Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ushindi kwa Ujumbe wa Uislamu Kimataifa

Mnamo Ijumaa, 19 Januari 2024, Waziri wa Usalama, Tom Tugendhat alitia saini kuwa agizo la kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir nchini Uingereza kama shirika la kigaidi. Hiyo ni baada ya Bunge la Uingereza kuidhinisha agizo kielelezo lililowasilishwa mnamo Jumatatu, 15 Januari 2024. Agizo hili linafanya kuwa mwanachama wa Hizb ut Tahrir au kuwalingania watu kushirikiana nalo ni kosa la kiuhalifu, lililo na uwezo wa kupelekwa gerezani miaka 14, ambayo ni pamoja na kulipa faini au kuchukua sehemu ya faini. [www.gov.uk/government/news].

Sababu kuu iliyotajwa kwa kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir nchini Uingereza ni kwamba ni kundi ambalo linachuki dhidi ya Mayahudi hususan kwa kupinga uvamizi wao wa Ardhi ya Baraka ya Palestina na kuwaua Wapalestina ndani ya Gaza!

Hakika, Uingereza kwa mara nyingine imeweka historia katika kufichua asili ya nyuso mbili za tawala za Kimagharibi za kikoloni ambazo zinadai kuwa ndio ngome za amani, walinzi wa haki za kibinadamu, uhuru wa maoni na kuandamana. Alas! Wao SIO LOLOTE bali ni pote tu la vinyago wa kisiasa wa kikoloni ambao wanatanua kwa kuvamia na kupora ardhi na rasilimali za ng’ambo huku wakimwaga damu na kuwaua watu wake. Zinazodai kuwa ni dola za kipolisi za Amerika, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Uchina zinabomoka katika maeneo yao, kwa kuwa zimefeli pakubwa kupambana na ajenda ya Kiislamu kimataifa ambayo imeshamiri duniani kote.

Maazimio yao ya mwisho ni kuzindua kwa mara ya kwanza kampeni pana ya propaganda inayolenga kuuchafua na kuutia shaka Uislamu kama mtazamo wa kimfumo pekee juu ya ulimwengu, mwanadamu na uhai ambao umebakia, uliojaribiwa na kufaulu. Nidhamu ya kirasilimali ya kisekula iliyoko madarakani inakaribia kuporomoka kwa kishindo ambacho hakijawahi kabla yake ikilinganishwa na kuporomoka kwa mfumo wa Kikomunisti chini ya Wasoviet. Mzunguko wa kidemokrasia wa bahati nasibu umetimia nyuzi 360 na hakuna chengine cha kudandia! Mfumo pekee ulioko ni Uislamu. Kwa kuongezea, Uislamu hautabishiki isipokuwa chini ya Serikali ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume.

Kwa hivyo, walinganizi wa Khilafah inayotarajiwa ndani ya Magharibi wanakabiliwa na vitisho vinavyojumuisha kubandikizwa kuwa wanachuki dhidi ya Mayahudi, wana misimamo mikali na magaidi. Fauka ya hayo, wanakabiliwa na ukatili wa kupindukia kutoka kwa tawala za kiimla ndani ya Mashariki ya Kati, Urusi, Uzbekistan, Uchina nk. Jambo la muhimu la kuzingatia ni kwamba hizi tawala za kidemokrasia zimefeli kushinda hoja kuhusu nini mbadala kwa nidhamu iliyoko na iliyofeli ya kirasilimali ya kisekula ya Kimagharibi. Hivyo basi, serikali za kidemokrasia hazina chochote cha kutoa kama mbadala isipokuwa kuwanyamazisha walinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.  

Ngamia amevunjika mgongo, matukio ya hivi karibuni yaliyoanzishwa na utawala wa Uingereza hayajatokea tu kibahati mbaya, bali ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kuweka vikwazo dhidi ya kuchipuza kwa Khilafah. Wanarudia yale yale waliyoyafanya Maquraysh lakini hakuna ambalo linafanyakazi upande wao. Sera zao za ndani zinawaangamiza raia wao ambao kila siku wanaandamana wakitaka kuvifungua vitanzi vilivyokazwa shingoni mwao vya kisiasa, kijamii na kiuchumi! Kwa upande mwingine, sera zao za kigeni kama ile ya Sykes-Picot zinasambaratika na watawala wao vibaraka wa kikoloni wamejawa na wasiwasi pomoni!

Hakika, ushindi wa ajenda ya Kiislamu kimataifa unakaribia kutimia kikamilifu muda wowote kutoka sasa. Mwenyezi Mungu akitujaalia (InshaAllah). La muhimu wakati huu nyeti sio kupunguza kasi na kushughulishwa na mateke ya punda anayekata roho wa mfumo wa kirasilimali wa kisekula. Badala yake lazima tuwe makini na kupatiliza fursa na kuzidisha moto wa mabadiliko kwa nishati na ushujaa. Lazima tukumbuke kuwa sisi ni watumwa wa Mwenyezi Mungu (swt), na lazima tuyape kipaumbele maisha ya Akhera kuliko hii dunya ya muda mfupi.

Muda wote lazima iwe wazi kwetu, kwamba adui anajuwa nguvu za Khilafah yetu inayotarajiwa na hivyo anaipigia njama dhidi yake. Alas! Meli inakaribia kutia nanga bandarini muda wowote kutoka sasa. Swali msingi zaidi ni kwa gharama ipi tuko tayari kulipa kuhakikisha kuwa meli inatia nanga bandarini? Kupoteza ajira zetu, uraia, kubandikizwa tuna misimamo mikali na magaidi, kutupwa gerezani, mali zetu kutaifishwa, kuandamwa na kuuliwa kiholela miongoni mwa mengine ni baadhi ya gharama zinazotarajiwa kuzilipa. Mwenyezi Mungu (swt) alisema : ﴿ أَمۡ حَسِبۡتُمۡ أَن تَدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ وَلَمَّا يَأۡتِكُم مَّثَلُ ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلِكُم‌ۖ مَّسَّتۡہُمُ ٱلۡبَأۡسَآءُ وَٱلضَّرَّآءُ وَزُلۡزِلُواْ حَتَّىٰ يَقُولَ ٱلرَّسُولُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُ ۥ مَتَىٰ نَصۡرُ ٱللَّهِ‌ۗ أَلَآ إِنَّ نَصۡرَ ٱللَّهِ قَرِيبٌ۬Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu.[Al-Baqarah: 214]

Mtume (saw) alizungumza kuhusu zama hizi katika Hadith yake maarufu. Anas bin Malik (ra) alisimulia kwamba Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema: ‏«يَأْتِي عَلَى النَّاسِ زَمَانٌ الصَّابِرُ فِيهِمْ عَلَى دِينِهِ كَالْقَابِضِ عَلَى الْجَمْرِ»‏“Zitakuja zama kwa watu ambapo yule atakayekuwa na subira juu ya dini yake atakuwa kama yule anayeshikilia kaa la moto." [Tirmidh #2260] Kwa kuongezea,  Abdullah (ra) alisimulia kwamba Nabii wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema: «إِنَّ الإِسْلاَمَ بَدَأَ غَرِيبًا وَسَيَعُودُ غَرِيبًا فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ»‏.‏ قَالَ قِيلَ وَمَنِ الْغُرَبَاءُ قَالَ «النُّزَّاعُ مِنَ الْقَبَائِلِ»‏“Uislamu ulianza ukiwa kitu kigeni na utarudi kuwa mgeni, kwa hiyo bishara njema kwa wageni.” Ikasemwa: ‘Ni kina nani hao wageni?’ Akasema: “Wageni ambao wameziwacha familia na kabila zao.” [Sunan Ibn Majah #3988] Hakika, katika zama hizi watu ambao wanakwenda mbio kurudisha tena maisha ya Kiislamu wameikataa (wametoka) nidhamu ya kirasilimali ya kisekula na inayohusiana nayo kama vile nidhamu ya kidemokrasia, sheria ya kimataifa, nidhamu ya kihuria ya kijamii – ukombozi wa wanawake!

Uingereza imepiga firimbi, wakati ni sasa wa kupambanua baina ya wachezaji wa siasa ya Kiislamu wa kweli na wanachuoni wa kisiasa. Kwa maana nyingine, hakuna njia ya mkato au mirengo miwili; ima uwe ni mchezaji wa siasa ya Kiislamu utakayepatiliza matukio ya hivi karibuni kusongeza mbele ajenda ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuivuta rai ya ummah upande wako. Kama wachezaji wa siasa ya Kiislamu, tunatakiwa kufikiria na kutenda kwa haraka, kimahesabu na kukatikiwa. Kilichoko mbele yetu ni kuiteka rai ya ummah na sio kingine. Kilichoko cha dharura ni sarafu ya rai ya ummah ambayo yatakiwa kuchochewa kuzidi na kuelekezwa kwa suala la kiuhakika ambalo ni kuunganisha kusambaratika uhalisia wa kisiasa ndani ya Magharibi unaofichuliwa na kufeli kwa sera zake haribifu za ndani na nje zinazodhikisha dunia.

Lazima tukumbuke kwamba kufikiria kisiasa ndio kilele cha kufikiria na hivyo gharama yake ni kubwa mno lakini inayostahiki kulipwa hususan pale ambapo ni kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu (swt) na sio kingine. Ummah wahitaji mashujaa ili uwape uongozi wa kisiasa, na uongozi hukabidhiwa wasioogopa, Kitendo kidogo tu cha kiujasiri wa kupindukia kitapelekea athari kubwa ambayo itayafanya Mapinduzi ya Bara Arabu ya 2011 kuwa ni mchezo tu.

Ulinganizi kwa wanajeshi Waislamu miongoni mwa majeshi ya Waislamu kunyanyuka kutoka katika kambi zao za kijeshi ndani ya Bangladesh, Pakistan, Saudi Arabia, Yemen, Egypt, Jordan, Tunisia, Uturuki nk, lazima uzidi kasi. Kila Muislamu dada, kaka, baba, shangazi au mjomba aliye na mtoto ndani ya majeshi ya Waislamu lazima aulizwe pasina kuchoka kuwalingania jamaa zao ili kutoa Nussrah (msaada wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kupitia njia ya Utume. Hizb ut Tahrir iko tayari kwa kazi hiyo na imechapisha kielelezo cha katiba kwa upana kuonesha utayari wa kutekeleza mfumo wa Kiislamu kwa ukamilifu chini ya Khilafah iliyosimamishwa tena kwa njia ya Utume.

Kwa kutamatisha, kuibandikiza Hizb ut Tahrir nchini Uingereza kama shirika la kigaidi lazima lichukuliwe kama baraka iliyofichika na fursa ya kupatilizwa kwa ajili ya ulinganizi wa kusimamisha tena Khilafah ndani ya ulimwengu wa Waislamu. Kwa kufichua Wamagharibi katika kufeli kwao kuhimili mihemko ya Hizb ut Tahrir kama chama cha kimfumo wa Kiislamu ambacho hakitumii mabavu bali mvutano wa kifikra kama silaha yake hatari. Ili kuwavunja Wamagharibi ambao wanatizamwa na watawala wao Waislamu vibaraka wa kikoloni ndani ya ulimwengu wa Waislamu. Hivyo basi, kuzidisha ulinganizi kwa watu jumla kuelekeza maandamano yao kwa makaazi ya watawala Waislamu vibaraka ili kuwang’oa mamlakani. Kinyume chake, waelekee katika makao makuu ya kijeshi na kuwalingania Majenerali wa Jeshi kuchangamka na kuwaondosha vikaragosi wa kikoloni ambao wanaweka vikwazo katika kunyanyuka kwa mfumo mbadala wa Kiislamu. Wakati ni sasa, muda haunasi na fursa haziji mara mbili.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro (Abu Taqiuddin)

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu