Jumanne, 14 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mafuta kwa Damu: Watawala wa Waislamu Wanawauza Wapalestina kwa Ajili ya Mafuta na Gesi

(Imetafsiriwa)

Mashambulizi ya Gaza yanaendelea kwa zaidi ya wiki 5 sasa, na wakati kuna ‘sitisho la muda la kibinadamu’ kuruhusu ubadilishanaji wa mateka, umbile la Kizayuni limeweka wazi kuwa wataendelea kuishambulia Gaza mara tu sitisho litakapoisha.

Hadi hivi sasa, umbile la Kizayuni limeruhusiwa kutekeleza mauwaji, kuwauwa zaidi ya watu 14,000 – idadi hii inahusisha zaidi ya watoto 6,000. Wameruhusiwa kuunganisha maeneo ya kaskazini ya Gaza, ikiweka wazi kuwa hawatoruhusu Mpalestina yeyote kurejea – wakiwashambulia raia wanapojaribu kurejea kukusanya mizigo yao wakati wa ‘sitisho hilo’.

Wameruhusiwa kufanya haya, na zaidi ya haya na Wamagharibi pamoja na viongozi wa ulimwengu wa Kiislamu. Katika wiki kadhaa nyuma, tumeona namna gani walivyo changamkia uungaji mkono mauwaji ya halaiki ya Wapalestina – wakiruhusu silaha kupitia ndani ya ardhi zao kulifikia umbile la Kizayuni na kukataa kuchukua hatua yoyote ya maana dhidi ya Mazayuni wakati wanapotumia silaha zisizoruhusiwa kuwashambulia raia ndani ya Gaza. Wamezuia maandamano ya waungaji mkono na kuhakikisha vyombo vya habari vya kawaida vinapotosha ukweli kwa maslahi ya umbile la Kizayuni. Wamekubali ukataaji wa umbile la Kizayuni kuruhusu misaada kupelekwa Gaza, na hata kuendelea kufanya biashara na umbile la Kizayuni. Pia wamekataa kuvunja mahusiano na umbile la Kizayuni au kuwawekea vikwazo kwa namna yoyote ile.

Kuna sababu tafauti kwa haya – nyingi zao zinatokana na ukweli kuwa wametoa uaminifu wao na utii kwa mfumo ambao mauwaji yanahalalishwa muda baada ya muda.

Wanajaribu kutuambia kuwa Waziri Mkuu wa Kiyahudi Benjamin Netanyahu yupo katikati ya haya yote; kutushawishi sisi kuwa kuondelewa kwake kutapelekea mabadiliko lakini haikuwa hivyo. Umbile la Kizayuni limekuwepo kwenye ardhi walioipora kutoka kwa Waislamu mwishoni mwa miaka ya 1940 na wanaendelea kufanya kazi kuelekea kuwa na udhibiti kamili juu ya maeneo ya Wapalestina walioyakalia kimabavu.

Damu kwa Mafuta imetokea wapi?

Nimetambua kuwa Damu kwa Mafuta sio istilahi ambayo ipo, japo kuwa ilistahili. Tunapoangalia vita vinavyopiganwa ili kupata rasilimali asilia – kwa muktadha huu ni gesi na mafuta – na kulinganisha na istilahi kama Almasi kwa Damu, na Fedha kwa Damu, istilahi ‘Mafuta kwa Damu’ inawafikiana moja kwa moja.

Gaza na maeneo yaliokaliwa kimabavu yana kiasi kikubwa cha mafuta na gesi asilia.

Kwa mujibu wa ripoti ya UNCTAD, “Maeneo ya Wapalestina yaliokaliwa kimabavu yapo juu ya hifadhi kubwa ya mafuta na utajiri wa gesi asilia, katika Eneo C la Ukingo wa Magharibi uliokaliwa na fukwe ya Mediterania ya Ukanda wa Gaza. Hata hivyo, uvamizi unaendelea kuwazuia Wapalestina kuendeleza maeneo yao ya nishati ili waweze kuitoa na kunufaika na mali hizo.” Ripoti inakisia kuwa akiba hizi zinaweza kuleta “mamia ya mabilioni ya dolari” kwa anayeziendeleza.

Tokea 2015, uendelezaji wa eneo la Gaza Marine umepangwa kuzalisha mapato ya dolari bilioni 2.5 hadi 2.7 lakini ‘Israel’ imeendelea kudhibiti hifadhi ya gesi asilia katika ufukwe wa Gaza. Pia wamedhibiti eneo la mafuta la Meged oil na gesi asilia, lililo ndani ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Taarifa za karibuni zinasema kuwa kumegunduliwa “rasilimali mpya ya mafuta na gesi katika eneo la Mashariki ya Mediterania yenye thamani inayoshangaza ya dolari bilioni 524” lakini kuna kiwango kikubwa cha rasilimali hiyo kitachotokea eneo linalokaliwa kimabavu la Palestina.”

Na kwamba “mnamo Oktoba 29, wakati vita vinaendelea bila kuwepo sitisho la vita, serikali ya Netanyahu imeyazawadia leseni 12 makampuni sita, ikiwemo BP na ENI ya Italia, kwa ajili ya kuchimba gesi katika eneo la Bonde la Mediterania.”

Hivyo, ni wazi kuwa ijapokuwa sio sababu pekee ya kushambuliwa Gaza, rasilimali ya mafuta na gesi zina mchango mkubwa katika hatua hizi za karibuni katika eneo hilo. Na rasilimali hizi sio tu zimeathiri hatua za umbile la Kizayuni, lakini pia zimekuwa ni sababu msingi ilio nyuma ya maamuzi yanayochukuliwa na serikali za Magharibi na za Waislamu kote duniani.

Kila moja inanufaika na uwepo wa umbile la Kizayuni na rasilimali zake

Sote tunafahamu kuwa Marekani muda wote imekuwa ikitoa msaada kamili kwa umbile la Kizayuni. Wana sababu za kimkakati kwa hili – inaitumia umbile la Kizayuni ili kudhibiti eneo hilo. Lakini kile kinachotia shauku ni kuwa Chevron, ambayo ni kampuni ya Marekani ina umiliki wa sehemu kubwa ya machimbo ya gesi kwenye umbile la Kizayuni.

“Chevron, pamoja na kile kinachojulikana kuwa ni NewMed Energy na washirika wao wadogo, ndio wahusika wa uvumbuzi wa gesi ‘Israel’ – Tamar na Leviathan – mnamo 2009 na 2010, na hatimaye kumiliki akiba na uzalishaji wa gesi ‘Israel.” Chanzo

Maeneo haya ya gesi yameliwezesha umbile la Kizayuni kuwa ni wauzaji wa gesi – gesi ambayo inakusanya kiasi ya asilimia 70 ya uzalishaji wa umeme, na ziada ikiuzwa Misri na Jordan.

* Mabomba ya EMG yameunganishwa moja kwa moja baina ya umbile la Kizayuni na Misri. Misri inategemea gesi kutoka umbile la Kizayuni wakati wa miezi ya joto kwa ajili ya taa na viyoyozi.

* Njia ya usafirishaji wa mauzo ya bidhaa nje kutokea kaskazini mwa umbile la Kizayuni kuelekea Jordan, lililounganishwa na Mabomba ya Gesi ya Arabuni nchini Jordan na njia ya kusini ya usafirishaji wa bidhaa nje zimeungana moja kwa moja na maeneo ya huduma za viwanda upande wa mashariki ya Bahari Mfu. Jordan ambayo inaagiza zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji yake ya nishati, inategemea gesi inayosafirishwa kupitia Misri na umbile la Kizayuni.

Hivyo, tunapostaajabu kwa nini inawezekana kwa umbile la Kizayuni kuzungukwa na nchi za Waislamu zinazoruhusu Wapalestina kuuliwa- hii ndio sababu. Umbile la Kizayuni na Marekani zimehakikisha kuwa majirani Waislamu wa umbile la Kizayuni wana maslahi ya pamoja katika kulihifadhi hili umbile la Kizayuni- licha ya ukweli kuwa nchi ya Kizayuni ipo kwenye ardhi ambayo imeporwa kutoka kwa Waislamu, kwa umwagikaji wa kiwango cha kutisha cha damu ya Wapalestina ndani ya mchakato huo. Hao wote wananufaika kutokana na hali ya sasa iliyopo – hata kama watapendekeza namna tafauti.

Sio tu majirani wa karibu zaidi wa umbile la Kizayuni wanaonufaika na hali hii.

“Mnamo mwezi Machi 2021, Mubadala Energy, kampuni tanzu ya Mubadala Investment Company, inayomilikiwa na serikali ya Abu Dhabi, inamiliki hisa asilimia 22 katika machimbo ya Tamar kwa zaidi ya dolari bilioni 1 -- ni mkataba mkubwa zaidi kwa sasa baina ya Imarati na ‘Israel’ “ Chanzo

Na kwa wale wanaoamini kuwa Pakistan haishiriki katika biashara, wanaweza kuwa hawana mahusiano ya moja kwa moja na umbile la Kizayuni lakini wanaagiza gesi kutoka Marekani na Misri. Hii inaweza kuonekana kuwa ni mahusiano yasio na uzito, lakini huwa ni yenye uzito sana unapozingatia ukweli kuwa Misri inategemea umbile la Kizayuni kwa mauzo yake ya gesi.

“Misri inategemea manunuzi ya gesi ya ‘Israel’ kutosheleza mahitaji yake ya ndani, pamoja na kuiuza tena ambapo imekuwa ni muingizaji muhimu wa fedha kusaidia uhaba wa fedha zake za kigeni.” (Reuters)

Na hivyo gesi imekuwa ni muhimu kwa maslahi ya umbile la Kizayuni na Marekani katika eneo.

Marekani imeunda mkataba wa ushirikiano wa nishati ‘baina yake na Israel’ unaoeleza kuwa “Ushirikiano wa nishati wa ‘Marekani na Israel’ na muendelezo wa rasilimali asilia za ‘Israel’ ni kwa maslahi ya mkakati wa Marekani”, ikiahidi kuisaidia Israel kwa “amani ya kieneo na masuala ya usalama”.

Pia kuna mahitaji ya gesi katika muda wa karibuni – mahitaji yalioletwa na Vita vya Ukraine. Hii ndio sababu kwa nini nchi za EU zinaonyesha uungaji mkono mkubwa kwa mauwaji ya halaiki yanayotekelezwa na umbile la Kizayuni. Kwa sababu ili kuzipata rasilimali ambazo Mwenyezi Mungu amezitunuku kwa Palestina, umbile la Kizayuni lazima liongeze udhibiti wake kwenye eneo hilo.

Lakini vipi kuhusu mafuta?

Umbile la Kizayuni hadi sasa linategemea mafuta kutoka nchi nyengine. Wanapata mafuta zaidi kutoka nchi mbili za Waislamu, Kazakhstan na Azerbaijan. Pia wanapata mafuta kutoka nchi za Afrika Magharibi kama Gabon, na pia wanapata kutoka Marekani na Brazil. Kwa kuzingatia haya, basi itashangaza kuwa umbile la Kizayuni linahitajia kupata mafuta katika ardhi ya Palestina?

“Uchunguzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) umebaini kuwa mafuta yaliyogunduliwa yanakisiwa kuwa ya kiwango cha mapipa bilioni 1.7.”

Umbile la Kizayuni linahitaji mafuta haya – wanapinga kuwaruhusu Wapalestina kumiliki rasilimali hii ya mafuta, ili kuwaweka watu wa Palestina wawategemee wao na huku wakibaki wamemiliki rasilimali hii kwa ajili yao.

Lakini huu sio mwisho wake- Gaza na maeneo ya Palestina yaliyokaliwa kimabavu ni muhimu kwa mpango mpya wa IMEC.

Mkutano wa mwaka huu wa G20 umebuni mipango ya kuunda Ukanda wa Kiuchumi wa India-Mashariki ya Kati-Ulaya (India-Middle East- Europe Economic Corridor). Mradi huu unakusudia kuweka uzani na ule wa Ukanda wa China na mpango wa Barabara (China’s Belt and Road Initiative), unatafsiri upya “njia za kibiashara za kilimwengu, kukuza uunganishaji, na kuwepesisha ukuaji na uuzaji nje wa nishati safi na mawasiliano ya kidigitali.”

Netanyahu ameuelezea kuwa ni “mradi wa ushirikiano ulio mkubwa zaidi katika historia”, akiongezea: “Nchi yetu ‘Israel’ itakuwa ni muunganishaji muhimu katika ukanda huu wa kiuchumi; njia zetu za reli na bandari zitafungua lango jipya kutoka India kupitia Mashariki ya Kati hadi Ulaya, na kurejea.” Chanzo

Utaanzia India, utavuka Bahari ya Arabuni na kupitia Saudi Arabia, Jordan, umbile la Kiyahudi, na Ulaya kufikia Imarati. Njia hii itajumuisha usafiri wa baharini na reli, na utajumuisha nyaya za kuunganisha gridi za umeme na njia za mawasiliano. Mipango ya ukanda huu pia unajumuisha mabomba ya kusafirisha gesi ya hydrojini inayozalishwa na Saudi Arabia na Imarati.

Na wakati kuna taarifa kuwa ukanda huo unaweza usiingize Uturuki, Erdogan alisema;

“Tunasema hakuna ukanda bila Uturuki… Sisi ni wazalishaji muhimu na kituo cha biashara. Njia yenye kufaa zaidi kwa usafirishaji kutoka Mashariki hadi Magharibi lazima ipitie Uturuki… na unaipatia njia mbadala kupitia mpango wa ujenzi wa Maendeleo ya Barabara wa Iraq, wenye lengo la kuiunganisha Uturuki na bandari ya Iraq ya Faw kwa barabara na reli.”

Na Waziri wake wa Usafirishaji na Miundo mbinu, Abdulkadir Uraloglu, amesema kuwa;

“Awamu ya kupangilia mpango takriban imekamilika. Hivi sasa tupo katika mazungumzo tukiwa nchi nne juu ya namna ya kuutengeneza na namna ya kuuendesha” Aliongeza kuwa Imarati na Qatar zitatoa msukumo imara na kwamba njia nyengine za uwezeshaji kifedha – ikiwemo benki za Ulaya, malipo kwa mafuta na uwekezaji wa Uturuki yenyewe – zipo katika kuzingatiwa. Na kama haikuwa wazi jinsi yote haya yanahusiana na mashambulizi katika Gaza – njia pendekezwa ya mfereji inapita moja kwa moja katikati ya Gaza.

Hivyo kwa namna moja au nyengine dunia inaruhusu maelfu ya watoto wa Kipalestina kufa… kwa ajili ya biashara.

Haya sio maendeleo mapya – mtandao wa biashara huenda kwa sababu watawala wa Waislamu wamechagua kuwauza Wapalestina kwa wavamizi wa Kizayuni miongo kadhaa nyuma. Na kila serikali tokea wakati huo imeshikilia chaguo hili, kwa namna moja au nyengine kutokana na maslahi yao ya pamoja ya kitaifa.

Mifano michache ya ukweli huu ni kuwa:

- Mafuta yanayoagizwa na umbile la Kizayuni yameendelea kupitia Uturuki licha ya mashambulizi katika Gaza.

- Majenerali wakuu wa Misri wanafanya kazi kwa karibu na wenzao katika umbile la Kizayuni tokea mkataba wa Camp David wa 1978. Na vikosi vya usalama vya Misri vinafanya kazi pamoja na umbile la Kizayuni kushurutisha vizuwizi vya mienendo ya kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, huku Wamisri na majasusi wa umbile la Kizayuni wanashirikiana kikamilifu. Pia Misri na umbile la Kizayuni wanashirikiana kuwadhibiti watu wanaoingia na kutoka Gaza – kabla na wakati wa vita.

- Umbile la Kizayuni na Jordan zinatekeleza ushirikiano wa pamoja kuhusiana na maji na nishati ya nguvu za jua. Umbile la Kizayuni linajenga mabomba mapya yatakayoongeza mara mbili kiasi cha maji inayouza kwa Jordan yenye uhaba wa maji. Jordan pia imeiruhusu Marekani kusafirisha vifaa vya kijeshi katika eneo hilo ikiwa ni sehemu ya Marekani ya kulilinda umbile la Kizayuni.

Hatuwezi kufanya chochote kuzuia umbile la Kizayuni au Marekani – wao (ati) wana nguvu sana

Jambo moja ambalo tunapaswa kuwa wazi nalo ni kwamba haya yote hayakuwezekana bila ya usaidizi wa watawala wa Waislamu. Wameliruhusu umbile la Kizayuni kuwakandamiza na kuwauwa Wapalestina. Wameiruhusu Marekani kupeleka msaada kwa umbile la Kizayuni kupitia ardhi, anga na bahari.

“Mamlaka za usafiri wa anga za Jordan na ‘Israel’ zimekubaliana kufungua anga zao kuwa ni “daraja la angani” baina ya Mashariki na Magharibi kuanzia Oktoba 9. Makubaliano hayo yataruhusu ndege na baadhi ya ndege za kivita kuruka juu ya nchi mbili hizo zikiwa katika safari zao kutoka na kuingia Amerika Kaskazini na Ulaya, kwa upande mmoja, na Mashariki ya Kati na Mashariki ya Mbali, kwa upande mwingine… ramani iliyounganishwa na mkataba inaonyesha njia inayohusisha upaaji na utuaji katika ‘Israel’, Jordan, Saudi Arabia, Kuwait, Imarati, Qatar na Iraq, pamoja na njia inayohusisha upaaji wa juu zaidi kupitia Iran.” Chanzo

Pia wamelifanya hili kuwa wazi zaidi kwa kuwa wataliruhusu umbile la Kizayuni kufanya mauwaji ya halaiki kwa sababu wanataka kuendelea kusawazisha mahusiano na umbile la Kizayuni. Hadi kwenda mbali zaidi kuyaonya majeshi ya Waislamu dhidi ya kulizuia umbile la Kizayuni kutekeleza mauwaji ya wanawake na watoto.

“Jeshi la Misri, rais amesema, “pamoja na uwezo wake wote, rasilimali na ufanisi lina lengo moja tu nalo ni kuilinda Misri na usalama wa taifa lake”. Alilionya jeshi lake dhidi ya kuhodhi mawazo ya “udanganyifu wa nguvu” na kuliambia kuwa uwezo wa jeshi utumike “kwa busara.””

Watawala wengine Waislamu wameliweka wazi suala la kuwa hawatotoa majeshi yao katika kuiunga mkono Gaza – wakichagua kutoa msaada wao kwa umbile la Kizayuni, Marekani, na kila mmoja huku mauwaji ya raia wa Palestina yakiendelea.

Wanafikiriaje kuwa yoyote kati ya haya yanakubalika kwa mbali?

Katika Uislamu, tunafahamu kuwa damu ya Muislamu ni muhimu zaidi kuliko Ka’aba na eneo lote linaloizunguka. Lakini ‘watawala wetu Waislamu’ wameamua kuwa kuna bei kwa maelfu ya roho za Wapalestina – wengi wao wakiwa Watoto - nayo ni gesi na mafuta. Je hii ndio aina ya watawala tunaowataka watuwakilishe sisi?

Wametuonyesha muda baada ya muda kuwa maisha yetu hayana thamani kwao- watatuuza ikiwa hiyo ndio itawabakisha wao katika nafasi zao za utawala. Basi kwa nini tunaendelea kufuata amri zao? Hivyo tunadhani kuwa hilo litatuhifadhi?

Hivyo tunafikiri kuwa kuchukua hatua kuwalinda ndugu zetu Waislamu na dada zetu itatudhuru sisi? (Bali) itatuacha huru kutoka kwa (udhibiti) wa Marekani, na marafiki zake wote, wanaomwaga damu ya Waislamu kila siku.

Kutofanya chochote katika Gaza si lolote isipokuwa ni kutushirikisha sisi katika umwagikaji wa damu unaotokea- na yote mengine kwa maslahi ya sehemu ya Mafuta kwa Damu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu