Jumamosi, 11 Rajab 1446 | 2025/01/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nidhamu za Mahakama Zilizodorora Ndani ya Ardhi za Waislamu Zina Wafelisha Wanawake na Familia

Ummah wa Waislamu ni mmoja, lakini kivitendo tumegawanyika zaidi ya mataifa 50. Kila dola ina katiba yake na utekelezwaji wa Uislamu safi unatofautiana katika kila nyanja kuanzia kubwa hadi ndogo. Dola nyingi za Waislamu zinadanganya kuwa zinatekeleza Uislamu lakini zinatekeleza sheria zinazotokamana na akili za wanadamu. Kwani hivi sasa muundo wa serikali unafanyakazi ndani ya vitengo vya bunge, baraza la mawaziri na mahakama. Sheria zinazotungwa, zinazotekelezwa na kulindwa na taasisi hizi tatu ndiyo msingi wa maisha ya raia wanaoishi ndani ya dola. Jukumu la wanachama wa taasisi hizi ni kutunga, kutekeleza na kulinda sheria ambazo lengo lake ni kusuluhisha matatizo ambayo wanadamu wanakabiliana nayo kila siku. Lakusikitisha, taasisi hizi zenyewe zinaweza kuwa ni sehemu ya tatizo na huu ndiyo uhalisia tunaouona ndani ya ulimwengu wa Waislamu leo.

Hususan wanawake wanakabiliana na hali ambayo maisha yao yamejaa matatizo ambayo hayatatuliwi. Kila siku, wanawake wengi Waislamu wanakabiliana na matatizo ya ndoa za lazima. Pindi wanapoolewa, wanakabiliana na matatizo yanayohusiana na dhuluma za kinyumbani. Na wanapotaka kuvunjwa kwa ndoa, huwa ni mchakato mgumu. Wanawake wanaofaulu kupewa talaka au khula mara nyingi hukumbana na matatizo ya kurudisha haki yao ya mahari na mali za kibinafsi, au matatizo ya ulezi wa mtoto na uhifadhi. Matukio haya yakuvunja moyo yanaripotiwa kila siku katika magazeti ya kitaifa. Sababu za matatizo haya zinakinzana. Mashirika ya haki za binadamu wanalaumu maadili ya kidini na tamaduni. Lakini pindi matatizo yanapotokea, wanawake ambao hawawezi kuyatatua kupitia familia wanazielekea nidhamu za mahakama za dola.  Nidhamu za mahakama ndani ya nchi za Waislamu ambazo zimekitwa juu ya sheria za kisekula, hazihakikishi kuwa matatizo ya wanawake yametatuliwa kwa urahisi. Sheria na serikali zinatenda kazi kizembe kiasi kwamba wanawake wanapata shida kupata haki ya kusuluhishiwa matatizo yao.

Mnamo 2011, Express Tribune ilitoa ripoti kuhusu mwanamke wa Pakistan, Mai ambaye alishambuliwa na kuvunjiwa heshimiwa baada ya kaka yake mdogo aliposhtumiwa kuwa na mahusiano na mwanamke kutoka katika familia yenye mamlaka kijijini. Aliwapeleka wanaume hao mahakamani lakini 1 pekee alihukumiwa ilhali wengine waliachiliwa na Mahakama ya Chini. Mai alikata rufaa Mahakama Kuu na iliwachukua miaka 5 kumpatia uamuzi ambao ulikuwa sawa na Mahakama ya Chini.

Mfano wa uzembe wa mahakama na kuchukua muda mrefu katika kesi sio suala la kipekee wala sio tatizo la kipekee la mahakama katika nidhamu zilizopo. Kigezo chengine ni gharama za juu ambazo mtu wa kawaida hazimudu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo hiyo, familia iliyotafuta haki baada ya mtoto wao wa kike wa miaka sita aliyevunjiwa heshima iliwabidi kutumia Rupee 150,000 licha ya kuwa wanapokea msaada kutoka kwa Shirika lisilokuwa la Serikali la 'Vita dhidi ya Ubakaji.' Babake mtoto alikuwa anapokea Rupee 3,000 kwa wiki.

Nidhamu ya haki ndani ya Ulimwengu wa Waislamu iko polepole, ya kizembe na gharama mno. Kwa mujibu wa takwimu zilizojumuishwa na Tume ya Sheria na Haki ya Pakistan, kulikuwa na jumla kesi 1,954,868 mahakamani ambazo hazijatolewa uamuzi ndani ya nchi mwishoni mwa 2016. Kuchelewa kwa kesi mahakamani ni kufeli kwa dola kwa kuwa kuharakishwa kupatikana kwa haki ni haki msingi ya kila raia chini ya Kipengee 9 na jukumu msingi la serikali chini Kipengee 37 (d) cha Katiba. Kwa mujibu wa ripoti ya Express Tribune, kesi mahakamani zinaweza kuchukua miongo kadhaa na gharama zake ziko juu kupita hata madai ya mlalamishi.

Uzembe wa nidhamu ya mahakama inaweza kuelezewa kwa idadi kubwa ya kesi ambazo zahitaji kushughulikiwa. Hivi sasa, Dawn News inaripoti kuwa zaidi ya kesi milioni 1.8 hazijashughulikiwa ndani ya mahakama za Pakistan. Hii ni kwa sababu ya matatizo mengi ambayo nidhamu ya kisekula inayazalisha. Jamii imejawa na tamaduni kinyume na Uislamu ambazo zinazalisha matatizo tofauti tofauti yakihusiana na mahusiano ya nje ya ndoa, vurugu, mizozo juu ya matarajio ya kifedha ndani ya ndoa na huku mume na mke na wanafamilia wengine kutotimiza majukumu yao juu ya wengine. Kule kujaa kwa kesi mahakamani ndani ya ardhi za Waislamu ni natija ya muundo mbovu wa nidhamu ya mahakama katika dola hizi ambazo zimebuniwa juu ya mtizamo wa Kimagharibi, ambao umeweka ngazi kadhaa ndani ya nidhamu ya mahakama – mfano mahakama ya kukata rufaa, mahakama ya juu na nyinginezo – ambazo huchelewesha utekelezwaji wa kesi. Hili husababisha kesi kuchukua miaka ili kusuluhishwa.  Napia ni kutokana na serikali za kisekula na zisizokuwa za Kiislamu ndani ya ardhi zetu ambazo hazijali uhakikishaji wa kupatikana kwa haki na kusuluhisha matatizo ya watu kiukweli bali wanajali tu kuhifadhi viti vyao vya mamlaka. Hivyo basi, hawawekezi vilivyo kuwepo kwa mahakama za kutosha, mahakimu na vigezo vya kisheria kwa watu.

Zaidi ya hayo, nidhamu za mahakama ndani ya ardhi za Waislamu hazifanyi kazi kama mkono wa dola kulinda umoja wa familia na muundo wa familia kama ilivyokuwa chini ya utawala wa Kiislamu uliotangulia. Mahakama hazishughulikii kwa ukamilifu kesi za ndoa za lazima, hali ambazo mahari haikutolewa au mizozo ya kifamilia. Hivi sasa mahakama sio njia ya utatuzi wa mizozo ya ndoa ili kuiunganisha ndoa pamoja, au vurugu za kinyumbani ili kumlinda mwanamke, au kuhakikisha mwanamume anaisimamia familia yake vyema, au kuhakikisha kuwa mume na mke wanatekeleza majukumu yao kila mmoja kwa mwenziwe. Zaidi ya hayo kesi za talaka au kesi kuhusu malezi ya watoto huchukua muda mrefu ili kutatua. Hivyo basi, mwanamume, mwanamke na watoto huachwa njia panda wasiweze kuendelea na maisha yao. Huku kukiwa na mzigo mkubwa wa kifedha, watu binafsi wanalazimishwa kuishi ndani ya ndoa za huzuni na dhuluma kwa muda mrefu. Ukiongezea ukosefu wa haki na mahangaiko juu ya kigezo kuwa mamlaka na fedha mara nyingi huathiri matokeo ya kesi mahakamani ndani ya nchi zetu.

Matatizo haya yanakumbana na watu duniani kote ndani ya nchi nyingi, lakini tukitilia maanani nchi za Waislamu tunapata kuwa kuna mtizamo mfulani wa tatizo. Vyanzo vya sheria ambazo ni  katiba humaanisha kuwa nchi ikiwa msingi wa siasa yake ni nidhamu ya kisekula ya kidemokrasia, basi pia nidhamu yake ya mahakama itakuwa hivyo. Tofauti kati ya Pakistan na dola nyingine ipo katika sheria ya kikatiba na sio katika dori ya mahakama. Nchi za Waislamu kama Pakistan, hudai kuwa zimejifunga na hukumu za Shariah. Lakini ukweli ni kwamba katiba zao na hivyo mahakama zao zimekitwa juu ya hukumu za kisekula. Hii ikimaanisha kuwa matatizo wanayokumbana nayo wanawake sio kwa sababu ya sheria za Kiislamu na wala sio suluhisho zinazotolewa au hukumu zinazotolewa na mahakama ambazo zinafeli kutatua masuala ambayo familia na wanawake wanakumbana nayo.  Ni kutokana na kuwa sheria ambazo zimepeanwa na Muumba ili kulinda na kusuluhisha matatizo ya familia hazipo ndani ya nchi yoyote ya Waislamu leo.

Mnamo Machi 2016, Muhammad Khan Sherani, mwenyekiti wa Baraza la Mfumo wa Kiislamu Pakistan, alisema kuwa haki za wanawake zimelindwa vyema ndani ya sheria za Kiislamu (CBSnews) na yuko sawa kabisa. Sheria ya Kiislamu inawalinda wanawake, haki zao na familia zao. Tatizo ni kuwa sheria ya Kiislamu katika usafi wake haitekelezwi ndani ya ulimwengu wa Waislamu hivi leo. Labda ushahidi kamili wa hili upo katika kauli iliyotolewa na Shaikh Saleh Bin Humaid, mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mahakama nchini Saudi. Alisema kuwa "Tutachukua bora kutoka kwa nidhamu za mahakama ulimwenguni kote." Lau Uislamu utakuwa ndiyo msingi wa maamuzi na lau Waislamu, tutakuwa na imani kwa Mwenyezi Mungu na kujua bila shaka kwamba Neno Lake ni Sheria kuu, inakuwaje tena tuseme tutachukua 'bora' kutoka kwa nidhamu za mahakama? Kwa nini sisi kama Waislamu tuangalie vyanzo vingine kwa ajili ya sheria zetu na ilhali tunayo sheria pana na nidhamu ambazo twaweza kutatulia matatizo yetu na kuhakikisha kwamba haki za kila mmoja ikijumuisha wanawake na watoto zinatekelezwa?

Kauli zilizotolewa na wawakilishi wa serikali ndani ya ulimwengu wa Waislamu zinaonyesha kwamba matatizo yanatokana na mahakama kutokuwa chini ya msingi wa Uislamu na hivyo basi kutotekeleza sheria za Kiislamu. Sheria zinadaiwa kuwa chini ya msingi au kuathiriwa na Shariah lakini si ukweli. Katika nchi za Waislamu, watawala wanatofautisha kati ya sheria za Kiislamu na katiba ya nchi, wakiweka wazi tofauti kati ya hizo mbili, ambayo haitakiwi kuwepo. Huku kutenganishwa kati ya Uislamu na nidhamu ya kutungwa inaonyesha kuwa Uislamu sio chanzo pekee katika kutoa hukumu za mahakama.

Kipengee 227 cha katiba ya Pakistan kinasema kuwa sheria zote zilizopo "zitaletwa pamoja ili ziwiiane na maamrisho ya Uislamu kama ilivyo kwenye Quran na Sunnah […] na hakuna sheria itakayopitishwa ambayo itakwenda kinyume na maamrisho hayo." Katiba ndiyo msingi wa nidhamu ya mahakama na kipengee hichi kinaashiria wazi maagizo katika mahusiano baina ya mchakato wa nidhamu ya mahakama ya hivi sasa na Uislamu. Lakini kiukweli badala ya kuagiza nidhamu ya mahakama kuhakikisha kuwa inatumia Quran na Sunnah kama chanzo cha sheria, wameagiza kuwa sheria zitafsifriwe kwa imani ya kisekula.

Hii ni kwa sababu nidhamu ya kisiasa, baraza la mawaziri na taasisi za bunge na mahakama ndani ya nchi za Waislamu zimetokamana na nidhamu za kisekula za utawala wa kikoloni. Ndani ya Pakistan, nidhamu za kisiasa na mahakama zimekitwa juu ya msingi wa Sheria ya Serikali ya India, 1935 ambayo imetokana na utawala wa kikoloni wa Uingereza na ikabakishwa kuwa Katiba shikilizi wakati wa uhuru. Ilhali kumekuwepo na marekebisho katika mitizamo ya katiba, muundo wa mahakama na mchakato kwa kutumia mabaki ya utawala wa Uingereza.

Afghanistan, nayo imeundwa kwa nidhamu ya kisekula. Hata mashirika yasiyokuwa ya Waislamu yanakubaliana na hilo kama ilivyoonyeshwa na ripoti maalum ya USIP (United States Institute for Peace) iliyotolewa mnamo Machi 2015 inayosema kuwa haikowazi 'migawanyiko' baina ya mila, sheria za kidesturi na sheria za kidini. Hii ni kwa kuwa nidhamu ya sheria ya nchi inatokamana na machimbuko hayo matatu katika kutafsiri sheria. Katika ripoti hiyo hiyo, shirika hilo linamnukuu kiongozi anayesema kuwa asilimia 99 ya desturi na maadili ya Afghanistan sio ya Kiislamu.

Licha ya hili kuna imani ya kimakosa kwamba dori ya mashirika ya Kiislamu ndani ya nchi hizi huhakikisha kuwa sheria haziendi kinyume na Uislamu, lakini hata wajuzi wa kisheria wenyewe ambao ni wanachama wa mashirika hayo nao pia wanaathiriwa na nidhamu ya kisekula. Kwa mujibu wa muungano wa Wachambuzi wa Afghanistan, wanavyuoni mara nyingi huiunga mkono serikali ili waweze kupata nafasi serikalini. Ndani ya Pakistan, baraza la mfumo wa Kiislamu lina wanachama 8, watatu pekee ni wanachuoni na wanachama wote huchaguliwa na Rais na baraza lake. Hii inaonyesha wazi kuwa kuna athari ya bunge na baraza la kisekula juu ya mashirika ya Kiislamu. Nidhamu ya kisekula pia imedhibiti nguvu za mashirika hayo mfano Baraza la Mfumo wa Kiislamu na Mahakama za Shariah nchini Pakistan na baraza la Wanachuoni la Afghanistan. Wanaweza kutangaza kuwa sheria fulani sio ya Kiislamu lakini hawawezi kuhakikisha kwamba sheria zenyewe zinabadilishwa. Hii ni kwa mitizamo yote ya hukumu za Shariah ikijumuisha sheria zinazohusiana na wanawake. Mapendekezo ya baraza hilo hayana nguvu. Dori yao ni ndogo na hawana mamlaka ya kuhakikisha kuwa haki za wanawake, zilizodhaminiwa na Uislamu zimepeanwa.

Matatizo yanayohusishwa na hili yanaonekana katika mjadala wa 2016 kuhusiana na sheria dhidi ya dhuluma za kinyumbani ndani ya Pakistan. Ulipigiwa debe na vyombo vya habari, na serikali kama njia ya kuhakikisha kuwa wanaume wanalindwa kutokana na vurugu. Sheria haikupitishwa baada ya Baraza la Mfumo wa Kiislamu kupinga kuwa baadhi ya maelezo yaliyojumuishwa ndani ya sheria hiyo yalikuwa sio ya Kiislamu. Lakini hakuna sheria mbadala iliyowekwa kwa sababu jukumu la Baraza hilo linazunguka katika kutathmini sheria zilizopo na kutoa ushauri kwa serikali ili kufanya mabadiliko. Hivyo basi, matatizo ya wanawake kwa mara nyingine tena hayaku suluhishwa, wala kulindwa chini ya nidhamu ya mahakama na wanawake hawakupata haki dhidi ya walio wakandamiza.

Mahakama iliyoko ina hakikisha kuwa haki za watu fulani zinapatikana lakini watu fulani wanadhulumiwa vibaya mno. Kwa mujibu wa utafiti ambao USIP-PTRO ulifanya na kuegemea katika ripoti maalum ya USIP, baadhi ya migongano baina ya desturi na dini ni juu ya masuala yanayohusiana na ndoa, talaka na haki za mwanamke kurithi.

Katika jamii ya Afghanistan, nidhamu ya mahakama inasemekana inawapendelea wanaume kwa kuwa ina ruhusu kudhulumiwa kwa wanawake. Tafiti ya 2006 iliyofanywa na Haki Duniani (Global Rights), shirika la kimataifa lisilokuwa la kiserikali liligundua kuwa asilimia 85 ya wanawake wa Afghan wameripoti kuwa wamepitia vurugu za kimwili, kingono au kiakili au ndoa za lazima. Ndani ya Pakistan, mfano ni namna haki ya mwanamke kuolewa huondoshwa kwake katika sherehe inayojulikana kama 'Haq bakshish,' ambapo mwanamke huolewa na Quran. Hairuhusiwi katika Uislamu lakini serikali ya Pakistan imefeli kuwalinda maelfu ya wanawake ambao wanalazimishwa kuingia katika hali hiyo. Inacholifanya zoezi hilo kuchukiza zaidi ni kwamba linafanywa ili mali ya familia isitoke nje ya familia.

Tatizo jengine ambalo linajulikana na linawakabili wanawake Pakistan na Afghanistan ni kuhusiana na suala la haki za kurithi. Tafiti iliyofanywa na Pakistan Today, takribani asilimia 60 ya wanawake ndani ya Pakistan hawapati haki yao ya kurithi. Wengine asilimia 40 wanapata lakini hawapewi udhibiti au mamlaka juu ya mali.  Lawama juu ya matatizo haya imesukumwa juu ya desturi ndani ya jamii na uzembe wa nidhamu ya mahakama. Ndani ya Afghanistan, wanawake hawajaribu hata kudai sehemu yao ya urithi ili kuhakikisha kwamba wanasimamiwa na familia zao. Haya ni natija ya desturi na tamaduni zisizokuwa za Kiislamu ambazo zimekitwa ndani ya jamii ya Afghan, na tatizo linaloathiri takribani asilimia 50 ya wanawake wa Afghan.

Kwa kuhitimisha, nidhamu za mahakama ndani ya ardhi za Waislamu zinakosa uwezo wa kutatua malalamishi kwa njia ya haraka na ukamilifu, zikifeli kutatua matatizo yanayokumba wanawake na familia. Hivyo basi wanaruhusu matatizo kuzidi na kuwa mabaya ikipelekea migawanyiko mikubwa katika ndoa na maisha ya familia. Kujaa, uzembe, gharama kubwa na ufisadi katika mahakama zimekuwa ni vigezo vya kuwakatisha tamaa wanawake wengi katika kupata haki. Suluhisho kwa matatizo ya wanawake sio kuweka viraka vya kibinafsi katika sheria bali ni kuleta mabadiliko msingi kwa jamii yenyewe. Mabadiliko yatakayo osha uchafu wote na kuleta mwamko mpya kupitia utelezwaji wa nidhamu inayo heshimu na kuwalinda wanawake, wanaume, watoto, ndoa na muundo wote wa familia na misingi yake, sheria zake na taasisi za dola. Ni nidhamu ya Kiislamu PEKEE inayoweza kufanya hili.

Imeandikwa Kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 07:13

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu