Jumatano, 19 Rabi' al-awwal 1445 | 2023/10/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ikomboeni Kashmir kutoka kwa Makucha ya Modi au Kaeni Kando na Utawala!

(Imetafsiriwa)

Kila siku inayopita, Modi anaimarisha mshiko wake juu ya Kashmir. Ndani ya Kashmir, uwiano wa idadi ya Waislamu unabadilika. Wasio wa Kashmiri wako huru kununua mali. Wakashmiri wanazimwa, sauti zao zinanyamazishwa, nyumba zao zinabomolewa na vijana wao wanajaza magereza.

Licha ya hayo yote, uongozi wa kiraia na kijeshi unapiga domo tupu la kuwanusuru watu wa Kashmir katika Siku ya Mshikamano wa Kashmir. Ni kana kwamba hawana amri na vikosi vya kijeshi vya wanajeshi laki sita, waliojihami kwa makombora ya nyuklia na ya kawaida. Ni kana kwamba wao ni waandaaji wa timu ya mitandao ya kijamii, wanaotaka kuikomboa Kashmir kupitia tweets, taarifa na kampeni za mtandaoni!

Waislamu wa Kashmir, Pepo Ardhini, ni Waislamu watukufu wanaotaka msaada wa kijeshi wa kisilaha kutoka kwa watawala wa Pakistan. Hawana haja ya maneno matupu ya kulaani. Wakati watawala hawa kivitendo wameng'oa muundo wa Jihad na kuisaidia dola ya Kibaniani kuanzisha utawala wao katika eneo letu. Watawala hawa ndio wawezeshaji wa mfumo wa Modi wa Hindutva, kwa sababu ndivyo Wamarekani wanavyo taka.

Enyi Maafisa Wenye Ikhlasi katika Jeshi la Pakistan!

Yeyote anayetaka kuelewa uhalisia wa uongozi huu wa kisiasa na kijeshi, ukweli uko wazi kwake. Yeyote ambaye amekwama tu kwenye gurudumu la taaluma, ajira, pensheni, manufaa na viwanja, atajipofusha mwenyewe. Yeyote anayesubiri mabadiliko yatokee kipeke yake na ilhali hafanyi chochote, lazima ajue kwamba Mwenyezi Mungu (swt) habadilishi Sunnah Zake. Hakika, Malaika huteremka kusaidia pale wenye ikhlasi wanapotenda kwa ajili ya mabadiliko, wakimtegemea Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ ٱللَّهِ تَبۡدِيلٗا]

“Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Ahzab 33:62].

Jitokezeni na mutoe Nusrah kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Batilisha mpango mzima wa mafisadi wa kimataifa na kikanda vichwani mwao. Imani yetu haituruhusu kuvaa minyororo ya mfumo huu wa kilimwengu, huku tukitembea kwenye dalili za ukoloni wa kimataifa. Kupitia nguvu ya Imani hii, ndugu zenu katika eneo hili hadi kufikia sasa wamewadhalilisha Mafirauni watatu wa dunia. Sasa ni zamu yenu kuukusanya Ummah kuanzia Indonesia hadi Morocco, chini ya Khilafah, kuwazika mafirauni waliobaki. Hii ni ahadi ya Mola wenu Mlezi, na bishara njema ya Mtume wenu (saw) na urithi wa babu zenu. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَما عَلَیْنا إِلاَّ الْبَلاغُ الْمُبین]

“Wala si juu yetu ila kufikisha ujumbe ulio wazi.” [Surah Yasin 36:17].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Yasir – Wilayah Pakistan

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu