Jumatano, 15 Rajab 1446 | 2025/01/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ruzuku ya Mafuta na Suluhisho la Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Katika hotuba yake ya kuapishwa mnamo tarehe 29 Mei 2023, rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu alimaliza ruzuku ya mafuta kwa mujibu wa upeanaji wa utawala wa rais wa zamani wa Nigeria Muhammadu Buhari. Kutokana na kuzorota kwa uchumi na wasifu wa madeni unaozidi kuwa mbaya, wazo kwamba ruzuku ilizuia maendeleo, miongoni mwa hadithi nyinginezo, hatimaye lilienezwa kwa wingi. Umati haukulazimika kungoja athari baada ya vituo vya mafuta kufungwa kote nchini. Kimaumbile, foleni ndefu ziliundwa katika vituo vichache vilivyofungua uuzaji wa mafuta kwa bei ya juu.

Tinubu alidai kuwa ruzuku siku zote imekuwa ni mpango ambao “... uliwapendelea matajiri zaidi kuliko maskini. Ruzuku haiwezi tena kuhalalisha gharama zake zinazoongezeka kila mara baada ya kukausha rasilimali” (Daily Post). Ni kweli kwamba matajiri wanafaidika zaidi kwa sababu wanamiliki kampuni za mafuta. Lakini dhana ambayo Tinubu alitaka kuipata kutoka kwa raia ni potofu, ambayo ni kwamba kuondoa ruzuku kunatanguliza masikini kuliko matajiri kwa kipindi cha muda mrefu.

Kinyume chake, matajiri walilipwa vizuri na serikali ili kutotoza umma bei kamili. Kuondolewa kwa ruzuku hakubadilishi ukweli kwamba matajiri bado wataendelea kupata malipo kamili na kutajirika zaidi, ila tu wakati huu inatoka kwa watu masikini kuliko serikali. Hii inaendelea tu kuwatajirisha matajiri kama kawaida. Hakuna ushahidi au makadirio yanayokubalika ambayo yanaweza kuonyesha jinsi masikini wanafaidika kutokana na hili.

Kusisitiza kwamba fedha zitakazotumika katika kutoa ruzuku ya mafuta ‘zitarejeshwa’ kwa sekta zilizofiwa ni ahadi tupu isiyo na matumaini ya kutimizwa. Hii ni kwa sababu serikali zilizopita zilibakisha asilimia za ruzuku ambazo zilikatwa kwa miaka mingi lakini hazikutumika ipasavyo katika kufadhili sekta hizi. Kwa hakika, hii ni dhahiri ni hatua ya kupunguza matumizi ya serikali ambayo pengine yatapunguza asilimia ya upataji wa deni. Ikiwa ndivyo, kwa nini tusipunguze kwa kiasi kikubwa kiasi cha kuchukiza ambacho wanasiasa hulipa wenyewe na malipo fiche wanayoiba kutoka kwa hazina ya serikali? Kwa nini umma siku zote lazima uwe kwenye mwisho wa kushindwa kwa sera za kidemokrasia na ufisadi wa asili?

Kusisitiza kwamba fedha zitakazotumika katika kutoa ruzuku ya mafuta ‘zitaregeshwa’ kwa sekta zilizoathirika ni ahadi tupu isiyo na matumaini ya kutimizwa. Hii ni kwa sababu serikali zilizopita zilibakisha asilimia za ruzuku ambazo zilikatwa kwa miaka mingi lakini hazikutumika ipasavyo katika kufadhili sekta hizi.

Kwa hakika, hii ni dhahiri hatua ya kupunguza matumizi ya serikali ambayo pengine yatapunguza asilimia ya upataji wa madeni. Ikiwa ni hivyo, kwa nini isipunguze kwa kiasi kikubwa kiasi cha kuchukiza ambacho wanasiasa hujilipa wenyewe na malipo fiche wanayoiba kutoka kwa hazina ya serikali? Kwa nini umma siku zote lazima uwe kwenye dhiki ya kufeli kwa sera za kidemokrasia na ufisadi wa asili?

Sera na maamuzi mabovu kama haya kimsingi hayasababishwi na vyama vya kisiasa na wanachama wao. Yanaitwa “maamuzi ya kisera” kwa sababu ni ya kimfumo. Mfumo wa uchumi wa ubepari, unaotekelezwa kote ulimwenguni, ni maarufu kwa kutojali kushiba kwa masikini. Pengo la kukosekana kwa usawa ambalo ulilitengeneza sio siri, ambapo asilimia 1 ya walio juu “... walinyakua karibu theluthi mbili ya utajiri wote mpya wenye thamani ya dolari trilioni 42 ulioundwa tangu 2020” (The Daily Star).

Nigeria na ulimwengu kwa jumla unahitaji mfumo wa Kiislamu zaidi kuliko hapo awali. Mfumo wa uchumi wa Kiislamu unazipa kipaumbele mbinu za ugavi, tofauti na ubepari, ambao unalenga tu ukuaji na mrundiko kupitia ubinafsishaji. Katika Uislamu, uzalishaji ni muhimu tu kwa sababu ya haja ya usambazaji. Kwa hivyo, faharasi ya Pato la Taifa (GDP) haiamui uchumi mwanana. Badala yake, ufikiaji wa umma kwa uzalishaji huamua. Ili kufikia hili, Uislamu unagawanya mali katika vigawanyo vitatu: dola, binafsi, na umma. Hebu tuangalie kwa ufupi kila moja.

Mali ya Kibinafsi - kitu chochote ambacho kinaweza kumilikiwa na mtu binafsi. Kawaida huashiriwa na ukomo wake. Kitu chochote ambacho kiko chini ya kigawanyo hiki kinaweza kumilikiwa na kuuzwa na mtu binafsi.

Mali ya Dola - mali yoyote ambayo raia wana haki lakini inasimamiwa na kumilikiwa na dola, k.m. ardhi za Kharaji. Mali kama hii haiwezi kubinafsishwa.

Mali ya Umma - hii ni mali ambayo watu binafsi hawaruhusiwi kumiliki. Ingawa, inasimamiwa na dola mithili ya mali ya dola, tofauti kati yao ni kwamba mali ya dola inatumiwa kulingana na mahitaji ya serikali katika kuendesha utawala. Ilhali mali ya umma ni ya wananchi na serikali ndiyo inayoisimamia ili kuhakikisha inatolewa kwa umma. Hivyo basi, hii haiwezi kubinafsishwa au kutaifishwa. Aidha, mali ya umma imegawanywa katika makundi matatu:

1. Kitu chochote ambacho kinachukuliwa kuwa cha matumizi ya umma, kiasi kwamba mji au jamii itawanyike kukitafuta kama hakingepatikana – mithili ya maji.

2. Hifadhi za madini yasiyohesabika – mithili ya mafuta.

3. Vitu ambavyo kwa asili vimekusudiwa kwa umma, sio umiliki wa mtu binafsi – mithili ya misitu.

Kwa hivyo, bidhaa kama vile mafuta ghafi haziwezi kubinafsishwa (au kuuzwa kibiashara, kama serikali ya Nigeria inavyosisitiza) au hata kufanywa mali ya dola kupitia utaifishaji. Hii ni kwa mujibu wa Hadith ya Muhammad (saw), kama Ibn Abbas alivyosimulia Mtume (saw) akisema: «الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ فِي الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ» “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu: katika maji, ardhi ya malisho na moto,” imeripotiwa na Abu Dawud. Anas pia amesimulia kutoka kwa Ibn ‘Abbas akiongeza,

«وَثَمَنُهُ حَرَامٌ» “Na bei yake ni Haram.”

Zaidi ya hayo, ruzuku ya mafuta haihitajiki chini ya Uislamu kwa sababu mafuta ni mali ya umma ambayo watu hawalazimiki kulipia bei ya kibiashara. Uislamu tayari umeliweka suala hilo kuwa na ruzuku ya kimaumbile kwa sababu unakichukulia kitu chochote kisichohesabika na kingi kuwa ni mali ya umma na hakiwezi kutumiwa na watu wenye nguvu, matajiri kujitajirisha zaidi. Haya yanadhihirika katika riwaya kutoka kwa Abyadh Ibn Hammal,

«أَنَّهُ وَفَدَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ ﷺ فَاسْتَقْطَعَهُ الْمِلْحَ فَقَطَعَ لَهُ، فَلَمَّا أَنْ وَلَّى قَالَ رَجُلٌ مِنْ الْمَجْلِسِ: أَتَدْرِي مَا قَطَعْتَ لَهُ؟ إِنَّمَا قَطَعْتَ لَهُ الْمَاءَ الْعِدَّ. قَالَ: فَانْتَزَعَهُ مِنْهُ»

“Kwamba yeye alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akamuomba amkatie kipande cha ardhi chenye madini ya chumvi basi akamkatia. Alipoondoka, mtu mmoja aliyekuwa katika kikao hicho akasema: ‘je, wajua umemkatia kitu gani? Hakika umemkatia maji yasiyomalizika (Al-‘udd).’ Yeye (saw) akakiregesha kutoka kwake.” (Imepokewa na at-Tirmidhi)

Kama vile Mtume (saw) alivyomzuia Abyadh kumiliki mgodi wa chumvi kwa sababu unafikia idadi ya mali ya umma, mafuta pia ni haramu kwa watu binafsi kwa gharama ya wengi.

Uislamu unawapa kipaumbele watu juu ya matamanio ya kipote cha wachache. Huu ndio mfumo ambao Waislamu wanapaswa kulingania hayo unapotabikishwa, haki itaenea na wanyonge watapewa haki zao. Mabadiliko ya nyuso za rais na vyama havijatatua matatizo yoyote ya nchi na ni dhahiri kamwe hayatatua. Hii ni kwa sababu tatizo kamwe halikuwa ni chama wala rais bali ni mfumo unaotabikishwa na vyama na marais.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Umar Abu Ammar Bin Ahmad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu