Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mauaji ya Halaiki ya Kimya nchini Congo:

Kimya cha Magharibi na Usaidizi kwa Jina la Faida

(Imetafsiriwa)

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni nyumbani kwa usambazaji mkubwa zaidi wa cobalt, chuma muhimu kinachotumika katika utengenezaji wa betri za lithiam-ion kwa ajili ya simu, tablets na magari ya umeme. Mnamo 2022, akiba ya cobalt ya Congo ilikadiriwa kuwa karibu tani milioni nne za metric, ambazo ziko mashariki mwa nchi, huku akiba ya kimataifa ikiwa ni tani milioni 8.3. Wakati mahitaji ya cobalt yanaendelea kuongezeka, milki yake imekuwa ikitafutwa sana. Kwa bahati mbaya, hifadhi hizi kubwa zimeifanya Congo kuwa shabaha ya makundi mbalimbali, kama vile 'Mouvement du 23 mars' (M23). Kundi la M23, kundi la waasi lililoanzishwa na kuongozwa na Utawala wa Kagame nchini Rwanda na kufadhiliwa moja kwa moja na nchi za Magharibi kama vile Marekani, Uingereza, 'Israel' na Muungano wa Ulaya, limetwaa udhibiti wa miji mikubwa ya Mashariki ya Kaskazini na barabara zinazoelekea Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini. Ghasia zinazozidi kuongezeka zimesababisha vifo vya watu milioni 5.4 tangu 1998 na watu milioni 7 kuhama makaazi yao, wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Cha kushangaza, takriban wanawake 48 hubakwa kila saa, huku manusura mmoja akisimulia, "Walipokuwa wakinibaka, mmoja alisema: 'Tumekuja kutoka Rwanda ili kukuangamizeni." Walw waliobaki wajumbani mwao aghlabu hukabiliwa na utumwa katika migodi, ambapo cobalt inachimbwa na kuuzwa kwa bei ya chini kwa makampuni ya Magharibi kama vile Tesla na Samsung, miongoni mwa nyenginezo.

Mnamo Februari 2024, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa tahadhari kuhusu hali ya Congo, likielezea wasiwasi wake "kuongezeka kwa ghasia na mvutano unaoendelea katika eneo hilo." Licha ya "kulaani mashambulizi ya M23 na kuthibitisha uungaji mkono ubwana, umoja, na uadilifu wa eneo la DRC", baadhi ya wanachama wa Baraza la Usalama, kama vile Uingereza na Marekani, wameendelea kufadhili na kunufaika na vitendo vya mauaji ya halaiki vya kundi la Rwanda.

Wakati nchi za Muungano wa Ulaya zilisitisha ufadhili kwa Rwanda mwaka 2023 baada ya kuchangia zaidi ya euro milioni 20, Uingereza iliregesha haraka na inaendelea kutoa ufadhili kwa utawala huo, ikifumbia macho hatua zake kwa manufaa yake wenyewe.

Hasa, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak amekaa kimya kuhusiana na hatua za Rwanda, wakati ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Suella Braverman nchini Rwanda mwezi Machi 2023, inayoonekana wazi kwa ajili ya majadiliano ya hifadhi, inapendekeza ujanja mpana wa kidiplomasia. Mipango imebuniwa kushughulikia tatizo la uhamiaji wa Uingereza kwa kuwahamisha "wahamiaji haramu" hadi Rwanda, ambako kuna uwezekano wa kufungwa jela, kunyongwa, au kuhamishwa hadi nchi zao za asili kama wangenyanyaswa tena.

Uingereza sio nchi pekee inayonufaika na mafungamano yake na Rwanda. Kuhusika kwa Israel ni dhahiri katika silaha zilizotumwa Rwanda kuendeleza mauaji ya watu wa Congo. Vile vile, Israel imejadiliana kuhusu kupeleka "wahamiaji wa Khiyari wa Kipalestina" nchini Congo, ambako wangestahimili utumwa na unyonyaji katika shughuli za uchimbaji madini.

Cha kusikitisha ni kwamba, Marekani pia imehusishwa katika kufadhili utawala wa Kagame, na hivyo kusitisha uungwaji mkono wake mara tu shinikizo la kimataifa lilipoongezeka dhidi ya mauaji haya ya halaiki. Rai jumla ilipobadilika, Marekani "ilijitahidi kuepuka mgogoro mwingine wa sera za kigeni na ikatayarisha makubaliano ya pande nyingi ili kukomesha mapigano nchini Congo," POLITICO iliripoti.

Ufichuzi kwamba nchi za Magharibi kwa mara nyingine tena zinafadhili mauaji ya watu wasio na hatia kwa ajili ya kujinufaisha haupaswi kushangaza, kwani historia imeonyesha kuwa mataifa haya yanatanguliza maslahi yao ya kifedha badala ya masuala ya kibinadamu, haswa wakati maisha ya watu wasio wa Magharibi yanapokuwa yako hatarini. Mtindo huu wa ukimya na uungaji mkono unaenea hadi kwenye hatua za umbile la Kiyahudi dhidi ya Palestina, licha ya vifo vya zaidi ya watu 29,000, ikionyesha mshikamano thabiti na malengo ya kijiografia na kiuchumi.

Katika jamii inayoendeshwa na faida, maisha ya mwanadamu yanakuwa uharibifu wa dhamana, ambao nchi za Magharibi ziko tayari kupuuza. Wamejenga bahati yao juu ya unyonyaji na mauaji ya wale wanaowachukulia kuwa raia wa ulimwengu wa tatu, wakitambua matendo yao wakati tu raia wao wenyewe wanapodai azimio. Kuweka makumbushoi na kutazama kila mwaka "dakika za kunyamaza kimya kwa wahasiriwa" katika jaribio la kujiondolea lawama na kuahidi kwamba hili "halitatokea tena", licha ya uthibitisho wa kihistoria kwamba hakika litatokea tena. Lakini katika jamii inayoshuhudia vifo hivi moja kwa moja, ishara kama hizo hazitoshi tena kudumisha hali halisi iliyopo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Amatullah Hechmi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu