Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urongo wa Mrongo

(Imetafsiriwa)

Katika makala yaliyochapishwa mnamo Julai 5, Amerika ilitangaza kwamba imeondoka Kambi ya Anga ya Bagram. Tovuti ya Al Jazeera iliripoti [1] kwamba, "Amerika iliondoka Uwanja wa Ndege wa Bagram wa Afghanistan baada ya karibu miaka 20 kwa kuzima umeme na kuponyoka usiku bila ya kumjulisha kamanda mpya wa Kiafghan wa kambi hiyo, ambaye aligundua kuondoka kwa Wamarekani zaidi ya masaa mawili baada ya wao kuondoka, maafisa wa jeshi la Afghanistan walisema."

Vikosi vya Amerika viliondoka Uwanja wa Ndege wa Bagram bila hata kuwaarifu wenzao wa Jeshi la Kitaifa la Afghanistan. Kwa hivyo jeshi la Amerika lilikuwa limenyenyekezwa, kwa kuondoka katikati ya usiku kama wezi, wakihofia shambulizi kutoka kwa Taliban. Kuondoka kwa vikosi vya Amerika ni ushindi mkubwa kwa Mujahidina wenye ikhlasi wa vikosi vya Taliban, kwani Mwenyezi Mungu (swt) amewapa ushindi wale waliopigana kwa dhati katika njia yake.

Tofauti iko wazi kwa wote kuona. Ni watawala wa Pakistan ndio waliowanyima majeshi ya Pakistan heshima ya ushindi huu, licha ya silaha zao za atomiki, JF-17 Thunderbird zao, F-16 block 52 zao, mizinga yao ya Khalid na nyenginezo, Wah Military Complex, SAAB AWACS, ndege za P5-Orion, nyambizi za nyuklia na nyenginezo. Katika siku ya kutisha wakati Jenerali Musharraf alipochagua kuwa upande wa kafiri Amerika, alifunga milango ya ushindi kwa Jeshi la Pakistan. Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) aliwapa ushindi wale waliokuwa na Iman, waliokuwa kwenye uwanja wa vita na kutumia kila walikuwa nacho kutimiza hukmu ya Jihad. Kwa wanachama wenye ikhlasi wa vikosi vya jeshi la Pakistan, ikiwa watafanya uchunguzi wa kina wa nafsi, wa kwa nini Mwenyezi Mungu (swt) hakuwapa ushindi, majibu yako wazi. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ أُولَٰئِكَ كَتَبَ فِي قُلُوبِهِمُ الْإِيمَانَ وَأَيَّدَهُم بِرُوحٍ مِّنْهُ وَيُدْخِلُهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ أُولَٰئِكَ حِزْبُ اللَّهِ أَلَا إِنَّ حِزْبَ اللَّهِ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Huwakuti watu wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho kuwa wanawapenda wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hata wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. Hao ameandika katika nyoyo zao Imani, na amewapa nguvu kwa Roho itokayo kwake. Na atawaingiza katika Mabustani yapitayo mito kati yake. Humo watakaa daima. Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na wao wawe radhi naye. Hao ndio Hizbullahi, Kundi la Mwenyezi Mungu. Hakika Kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufanikiwa.” [Surah al-Mujaadilah 58:22].

Kwa hivyo madai kwamba Pakistan ilikuwa na mkono katika ushindi wa Taliban yanapingana hayana ukweli wowote kulingana na ushahidi huu. Hatupati ushahidi wowote wa kiwahyi wa kucheza kwao mchezo huo maradufu, kama wanavyodai walifanya hivyo, ingawa ni wazi kuwa walikuwa wakiunga mkono upande wa Amerika kikamilifu kwa juhudi zake zote. Hatupati ushahidi wowote wa kiwahyi unaowaruhusu Waislamu kuisaidia Amerika kwa njia usambazaji, ili Amerika iweze kushiriki katika vita vya kijeshi na mujahideen. Mwenyezi Mungu (swt) kinaganaga anasawazisha imani na kutofanya urafiki na wale wanaompinga Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake. Kwa hivyo, ima uongozi wa jeshi la Pakistan hauichukulii Amerika kama wale "wanaompinga Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw)" au wanafikiria kuwa wanaweza kukiuka aya hiyo, kuwasaidia makufiri dhidi ya Waislamu na kisha bado kunadai ushindi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Kwa kuzingatia huu unaoitwa ustadi wa kisiasa wa uongozi wa Pakistan katika kucheza mchezo maradufu, wacha tuchunguze kanuni hiyo hiyo ya mchezo maradufu kwenye mpaka wao na India. Mnamo 5 Agosti 2019, Uhindi ilibatilisha kifungu 370 ili kuikalia Kashmir kikamilifu. Hatuoni uongozi wa Pakistan ukicheza mchezo maradufu hapo, au hata kudai kuwa ilikuwa ikifanya hivyo. Hatuoni ungaji mkono wa makundi ya Kashmiri kwa uasi wa kisilaha dhidi ya wanajeshi wa India. Badala yake tunaona usaliti mkubwa, mkubwa zaidi kwa mtazamo wa ukweli kwamba uongozi wa Pakistan uliunga mkono upinzani wa kisilaha hapo zamani. Kwa kweli, India sio nguvu ya kijeshi ikilinganishwa na ligi ya Amerika, kwa hivyo itakuwa rahisi kuwapigisha magoti Wahindi. Kinyume chake, tunaona tu msaada kwa uvamizi wa India kwa kuwazuia Waislamu kuvuka mpaka wa udhibiti. Fauka ya hayo, kujitolea kuwasaidia Wahindi ilikuwa kiasi kwamba uongozi wa Pakistan uliweka uthabiti katika Laini ya Udhibiti wakati wa mzozo wa India na China. Kama ilivyoripotiwa [2], India iliweza kuhamisha wanajeshi kutoka kwa mzozo wa Kashmir kwenda mpaka wa China, ikionyesha imani yao kwamba Pakistan haitaongeza taharuki mpakani. Kwa hivyo mtu anaweza kuona kwamba madai ya mchezo maradufu hayakufanywa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika Quran:

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ وَالَّذِينَ أَشْرَكُوا وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ قَالُوا إِنَّا نَصَارَى ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ]

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi.” [Surah al-Maidah 5:82].

Ayah hiyo inawasifia Washirikina kama wale wenye uadui mkubwa dhidi yetu, lakini tunaona kwamba uongozi wa Pakistan haujajaribu hata kuanzisha mchezo maradufu. Badala yake Jenerali Bajwa aliwasihi Washirikina "wasahau yaliyopita" na wasonge mbele na ujumuishaji wa kikanda. Hivyo kwa mara nyengine tena, uongozi wa Pakistan haumchukulii Modi na BJP kama Washirikina, au wanapingana na aya ya Quran.

Mtu anashangaa ni vipi uongozi wa Pakistan unaweza kuzungumza kwa ujasiri juu ya kutowapa Wahindi nafasi nchni Afghanistan, wakati wamewapa Wahindi uhuru kamili huko Kashmir na kwengineko. Hata madai ya kutowapa Wahindi nafasi nchini Afghanistan ni uwongo. Si mwengine ila Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Waziri Mkuu wa Pakistan, Moeed Yusuf ambaye katika mahojiano aliwatuhumu Wahindi kwa kufadhili mashambulizi ya kigaidi nchini Pakistan, haswa mauaji ya Shule ya Umma ya Jeshi. Ikiwa uongozi wa Pakistan hauwezi hata kuzuia afisi za ubalozi wa India nchini Afghanistan kuanzisha mashambulizi kama hayo ya kinyama, basi ni kwa mantiki gani wanaweza hata kudai kwamba wamewazuia Wahindi kufanya operesheni nchini Afghanistan? Ripoti za habari [3] zilionyesha picha za pesa nyingi za Pakistan zilizopatikana ndani ya afisi za ubalozi wa India. Kwa hivyo, kabla ya mapinduzi ya Taliban, Wahindi walikuwa wakifanya kazi bila kujali sheria. Hakika ni kwa kuibuka kwa Taliban ndiko kuliko kuwa muhimu katika kuondoka kwa Wahindi kutoka Afghanistan.

Unafiki wa uongozi wa Pakistan kwa kudai kuwa na mkono au kuwa muhimu katika kufanikiwa kwa Taliban uko wazi. Mwenyezi Mungu (swt) kamwe hatawapa ushindi wale wanaowaunga mkono makafiri dhidi ya Waislamu. Na Waislamu wote wanajua hili. Uongozi wa Pakistan umesujudia tu shinikizo la Amerika, kama vile mtumwa fanyavyo kwa bwana wake. Amerika ilihitaji uongozi wa Pakistan kuishinikiza Taliban katika makubaliano. Amerika ilihitaji uongozi wa Pakistani kuunga mkono ubatilishaji wa India wa kifungu cha 370, ambapo Pakistan ilifanya kimyakimya kwa kutowasha taharuki na kuvidhibiti vikosi vyake.

Ni unafiki ndani ya akili na nyoyo za uongozi wa Pakistan ambao umewataka watoe simulizi kama hizo za kupotosha. Uongozi wa Pakistan unajaribu kujitenga na usaliti ulio wazi walioufanya wakati walipokuwa waliposhirikiana mfululizo na Amerika, wakiwa kama mawakala wa Amerika dhidi ya Taliban, wakitia kila aina ya shinikizo kwa wana mazungumzo wa Taliban.

Leo tuko pale tulipokuwa miaka ishirini isiyo ya kawaida iliyopita, kabla tu ya matukio ya 9/11, lakini kukiwa na tofauti. Taliban wamekuwa washindi dhidi ya Amerika, wakisisitiza juu ya matakwa yao ya kuondoka kwa wanajeshi wote wa Amerika, na uongozi wa Pakistan umefanikiwa kuonyesha sura yake halisi ya unafiki. Hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) itapita, Khilafah kwa Njia ya Utume itasimamishwa kwa Idhini yake, licha ya juhudi za makafiri na watawala wasaliti. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [TMQ Surah at-Tawbah 9:32].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Khalid Salahudin – Wilayah Pakistan

[1] https://www.aljazeera.com/news/2021/7/5/us-left-bagram-airfield-without-notice-afghan-officials-say

[2] https://www.aa.com.tr/en/asia-pacific/sizable-indian-soldiers-move-to-china-border-analyst/2102077

[3] https://tribune.com.pk/story/2310913/huge-stacks-of-pakistani-currency-recovered-in-afghanistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu