Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mtego Mbaya wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI)

(Imetafsiriwa)

Gazeti la Express Tribune liliripoti mnamo Jumatatu, Agosti 07, 2023 kwamba "uwekezaji wa China chini ya Ukanda wa Uchumi wa China na Pakistan (CPEC) ulifikia dolari bilioni 30, huku awamu ya pili ya mradi huo mkubwa itafungua mtazamo zaidi wa ushirikiano wa nchi mbili, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alisema.”

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alikuwa akihutubia kwenye hafla ya kutoa tuzo kati ya kampuni bora za Kichina nchini Pakistan, haswa zile zinazofanya kazi kwenye miradi ya CPEC. Shehbaz alisema kuwa CPEC imebadilisha hali ya kiuchumi ya Pakistan. Waziri Mkuu huyo alidokeza kuwa serikali imezindua Baraza Maalum la Uwezeshaji Uwekezaji (SIFC) ili kukuza Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI), ambao utajumuisha wadau wote wakuu nchini. Sherehe hiyo ilikuja wakati nchi hizo hivi karibuni zikiadhimisha muongo mmoja wa CPEC, mradi mkuu wa Mpango wa Rais wa China Xi Jinping wa Belt and Road Initiative (BRI).

Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) unatajwa kama mabadiliko ya uchumi wa Pakistan, na sio tu na serikali, bali na kipote chote cha watawala wa nchi hiyo. Inaonekana kana kwamba kuna itifaki ya kushtua na kunyonga miongoni mwa kipote cha watawala wetu kuhusu hili. Utawala wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan umeunda Baraza Maalum la Kuwezesha Uwekezaji kwa madhumuni ya kuvutia Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni nchini. Kupitia Baraza hili, serikali ya Pakistan imechukua hatua za kuvutia FDI, kama vile kutoa motisha, vibali vya haraka, na taratibu za udhibiti zilizorahisishwa ili kuunda mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji. Hii ina maana kuwa kutakuwa na mfumo mmoja nchini kwa wawekezaji wa ndani, wafanyibiashara na makampuni, huku kutakuwa na mfumo mwingine wa wawekezaji wa nje, ambao sheria maalum kwao zitatungwa, na muamala wa hali ya juu utatolewa kwao.

Wazo la Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni linatokana na kijitabu cha mfano cha maendeleo cha Magharibi. Nchi za Magharibi kiasili ni za wakoloni. Hii kimsingi ina maana kwamba wanapora na kufuja rasilimali za nchi nyingine ili kuendeleza ustawi wao wenyewe wa kiuchumi. FDI ni chombo chengine ambacho kwacho makampuni ya Magharibi hunyonya rasilimali kimuundo kutoka kwa ardhi za Waislamu. Mwelekeo huu wa kupora ulimwengu uliobaki umeundwa kwa njia nne zifuatazo:

1- Ubunifu wowote au teknolojia mpya, ambayo inatengenezwa katika vyuo vikuu na vituo vya utafiti vya Magharibi, inalindwa mara moja kwa jina la haki miliki. Kwa hivyo kampuni hazina ushirika na mawazo yao, teknolojia, na masuluhisho. Wanaamini kwamba wanaweza kuongeza faida zao kupitia kulinda Haki yao ya Umiliki (IP). Matokeo yake, wanaufunga umiliki wa uvumbuzi mpya.

2- Taasisi za Magharibi kama vile IMF na Benki ya Dunia, kwa jina la soko huria na biashara ya kimataifa, huweka masharti katika programu zao za misaada na mikopo. Kupitia masharti haya, uchumi wa nchi nyingine unafunguliwa. Badala ya kugawanya teknolojia yao, nchi za Magharibi huuza bidhaa na huduma zao katika masoko haya. Makampuni makubwa ya teknolojia ya kimataifa kama Apple, Microsoft na Nvidia yasingeweza kamwe kuwa makampuni ya matrilioni ya dolari, kama yangejifunga katika masoko ya Marekani.

3- Makampuni ya Magharibi kisha huleta Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) kwa nchi zinazoendelea kiuchumi. Uwekezaji huu unalindwa kupitia vishajiishi mwanana, mapumziko ya kodi, na taratibu za udhibiti zilizorahisishwa, ili kujenga miundombinu inayohitajika katika nchi mpya. Wanawekeza katika nchi hizi ili nchi hizi zifanye kazi kama viwanda vya kutengeneza bidhaa na huduma za Magharibi, kwa kutoa nguvukazi nafuu na kupunguza gharama za uzalishaji. Inaboresha zaidi faida ya makampuni ya Magharibi. Faida hizi huregeshwa kutoka nchi zinazoendelea, na hivyo kusababisha mtaji kwenda Magharibi.

4- Nchi hizi zinazoendelea kisha hununua bidhaa na huduma ghali za makampuni ya Magharibi, ambazo zinauzwa tena katika masoko yao na kusababisha utokaji nje wa mtaji wa kigeni kurudi kwenye mifuko ya makampuni hayo hayo, na hivyo kuunda mzunguko mbaya ambao kwao hakuna pa kukimbia.

China imekopa kutoka kwa kitabu hiki cha michezo cha Magharibi na kuunda muundo wake wa uwekezaji wa Ukanda na Barabara kwa njia zile zile. Sasa, benki na taasisi za fedha za China zinatoa mikopo ya maendeleo kwa nchi. Mikopo hii hutumika kulipa makampuni ya Kichina kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo. Hivyo, riba ya mikopo ya kibiashara kwa taasisi za fedha za China, na faida inayopatikana kwa makampuni ya China kupitia miradi ya miundombinu, husababisha mtaji mkubwa kutoka nchi zinazoendelea hadi China. Leo kati ya trilioni 1 ya uwekezaji au mikopo ya China kwa nchi tofauti, dolari bilioni 700 ziko chini ya dhiki. Inaonyesha asili ya uchimbaji wa mikopo ya China na uwekezaji wa maendeleo.

Unyonyaji huu kwa jina la Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni hauwezi kuisha isipokuwa mfumo wa sasa wa uchumi wa Kibepari na utaratibu wa sasa wa kilimwengu wa kiliberali mamboleo upingwe. Ni lazima ubadilishwe  kwa Adl (uadilifu) ya Uislamu. Mfumo wa kiuchumi wa Uislamu ndio mfumo wa kipekee unaoegemezwa juu ya Shariah zilizovuliwa kutoka katika Quran Tukufu na Sunnah za Mtume (saw). Pakistan, na ulimwengu mzima wa Kiislamu kwa jumla, unahitaji mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ambao utauondolea ulimwengu maovu ya mfumo wa uchumi wa Kibepari.

Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu unazingatia ugavi wa mali na sio tu uzalishaji wa mali. Uislamu hauamini katika ukuzaji wa sekta ya kibinafsi kwa viwanda vizito na miradi mikubwa. Katika Uislamu, utajiri humilikiwa na sekta binafsi, sekta ya umma na serikali, jambo ambalo linaipa serikali nafasi kubwa katika uchumi. Hakuna mabenki, masoko ya hisa, masoko ya mitaji katika Uislamu. Hii inazuia uundaji wa biashara kubwa za kibinafsi zisizo za kweli. Zaidi ya hayo, riba na aina zake zote ni haramu katika Uislamu. Uislamu hauruhusu ubinafsishaji wa rasilimali za nishati. Zaidi ya hayo unapunguza dori ya watendaji binafsi katika sekta ya nishati. Inaruhusu dola ya Kiislamu kudhibiti kwa kiasi kikubwa sekta hizi kubwa za mapato ya uchumi.

Mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu ulistahimili mtihani wa wakati kwa zaidi ya miaka elfu moja. Jukwaa liko tayari kwa ajili ya kutokeza kwa Dola ya Kiislamu ya Khilafah. Kwa mara nyingine tena itatabikisha mfumo huu sio tu kwa manufaa ya Waislamu bali wanadamu wote. Itaongoza ulimwengu katika enzi ya ustawi na utulivu usio na kifani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Junaid – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu