Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vifo vya Wahamiaji

(Imetafsiriwa)

Tarehe 25 Novemba 2022 iliadhimisha mwaka mmoja wa kifo cha wahamiaji 31 ​​wengi wao wakiwa Waislamu waliokuwa wakivuka Mkondo wa Kiingereza ndani ya mashua ya mpira.

Vifo hivyo vimetajwa kuwa janga baya zaidi la baharini kuwahi kutokea kwa miaka 30. Dhurufu za matukio hayo ya kutisha zinaogofya zaidi.

Muokozi wa kujitolea Charles Devos alikuwa mmoja wa watu wa kwanza katika eneo la tukio. Anafahamu na mamia ya vyombo hivyo visivyofaa baharini na vilivyojaa kupita kiasi vinavyosafiri kupitia njia ya meli zenye shughuli nyingi zinazotumiwa pia na wasafirishaji mizigo mikubwa. Hali mbaya ya anga, mawimbi na vimbunga imechukua uhai wa mamia ya watu kwa miaka mingi, lakini matukio ya tarehe 27 Novemba yalikuwa ya kutisha sana.

Mashua inayozungumziwa iliyumba na abiria wake walijua kuwa wako hatarini. Simu za rununu zilitumika kuita uokoaji. Mashua hiyo ilikuwa katika bahari ya Ufaransa; hata hivyo, mamlaka za Ufaransa hazikutaka kuchukua jukumu la uokoaji. Wahamiaji hao waliambiwa waite huduma za uokoaji za Uingereza; hata hivyo, walisisitiza kwamba mashua hiyo lilikuwa katika bahari ya Ufaransa na wakakataa kutoa msaada wa aina yoyote.

Ubadilishanaji huu wa kikatili wa uwajibikaji "tenisi" ulifanyika kwa masaa mingi hadi kila mmoja wa wahamiaji 27 alikufa kwa baridi kali mwilini (hypothermia).

Kulikuwa na wanawake 7 na watoto 3 kwenye mashua hiyo. Mmoja wa wanawake hao alikuwa mjamzito. Hakuna yeyote aliyepewa hadhi ya nafasi ya kuishi na walionekana kutostahili kusaidiwa.

Katika wakati huu wa Novemba 2022, idadi inayoongezeka ya watu wanaokimbia mizozo au umaskini nchini Afghanistan, Sudan, Iraq, Eritrea na maeneo mengine wanahatarisha safari yenye hatari katika vyombo vidogo, visivyofaa baharini kutoka Ufaransa, wakitumaini kupata hifadhi au kupata fursa bora zaidi nchini Uingereza. Walanguzi wa binadamu hawana huruma na kumekuwa na tetesi za wahamiaji kuona kwamba mashua haziko salama na zimejaa kupita kiasi. Wanapokataa kupanda, wanashikiwa bunduki ili waendelee au watoto wao watapigwa risasi. Pesa kabla ya maadili ndiyo kichocheo pekee na thamani inayoshirikiwa na serikali na magenge ya wahalifu vile vile.

Maadili mabovu ya utaifa ndio ya kulaumiwa kwa hali hii ya kufedhehesha. Wahamiaji hawaonekani kama wanadamu wenza wanaoteseka na matokeo ya vita vya kikoloni na sera kilafi za kiuchumi.

Mataifa ya Magharibi yanasababisha tatizo katika ardhi za Kiislamu na kutarajia raia kukaa na kusubiri kifo kwa mabomu na njaa. Masuala ya haki za binadamu ya bendera za upinde wa mvua huchukua kipaumbele zaidi katika maadili ya kiliberali ya mataifa ya kirasilimali.

Tunaweza tu kuendelea kuwa na kumbukumbu zaidi za matukio haya ya kusikitisha kwa kukosekana Khilafah. Kamwe haiwezi kuwa hivyo kwamba Amiri wa Khilafah angekubali kwamba binadamu yeyote achwe afe akiwa na haja. Maadili bora ya Sharia yanaharamisha kupotea hata kwa uchache kabisa kwa maisha na maisha ya mtu mmoja yana thamani zaidi kwa Mwenyezi Mugu (swt) kuliko dunia nzima.

(مِنْ أَجْلِ ذَلِكَ كَتَبْنَا عَلَى بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا وَلَقَدْ جَاءتْهُمْ رُسُلُنَا بِالبَيِّنَاتِ ثُمَّ إِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم بَعْدَ ذَلِكَ فِي الأَرْضِ لَمُسْرِفُونَ)

“Kwa sababu ya hayo tuliwaandikia Wana wa Israili ya kwamba aliye muuwa mtu bila ya yeye kuuwa, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi.” [5:32].

Maisha na heshima ya Muislamu kamwe hayatawahi kuwa na usalama au thamani ikiwa mifumo iliyobuniwa na mwanadamu itaendelea kutawala. Suluhisho pekee sahihi ni kuregea Khilafah kikamilifu.

Imepokewa kutoka kwa Abu Maryam al-Azdi: Nilipokwenda kumuona Mu’awiyah, alisema: “Ni nzuri ilioje ziara yako kwetu, ewe babake fulani.” (Hii ni nahau inayotumiwa na Waarabu katika hali kama hizo). Nikasema: "Nitawaambieni Hadith niliyoisikia. Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (rehema na amani zimshukie) akisema:

«مَنْ ولَّاهُ الله عز وجل شيئًا مِنْ أَمْر المسلمين فاحْتَجَبَ دُونَ حاجَتِهم وخَلَّتِهِم وفقرهم، احْتَجَبَ الله عنه دون حاجَتِه وخَلَّتِهِ وفقره»

 “Yeyote atakayetawalishwa na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, mambo ya Waislamu na akajitenga na kutowatimizia haja zao, mapungufu yao, na ufukara wao, Mwenyezi Mungu atajiweka mbali naye, asimtimizie haja zake, mapungufu yake, na umaskini wake.” Akasema: “Amemteua mtu wa kukidhi mahitaji ya watu.” [At-Tirmidhi]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu