Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Amerika Imekuwa Vipi Muathirika wa Hivi Karibuni Ndani ya Makaburi ya Himaya?

(Imetafsiriwa)

Dunia inaendelea kuiangalia Afghanistan huku wengi bado wakishangaa vipi uvamizi wa miaka 20 umeshindwa kwa kiasi hicho cha kustaajabisha. Kiwango cha Raisi wa Amerika cha kukubalika kwa wananchi kimekuwa cha chini kabisa wakati watu wengi wakiangalia maamuzi ya kuboronga ya Amerika kwa kuwaondoa wafanya kazi wake na kuwaacha wale waliofanya kazi pamoja na Amerika. Mara tu baada ya kuondoka kwa Amerika mnamo Agosti 15, 2021 shirika lenye utata la serikali ya Amerika, Afisi Maalum ya Inspecta Mkuu kwa ajili ya Kuijenga Upya Afghanistan (Office of the Special Inspector General for Afghanistan Reconstruction), au SIGAR ilichapisha uchunguzi wake wa miaka 13 katika mafunzo ambayo yanahitaji kuchunguzwa katika uvamizi na ukaliaji wa Afghanistan. Shirika hili liliwahoji mamia ya washiriki katika vita ambapo ilikusudiwa kubaini kushindwa kwa sera nchini Afghanistan. SIGAR ilifanya mahojiano kwa zaidi ya miaka 13 na waundaji sera kadhaa, wanajeshi, wanasiasa na wengineo ambao walishiriki katika vita nchini Afghanistan. Ufahamu huu umefichua mwanga kwa uvamizi wa Amerika nchini Afghanistan na kwa nini ulishindwa.

Wengi kati ya waliohojiwa walikuwa wawazi katika tathmini yao kwani walitegemea kutofichuliwa wazi kauli zao. Nyaraka za SIGAR zinaonyesha kuwa Amerika haikutambua kabisa nini ilikuwa ikifanya Afghanistan. Je wanajeshi walikuwa kwa ajili ya kupambana na Al-Qaida au kuigeuza Afghanistan kuwa nchi ya kidemokrasia ya kisasa ya Kimagharibi? Inaelekea kana kwamba misheni haikuwa imeundwa, ikiruhusu siasa za Amerika kuburutwa kwa miongo, bila kuwa na lengo la wazi, mbinu zilibadilika vile vile. Vikosi vilisukumizwa nchini kisha vikatolewa. Dolari za Amerika zilienezwa katika uchumi wa Afghanistan, zikitengewa idadi isiyokwisha ya miradi bila kuwepo mpango mpana, ikihifadhi kila dolari iliotengwa na Bunge la Amerika.

Kuhusu vita vyenyewe, wale walioshiriki na wale waliowapeleka wanajeshi wa Amerika vitani kulikuwa na jitihada za wazi na endelevu kwa serikali ya Amerika kuudanganya umma kwa makusudi. Maafisa jijini Kabul – na katika ikulu ya White House – walikuwa wakiharibu takwimu ili ionekane kuwa Amerika ilikuwa ikishinda vita na hali ya kuwa hali haikuwa hivyo. Wote waliohojiwa kwa ajili ya ripoti ya mwisho walikubali kuwa hakukuwa na mkakati licha ya matamko yaliotolewa kwa umma.

Wengi bado wanajaribu kufahamu vipi jeshi la Afghanistan lililofunzwa na Amerika, likidhaminiwa kifedha na silaha lilijisalimisha kwa haraka mnamo Agosti 2021. Amerika imejaribu kuibua jeshi kutoka kwenye majivu nchini Afghanistan. Miaka baada ya miaka, maafisa wa Amerika wameuhakikishia umma wa Amerika kuwa mpango ulikuwa ukifanya kazi na kuvipatia sifa vikosi vya Afghanistan. Lakini Amerika ilijaribu kuliunda jeshi kwa namna sawa na jeshi la Amerika, lenye kambi za kijeshi na miundo mbinu huku nchi ikiwa na miundo mbinu yake dhaifu, mwishowe jeshi lilibakia tu kwenye karatasi kwa kuwa wengi walihitaji kulipwa mishahara tu wakati uchumi ukianguka. Maafisa wengi pia waliunda wanajeshi hewa ili kujaza fedha mifukoni zilizotolewa na Amerika.

Barack Obama aliifanya Afghanistan kuwa ni kipaumbele chake kikuu katika kampeni yake. Aliamini kuwa Amerika imevipuuza vita halisi ilipovamia Iraq. Baada ya kufanya tathmini yake, aliamini kama mtangulizi wake kushinda vita na akamchagua David Petraeus na Generali Stanley McChrystal ili hatimaye kuibuka na ushindi nchini Afghanistan. Majenerali wote wawili walibuni mkakati wa kupambana na uasi ambao kwa kweli haukushughulikia suala husika. Mkakati wa kupambana na uasi ulikuwa ni sawa na uliojaribiwa mwaka 2004, lakini wakati huu ukiwa na kipote kidogo cha vikosi. Mpango wa McChrystal-Petraeus ulishindwa kutambua ima ni kupigana vita hasa Afghanistan, kushughulika na operesheni za amani, kuongoza mpango wa mafunzo, au kutekeleza kitu chengine. Licha ya kasoro hizi za wazi, Obama na serikali ya Amerika waliwaziba watu macho na kuutamkia umma kuwa mambo yalikuwa yanakwenda vizuri.

Wakati Donald Trump alipochukua uongozi wa ikulu ya White House licha ya mazungumzo yote juu ya mapigano, mkakati wake haukuwa tofauti na wa watangulizi wake na kitu pekee cha ziada kilikuwa ni uongo uliotumika kuhalalisha kubakia kwao nchini.

Ripoti ya SIGAR na msururu uliofuata wa (gazeti la) Washington Post wa nakala asili za zaidi ya kurasa 2,000 za mahojiano kwa watu 428 walioshiriki dori ya moja kwa moja katika vita unatoa uoni wa ndani kwenye vita vya Amerika nchini Afghanistan na orodha ya kushindwa pamoja na majigambo ya utekelezaji wa Amerika katika vita. Huku ripoti ya SIGAR ikiwa haiangazii kwenye malengo ya mikakati ya kwa nini Amerika imeivamia Afghanistan inatoa ufichuzi wa ufahamu wa namna Amerika imekuwa muathirika wa hivi sasa ndani ya makaburi ya Himaya (madola makuu).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu