Jumapili, 02 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mapigano kati ya Dola ya Pakistan na Serikali ya Afghanistan, na Dola ya Pakistan na TTP

(Imetafsiriwa)

Watawala wa Pakistan wanatafuta makini ya kimataifa juu ya tishio la wanamgambo katika maeneo ya mpakani kwa matumaini ya kubadilisha makini kama hiyo kuwa kodi za kisiasa za kijiografia. Hii ni sababu mojawapo inayowafanya waangazie tishio la wanamgambo katika maeneo ya mpakani.

Utekelezaji mkali wa sheria mpakani wa mamlaka za Pakistan ni chanzo cha mvutano kati ya Pakistan na Taliban ya Afghanistan. Mamlaka za Pakistan zinaogopa kufungua mipaka na Afghanistan kwani hii itasababisha muunganisho wa kimaumbile wa uchumi wa nchi zote mbili na uwezo wa uzalishaji wa Pakistan utalazimika kuhudumia soko la Pakistan na Afghanistan (jambo ambalo kwa kweli ni faida kwa sekta za ndani). Ulanguzi wa dolari, mbolea, ngano, nk hadi Afghanistan ni jambo lenye kutia wasiwasi kwa watawala watepetevu wa Pakistan. Mamlaka za Pakistan pia zinahofia harakati za wanamgambo kutoka Afghanistan hadi Pakistan na uingizaji misimamo mikali kwa Madrasa za Pakistan kupitia mwingiliano wao na makada wa Taliban wa Afghanistan. Kwa Taliban wa Afghanistan uhusiano na Pakistan na uchumi wake ni njia ya uhai kwa uchumi wao na hivyo wana nia ya kufungua mpaka. Mpaka pia ni suala nyeti sana kwa makabila ya Pashtun ambayo kamwe hayakuukubali, wakiuona kama unaogawanya makabila na watu hao hao katika nchi mbili tofauti.

Kuna mapigano kati ya wanamgambo katika maeneo ya mpaka wa Pakistan na Dola ya Pakistan kwa usaidizi wa kimya kimya lakini sio wa kiuchangamfu kutoka kwa Taliban ya Afghanistan. Makabila ya mipakani kamwe hayajawahi kukubali kupenya kwa kina kwa miundo ya serikali katika maeneo yao na kuona miundo kama hii kama ukiukaji wa uhuru na kujitawala kwao. Ndio maana wanaona kuunganishwa kwa eneo la FATA na KPK kama shambulizi la serikali ya Pakistan juu ya uhuru wao wa kujitawala na wametaka kubatilishwa kwa muunganisho huu. Hii na kukinaika kwao kimfumo kwa uharamu wa dola ya Pakistan kama dola ya kisekula kibaraka kwa Amerika imesababisha wao kubeba silaha dhidi ya dola ya Pakistan.

Taliban wa Afghanistan hawaungi mkono kikamilifu Tehrik-e Taliban Pakistan (TTP) lakini wanakataa kulenga kambi zao nchini Afghanistan. Taliban wa Afghanistan hawako tayari kufanya msako wa kambi za TTP zilizo upande wao kwa sababu:

a- Kwa mtazamo wao endapo Pakistan na Amerika hazingefaulu katika kuangamiza wanamgambo katika maeneo ya mpakani, Taliban wa Afghanistan hawatafanikiwa katika juhudi kama hiyo pia.

b- Taliban wa Afghanistan hawana uwezo wa kuendesha operesheni kubwa kama hizi dhidi ya wanamgambo katika maeneo ya mpaka.

c- Taliban wa Afghanistan watahujumu uhalali wao wa Jihad ikiwa watachukua hatua dhidi ya Wanajihadi wenzao. Wanahofia kupoteza uhalali ndani ya kada zao ikiwa watapambana dhidi ya kambi za TTP nchini Afghanistan.

d- Serikali ya Afghanistan chini ya Taliban yenyewe imekumbwa na wimbi la mashambulizi ya mara kwa mara yanayodaiwa na Dola ya Kiislamu huko Khorasan. Wanahofia kwamba operesheni zozote dhidi ya TTP huenda zikawashajiisha wanachama wa TTP kujiunga na Dola ya Kiislamu katika safu za Khorasan au wanaweza kutumia silaha zao dhidi ya serikali ya Kabul wao wenyewe. Ikiwa halitashughulikiwa kwa busara, tishio la wanamgambo huko Mashariki mwa Afghanistan, kwa mtazamo wao, linaweza kubadilika na kuwa dhidi ya Taliban ya Afghanistan.

e- Kundi la Taliban la Afghanistan linataka kulainisha mpaka kati ya Pakistan na Afghanistan. Tishio la TTP katika maeneo ya mpaka na operesheni za kijeshi za Jeshi la Pakistan dhidi ya TTP litafanya lengo lao la kuufanya Mstatari wa Durand kuwa mpaka laini kuwa gumu zaidi. Hii ndiyo sababu wanataka kusaidia Pakistan kutatua tishio la TTP bila gharama kubwa kwao wenyewe. Wanaona njia bora zaidi ya kufanya hivi kupitia kuwezesha mazungumzo kati za mamlaka ya Pakistan na TTP, ambayo walijaribu kufanya udalali lakini hayakuleta matokeo maana.

Kundi la Taliban la Afghanistan wanaliona tishio la TTP kwenye eneo la mpaka wa Pakistan kama njia ya kurudisha nyuma ushawishi wa Pakistan ndani ya Afghanistan. Na huenda wakaliona hili kama ushawishi dhidi ya dola ya Pakistan. Hata hivyo sera kama hiyo haiungwi mkono kikamilifu na TTP badala yake, kama ilivyotajwa hapo juu, huu ni usaidizi wa kimya kimya kupitia kujaribu kusaidia kuwezesha mazungumzo kati ya TTP na dola ya Pakistan.

Mashambulizi ya wanamgambo kutoka kwa TTP katika dola ya Pakistan yanaakisi mapambano yao ya kiwango cha chini ili kuhifadhi uhuru wa maamuzi wa makabila ya mpakani na kufikia aina fulani ya suluhu na mamlaka za Pakistan ambapo wanaweza kutengeneza uhuru na kujitawala kwa eneo la FATA. Jeshi la Pakistan hata hivyo haliko tayari kutoa nafasi hiyo kwa wanamgambo katika maeneo ya mpakani wakihofia uhusiano wa Jihad ambao unaopanuka kutoka Wana hadi Kabul. Jeshi la Pakistan linawataka Taliban wa Afghanistan kuweka shinikizo kwa TTP na halitaki kufanya operesheni kubwa dhidi ya wanamgambo katika maeneo ya mpakani kwani operesheni hizo zitajumuisha gharama kubwa za kiuchumi na kijeshi. Pia wanahofia madhara ya kiuchumi ya oparesheni hizo za kijeshi katika suala la kutishia uwekezaji wa kigeni kutoka Pakistan. Utawala wa Pakistan kupitia matamshi ya umma unataka kuwashinikiza Taliban wa Afghanistan na kutafuta msaada wao katika kukabiliana na TTP.

Amerika inaliona suala la wanamgambo kwenye maeneo ya mpaka wa Pak-Afghanistan kama kisingizio cha kuingilia masuala ya usalama ya eneo hilo na kuweka miundombinu yake ya kukabiliana na ugaidi katika eneo hilo. Inaonekana kana kwamba Marekani inataka kutumia shinikizo kutoka kwa jeshi la Pakistan kwa kundi la Taliban la Afghanistan kama fimbo ya kuwalazimisha kufuata matakwa yake ya kujisalimisha kikamilifu mbele ya mfumo wa kiliberali wa kimataifa na kukubali matakwa ya Marekani ya kufungua mfumo wa kisiasa wa Afghanistan kwa vibaraka wa Marekani kutoka kwa utawala wa zamani na kuanzisha mageuzi katika dola ya Afghanistan. Mgogoro wa Taliban wa Afghanistan na Pakistan unasaidia kuiweka Pakistan kuzingatia mpaka wake wa Magharibi na kuweka umakinifu wa Jeshi la Pakistan mbali na mpaka wake wa Mashariki na hivyo kuruhusu India kuelekeza maandalizi yake ya kijeshi kwa China badala ya Pakistan.

Kwa kumalizia, mgongano kati ya mamlaka za Pakistan na Taliban wa Afghanistan ni mgongano baina ya Waislamu ambayo ni matokeo ya moja kwa moja ya mpaka bandia uliochorwa kati ya watu wawili wa Kiislamu na ukoloni wa Kiingereza. Ni Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pekee ambayo itawaunganisha Waislamu wa Pakistan, Afghanistan na Asia ya Kati chini ya mamlaka ya Uislamu, na kuondoa uadui baina ya ndugu na kuunganisha ardhi za Waislamu, nguvu na rasilimali na kuleta usalama na ustawi kwa mujtamaa wa Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Moez – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu