Ijumaa, 10 Rajab 1446 | 2025/01/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mafunzo kwa Ummah
katika Mwangaza wa Uislamu juu ya Janga la Maambukizi la Covid-19

Utangulizi

Tumekuwa tukishuhudia janga kubwa la maambukizi tangu mwanzoni mwa mwaka huu ambalo liliwafanya wengi kuchanganyikiwa, au angalau kuwa na wasiwasi, katika kuelewa baadhi ya fahamu za Kiislamu zilizo wazi bila ya kuwa na ikhtilafu. Sababu ya mkanganyiko huu sio tu ukosefu wao wa maarifa, lakini kwa sababu ya hofu iliyoundwa na mfumo wa kisekula wa Kimagharibi kwa jina la virusi vya Korona, ingawa ugonjwa huu sio hatari kama magonjwa mengine ya maambukizi kama Kifo Cheusi na mengineyo. Matokeo yake, hukmu nyingi za Sharia zinapuuzwa au kuavywa kwa jina la janga la maambukizi, kama ambavyo tumekuwa tukipuuza mama wa faradhi zote, Khilafah tangu kuvunjwa kwake. Misikiti ilifungwa kwa zaidi ya wiki kumi na tano, swala za jamaa na Ijumaa ziliachwa kwa madai ya kuzuia kuenea kwa janga la maambukizi hata katika nchi ambazo hakukuwa na maambukizi wakati huo wa kufungwa kwa Misikiti. Upuuzaji wa Hukmu za Sharia uliendelea hata baada ya Misikiti kufunguliwa kwa kuswali swala za jamaa na Ijumaa kwa kuweka masafa ya kijamii, wakidai kwamba hii itazuia kuenea kwa janga la maambukizi bila kuzungumzia kiuhalisi kile ambacho Sharia inasema katika suala hili. Wengine hata walitoa fatwa juu ya kulipa fidia vichinjo vya Eid Ul Adha kwa michango kwa sababu ya hofu ya janga [1]. Karibu kila mahali, hali ya hofu ilikuwa dhahiri. Makala haya yatafafanua maoni potofu na mitazamo ya kimakosa ili Waislamu wanaomiliki Aqeeda ya Kiislamu lazima pia wamiliki fahamu za Kiislamu na kulishughulikia suala hili la kisasa kutoka kwa mtazamo wa Kiislamu. Hii itawafanya Waislamu waridhike na watosheke na yale ambayo Mwenyezi Mungu ameyakidhia ili kufuata na kutekeleza Hukmu za Sharia wakati wa raha na shida.

Ajal ndio sababu ya pekee ya Mauti na Mwenyezi Mungu Ndiye anayepitisha Ajal

Kila kiumbe kina muda wake wa kuishi baada ya hapo kitakufa. Hakuna kiumbe chenye kuishi milele kama anavyosema Mwenyezi Mungu (swt),

(كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ)

“Kila nafsi itaonja mauti” [Al-Anbiya: 35]. Mwenyezi Mungu amepitisha kila kiumbe muda wa maisha, ambao haucheleweshi wala kutangulizwa. Kipindi hiki cha maisha huitwa Ajal na kifo hutokea tu wakati Ajal anapokoma. Sababu (sabab) ya kukomeshwa kwa Ajal sio nyingine ila ni Mwenyezi Mungu (swt). Hii ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ndiye anayetoa uhai na mauti na ndiye aliyeweka Ajal kama vile Yeye (swt) alivyoweka rizq (riziki) ya kila kiumbe. Hakuna hali yoyote nyengine kama tauni au ajali au kitu chochote kinachoweza kuwa sababu ya kifo.

Mwenyezi Mungu Allah (swt) asema,

(وَاللّهُ يُحْيِـي وَيُمِيتُ)

“Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha.” [Aali-Imran: 156],

(رَبِّيَ الَّذِي يُحْيِـي وَيُمِيتُ)

“Mola wangu ni yule ambaye huhuisha na kufisha.” [Al-Baqarah: 258],

(أَيْنَمَا تَكُونُواْ يُدْرِككُّمُ الْمَوْتُ وَلَوْ كُنتُمْ فِي بُرُوجٍ مُّشَيَّدَةٍ)

“Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu.” [An-Nisaa’: 78],

(وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَنْ تَمُوتَ إِلاَّ بِإِذْنِ الله كِتَابًا مُّؤَجَّلاً)

“Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo andikwa ajali yake.” [Aali-Imran: 145].

Aya hizi na zingine ni dalili ya kukatikiwa kwamba kifo kinatoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), na aya hizi zina maana ya kukatikiwa kwamba Mwenyezi Mungu ndiye anayesababisha kifo, na sababu hiyo ya kifo ni kumalizika wa muda wa uhai (intihaa 'ul-'ajal ), na sio hali ambayo kifo kimetokea ndani yake.

Haipaswi kusema kwamba ikiwa moyo utaacha kupuma, maisha yatamalizika. Maisha sio chochote isipokuwa ni sifa ya moyo. Kwa hivyo uwepo wa maisha moyoni haimaanishi ni sababu ya maisha na kutokuwepo pia haimaanishi sababu ya kukomesha maisha. Sababu halisi ya maisha ni Mwenyezi Mungu (swt) na sababu ya kifo pia ni Mwenyezi Mungu. Kufa kwa ajali au ugonjwa au tauni sio chochote isipokuwa mazingira na sio sababu za kifo. Kwa hivyo, ni wazi kwamba kifo kinatokana na kukomeshwa kwa Ajal ambaye sababu yake ni Allah (swt). [2]

Fahamu ya Ajal inawapa nguvu waumini kubaki imara katika kutii amri za Mwenyezi Mungu katika hali ngumu

Wakati muumini anapothibitisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye ambaye hutoa uhai na kifo na Yeye ndiye aliyepitisha Ajal (umri wa maisha), moyo wake unakuwa raha na kuridhika katika dhurufu zenye kutishia maisha kama vile kusema neno la ukweli mbele ya watawala madhalimu, kuenea kwa magonjwa hatari, kupigana dhidi ya maadui na mengineyo. Hii pia huondoa ajizi yake na kumfanya awe thabiti katika kutii amri za Mwenyezi Mungu (swt) bila ya kumuogopa mtu yeyote. Kwa upande mwingine, kutothibitisha jambo kama hilo husababisha papatiko na mateso, haswa wakati wa matatizo. Matokeo yake, hii inaweza hata kusababisha mtu kufikiria vibaya juu ya qadhaa ya Mwenyezi Mungu, badala ya kuwa mvumilivu juu ya hilo.

Mwenyezi Mungu (swt) alifafanua hili kwa Maswahaba (ra) wa Mtume (saw) baada ya wao kurudi nyuma kwenye Vita vya Uhud baada ya kusikia uvumi wa kifo cha Mtume (saw). Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 (ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَى طَآئِفَةً مِّنكُمْ وَطَآئِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللّهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الأَمْرِ مِن شَيْءٍ قُلْ إِنَّ الأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّهِ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لاَ يُبْدُونَ لَكَ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَى مَضَاجِعِهِمْ وَلِيَبْتَلِيَ اللّهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحَّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ وَاللّهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ)

“Kisha baada ya dhiki alikuteremshieni utulivu - usingizi ambao ulifunika kundi moja kati yenu. Na kundi jengine nafsi zao ziliwashughulisha hata wakamdhania Mwenyezi Mungu dhana isiyo kuwa ya haki, dhana ya kijinga. Wakisema: Hivyo tuna lolote sisi katika jambo hili? Sema: Mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Wanaficha katika nafsi zao wasiyo kubainishia. Wanasema: Lau ingelikuwa tuna lolote katika jambo hili tusinge uliwa hapa. Sema: Hata mngeli kuwa majumbani mwenu, basi wangeli toka walio andikiwa kufa, wakenda mahali pao pa kuangukia wafe.(Haya ni hivyo) ili Mwenyezi Mungu ayajaribu yaliyomo vifuani mwenu, na asafishe yaliyomo nyoyoni mwenu. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo vifuani.” [Aali-Imran: 154]

Katika aya hii, Mwenyezi Mungu (swt) anasimulia maombolezo ya Wanafiki ambao hawakuweza kuvumilia hasara zao kwenye Vita vya Uhud na wakaanza kumfikiria Mwenyezi Mungu vibaya kwa wazo la ujinga. Yeye (swt) pia aliwafafanulia Wanafiki kwamba hata kama wasingeondoka kwenda kupigana, kifo kitawajia kama ilivyopitishwa. Mwenyezi Mungu (swt) kisha akawashauri waumini katika aya zifuatazo wasiwe kama wale wanafiki ambao walilalamikia hasara zao kwenye Vita vya Uhud. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ لاَ تَكُونُواْ كَالَّذِينَ كَفَرُواْ وَقَالُواْ لإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُواْ فِي الأَرْضِ أَوْ كَانُواْ غُزًّى لَّوْ كَانُواْ عِندَنَا مَا مَاتُواْ وَمَا قُتِلُواْ لِيَجْعَلَ اللّهُ ذَلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ وَاللّهُ يُحْيِـي وَيُمِيتُ وَاللّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ)

“Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio kufuru na wakawasema ndugu zao walipo safiri katika nchi au walipo kuwa vitani: Wangeli kuwa kwetu wasingeli kufa na wasingeli uwawa. Ili Mwenyezi Mungu afanye hayo kuwa ni majuto katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu huhuisha na hufisha. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona myatendayo.” [Aali-Imran: 156]

Katika aya hii Mwenyezi Mungu aliwakumbusha waumini kwamba Yeye (swt) ndiye anayetoa uhai na mauti ili nyoyo zao zipate raha na kuridhika na yale alivyopitisha Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo fahamu ya Ajal huwafanya waumini wabaki imara katika kutii amri za Mwenyezi Mungu bila kugeuza migongo yao hata katika mazingira ya kutishia maisha, kama vile kupigana na adui na kusema neno la ukweli dhidi ya watawala madhalimu na mengineyo.

Shariah ndicho kipimo cha matendo ya Waislamu

Ijapokuwa Sharia imeruhusu kuziacha baadhi ya Hukmu za Sharia chini ya dharura (haja) kama hali za kutishia maisha, njaa kali inayosababisha kifo, ruhusa hii haikuja kwa 'jumla' kuacha majukumu yote kwa kisingizio cha 'Dharura'. Badala yake, kila hali inahitaji dalili maalum ya kuruhusiwa na sharia kuziacha Hukmu za Sharia. Kwa mfano, katika aya ifuatayo,

 (فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيْرَ مُتَجَانِفٍ لِّإِثْمٍ فَإِنَّ اللّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ)

“Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.” [Al-Ma’ida: 3].

Ruhusa hapa ni kula tu vitu vilivyokatazwa kwa sababu ya njaa kali ambayo itasababisha kifo. Lakini, ruhusa hii haiwezi kujumlishwa kuruhusu vitu vyote vilivyokatazwa kwa kisingizio cha 'haja', sembuse hali zinazodhaniwa za kutishia maisha kama Covid-19, ambapo hali ya maambukizi inatumiwa kama kisingizio cha kuachana na wajibu wa kusimamisha swala za jamaa na Ijumaa Misikitini. [3] Baya zaidi ni hali ya watu, ambao wanaweza kuzuia vitisho vya serikali dhalimu, na wanaendelea kuachana faradhi za Mwenyezi Mungu kwa kisingizio cha hali ya maambukizi ya virusi hivi, wakiogopa kifo wakati ugonjwa huu sio hatari kama magonjwa mengine ya maambukizi. Kinyume chake, fahamu ya Ajal inapaswa kuwakumbusha Waislamu kutopuuza maagizo ya Mwenyezi Mungu hata wakati wa hali za kutishia maisha. Badala yake, inapaswa kuwashajiisha Waislamu kufuata utiifu wao kwa Mwenyezi Mungu hata katika hali za kutishia maisha. Miongoni mwa hali hizo ni 'mapigano ya lazima' katika njia ya Mwenyezi Mungu ambayo tishio la maisha haliepukiki na kwa hivyo kurudi nyuma kutoka katika uwanja wa vita kunachukuliwa kama dhambi kubwa. Mwenyezi Mungu (swt) anasimulia hadithi ya watu ambao waliondoka nyumbani kwao bila kupigana na adui, wakati walikuwa na uwezo wa kupigana na wengi kiidadi, ili kuwatia moyo Waislamu wasipuuze amri zake, haswa 'mapigano ya lazima'. Mwenyezi Mungu (swt) alichukua roho zao na kuziregesha ili kuthibitisha kuwa ni Mwenyezi Mungu Anayehuisha na kufisha. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 (أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ خَرَجُواْ مِن دِيَارِهِمْ وَهُمْ أُلُوفٌ حَذَرَ الْمَوْتِ فَقَالَ لَهُمُ اللّهُ مُوتُواْ ثُمَّ أَحْيَاهُمْ إِنَّ اللّهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَـكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لاَ يَشْكُرُونَ)

“Hukuwaona wale walio toka majumbani kwao kwa maelfu kwa kuogopa mauti? Mwenyezi Mungu akawaambia: Kufeni! Kisha akwahauisha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini wengi wa watu hawashukuru.” [Al-Baqarah: 243]

Katika aya hiyo hapo juu, maelezo ya watu kuwa maelfu (yaani juu ya elfu kumi) yanaonyesha uwezo wao wa kupigana na waliogopa kifo kupuuza amri za Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hivyo Mwenyezi Mungu (swt) alichukua nafsi zao na kurudisha uhai kwao ili kuonyesha kuwa ni Mwenyezi Mungu ndiye ambaye anahuisha na kufisha. [4]

Hofu ni katika umbile asili la wanadamu; lakini, haitokei isipokuwa kwa uwepo wa kitu kinachoichochea. Hofu ni moja ya matatizo hatari ambayo kwayo watu na taifa dhaifu husibiwa na kubakia nyuma.

Hofu ni hatari na ni haribifu katika baadhi ya hali ilhali ina faida na inafaa katika hali zingine. Ikiwa hofu itachochewa na msingi au hali mbaya, kama hofu ya kifo au madhara yoyote ambayo husababisha kuacha majukumu (isipokuwa kwamba Sharia iwe imeruhusu), basi hofu hii inapaswa kutibiwa na kuondolewa, huku ikiwa imechochewa kutokana na hali sahihi na inayohitajika hiyo lazima ishajiishwe. Kwa hivyo, Waislamu lazima waogope kwa msingi na hali sahihi, kama hofu kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu ambayo huwashajiisha Waislamu kukaa mbali na makatazo ya Mwenyezi Mungu (swt) na kutimiza majukumu.

Hofu ya kifo kutokana na ugonjwa haifai kwa Waislamu. Hofu hii ni mbaya kwa sababu magonjwa sio sababu ya kifo lakini ni mwisho wa Ajal (uhai). Itikadi ya usekula (yaani utenganishaji dini na dola) iliwasukuma watu kwa fikra na kaulimbiu kama "Furahiya maisha unayoishi mara moja tu", "Ishi maisha yako moja kwa njia unayotaka wewe". Kwa hivyo maisha haya ya kidunia ndio kipaumbele kwao na janga hili limewatia wazimu kwa sababu ya kuogopa kifo, kwani kifo hiki kinasimamisha raha yao yote. Lakini kwa yule anayeamini itikadi sahihi (yaani Uislamu) na anamiliki shakhsiya wa Kiislamu, anaishi katika ulimwengu huu kama msafiri bila ya kupuuza mahitaji yake ya kidunia na bila ya kusahau kuhusu maisha yake ya baadaye. [5]

Urasilimali wa Kisekula hauzingatii Thamani ya Kiroho katika jamii

Tumeona Misikiti ikifungwa wakati wa janga hili la maambukizi kwa kisingizio kwamba mkusanyiko wa wenye kuabudu katika Misikiti ungeeneza virusi. Lakini inajulikana vyema kuwa shughuli za kiuchumi ziliruhusiwa; badala yake, kulikuwa na maendeleo ya kiteknolojia yaliyoletwa ili kuongeza shughuli za kiuchumi ambazo zilisababisha kuongezeka kwa ununuzi mtandaoni, hata vileo viliruhusiwa chini ya maagizo ya mtandaoni kufikisha bidhaa hadi milangoni kulingana na agizo la mahakama katika baadhi ya majimbo nchini India. Tofauti hii dhahiri kati ya kuboreshswa katika shughuli za kiuchumi na kufungwa  kwa misikiti inathibitisha ukweli kwamba mfumo wa urasilimali humtazama mwanadamu kama kiumbe wa kimada (kupenda mali), asiye na mahitaji ya kiroho na malengo ya kiakhlaqi. Urasilimali haujali kuasisi akhlaqi katika jamii wala kuwa na wasiwasi juu ya mwinuko wa kiroho, yaani, kuweka utambuzi wa uhusiano wa mwanadamu na Mwenyezi Mungu (kutambua uwepo wa Mwenyezi Mungu), msukumo ulio nyuma ya mahusiano yote ni kwa ajili ya kupata radhi za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo shughuli za ibada katika misikiti zimetengwa au zimepuuzwa kabisa, ambapo hili lilikuwa wazi katika maagizo ya serikali za kisekula katika nchi za kirasilimali; kibaya zaidi ni kwamba hata nchi zingine za Kiislamu zilifunga misikiti kwa kufuata nyayo za Magharibi. Kuna kampuni za kirasilimali na Maafisa Wakuu Watendaji waliongeza utajiri wao wakati wa janga hili kwanilengo lao msingi kuongeza thamani halisi na thamani ya kampuni. [6]

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika aya hii:

 (أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ * حَتَّى زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ * كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ * ثُمَّ كَلَّا سَوْفَ تَعْلَمُونَ * كَلَّا لَوْ تَعْلَمُونَ عِلْمَ الْيَقِينِ * لَتَرَوُنَّ الْجَحِيمَ)

“Kumekushughulisheni kutafuta wingi* Mpaka mje makaburini!* Sivyo hivyo! Mtakuja jua!* Tena sivyo hivyo! Mtakuja jua!* Sivyo hivyo! Lau mngeli jua kwa ujuzi wa yakini* Basi bila ya shaka mtaiona Jahannamu!.” [At-Takaathur: 1-6)]

Ibada hutajwa kama hukmu zisizo badilika (Tawqifiyyah)

Kimsingi, matendo ya Ibada hayana sababu za hukm yake (kwenye shina lake) na hakuna qiyas unaoweza kufanywa kwenye hukmu isipokuwa andiko liwe na illah (sababu ya kisheria) yake. Ufungaji wa Msikiti, uwekaji masafa katika sala, kupeana michango kama badali ya udhiya (kichinjo) ni baadhi ya rai za kushangaza ambazo zimekuja katika nyakati za hivi karibuni kwa sababu ya janga la maambukizi. Katika fatwa nyingi, hali au uhalisia ulikuwa umechukuliwa kama chanzo cha kutoa maoni, lakini uhalisia au hali ni lazima ichunguzwe na kwa ajili ya dalili ya hukmu Shariah (yaani Quran, Sunnah, Ijma As-Swahaba na Qiyas) lazima ichunguzwe ili kuvua hukmu. Makosa makubwa katika rai hizi ni kutoa sababu (kutafuta Illah) kwa hoja kama "ustawi wa jamii". Ni hatari sana kutafuta sababu na manufaa kutoka kwa ibada; badala yake, Ibada ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee kupata radhi Yake ambayo inapaswa kufanywa kulingana na Sunnah na sio kulingana na manufaa au ustawi wa jamii. Hizi pia zinatajwa kuwa hukmu za tawqifiyah ambapo hukmu huvuliwa kutoka kwa andiko na sio kutokana na qiyas. Kufunga misikiti na masafa ya kijamii katika swala ni haram na Bidah mtawaliwa ambayo dhambi lake liko juu ya mtawala anayelazimisha sheria hii. [7] Kuhusiana na udhiya, ni hukmu iliyothubutu sawasawa; kuna maelezo ya hukmu yanayopaswa kufuatwa wakati wa kumchinja mnyama. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(لَن يَنَالَ اللَّهَ لُحُومُهَا وَلَا دِمَاؤُهَا وَلَكِن يَنَالُهُ التَّقْوَى مِنكُمْ كَذَلِكَ سَخَّرَهَا لَكُمْ لِتُكَبِّرُوا اللَّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَبَشِّرِ الْمُحْسِنِينَ)

“Nyama zao hazimfikii Mwenyezi Mungu wala damu zao, lakini unamfikia uchamngu wenu. Namna hivi tumewadhalilisha kwenu ili mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa alivyo kuongoeni. Na wabashirie wafanyao mema.” [Al-Hajj: 37]

Aya hiyo hapo juu inaonyesha wazi kuwa tendo la udhiya ni ibada kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pekee Mwenyezi Mungu hana haja ya nyama wala damu bali uchaji wa kweli.

Hitimisho:

Mwenyezi Mungu (swt) ameumba uhai na mauti ili kuwajaribu wanadamu ni nani walio bora katika matendo yao; hakika, matendo yanategemea mawazo na mwelekeo ambao mtu anayo. Itikadi ya kisekula ya kirasilimali na mfumo wake imeunda fikra za watu wasio na hitajio la kiroho, wanaolenga tu starehe za kidunia kwa kupuuza maisha ya akhera. Uislamu, baada ya kuwakinaisha wanadamu kwa itikadi yake ya kweli, iliojengwa juu ya msingi wa kiroho. Inawalazimisha Waislamu kutabanni fahamu maalum kama kumtii Mwenyezi (swt) na kumwabudu Yeye peke yake ili kupata radhi Yake. Yeye ndiye mwenye kuhuisha na kufisha kwa muda uliowekwa. Fahamu ya Ajal inawashajiisha Waislamu kufuata utiifu kwa Mwenyezi Mungu, bila ya kutoa visingizio ambavyo sio halali kwa mujibu wa sharia ili kukiuka amri za Mwenyezi Mungu. Kwa ufahamu huu thabiti, Waislamu watakuwa katika raha na kuridhika na qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) katika hali ngumu, kama janga hili la maambukizi, na wataendelea kuzitii amri za Mwenyezi Mungu bila kumwogopa yeyote ila Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad bin Farooq

Maregeleo:

1) https://www.siasat.com/covid-times-jamia-nizamia-issues-fatwa-on-eid-ul-adha-sacrifice 1918920/

2) Shakhsiya Islamiyya (Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu 1- ‘Ajal ndiyo sababu pekee ya Mauti, Machapisho ya Hizb ut Tahrir)

3) Q/A- “Msingi: La Haramu Huruhusiwa Kutokana na Dharura” na Sheikh Ata Bin Abu Khalil Rashtah (Hz), 16 Rabii’ II 1437 H, 26/1/2016 M.

4) Usherehesho wa “Taysir Fi Usuli Tafsir” kwa Aya 2:243.

5) Fikra ya Kiislamu – Hofu (Khawf), Machapisho ya Hizb ut Tahrir

6) Nidhamu ya Uchumi katika Uislamu – Utangulizi wa Nidhamu ya Uchumi, Machapisho ya Hizb ut Tahrir

7) http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/qestions/jurisprudence-questions/19635.htm

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 29 Septemba 2020 16:30

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu