- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Unafiki wa Ulimwengu wa Kimagharibi: Uamuzi wa ICJ juu ya 'Israel' na Madai ya Uhusiano wa UNRWA na Hamas
(Imetafsiriwa)
Uwanja wa kimataifa mara nyingi hushuhudia dhihirisho la unafiki, hasa linapokuja suala la hatua za dola za Magharibi katika kushughulikia mizozo katika Ulimwengu wa Kiislamu. Matukio mawili ya hivi majuzi, kwa mara nyengine tena, yameleta jambo hili katika mwelekeo mkali: uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kuhusu 'Israel' ambao ulianzishwa na Afrika Kusini mnamo Disemba 29, 2023, na madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na 'Israel' kuhusu UNRWA (Shirika la Umoja wa Mataifa la Usaidizi na Kazi kwa Wakimbizi wa Palestina) kuwa na mafungamano na Hamas. Kutofautiana kwa miitikio na hatua zinazochukuliwa na dola za Magharibi katika hali hizi kunafichua, kwa uwazi na bila aibu, kutokuwa na dawama katika mtazamo wao wa kile kinachoitwa haki na njia yao ya uwajibikaji.
Mnamo Disemba 2023, Afrika Kusini iliwasilisha ombi kwa ICJ ikitaka ushauri wa maoni kuhusu matokeo ya kisheria ya mauaji ya halaiki ya umbile la Kiyahudi kwenye Ukanda wa Gaza, pamoja na ubaguzi wa rangi wa miaka 75, uvamizi wa miaka 56 na uzuizi wa miaka 16 wa Ukanda wa Gaza (kulingana na Afrika Kusini). Licha ya ushahidi unaoongezeka wa uvunjaji wa sheria za kimataifa wa umbile la Kiyahudi, ukiwemo Mkataba wa Mauaji ya Halaiki, dola za Magharibi zimekuwa zikisita kuchukua hatua na kupuuza kabisa hukumu ya ICJ. Huku baadhi ya nchi, kama vile Ujerumani, hata kulisaidia na kuliunga mkono umbile la Kiyahudi.
Kinyume chake, ‘madai ya hivi majuzi ya Israel dhidi ya UNRWA, kulituhumu shirika hilo kwa kudumisha uhusiano na Hamas na hata kuhusika na matukio ya tarehe 7 Oktoba, yamekabiliwa na shutma za haraka na hatua madhubuti kutoka kwa mataifa ya Magharibi. Madai ya umbile la Kiyahudi, ingawa hayana ushahidi wowote, yamesababisha vikwazo vya haraka na vya moja kwa moja dhidi ya UNRWA. Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uholanzi zimesitisha malipo yao ya UNRWA na Uingereza ikitaka uhakikisho kamili kwamba UNRWA haitaajiri 'magaidi' kabla ya kuregesha ufadhili. Hata Tume ya Ulaya imechapisha taarifa rasmi ambapo inatangaza kwamba maamuzi yajayo ya ufadhili wa UNRWA yatahakikiwa upya na kwamba uchunguzi wa kina unapaswa kuanzishwa ili kuhakikisha kwamba shirika hilo au wafanyakazi wake hawajashiriki katika mashambulizi hayo.
Tofauti za majibu na matumizi ya kuchagua ya kanuni hizi katili za Magharibi pindi zipochunguzwa hatua zinazochukuliwa na Magharibi katika kila hali, yamefungua macho sio tu ya Waislamu, lakini wengi wasiokuwa Waislamu pia. Imedhoofisha uaminifu wa mataifa ya Magharibi na kubadilisha simulizi ya kilimwengu dhidi ya umbile la Kiyahudi na viongozi wengine madhalimu wa Magharibi.
Hata hivyo, tabia na mwitikio huu haipaswi kutushangaza sisi Waislamu. Ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na ICJ na UNRWA na mashirika mengine mengi, ni matokeo ya mikataba miwili ya amani iliyotiwa saini mwaka 1648 huko Westphalia, ambayo pia inajulikana kama Amani ya Westphalia. Mkataba huu ulianzisha utaratibu mpya wa kisiasa wa Ulaya na kuweka msingi wa diplomasia ya kisasa na mahusiano ya kimataifa, kwa ajili ya Magharibi na ili kulinda ubwana wa Magharibi juu ya ulimwengu wa Kiislamu. Kwa hivyo, kila shirika ambalo ni matokeo ya mkataba huu moja kwa moja na bila shaka yoyote linafanya kazi na kutumiwa na ajenda ya Magharibi dhidi ya Umma wa Mtume Muhammad (saw).
Na huku Umma ukiweka wazi pale uliposimama, kutoa sauti na kuandamana kwa kiwango kikubwa ili hatua madhubuti zichukuliwe ili kuwaokoa ndugu zetu na dada zetu wa Palestina na kukomesha makaazi katili ya Wazayuni, wale wanaoitwa viongozi wa Waislamu wamekuwa kimya wakitazama haya yote yakitokea. Hivi sasa, zaidi kuliko wakati mwingine wowote, tunahitaji Khilafah kwa njia ya Utume ili kurudisha uadilifu na amani kwa ulimwengu wa Kiislamu na kwengineko, kuwaondoa viongozi washenzi na wanafiki wa ardhi zetu na kukomesha ajenda ya makafiri.
[وَالَّذِينَ كَفَرواْ وَكَذَّبُواْ بِآيَاتِنَا أُولَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ]
“Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio watakao kuwa watu wa Motoni, humo watadumu.” [Al-Baqarah 2:39]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Sumaya Bint Khayyat