Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Uislamu: Dawa ya Ubaguzi wa Rangi

Machafuko ya 2020 ya Maisha ya Weusi ni ya Kuzingatiwa (Black Lives Matter) hivi sasa yamefikia kwenye mwezi wake wa nne, yakiweka kivuli kirefu juu ya uchaguzi wa urais wa Amerika. Machafuko ya umma yaliripuka kutokana na kifo cha George Floyd mnamo tarehe 25 Mei 2020 na yamechochewa kwa miongo ya miaka ya ubaguzi wa kitaasisi. Wanachama na washirika wanaobaguliwa wa jamii za Wamarekani wa asili ya Kiafrika wanaandamana kwenye mitaa katika kupinga ubaguzi na ukandamizaji ambao muda mrefu umekuwa ukiiangamiza nchi.

Maradhi ambayo ni ubaguzi sio kitu kipya. Umekuwa ukizitesa taasisi za watu kwa karne kadhaa, ukiibua baadhi ya mifano zaidi inayotambulikana ya mauwaji ya halaiki, utumwa, udhalimu wa kijamii na vita.

Mfano mkuu wa ubaguzi huu ni chuki za wakoloni wa Kiingereza dhidi ya wenyeji wa Bara Hindi. Walikuwa ni mabeberu wa Kiingereza waliojizingatia kuwa ni bora zaidi ya wenyeji, hisia zinazofafanuliwa vizuri zaidi katika maneno ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Winston Churchill, alipowataja wenyeji kuwa ni “wenye tabia za kinyama”. Ilikuwa ni serikali yake iliyopora ardhi ya matajiri wake, ikinyonya mazao yake na kuongeza akiba ya Uingereza, na kuulemaza uchumi wa Bara Hindi, ikiwaacha mamilioni wakifariki au kuwa katika ufukara uliokithiri. Matokeo ya moja kwa moja ya uharibifu na uporaji huu ulikuwa ni Ukame wa Bengal ambao umepelekea vifo vya wenyeji milioni tatu. Hata hivyo, badala ya kukiri dhima kwa janga hilo, Waziri Mkuu huyo alichagua kuelekeza lawama juu ya wenyeji wenyewe, akidai kuwa “walikuwa wanazaana kama sungura,” na kuwa hiyo ndio sababu ya uhaba wa chakula.

Ni wazi kuwa hakuna chochote ambacho ubaguzi umetoa ambacho ni cha kimaadili au chema na Uislamu umeuharamisha vikali. Kuhusiana na wale wanaobagua kwa misingi ya ukabila, Mwenyezi Mungu (swt) amemshushia ilhamu Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kusema,

      «يا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ رَبَّكُمْ وَاحِدٌ وَإِنَّ أَبَاكُمْ وَاحِدٌ أَلا لا فَضْلَ لِعَرَبِيٍّ عَلَى عَجَمِيٍّ وَلا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ وَلا لأَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ وَلا أَسْوَدَ عَلَى أَحْمَرَ إِلا بِالتَّقْوَى إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِنْدَ اللهِ أَتْقَاكُمْ»

“Enyi watu, Mola wenu ni mmoja na baba yenu (Adam) ni mmoja. Hakuna ubora kwa Mwarabu juu ya asie Mwarabu, wala kwa asie Mwarabu juu ya Mwarabu, wala kwa mweupe juu ya mweusi, wala kwa mweusi juu ya mweupe isipokuwa kwa ucha Mungu. Hakika, alie mbora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni  mcha Mungu wenu zaidi.” [Bayhaqi]

Ni hakika, kuwa Mtume (saw) hakubagua juu ya msingi wa tofauti za kikabila na juu ya kuwa kizazi cha mwanzoni cha Waislamu kilikuwa ni cha mkusanyiko wa makabila. Walikuwa kina Bilal ibn Rabah (ra) Mhabeshi, Salman al-Farsi (ra) Mwajemi, Suhayb ibn Sinan (ra) Mroma.

Masahaba (ra) wa Mtume (saw) walitafautiana katika koo na makabila waliokuwa nayo lakini ulikuwa ni Uislamu ndio uliowaunganisha wote. Kwa hakika, hakuna fungamano linaloweza kushindana na lile lililopo baina ya waumini kwa kuwa halikujengwa juu ya matamanio ya kibinafsi au maslahi ya kidunia, bali ni juu ya ikhlasi ya kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) Ameteremsha katika Quran,

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Hakika waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.” [Surah al-Hujarat 49:10]

Falsafa yoyote au fikra inayotishia kuhujumu udugu huu inalaaniwa na Uislamu. Udugu haugawiki juu ya asili, misingi ya lugha au majimbo na hakuna chama cha kisiasa kinachoweza kusimamishwa juu ya migawanyiko hiyo ya kijinga. Mtume (saw) amesema,                                                                                                                                          

»مَنْ قُتِلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُمِّيَّةٍ يَدْعُو عَصَبِيَّةً أَوْ يَنْصُرُ عَصَبِيَّةً فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ«

“Yeyote anayekufa chini ya bendera ya aliye kipofu (katika njia ya sawa), anayeitia wito wa kiasabiyya au kunusuru asabiyya anakufa kifo cha kijahilia.” [Muslim]

Kutokana na dalili hizi zilizopokelewa, ni wazi kuwa ukabila hauna nafasi katika Uislamu.

Wema wa kweli wa Uislamu, hata hivyo, unadhihirishwa katika hali ambayo sio tu unakataa kusamehe juu ya imani isiojengwa juu ya dalili, lakini wakati huo huo unafuta fikra inayoweza kuelekeza huko.

Ukabila si zaidi ya tendo la chuki, mtu anazaliwa katika hali ya kutokuwa salama ambayo inaibuka ndani ya mtu binafsi wakati wanapohisi mgogoro wa utambulisho. Mtu huyu anachukulia mgogoro huu kuwa ni tishio na hili huamsha hisia ya kuendeleza maisha. Hii humpelekea mtu kuthibitisha tena utambulisho wao na kujithamini, kufanya hivyo kwa kuhusisha utambulisho wao kwa sifa moja ya nafsi zao na kisha kuifungamanisha na watu binafsi wanaomiliki sifa sawa.

Wakati fungamano hili linapokuwa, linamuweka mbali mwenye nalo na wengineo ambao huzingatiwa kuwa ni tofauti. Yote haya ni jaribio la kutangaza utambulisho wao. Wakati thamani kubwa inapopewa sifa hii moja ambayo kundi linaimiliki, hupelekea kwenye ubwana ambao husanifiwa katika namna ya ukandamizaji na chuki kwa makundi hayo ambayo yanaonekana kuwa ni tofauti. Kwa hivyo, fungamano sasa linakuwa lenye kubomoa kwa kuwa lina wapanga watu dhidi ya watu wengine kwa namna isio ya kibinaadamu.

Ni Uislamu ndio unaoweza kutoa suluhisho kwa mgogoro huu kama ambavyo Uislamu ndio unaoweza kuung'oa kutoka kwenye mizizi yake. Inafahamika kuwa katika Uislamu utambulisho wa Muislamu hautegemei juu ya wengine wala juu ya taasisi yoyote ya kilimwengu, bali umehifadhiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kupitia kile ambacho Yeye (swt) ameteremsha kwa muundo wa Quran Tukufu. Ni Quran Tukufu ambayo inamuongoza mtu katika mambo yake ya kimaisha, kuondoa kila shaka alionayo ya azma yake au utambulisho, na kumhakikishia kuwa sifa zake za msingi – uonekano wake, uelewa wake, nguvu zake nk. – sio vya kujifakharisha, lakini tabia bora zaidi katika uoni wa Mwenyezi Mungu (swt) ni  ucha Mungu na wema. Mwenyezi Mungu (swt) anatukumbusha katika Quran:

(يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ)

“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mcha mungu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye khabari.” [49:13]

Hata wakati Mwenyezi Mungu (swt) anapotutaka kuchukia ukafiri na kinachoumiliki, Yeye (swt) ametutaka kufanya uadilifu na upole kwa wasio Waislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(لَّا يَنْهَاكُمُ اللَّهُ عَنِ الَّذِينَ لَمْ يُقَاتِلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَلَمْ يُخْرِجُوكُم مِّن دِيَارِكُمْ أَن تَبَرُّوهُمْ وَتُقْسِطُوا إِلَيْهِمْ ۚ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ)

“Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu.” [Surah al-Mumtahinah 60:8].

Na ndipo Ahmad amenukuu kuwa Abdullah b. Rawaahah amesema kuwaambia Mayahudi wa Khaybar, “Enyi Mayahudi, nyinyi ni viumbe mnaochukiza zaidi kwangu. Mumewauwa Mitume wa Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla na mumezua uongo kwa Mwenyezi Mungu, lakini chuki yangu kwenu haitonifanya nisikufanyieni uadilifu”

Kwa namna hii, Uislamu umehakikisha kuwa muumini haangukii kwenye mawindo ya fikra za kijahili na mawazo ya hisia pekee. Bali, Uislamu umemnyanyua muumini katika fikra na uelewa, umemuendeleza sifa zake na kuusafisha moyo wake ujinga na chuki. Unawalinda waumini kutokana na maovu yote na kuingiza kwao wema na mapenzi kwa Mwenyezi Mungu (swt), muamala wa haki na wema.

Ni wazi, Uislamu ni Dini iliokamilika na ni Rehma kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

#UislamuUnasemaNini

#VijanaWaKiislamu

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Khalil Musab – Pakistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 18 Septemba 2020 13:47

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu