Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Watoto Wanazaliwa Kufa kwa Njaa nchini Afghanistan bila ya Khilafah!

 (Imetafsiriwa)

BBC iliripoti mnamo tarehe 2 Disemba kwamba miundombinu inayoporomoka ya Afghanistan imesababisha kukaribia kutoweka kwa mfumo wa huduma za afya na ustawi wa jamii.

Madaktari wengi sasa wanafanya kazi bila malipo na janga la chakula limeongeza mzigo usio na kifani kwa hospitali zinazofurika wananchi wanaoteseka kutokana na hali mbaya ya umaskini.

Dkt Nuri daktari wa uzazi anayefanya kazi eneo la Afghanistan ya Kati aliripoti kisa cha mama mmoja ambaye aliomba mauti kabla tu ya kujifungua kwa upasuaji. Alikuwa akililia msaada bila kuelewa jinsi angeweza kumtunza mwanadamu mwingine wakati yeye mwenyewe alikuwa na utapiamlo sana hivi kwamba hangeweza kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto mchanga. Nukuu yake ni kama ifuatavyo; "Wodi ya wajawazito ni mojawapo ya wodi zenye furaha zaidi katika hospitali yoyote, lakini sivyo tena nchini Afghanistan, mnamo Septemba nilitazama watoto watano waliozaliwa wakifa kwa njaa. Ni kama kuzimu humu ndani."

Mgogoro huu mbaya ambapo Umoja wa Mataifa unanukuu watoto milioni 14 wako katika hatari ya njaa. Jumuiya ya Kimataifa imezuia ufadhili na misaada ya nje ili kuadhibu uongozi wa Taliban na hivyo kutumia fedha kama silaha ya vita dhidi ya Waislamu.

Dkt Siddiqi anayefanya kazi jijini Kabul alishuhudia watoto 4 walio chini ya miaka 10 wakifa kila wiki katika hospitali yake sio tu kutokana na maradhi yanayohusiana na udhaifu bali kwa kula sumu inayotokana na chakula duni.

Hili ni janga ambalo linatolewa kimkakati na mataifa ya kikoloni yanayosimamia uzuiaji wa utawala wa Kiislamu duniani. Kuwaweka watu kwenye ukingo wa mauti ni ala ya kuwazuia kufanya kazi kwa ajili ya mwamko wa Kiislamu. Lakini Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi kwamba daima kutakuwa na kheri katika Ummah Wake (swt). Kamwe hatuwezi kuweka chochote juu ya uwezo wa Mola wa walimwengu wote;

 (كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللّهِ)

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu...” [Aali-Imran 3:110].

Umaskini ulioratibiwa ni maagizo ya sawia yanayoweza kuonekana nchini Yemen, Syria na maeneo mengine muhimu ambapo udhibiti wa kisiasa ni muhimu mno kwa utawala wa Magharibi.

Wanachohitaji watoto wasio na hatia wa ulimwengu ni kiongozi wa kweli wa kuwakomboa kutokana na umaskini na ukosefu wa mgao wa rasilimali wa kulazimishwa. Amiri wa Khilafah angehakikisha mara moja kwamba mahitaji ya kimsingi yanatolewa kwa haki kwa wote bila ya hatari ya makusudi kwa mtoto au masikini hata mmoja. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Umma wa Muhammad (saw) ufanye kazi ili kuleta jambo hili kuwa ni jambo la dharura kubwa zaidi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammed

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu