadhi ardhi za Waislamu na damu zao, tunahitajia kubadilisha mfumo. Kwa sababu ni kwa kuisimamisha tena dola ya Khilafah pekee ndipo Waislamu wa Palestina watakuwa na hifadhi na haki wanayostahili kuipata.
«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ فَإِنْ أَمَرَ بِتَقْوَى اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ وَعَدَلَ كَانَ لَهُ بِذَلِكَ أَجْرٌ وَإِنْ يَأْمُرْ بِغَيْرِهِ كَانَ عَلَيْهِ مِنْهُ»
“Hakika Imamu ni ngao, hupiganwa nyuma yake na hujikinga kwake, basi akiamrisha kwa taqwa ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na akafanya uadilifu atakuwa na ujira kwa hilo na kama ataamrisha kwa chengine kisicho hicho atakuwa dhidi yake.” (Muslim)
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#Aqsa_calls_armies #AqsaCallsArmies
#OrdularAksaya
#AqsaYawaitaMajeshi
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir