- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kitu Kile Walichojengwa Nacho Wapalestina
(Imetafsiriwa)
Tokea mwanzoni mwa mashambulizi ya vita, hofu kwa watu wa Gaza ilitukumba kwa sababu tunaelewa umbile la Kiyahudi halina kikomo ima linapokuja suala kama la sheria za kimataifa au rai jumla ya watu kutumia mabomu ya kemikali yaliopigwa marufuku, kuvuka mistari yote mekundu. Wakiwa na silaha nzito na mabomu ya kila aina, haya yanatumika kwa wasio na hatia kama tunavyoona katika habari za kimataifa na video za mitandao ya kijamii na picha.
Wakati wa mwanzo wa shambulizi la Brigedi ya Qassam, mshangao ukawa ni kuwa Wapalestina wana uwezo wa kuvizubaisha vikosi vya ‘Israel’ – hii inakuja kutokana na kuwepo kitengo nyeti cha hali ya juu chenye uwezo mkubwa wa upelelezi duniani kikiwa na kamera zao na mashushushu kila mahali. Hili liliwastua umbile la ‘Kiyahudi’ hadi kooni na kuwapa Wapalestina wa kawaida matumaini kuwa ukombozi unawezekana kutoka kwa uvamizi. Matumaini yalikuwa wazi kabisa, furaha za kuwa ‘Israel’ ni kweli inaweza kushindika kirahisi!
Lakini bila shaka, umbile la Kiyahudi liliwasaga saga wale wasio na hatia kabla ya kuwatafuta Qassam au Hamas, mauwaji baada ya mauwaji, wamewakamata maelfu ya watu katika Ukingo wa Magharibi na vituo vipya vya ukaguzi na vizuizi vilianzishwa kuzuia harakati za mienendo ya watu na kuzusha hali ya hofu. Hali ya eneo la Al-Quds ni mbaya zaidi kuliko Ukingo wa Magharibi – hapa jeshi la IDF na maafisa wanafanya vamizi za kuendelea kwa watu wa kawaida wanaokwenda maeneo ya umma na kuchunguza simu za watu wapendavyo kwa kila picha au majibu ya huruma au machapisho ya vita, na Wapalestina wanaume au wanawake au watoto bila shaka kufuatiwa na kipigo kikali. Watu wako katika hadhari; hufuta kila kitu kinachoweza kusababisha kukamatwa au kushambuliwa. Matokeo mabaya ikiwemo vamizi zisizotangazwa majumbani, ukamataji kwa kila mtu anayedhaniwa kuwa mwanaharakati hata kama ni dondoo ya ‘Hasbiya Allah wa ni’m Al-Wakiil’ katika machapisho ya mitandao ya kijamii mbali ya kutaja jina Kimbunga cha Aqsa.
Lakini hapa kunakuja mfichuo wa jengo la watu – msemo wa Kiarabu “wamejengwa na nini.” Hapa vita vimeengua hofu na kutojiweza kwa watu wa kawaida. Imeonyesha kuwa watu wa Palestina wapo tayari kuvitoa muhanga vya thamani kwa ajili ya kukinzana na mvamizi huyu mwenye kiu ya damu na hata kumfanya mtu ageukie kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa ni Mhifadhi halisi Mtoaji Pekee.
Watu wanageukia kwenye maombi na wamewaonyesha vijana wao kuwa wakakamavu na wastahamilivu … kile kitachotokea kimeandikwa … hakuna kuhofu … kifo sio cha kuhofiwa kwa sababu kila chenye uhai kitakufa … ni jinsi gani unakufa ndio jambo la kuzingatiwa.
Fariki wakati unasema haki, ilinde Ardhi Tukufu ya Palestina. Hapa kuna hekima na uwazi kwamba walinzi halisi wa mvamizi ni tawala za Kiarabu na nguvu halisi ya kumaliza vita hivi ni majeshi ya Waislamu ambao ni watu wa Ummah huu. Wanawaita watu wa Palestina wakitaka kuwalinda na kuwakomboa lakini watawala wao waovu wanawazuia.
Wanawake hapa wanawafundisha vijana wao kutokuwa waoga, fikra ya kuwa wanaume wa wanaume inafundishwa na kusukumwa. Kuwa wanyenyekevu kwa wanyonge, na sio kuwa waoga wa njaa au kiu au kutokuwa na makaazi.
Msemo mwengine kwa Kiarabu – kile kinachoanguka kutoka mbinguni, ardhi itakipokea- unakaririwa na watu wazima.
Watoto wana utambuzi juu ya vita- watu hapa hawawakingi (watoto) jambo ambalo mwanzoni linasikitisha lakini inawasaidia kufahamu mabomu na kuwa na ufahamu wa vita. Misikitini baada ya kila swala inaishia na dua kwa Gaza na Palestina, wadogo kwa wakubwa husema Amin kwa dua hizi.
Baadhi ya maeneo wanasikia mabomu na kuyaona na kuyahisi yakitua kwenye sehemu ambapo baadhi ya watu wanaishi katika Ukingo wa Magharibi karibu na Tel Aviv na makaazi ya Mayahudi. Lakini kile kinachoonekana kwa watu ni kuwa hawakimbii na kujificha au kutaka makaazi kama Mayahudi. Ushujaa na uimara upo kwa watu wanaoishi Jenin, Tulkarm na Nablus hasa katika kambi ambapo IDF wanafanya vamizi kwa kutumia makumi ya makumi ya vifaru vilivyoimarishwa sana, lakini bado vijana na watu wazima wanatoka kuwakabili kwa mawe au silaha za msingi kuwalinda watu wao, majumba na miji yao mchana au usiku.
Vita, ndio vinatokea hivi sasa lakini namna hii ndio inayoleta mashujaa na mabingwa wanaokataa ukandamizaji na udhalilishwaji.
Wapalestina hawalilii chakula au maji au umeme – wanajua kuwa huu ni msukumo kuwadhoofisha hivyo wanakataa hilo. Taarifa za watu kupitia kwenye klipu zinasema msituletee chakula au mablanketi, bakini navyo – tuleteeni majeshi ya Waislamu- hapa ndipo kwenye mtengano katika mzunguko mbaya na ufahamu.
Kina mama na kina baba kwenye TV mubashara katika wakati halisi… wanasema Alhamdulilah wakati nyumba zao zinabomolewa na watoto wao kuuliwa. Huku wakilia wanasema kuwa watawatoa muhanga watoto wao tena na tena kwa kuwa haitopita bure … wao ni Mashahidi katika njia ya Allah. Hili linalihofisha umbile lote la Kiyahudi na waungaji mkono wake.
Watu wa kawaida wanasisitiza kwamba hii lazima ifanyike ili ulimwengu uone uonevu na uhalifu! Al-Quds itakombolewa na pia Palestina yote na watu watajifakhiri kuwa ni kutoka Palestina.
Dua ni safi, machozi hukausha nyuso za vijana na wazee, moyo hupasuka tena na tena. Baadhi ya wakati uzito unajaribu kuingia ndani lakini imani kwa Mwenyezi Mungu inatapakaa mwilini kwenye kila swala ikimshtua mwenye kufanya ibada kuomba dua zaidi kuwapa uimara kwa mchana na usiku unaofuata. Imani katika ahadi ya Mwenyezi Mungu na chuki dhidi ya uvamizi wa Mayahudi upo wazi. Hasbiya Allah wa Ni’ma-lwakiil. Kwa hakika ushindi na ukombozi ni ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt).
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Minnatullah Saleh
Dada Mwenye Matumaini kutoka Ardhi Tukufu – Palestina