Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni ipi Hatua Inayofuata?

(Imetafsiriwa)

Tangu kuvunjwa kwa Khilafah, tunaona kwamba siku baada ya siku Ummah wetu unadhalilika zaidi na zaidi. Kuanzia vita dhidi ya nyumba ya familia, hadi mabomu yanayoangushwa, na hadi watawala wanaotuma vikosi vyetu vya majeshi kwenye matukio kama vile Phoenix Express. Haya ndiyo ambayo sisi kama Ummah tunayaona na hatuwezi kufahamu jinsi tulivyofika mbali hivi sana na pale tulipowahi kuwa mahali pa heshima na adhama. Tulikuwa Ummah ambao ulikuwa juu ya dunia, ambao wanadamu walitamani kuwa sehemu yake kuanzia kwa mfumo wetu wa elimu hadi mfumo wetu halisi wa mahakama. Tulikuwa na haki na uadilifu tofauti na mfumo mwingine wowote duniani, unaoleta amani na utulivu kwa wanadamu wote.

Ni aibu tunapotazama nyuma na kuona jinsi inavyoonekana kuwa mbali. Ni kama ndoto tuliyokuwa nayo na sio uhalisia. Labda baadhi yetu huanguka katika mawazo ya kuwa tuko mbali sana na kurudi. Tunasikia mambo kama, “Lo, Waislamu hao hawapo tena.” Au hata tunapowalea ndugu zetu katika jeshi tunaweza kuambiwa, “Hakuna tumaini kwao wala kutoka kwao.” Inaonekana baadhi ya watu wa Ummah huu, Umma wa Muhammad (saw), kutokana na shida tunazoziona na giza na ukungu wa Magharibi iliotuweka ndani yake, wanafikiri kwamba nuru iliyo mwisho wa handaki haipo, kana kwamba wameupa mgongo Ummah. Wanafikiri kwamba kuyaita majeshi, mara kwa mara kuleta dori yetu kama Ummah ili kuhuisha, au kwa kweli kuyaweka katika kazi ya kuleta mabadiliko si jambo ambalo ni lazima tujitahidi na kulitamani kila mara, bali je ni hilo ndilo ambalo Umma unapaswa kufanya? Kukata tamaa?

Jibu linaweza kupatikana tu katika Sera ya Mtume Muhammad (saw).

Mtume wa kwanza aliyetajwa kwa Muhammad (saw) alikuwa ni Yunus (as). Alikuwa ni mfano mkuu wa kile ambacho kingetokea unapoupa mgongo wajibu wako ambao ni kulingania njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Yeye (as) alipogeuka nyuma, aliishia kwenye tumbo la nyangumi. Kufadhaika kwake na Qawm yake kulimpelekea kukosa subira, na bila ya amri ya Mwenyezi Mungu (swt), yeye (as) akawapa kisogo watu wake. Naye akatambua, ndani ya tumbo la nyangumi, kosa alilokuwa amefanya.

[وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ فَنَادَى فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ]

“Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.” [Surah Al-Anbiya: 87]

Tunapoangalia jinsi Muhammad (saw) alivyojibu mashambulizi ya watu wake, ambayo hayakuwa tu mashambulizi ya maneno bali pia ya kinguvu, ambapo alitakiwa kuondoka nyumbani kwake na ambako alijitolea mhanga yote aliyokuwa nayo ili kutoa Dawah, tunamuona (saw) hakukata tamaa. Alikaa na subira, akiwalingania wengine kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu (swt), akiwalingania wengine kwenye njia ya Mwenyezi Mungu (swt), akiwalingania wenye uwezo wampe Nusrah. Kukataliwa baada ya kukataliwa baada ya kukataliwa, lakini bado hakuwa amekata tamaa. Kisha siku moja, Faraja (ufueni) kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ikaja. Mwenyezi Mungu (swt) akatoa Nusrah, kupitia kwa Ansari. Hatimaye ikatokea.

Enyi Umma wa Muhammad (saw), Umma bora kabisa ulioletwa kwa ajili ya wanadamu.

Msipoteze matumaini katika Ummah, wala ndugu zenu katika jeshi. Ndio, wengi wetu tumepotea njia, lakini kama kaka na dada katika Uislamu, ni juu yetu kuhuisha na kuvutana katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni lazima tukumbuke daima kwamba Mwenyezi Mungu (swt) haachi kitendo bila ya kuandikwa. Ni lazima tukumbuke kuwa sisi ni mwili mmoja na homa tunayohisi sote ni ile inayohitaji kupewa dawa na sio kupuuzwa. Tutaruhusu tu ugonjwa utuzonge ikiwa hatutatibu ugonjwa huu ambao wakoloni wameuweka kwenye mifumo yetu. Hivyo basi hebu na tuendelee kukumbushana juu ya wajibu alioamrisha Mwenyezi Mungu (swt). Hebu na tuendelee kuyaita majeshi, na tusikate tamaa, kwa sababu wao ni Waislamu kama sisi na sisi ni ndugu zao. Hatupaswi kukata tamaa juu yao. Kumbukeni kwamba Mtume (saw) amesema, «إذا قالَ الرَّجُلُ: هَلَكَ النَّاسُ فَهو أهْلَكُهُمْ» “Iwapo mtu atasema watu wameangamia, basi yeye ameangamia zaidi miongoni mwao.

Enyi Majeshi ya Waislamu,

Ummah unateseka kwa kila njia. Wameshambulia familia, wamewapiga mabomu watoto na wanawake wetu, na wametupeleka kwenye eneo hili lenye kina kirefu na lenye giza. Wametudhalilisha tena na tena. Sasa imetosha, na ni wakati wa nyinyi sasa kuchukua hatua. Tunajua kwamba nyoyo zenu zinauma kwa ajili ya Ummah. Sasa ni wakati wa kuweka hisia hizo katika mwendo na kusonga mbele kuukomboa ulimwengu wa Kiislamu. Ni wakati sasa wa kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir, na kufanya kazi kuleta mabadiliko. Kufanya kazi ya kurudisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Ni wajibu ambao mtaulizwa siku watakaposimama mashahidi. Komesheni mapungufu yenu na mutubu. Ni wakati sasa wa kuchukua hatua mpya kuleta mabadiliko. Kuweni miongoni mwa watu kama Ansari na mukomeshe udhalilifu. Ni wakati sasa wa kusimama na kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt).

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللَّهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad: 7]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Khadijah Hafidh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu