- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hotuba ya Tunisia katika Kongamano: ‘Vijana Waislamu…Waanzilishi wa Mabadiliko Msingi’
Tahadhari ya Kijana Muislamu Mwanzilishi wa Mabadiliko Halisi
(Imetafsiriwa)
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Bwana wa Walimwengu, na swala na salamu zimshukie Mtume Mtukufu Mteule na familia yake, maswahaba zake na wale wanaomfuata kwa ihsani hadi Siku ya Malipo. Mola wetu, tusamehe dhambi zetu, tupe afueni kutokana na mitihani yetu, tulinde na hofu zetu na tujaaliye miongoni mwa waja wako watakatifu na wenye ikhlasi; ambao hawakiuki mipaka wala kudhulumu. Mola wangu, nifungue kifua changu, na unifanyie wepesi jambo langu, na ufungue fundo katika ulimi wangu na kauli yangu ifahamike.
Dada zangu waheshimiwa, nawaamkua kwa maamkizi ya Uislamu, As-Salaamu Alaikunna Wa Rahmatullahi Wa Barakaatuhu, jumuiko lenu na kukusanyika kwenu huku kubarikiwe na natoa shukrani zangu kwa kila mmoja aliye itikia mwaliko huu na kila aliye chukua nafasi ya kufanikisha mkutano huu…
Vijana wanawakilisha dhihirisho la nishati na ubunifu, ni kichwa cha utoaji na kilicho chonjo. Lakini, vijana wanateseka leo kutokana na uhalisia mchungu na wakuhuzunisha, usimamizi mbaya na kutelekezwa, na kutokana na ukosefu wa uwakilishi wa matarajio yao kama vijana Waislamu wanaotaraji kuregesha ubwana wao, ardhi yao iliyo nyakuliwa na rasilimali zilizo fujwa.
Mkoloni amefanya kazi kwa takriban karne moja kumtia umagharibi kijana wa Kiislamu, ili kumfanya awe na shaka na kukinai kwake na utambulisho wake. Na mkoloni huyu aliivunja Khilafah na kuchagua kikundi kukielimisha na kukilea kwa fahamu za kimagharibi. Kisha wakakitumia kushambulia Uislamu na kulingania ukombozi kutokana na fahamu zote ambazo Ummah umelelewa na kuelimishwa nazo. Hii ni ikiongezewa na kujisalimisha kwa fikra kuwa maendeleo na ufanisi kamwe hayawezi kutokea isipokuwa turathi jumla ya kifikra ya Kiislamu ishambuliwe na ikifuatiwa na kuikimbilia hadhara ya kimagharibi pamoja na viungo vyake vyote. Na hivyo basi vijana wakachanganyikiwa na fikra hizi zenye sumu zilizo legeza ghariza zake na kuvifanya vipimo vyake kuwa kupata maslahi huku akiondoa Aqeedah ya Kiislamu kuwa msingi wa fikra yake. Hii ilisababisha kuyumba kwa utambulisho (shakhsiya) wa kijana Muislamu ambapo hamasa zake zingeamshwa kupitia miito duni, kama vile uhuru miongoni mwa mengineyo, na kuzalisha vitambulisho visivyokuwa na utulivu. Kisha serikali zilizoko mamlakani zilitenganishwa kutokana na majukumu yote kwa madai kuwa vitambulisho hivi vilikuwa ni natija ya kimaumbile ya mabadiliko ya kimwili ambao waliuita umri wa ubarobaro au utineja. Wanabeba lawama kwa kufeli kwao kiakili katika rika hili na fikra zao, ambapo imesababisha mateso na msongo wa mawazo.
Na hili wala si geni kwa yule aliyecheza kamari kwa kuushambulia Ummah wa Kiislamu ili kujibunia cheo chake miongoni mwa mataifa. Si geni kwa juhudi za papatiko kufanywa ili kupata lengo lake. Hii hapa ni miongoni mwa taarifa zilizo chaguliwa zinazo ashiria nia za wakoloni: “Kikombe na msichana mrembo vinafanya kazi pamoja kuuangusha Ummah wa Muhammad zaidi kuliko vile ambavyo bunduki zingefanya”. Na hivyo basi wamezificha ndani ya mapenzi kwa mali za kimada na matamanio.
Na pindi Magharibi ilipopata dhamana kutoka kwa serikali hizo kuwa zimezika shingoni mwa Waislamu ambao wanabeba ajenda zao, waliridhika na makao (waliyopewa) ili kuwatelekeza vijana ndani ya mpangilio fisidifu wa elimu, muundo mbovu wa kiuchumi na muundo uliofeli wa kiutumwa wa kisiasa. Vijana hatimaye walijipata ndani ya hali ya mateso wasijue jinsi ya kujitoa kutokana nayo.
Wakati huo huo, katika miongoni mwa Mashabab kuna kikundi kibunifu ambacho wakoloni wanaridhika kukiruhusu kuhamia nchi zao na kuwafanyisha kazi ndani ya maabara zao. Tutawasilisha baadhi ya takwimu kama mfano mdogo wa uhalisia huu. Kwa mujibu wa Shirikisho la Kiarabu, asilimia 50 ya madaktari na asilimia 23 ya wahandisi kutoka maeneo jumla ya Kiarabu huelekea Ulaya huku asilimia 54 ya wanao kwenda huko kusoma hawarudi nchini mwao. Na kutokana na ripoti ya serikali kuhusu uhamiaji katika mwaka wa 2012, wanafunzi elfu 57 kutoka Tunisia huhamia nchi za kigeni huku kiwango cha wanaorudi kikiwa si zaidi ya asilimia 10. Idadi ya wafanyi kazi wanaohamia kutoka Tunisia ikiwa ni 83,529, huku pia ikitajwa katika ripoti nyengine kupitia Idara ya Makao na sera za Uhamiaji katika Chuo Kikuu cha Arab kuwa Waarabu hupoteza dolari bilioni 1.57 kila mwaka kutokana na uhamaji wa akili au mabongo.
Na katika vijana ni wale wanaojipata wamekwama katikati ya lindi la ukosefu wa ajira, uhalifu na uhamiaji huku wakiokoka kutoka katika janga moja na kutumbukia katika janga jengine ambalo hata ni baya zaidi. Hiyo ni kwa sababu Magharibi imetabanni sera yake ya kutoa makao na kufurusha kwa mujibu wa mahitaji yake.
Katika kiwango cha Maghribi (yaani Morocco, Algeria na Tunisia), idadi ya vijana inafikia takriban nusu ya wakaazi. Wengi wao wako nje ya soko la ajira na wengi wao wangali waseja na wanawategemea baba zao kusimamia mahitaji yao ya kimaisha. Na inashangaza kuwa katika kila eneo kuna wizara inayoitwa ‘Wizara ya Vijana’ lakini ambacho hakishangazi ni kuwa wizara hizo hazijaleta manufaa yoyote, na hiyo ni kwa sababu ndio sifa yao kutoa sura isiyo na thamani ya kihakika.
Ama kuhusu taasisi za kielimu, zinawakilisha nafasi wazi ya kuwapiga muhuri vijana kwa maadili na masrufu yao. Zinafanya kazi waziwazi kudhamini uzalishaji wa wawakilishi wanao hudumia maslahi ya wenye ushawishi ndani ya mujtama na haswa wakoloni na wasaidizi wao. Maalumati ya kielimu yaliyo fafanuliwa katika mipango na mitaala bila ya kusitasita ni feki ingawa kuna wito wa mageuzi, kwa kuwa kimsingi yanazunguka pambizoni mwa mabadiliko bandia kuhusiana na nyakati, nafasi ya shule na mbinu zilizo tabanniwa.
Kwa hivyo Tunisia, kwa mfano, wanadai kuwa wanafanya mabadiliko ya elimu huku wakitumia juhudi na pesa zao kusambaza amali na vilabu vya kithaqafa, kwa mujibu wa kisingizio chao. Lakini ni thaqafa ipi wanayo zungukwa nayo? Michezo inayoitwa ya kiini macho na uchezaji densi wa muziki wa kelele iliyokosa alama za aibu na heshima ambayo yalipaswa kutekelezwa kama thamani muhimu zaidi na kujengwa ndani ya thaqafa ya yule anayekulia. Vipi watawajibika kwa ajili ya mipango ya kielimu wakati ambapo hawajapewa idhini? Hakika, wanasubiri marekebisho kutoka kwa wale walio waajiri.
Ndani ya hali hii mbaya kwa vijana, vyama na mashirika yameendesha usajili, yakitoa wito kwa Mashabab/vijana kuwa kiungo muhimu na chenye athari katika mchakato wa mageuzi kama wanavyouita. Yakisaidiwa kinidhamu na vyombo vya habari kwa hofu kuwa mageuzi msingi na sahihi yatatokea mikononi mwa watoto wa Ummah walio na ikhlasi.
Kuongezea haya ni vyama vya kigeni vinavyo fanya kazi chini ya kichwa “Viongozi wa mustakbali” ambavyo vinawavutia vijana na kuwakuuza kwa thaqafa ya kimagharibi kwa kutumia miundo ya kuvutia. Vinawatafuta wale wanaomiliki sifa za uongozi ili kuwahusisha katika hali za kutatanisha na kisha kujadiliana nao hadi wawe ni sauti zao na vibaraka mikononi mwao.
Ndani ya uhalisia huu, kumekuweko na utafiti mwingi unaoendelea kuhesabu sababu za kutelekezwa vijana na maadili yao yaliyooza. Lakini, wameikosa nukta pindi walipo pendekeza kuwa ni kutokana na kuvunjika kwa familia, au ukosefu wa elimu, au kufungiwa au dhurufu zake za kimada. Maelezo yote waliyo yataja sio sababu wala vyanzo bali zina wakilisha natija ya mateso. Chanzo msingi ni utawala wa Kimagharibi juu yao unaotumia ala za kieneo kwa sura ya serikali vibaraka mtawalia zinazo fuata amri ya Magharibi na kutabikisha njama zake.
Lakini, hata kama wanajaribu kuwatia umagharibi, licha ya hayo wangali ni vijana Waislamu ambao mtazamo wao unachipuza kutoka katika Aqeedah yao. Hivyo basi katika kura za takwimu zilizo fanywa na kikao cha Magharabi, kutokana na sampuli jumla ya vijana asilimia 79 wanakubaliana na wajibu wa kutabikisha Shari’ah kama nidhamu ya maisha huku wale wanaounga mkono vazi la kisheria la mwanamke wakiwa ni asilimia 95.
Mapinduzi ya vijana nchini Tunisia ni dalili nzuri zaidi ya kuthibitisha mwamko wao. Yalikuwa ni mapinduzi yaliyo washtua wakoloni na washirika wao, tawanya makaratasi yake na kukanganya mipango yao. Yangesambaa kote katika ulimwengu wa Kiislamu lau si kwa vibaraka hao kuwasaidia Wamagharibi kuyavuruga na kuyapoteza njia.
Sasa vipi vijana watakuwa waanzilishi wa mabadiliko kama walivyo kuwa wakati wa zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)? Historia ya Kiislamu imejaa mifano yenye kuishi milele kuhusiana na vijana wanaounga mkono kadhia zao nyeti na kushiriki katika kuunda serikali. Kwa hivyo kama ambavyo kazi ya kuongoza jeshi ilipewa vijana, uzito wake kuhusiana na uwajibikaji, na uongozaji swala, uandikaji Wahyi na mamlaka ya mahakama, yanapaswa kutafutwa na wao ili leo wawe kama walivyo kuwa zamani. Mtume (saw) asema: «أوصيكم بالشباب خيراً، فإنهم أرق أفئدة... لقد بعثني الله بالحنيفية السمحة... فحالفني الشباب وخالفني الشيوخ» “Nawahusieni kuwatendea wema vijana. Kwani wao ni wenye nyoyo nyepesi mno…hakika Mwenyezi Mungu amenitumiliza kwa Al-Haneefiyah As-Samhah… Vijana wakashirikiana nami na wazee wakanipinga”.
Na yeye (saw) asema: «سبعة يظلهم الله في ظله يوم لا ظل إلا ظله إمام عادل، وشاب نشأ في عبادة الله...» “Watu aina saba Mwenyezi Mungu atawafinika na kivuli chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa chake yeye: kiongozi muadilifu, na kijana aliyekulia katika ibada ya Mwenyezi Mungu …”. Hivyo basi, ni muhimu kwa vijana kuwa viongozi wa dola na sio tu matineja au mabarobaro kwani umri wao unapaswa kuzingatiwa kuwa ni ule wa kufikia ukomavu unao andamana na mabadiliko ya nguvu na mabadiliko ya kiakili. Huku pia umri huu ukikadiriwa kuwakilisha mwanzo wa majukumu na huhesabiwa katika hali ambayo nguvu ya Uislamu itachanganyika na nguvu na uwezo wa umri wa ujana ili kuzalisha viongozi wakubwa na waanzilishi wa mabadiliko.
Na ili vijana wakuzwe katika ibada ya Mwenyezi Mungu, utawala wa wakoloni ni lazima ung’olewe kutoka kwa Waislamu na hilo halitatokea isipokuwa kwa kuangushwa serikali iliyo watawala juu yao. Halitatokea kupitia kubadilisha nyuso kwa nyuso nyenginezo au kupitia kubadilisha vifungu vya katiba kwa vifungu vingine vilivyo tungwa na wanadamu mithili yake. Bali litatokea pekee kwa kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo nidhamu yake inachipuza kutokamana na Aqeedah ya Ummah huu.
Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُم بِالْحَقِّ إِنَّهمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هدًى] “Sisi tunakusimulia khabari zao kwa kweli. Hakika wao walikuwa ni vijana walio muamini Mola wao Mlezi. Na Sisi tukawazidishia uwongofu” [Al-Kahf: 13]. Sadaqallahul-Adheem.
Kwa hivyo musiwaegemee wale wanao wadhulumu na kuwatuhumu kutokuwa na uwezo, kuwa walegevu na kutokuwa na utulivu. Kama walivyokuwa wale kabla yenu – wanaume walio unda izza ya Ummah huu na hadhara yake, na kuilinda Dini hii, ardhi na heshima, nyinyi pia muna nguvu kuhusiana na Dini yenu na Ummah wenu, iliyo angazwa kupitia Aqeedah yenu, kuitikia mwito wa Dini yenu na kufanya kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu, yatakayo rekebisha hali ya watu na kumridhisha Mola wao.