Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ushindi wa Waislamu Utafuata kwa Kusimamishwa kwa Khilafah

(Imetafsiriwa)

(قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُّؤْمِنِينَ)

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini”

Kofi lililolengwa na wafungwa sita waliojikomboa kutoka gereza la Gilboa; kofi hili lenye nguvu lililofichua umbile la Kiyahudi na mfumo wake dhaifu wa usalama liliufurahisha Ummah wote wa Kiislamu. Furaha kubwa iliingia moyoni mwa kila Muislamu kwa kushindwa kwa Mayahudi mikononi mwa Mujahideen sita. Walisifu ushujaa, dhamira, ukomavu na uvumilivu wa Mujahidina hawa mashujaa. Muda mfupi kabla ya hapo, Ummah wa Kiislamu ulifurahishwa na kushindwa kwa Amerika mikononi mwa Taliban. Baada ya miaka ishirini, Amerika ilishindwa kijeshi dhidi ya harakati ya Taliban, na uvumilivu na uthabiti wa Mujahidina wa Afghanistan kwa kukataa kwao kujisalimisha chini ya uvamizi wa Amerika, kitu ambacho kinathibitisha Umma wa kiislamu ni kama ulivyoelezewa na Mtume (saw):

«مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى»

“Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuoneana huruma kwao, na kuoneana upole kwao ni kama mfano wa mwili; pindi kiungo kinaposhtakia maumivu, mwili mzima huitikia kwa kukosa usingizi na homa.”

Kwa sababu vyombo vya habari vya Kiarabu havitaki Waislamu wawe kama Nabii wa Ummah (saw) alivyowaelezea kuwa kama mwili mmoja, kila aina ya tovuti za habari ziliangazia suala la wafungwa wa Palestina. Kwa ujumla, zilielezea magereza, kiwango cha kuimarishwa ndani na karibu nao, na hali ya kisaikolojia, mwili na afya za wafungwa wa Palestina.

Hapa tunauliza: Ni nani atakayewaokoa wafungwa hawa? Maelfu ya wafungwa, wengi wao wamehukumiwa kifungo cha maisha, na baadhi yao wanakabiliwa na magonjwa yasiyotibika, wakiwemo watoto, Ni nani atawaweka huru? na sio wao tu wanaotaabika kwa mateso ya walinzi wa jela, kwani ardhi iliyobarikiwa ya Palestina imechukuliwa na watu wake wote tangu kuvunjwa kwa Khilafah Uthmani, na Mayahudi waliletwa na kuikalia ardhi hii kutoka pembe zote za duniani, walikuwa wakiishi katika gereza kubwa, wakiteseka kama wafungwa waliofungwa katika magereza membamba, yenye minyororo ya uvamizi; ukosefu wa haki, uonevu, umasikini, kunyang’anywa ardhi, kubomolewa nyumba na kushambuliwa kwa matukufu na misikiti, mabaya zaidi ni mashambulizi na uvamizi ndani ya msikiti wa Al-Aqsa, masra ya Mtume (saw).

Watu wote wa Palestina wanatamani uhuru, na wanatamani kuikomboa kutoka kwa umbile la Kiyahudi. Katika kipindi cha miongo kadhaa ya kukaliwa kimabavu, watu wa Palestina wamekuwa thabiti na wamesimama madhubuti, wakiwa na silaha ya imani ya Kiislamu, wakiwa imara kama utulivu wa mlima katika milima, wakiwa na imani na ushindi wa Mwenyezi Mungu na kwamba unakuja bila shaka. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

(وَكَانَ حَقّاً عَلَيْنَا نَصْرُ الْمُؤْمِنِينَ)

 “Na ilikuwa ni haki juu yetu kuwanusuru Waumini.” [Surah Ar-Rum: 47]

Lakini uthabiti huu, kuwa na muendelezo, unahitaji nguvu ya silaha ili kuongeza nguvu ya uthabiti, na hivyo kuweza kuikomboa. Ni nani anayeweza kuikomboa kutoka mikononi mwa Mayahudi?, Na ni nani mwenye nguvu na uwezo wa kuwakomboa wafungwa na Msikiti?

Palestina ilikuwa chini ya uvamizi wa majeshi ya Msalaba kwa takribani miaka mia moja, na ukombozi ulikuwa mikononi mwa kiongozi shujaa Salah al-Din-Ayyubi wakati alipoongoza majeshi ya Kiislamu na nchi hii ikakombolewa.    

Ukombozi upo mikononi mwa majeshi ya Kiislamu, pindi tutakapo ongozwa na Khalifah wa Kiislamu, ambaye atanyanyua bendera ya Jihad na kuleta ukombozi si kwa Palestina pekee bali kwa nchi zote za Waislamu ambazo zinapata shida ya uonevu wa Makafiri na Washirikina, ambao utawala wao unafuata sheria na kanuni za kibinadamu ambazo haziendani sawa na kutofautiana na sheria za Kiislamu.

Hivyo basi, Waislamu wanatakiwa kuweka juhudi na utiifu wao ikiwa wanampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw) na kufanyakazi pamoja na wafanyakazi watiifu ili kurejesha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Hapo ndipo mapinduzi ya kweli yatakuwa yamepatikana, na itakuwa furaha kubwa ya ushindi, mapinduzi ambayo yatarejesha heshima na utu kwa Waislamu, ili Muislamu aweze kutembea katika nchi yake kwa amani na usalama, na sio kukimbizwa au kujificha kwa kuhofia kufanyiwa hiyana na kusalitiwa na wale waliouza nchi na vibaraka. Hakutakuwa na "uratibu wa usalama" au majasusi! na kama watapatikana, Khalifah wa Waislamu atasimama katika njia ya kila msaliti na kibaraka.

Enyi Waislamu! Toeni mnusuruni Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu atawanusuru na kuithibitisha miguu yenu, kuweni pamoja na Mwenyezi Mungu naye atakuwa pamoja nanyi.

Enyi Wanajeshi wa Kiislamu! Je, Nyinyi si Waislamu mnaomwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw)?! Je! nyoyo zenu hazitaki kuswali msikiti wa Al-Aqsa?! Watu wa Palestina wanawalilia, hamtaki kuwaitikia, kuwasaidia na kuwanusuru?

Je! Waislamu wana nani zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kisha nyinyi ambao mnaamini Imani ya Kiislamu, na mnayo nguvu ya vifaa vya kijeshi na vifaa vinavyojaza kambi zenu, Je! Hakuna mtu mwenye busara kati yenu?

Enyi Waislamu, Enyi Wanajeshi! Muitikieni Mwenyezi Mungu wakati anapowaita, kama vile Mwenyezi Mungu tukufu anavyosema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfal: 24]

Imeandika kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Um Asim Ataweel – Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu