Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ulaya na Washirika wake Wanadhamini Upendeleo wa Kuwahifadhi Wazungu Ambapo Uislamu Unatekeleza Dhamana ya Kuwahifadhi Walimwengu

(Imetafsiriwa)

[كَيْفَ وَإِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ لاَ يَرْقُبُواْ فِيكُمْ إِلاًّ وَلاَ ذِمَّةً يُرْضُونَكُم بِأَفْوَاهِهِمْ وَتَأْبَى قُلُوبُهُمْ وَأَكْثَرُهُمْ فَاسِقُونَ]

“……itakuwaje! Nao wakikushindeni hawatazami kwenu udugu wala ahadi. Wanakufurahisheni kwa midomo yao tu, na nyoyo zao zinakataa hayo. Na wengi wao ni wapotovu.”. [Surah At-Taubah:  8]

Uvamizi wa Urusi Ukraine ulioripuka mnamo Februari 24 ya mwaka huu umepelekea mzozo mkubwa wa wakimbizi ambapo Ulaya imeshuhudiwa ikifungua mipaka yake ya kitaifa, ikiwakaribisha zaidi ya Waukraine milioni tatu katika kipindi cha chini ya wiki mbili! Mwitiko huu usio wa kawaida kutoka Ulaya umefichua uwezo wao mkubwa wa kuhimili mzozo huu mzito wa wakimbizi kutokana na muunganiko imara wa kifikra wa Kiulaya, utashi wa kibaguzi wa kisiasa unaoonyeshwa na viongozi wa Ulaya na vyombo vya habari vya Magharibi.

Raisi wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen ametangaza jambo hili aliposema, “Kila  anayelazimika kukimbia mabomu ya Putin atapokewa kwa mikono miwili.”

Pia, Waukraine tokea 2017 walishapatiwa hifadhi ya muda, kuwawezesha wanaume, wanawake na watoto, pamoja na wanyama wao vipenzi, ruhusa ya kuingia nchi za EU bila viza au pasi ya kusafiria kwa vipenzi wao na wanaweza kuchagua nchi wanayotaka kwenda bila kupitia mfumo wa kuombea hifadhi.

Mattias Tesfaye, waziri wa mambo ya nje na mafungamano wa Denmak, pia amerudia maneno ya upendeleo wa mfungamano wa Ulaya wa Denmark kuwahifadhi Waukraine aliposema, “Wakati kuna vita Ulaya na jirani wa Ulaya wamekabiliwa na kile tunachokiona Ukraine, hakuna tone la shaka akilini mwangu: Lazima tusaidie kadiri tuwezavyo … kuwasaidia Waukraine katika ardhi ya Denmark.” Juu ya hayo, Serikali ya Denmark, inawepesisha ukarimu huu kwa Waukraine kwa sheria ambazo zitasitisha kanuni za ukimbizi kwa ajili yao. Msemaji wa mambo ya nje wa Chama kinachotawala cha Social Democrat cha Denmark, Rasmus Stoklund, aliiambia CNN: “Hawatokuwa sehemu ya mfumo wa waombaji hifadhi,” badala yake, sheria pendekezwa itawarahisishia Waukraine kupata hati ya ukaazi “ili iwaharakishie kuanza shule, kwenye elimu au kwenye kazi,” kwa mujibu wa kauli ya wizara ya uhamiaji na ushirikiano ya Denmark.

Waziri wa zamani wa Uhamiaji wa Chama cha Kiliberali, Inger Stojberg, ambaye chama chake kimesukumwa kwenye mswada uitwao ‘jewellery bill’, pia alielezea bila kificho maoni yake ya kibaguzi ya Ukristo wa Kiulaya wakati alipoandika kwenye Facebook (9/3/22). “Labda vilevile tuwe waaminifu kuhusiana na ukweli kuwa ni afadhali kuwasaidia wakimbizi wa Ukraine kuliko Wasomali na Wapalestina. “Hakuna asiyethubutu kusema hayo kama yalivyo: Ni kwa sababu Waukraine wanashabihiana sana na sisi na kwa sababu wao kimsingi ni Wakristo.”

Kuna pia Waziri Mkuu wa Bulgaria, Kiril Petkov, alisema: “Watu hawa ni wenye akili; ni wasomi… Hili sio wimbi la wakimbizi tulilolizowea, watu tusio na uhakika nao kuhusu utambulisho wao, watu wasiofahamika, ambao wangeweza kuwa hata magaidi.” Mwisho, na kwa kauli moja kiongozi wa chama cha Mrengo wa kulia cha Uhispania cha Vox, Santiago Abascal, alisema wakati akipokea mtiririko wa vifijo alipohutubia Bunge la Uhispania, “Hawa ni wakimbizi wa kweli: wanawake, watoto, na wazee wakaribishwe Ulaya. Sasa kila mtu afahamu tafauti baina ya wakimbizi hawa na uvamizi wa kijana wa Kiislamu wa umri wa kupigana vita anayevuka mipaka yetu akijaribu kuvunja utulivu na kuikoloni Ulaya.”

Vyombo vya habari vya Magharibi pia vimeelezea kwa kinywa kipana na kwa uwazi tabia yao ya kibaguzi na ya kishenzi ya kuwa na sheria moja kwa Wazungu na nyengine kwa Waislamu na Waafrika.

Akiwa hewani, mwanahabari mkuu wa kigeni wa CBS News, Charlie D’Agata, ameeleza kuwa Ukraine “kwa heshima zote, sio mahala kama Iraq au Afghanistan, ambako kumeshuhudiwa mizozo inayoendelea kwa miongo kadhaa. Hii ni nchi iliyostaarabika, kwa kiasi fulani ni Wazungu – ninapaswa kuchagua maneno hayo kwa uangalifu, sana – ni mji, ambao hutegemei hayo, au kutumaini kuwa yatatokea”.

Kisha kuna BBC ambayo ilifanya mahojiano na naibu mwendesha mashataka mkuu wa zamani wa Ukraine, aliyeuambia mtandao: “Ni jambo linalogusa hisia sana kwangu kwa sababu ninaona watu wa Ulaya wakiwa na macho ya buluu na nywele za rangi ya shaba … wakiuliwa kila siku.” Badala ya kuuliza au kupingana na kauli, mtu wa BBC aliitika kwa uwazi kabisa, “Ninafahamu na kuheshimu hisia hizo.”

Katika BFM TV ya Ufaransa, mwana habari Phillipe Corbe ameelezea hivi kuhusu Ukraine: “Hatuzungumzii hapa kuhusu Wasyria wanaokimbia mabomu ya utawala wa Syria wanaoungwa mkono na Putin. Tunazungumzia kuhusu Wazungu wanaoishi magarini ambao wanafanana na sisi ili kuhifadhi maisha yao.” Mwisho, mwanahabari wa ITV akiripoti kutoka Poland amesema: “Sasa kile kisichofikirika kimetokea kwao. Na hii sio nchi inayoendelea, ya ulimwengu wa tatu. Hii ni Ulaya!”

Mwanahabari na mwandishi Peter Oborne amesema, “Sisi katika Magharibi turipoti haja ya kuwa na jamii ya watu wenye hali moja ya kujitathmini wenyewe, na kujiuliza ni yapi maadili yetu? Hivyo ni kweli tuna kigezo kimoja cha maadili ambayo tumejifunga nayo katika muda wote na mahala popote? Kwa sababu kama sio hivyo na tukawa tuna aina moja ya maadili kwa watu wa ndani ya Ulaya na aina nyengine ya maadili kwa wasio Wazungu, wasio weupe, basi sisi ni wabaguzi, ni makatili pia.”

Kwa hivyo, historia ya kipaumbele kwa Ulaya kuwahifadhi wakimbizi Wazungu wakati wa Vita Vikuu Vya Pili, ambayo inarudi nyuma katika Mkataba wa Geneva wa 1951, uliowekwa kwa mtindo wa kimataifa na lugha “jumla kwa watu wote”, inayoahidi “kila mtu” kuwa na haki ya kuomba na kufurahia katika nchi nyengine hifadhi kutokana na mateso; ukweli ni kuwa kuomba hifadhi barani Ulaya, Amerika, Canada, Australia au New Zealand inapeanwa pekee kwa weupe, Wakristo wa Kizungu.

Ama kwa Uislamu, ahadi ya ulinzi kwa wale wanaoomba hifadhi na ulinzi imeweka juu ya Khilafah ya Kiislamu baadhi ya wajibu kwa watu wa dhimmi (watu wa ahadi). Hao ni majirani zetu, wako chini ya makaazi yetu na hifadhi chini ya uhakikisho wa Mwenyezi Mungu (swt), Mtume (saw) na Dini ya Uislamu. Yeyote anayekiuka wajibu huu dhidi ya yeyote kati yao kwa kiasi hata cha neno la kumuudhi, kwa kukashifu heshima yake, au kwa kumdhuru au kusaidia kumdhuru, amevunja ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume Wake (saw), na dini ya Uislamu. Mtume (saw) amesema:

«ألا من ظلم معاهداً أو انتقصه أو كلفه فوق طاقته أو أخذ منه شيئاً بغير طيب نفس فأنا حجيجه يوم القيامة» 

“Tambueni kuwa! Yeyote anayemdhulumu Mu’ahid (aliyepata hifadhi), au kumkashifu au kumkalifisha zaidi ya uwezo wake au kuchukua kitu chochote kwake bila ya ridhaa ya nafsi yake, basi mimi nitapambana naye siku ya Kiyama.”

Kuna mifano mingi kutoka historia ya Khilafah inayoonyesha namna Dola ya Kiislamu ilivyotoa hifadhi kwa wakimbizi na kuwalinda:

- Kufuatia kufurushwa kwa Mayahudi kutoka Uhispania mnamo 1492, Khalifah Bayazid II, aliweka sheria ya kuwakubalia hifadhi katika Khilafah ya Uthmani, na hata kupeleka meli Uhispania kuwachukua. Wakimbizi 250,000 waliwasili na kuishi zaidi kwenye miji ya Istanbul na Salonika.

- Mnamo miaka ya 1570, Waumini wa Umoja wa Kristo (wanaokataa Utatu) walikimbia mateso kutoka kwa ndugu zao Wakristo na kupewa hifadhi katika ardhi za Kiislamu.

- Baada ya uvamizi wa Urusi Crimea mnamo 1784 na Caucasus mnamo 1864, Waislamu walioishi katika maeneo haya walikuja Anatolia ima kwa meli au njia za ardhini. Waliishi kwenye vijiji vilivyokuwepo na mijini.

- Katika karne ya 18, Warusi wa Cossack walikimbilia Dola ya Uthmani kutokana na mateso chini ya mikono ya Kanisa la Orthodox lililopo katika mji wa Balikesir.

- Hadi Warusi wa Tsarist 200,000 walichukuliwa kwa meli hadi Istanbul baina ya 1917-21, waliopinga mapinduzi ya Bolshevik na kukimbia vita vilivyofuatia; mwanzoni waliwekwa katika kambi za wakimbizi kabla ya kupelekwa kwenye nyumba na makaazi ya kudumu.

- Mwanahistoria Stanford Shaw aliandika katika kitabu Mayahudi, Waturuki, na Wauthmani: Karne ya kumi na tano hadi ya ishirini, “Himaya ya Kiuthmani imekuwa kwa karne nyingi ikiwapa wakimbizi wa Kiyahudi mahala salama kutokea Ulaya. Uhamiaji mkubwa wa Mayahudi kutokea Uhispania, Ureno, na nchi nyengine za Ulaya katika karne ya kumi na tano na kumi na sita unafahamika sana …… Hata hivyo, baadaye uhamiaji wa Mayahudi kuja Himaya ya Kiuthmani umekuwa haujulikani sana. Lakini bado, katika miaka kadhaa, Mayahudi wengi wa Ulaya mmoja mmoja au kwa vikundi vidogo vidogo waliendelea kuishi katika himaya ya Kiuthmani kwa sababu za kisiasa, kiuchumi, au kidini. Mnamo karne ya kumi na tisa na mwanzoni mwa karne ya ishirini, mmiminiko wa wakimbizi wa Kiyahudi katika ardhi zilizokuwa zikipungua za Kiuthmani uliongezeka tena.”

Ukarimu wa Khilafah ya Uthmani wakati wa Ukame Mkubwa wa Ireland mwaka 1845 umenakiliwa vizuri [7]. Katika kuwasaidia wengine, Khalifah Abdul Majid I, alielezea wito wa Kiislamu kwa maneno yake; “Ninalazimika kwa mujibu  wa dini yangu kuheshimu sheria za ukarimu.” Waislamu tayari kwa muda mrefu wamekuwa na fikra iliyo kita mizizi ya utoaji sadaka binafsi bila hata malipo yoyote. Kile kinachohitajika hivi sasa ni kuinua ufahamu huu na kutumika kisiasa katika hatua ya dola ili mamilioni ya wakimbizi duniani hivi leo waweze kusimamiwa na kuruhusiwa kukaa katika ardhi kwa ajili ya ulinzi wao. Kwa kufanya hivyo, Ummah sio tu utakuwa umetekeleza wajibu wake kwa walimwengu, bali pia kuionyesha dunia uadilifu wa Uislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Tsuroyya Amal Yasna
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu