Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuamiliana na Ulimwengu Huku Nyoyo Zetu Zikimuona Mwenyezi Mungu (swt)

(Imetafsiriwa)

“Kila pumzi yako ni kito chenye thamani kubwa mno, kwa kuwa kila moja haina mbadala, na mara iondokapo, haipatikani tena. Usiwe kama wajinga wanaohadaiwa ambao huwa na furaha kwa sababu kila siku utajiri wao unaongezeka huku maisha yao yakipungua. Kuna uzuri gani katika kuongezeka utajiri wakati maisha yanazidi kuwa mafupi? Kwa hivyo uwe na furaha kwa kuongeza maarifa au kazi njema, kwa kuwa ni wenzi wako wawili watakaokuwa nawe kaburini kwako wakati familia yako, mali, watoto na marafiki watabaki nyuma.” (Imam Al-Ghazali).

Katika dunia ambapo maisha ya tamaa ya vitu, moja ya mazao yenye sumu ya Urasilimali, imekuwa ni kipimo cha kupima mafanikio ya mtu katika maisha haya, kina cha ujumbe wa hapo juu ni kikuu sana. Unamsaidia yule anayeusoma kufahamu mara moja lengo lake la kweli katika dunia hii kwa kuwa unatueleza kuwa maisha haya bila shaka yatamalizika na kwamba vile ambavyo tumeishi katika safari hii ya kupita itaamua namna gani tutaweza kufanikiwa katika maisha ya Akhera.

Ili kupata mafanikio haya hatuna budi kufahamu sababu ya sisi kuishi maisha haya. Mwenyezi Mungu (swt) ametuumba sisi na ulimwengu uliotuzunguka ili tuishi hapa kwa kipindi maalum. Hakutuacha wapweke bali ametuletea mwongozo kupitia Mitume pamoja na Ujumbe Wake. ametuelekeza maisha tunayopaswa kuishi lakini ametuwacha huru kuamua ima kufuata uongofu huo ama la. Akatuonya kuwa maisha haya yatapomalizika, tutarejea Kwake na itakuja siku ambayo Atatutambulisha mazuri na mabaya tulioyafanya wakati wa safari yetu na kwamba tutazawadiwa au kuadhibiwa kwa mujibu wa matendo yetu.

Kujielekeza juu ya lengo muhimu katika maisha haikuwa rahisi tokea kuanguka kwa Khilafah, ngao yetu kuu, utawala wa Kiislamu. Dola ilioweka mazingira ya Kiislamu na hifadhi miongoni mwa jamii kwa namna ambayo wale wanaoishi chini yake hukumbushwa juu ya lengo muhimu zaidi katika maisha kupitia kila kitu kinachowazunguka. Na ambapo kuna mazingira ya utii kwa amri za Mwenyezi Mungu (swt) na kujizuia na makatazo wakati wote huku kukifanywa hima ya kujifunga na matendo mema na kuepuka maovu. 

Hivyo nini kinaweza kutusaidia sisi kubaki tukilenga kupata radhi za Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa aya ifuatayo:

(إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَٰئِكَ هُم الْمُفْلِحُونَ * وَمَن يُطِعِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّهَ وَيَتَّقْهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ)

“Haiwi kauli ya Waumini wanapoitwa kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, ila ni kusema: Tumesikia na tumetii na hao ndio wenye kufanikiwa.” [Surah An-Nuur 24:51-52].

Wakati tukiishi katika jamii ilionyimwa uongofu wowote kutoka kwa Muumba na ambapo imekuwa vigumu kushikamana na Dini Yake, basi vipi tutamkumbuka Mwenyezi Mungu na kuwajibika kukamilisha maagizo Yake na kutobakia katika hali kama ilivyo?

Kwa hili, Mwenyezi Mungu (swt) ametupatia fikra nzuri ya Ihsan kutusaidia kufikia hili. Ihsan kwa Kiarabu inahusiana na neno la Kiingereza la uzuri, ukamilifu, au ubora. Linatokana na kitendo ‘ahsana’, lenye maana kufanya mambo kwa uzuri zaidi na kwa namna bora zaidi.

Mtume wetu mpendwa Muhammad (saw) ameeleza namna ya kufikia Ihsan katika hadithi ifuatayo:

Jibril aliuliza nini Ihsan. Mtume (saw) akajibu:

 «أَنْ تَعْبُدَ اللَّهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ» “Kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa humuoni basi Yeye anakuona”

Hili ni kama jambo jepesi, lakini wakati huo huo, ni kauli nzito. Nini maana ya kumuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba tunamuona?

Ukiwa na mazingatio kwa Mwenyezi Mungu (swt) wakati ukitekeleza jambo inakufanya uweze kuwa na utambuzi juu ya nafasi yako na Mwenyezi Mungu. Inamakinisha mahusiano yako na Mwenyezi Mungu (swt) kwa namna ambayo matendo yako yataambatana na matakwa Yake (maamrisho).

Taaliki juu ya tafsiri ya Ihsan kutoka Hadithi ya Jibril inaeleza: “Tendo halitoweza kuwa zuri kama litatendwa bila ya utambuzi wa Mwenyezi Mungu. Yeye ni kigezo cha uzuri, jambo jema na sahihi”.

Zaidi ya hayo, kushughulikia dunia hii wakati nyoyo zetu zikiwa na utambuzi wa uwepo wa Mwenyezi Mungu (swt) inatupa ufahamu ambao unatuchukua sisi zaidi ya mipaka ya dunia hii. Inanyanyua uelewa wa ukubwa wa Mwenyezi Mungu na kwamba kila kitu kiko katika uwezo Wake. Ufahamu huu ni nguvu isiovunjika inayompatia muumini Tawakkul. Inampatia muumini imani kwa Mwenyezi Mungu (swt) na matumaini katika Mipango Yake bila kujali nini kinatokea katika ulimwengu huu. Inatusaidia sisi kubaki tumejifunga na maamrisho yake kwa namna inayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt) katika hali zote.

(فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى ٱللَّهِ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلْمُتَوَكِّلِينَ)

“Na ukishakata shauri basi mtegemee Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaomtegemea”. [TMQ 3:159].

Vile vile, Ihsan, utambuzi wa uwepo wa Mwenyezi Mungu, utatufanya kujiamini katika kuushika Uislamu na kusimama nao. Tutaweza pia kuondokana na vipingamizi vya madhalimu na kufanya kazi kwa ajili ya kurejesha Khilafah ngao yetu kuu. Kama ilivyo Ihsan – utambuzi wa uwepo wa Mwenyezi Mungu (swt)  – huja utambuzi ulio nje ya ulimwengu huu na uelewa wa visivyoonekana. Hii itatusaidia kukubali kikamilifu kuwa Mwenyezi Mungu (swt) ndie mmiliki wa Rizki zetu na Ajal (muda wetu wa kuishi).

Imepokewa kuwa Khalid b. Ma’dan – Mwenyezi Mungu awe radhi naye – amesema:

“Hakuna mtu isipokuwa ana macho manne: mawili yapo kichwani mwake ambayo anaonea masuala ya maisha ya duniani, na macho mawili katika moyo wake ambayo anaangalia masuala ya Akhera. Hivyo pindi Mwenyezi Mungu (swt) anapotaka wema kwa mja wake, Anaufungua moyo wake, na hivyo anaona kile alichoahidiwa katika ulimwengu usioonekana. Hivyo anaepushwa kutokana na (adhabu) isiyoonekana kupitia (malipo kwa utiifu wake) yasiyoonekana.” [Al-Dhahabi, Siyar A’lam Al-Nubala’ 4:543]

#رمضان_والإحسان

#Ramadan_And_Ihsan#
#Ramazan_ve_İhsan

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu