Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhadaifu wa Utaifa

(Imetafsiriwa)

Leon Effendi Baos alikuwa ni mjukuu wa daktari wa kijeshi wa Kiuthmani ambaye alikuwa amehamisha familia yake kutoka Ugiriki hadi Iraq, wakati fulani katika karne ya kumi na tisa. Chini ya sheria ya Kiuthmani, baba yake alichukuliwa kuwa Mgiriki. Mnamo 1897, wakati vita vilipozuka kati ya Ugiriki na Khilafah ya Uthmani, baba yake alikula kiapo cha utiifu cha kuhifadhi uraia ndani ya Khilafah.

Baada ya kugawanywa kwa maeneo ya Kiuthmani mnamo 1918 na Vikosi vya Washirika, Baos ilipewa uraia wa Kiarabu. Mnamo 1919, Baos alimwandikia barua Kamishna Mkuu wa Uingereza akitaka kuelewa ni jinsi gani angeweza kulazimishwa kuwa Muarabu. Pia alishangaa ni kwa jinsi gani Waingereza wangeweza kuunda “Hedjaz, Mesopotamia, Transjordanie, Misri, na Uturuki na sasa kuwalazimisha watu kuwa raia wa nchi hizi mpya”. Maafisa wa mamlaka ya Uingereza hawakuwahi kushughulikia wasiwasi wake na kesi yake ilibakia bila kutatuliwa.

Mnamo 1921, serikali ya Uingereza ilianzisha Imarati ya Transjordan na kumpa utawala Abdullah, kaka yake Mfalme Faysal. Eneo hilo lilichongwa na maafisa wa Uingereza ili kutumika kama zawadi kwa Abdullah kwa nafasi yake katika uasi wa Waarabu na pia kutumika kama eneo la kingo kati ya Syria na Palestina. Haya yalijiri baada ya majaribio ya Baraza Kuu la Syria (GSC) kupinga kutenganishwa kwa Palestina na Syria na Waingereza, na kukoloniwa kwake na walowezi wa Kizayuni.

Mnamo 1924, baada ya kuondolewa kwa Khilafah na Mustafa Kemal, Sharif Husayn, ambaye alikuwa amepewa cheo cha “Mfalme wa Hijaz” na Waingereza baada ya kuanzisha uasi wa Waarabu, alijitangaza kuwa Khalifa mpya. Hata hivyo, utawala wake kama Khalifa ulikuwa wa muda mfupi. Maafisa wa kikoloni wa Uingereza walihamisha msaada wao kutoka kwa Husayn hadi kwa Ibn Saud ambaye, mwaka 1925, aliiteka Makka na kumpeleka Husein uhamishoni. Ibn Saud alijitangaza kuwa “Mfalme mpya wa Hijaz”.

Baadaye, mwaka wa 1932, familia ya Saud iliunganisha maeneo yao katika kanda ya Hejaz na Nejd kufanya Ufalme wa Saudi Arabia. Mnamo 1936, wakati Wafaransa walipoandika mkataba wa Lebanon, maandamano yalizuka jijini Beirut, Sidon, na Tripoli, yote yakidai muungano na Syria. Maandamano haya yalipuuzwa na maafisa wa mamlaka ya Ufaransa ambao waliendelea na mipango yao ya kuitenganisha Syria na Lebanon.

Maeneo haya yote yaliwahi kuwa sehemu ya Khilafah ya Kiuthmani. Na kama Baos alivyodokeza katika barua zake, dola za kitaifa zilizojengwa juu yake hazikuwa chochote zaidi ya ujenzi wa kisanii wa maafisa wa kikoloni.

Baada ya wakoloni kuugawanya ulimwengu wa Kiislamu, walifanya kazi kuelekea kubadilisha mfumo wake wa utawala. Mifumo ya bunge ilianzishwa na maafisa wa kikoloni wangejihusisha na raia wao iwapo tu wangekubali kujipanga katika muundo wa vyama vya kidemokrasia. Walioletwa madarakani na wakoloni ni wale waliokubali sheria na kanuni zao. Kuibuka kwa dola za kitaifa katika ulimwengu wa Kiislamu kwa hiyo kunahusishwa kwa namna isiyoweza kutenganishwa na historia ya ukoloni na kulazimishwa na dola za Ulaya zilizotaka kuona ulimwengu wa Kiislamu ukigawanyika.

Swali, basi, ni kwa nini tunaendelea kukubali aina hii ya utawala kwetu sisi? Jibu, pengine, linaweza kupatikana katika kile Ibn Khaldun (rh) alichoandika karne nyingi zilizopita katika Muqaddimah yake.

Ibn Khaldun (rh) aliandika, أن المغلوب مولع أبدا بالاقتداء بالغالب في شعاره وزيه ونحلته وسائر أحواله وعوائده والسبب في ذلك أن النفس أبدا تعتقد الكمال في من غلبها وانقادت إليه إما لنظره بالكمال بما وفر عندها من تعظيمه أو لما تغالط به من أن انقيادها ليس لغلب طبيعي إنما هو لكمال الغالب “Mwenye kushindwa siku zote yuko makini kumuiga mwenye kumshinda katika kauli mbiu, mavazi, madhehebu, na hali na desturi zake zote. Sababu yake ni kwamba nafsi daima huamini ukamilifu kwa yule aliyeishinda, na amejisalimisha kwake. Ima ni kwa sababu anaona ukamilifu katika yale aliyompatia, ya kumtukuza, au ni kwa sababu ya kudanganywa na ukweli kwamba unyenyekevu wake hautokani na asili ya ushindi mwenyewe, bali ni kwa sababu ya ukamilifu wa mshindi.”

Kwa mgogoro wa hivi majuzi nchini Palestina, imekuwa muhimu kwamba ulimwengu wa Kiislamu uanze kutathmini upya aina yake ya utawala na kutabanni kwake kwa kanuni za Magharibi. Magharibi “bora” ndiyo iliyohusika na kuundwa kwa dola ya Kizayuni ambayo leo inafanya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu wa Palestina. Matendo yake yanahalalishwa na lugha ya dola ya kitaifa (“haki ya kuwa na dola”, “haki ya kulinda mipaka”) na ni lugha hiyo hiyo ambayo serikali za ulimwengu wa Kiislamu zinatumia kuhalalisha ukosefu wao wa kuchukua hatua dhidi ya Utawala wa Kizayuni.

Nukta ya Ibn Khaldun (rh) ni kwamba badala ya kudhani kwamba mshindi ni mkamilifu, lazima tuzingatie sababu za kushindwa. Ilikuwa ni kutelekezwa kwa Shariah na kuondolewa kwa Khilafah na Mustafa Kemal ndiko kulikouweka ulimwengu wa Kiislamu katika hali yake ya udhalilifu hivi leo. Ni kwa njia ya kuhuisha Shari’a pekee na kurejgshwa kwa Khilafah ambapo ulimwengu wa Kiislamu unaweza kujinasua hali zao za sasa.

[وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنكُمْ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ كَمَا ٱسْتَخْلَفَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ ٱلَّذِى ٱرْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّنۢ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًۭا ۚ يَعْبُدُونَنِى لَا يُشْرِكُونَ بِى شَيْـًۭٔا ۚ وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An Nur: 55]

Imepokewa kutoka kwa Jundab bin Abdullah kuwa amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) «مَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عُمِّيَّةٍ يُقَاتِلُ عَصَبِيَّةً وَيَبَّةً لِعَصَبِيَّةٍ فَقِتْلَتُهُ جَاهِلِيَّةٌ» “Mwenye kupigana kwa jambo lisilo bainika, kutetea ukabila, kukasirika kwa ajili ya ukabila, basi amekufa kifo cha Jahiliyyah.” Amesema Imam an-Nawawi katika Sharh yake,وَإِنَّمَا يَغْضَبُ لِعَصَبِيَّةٍ لَا لِنُصْرَةِ الدِّينِ، وَالْعَصَبِيَّةُ إِعَبِيَّةُ إِعَانَّةُ إِعَبِيَّةِ الظُّلْمِ “Hakika yeye hukasirika kwa ushabiki wa kikabila na kutoiunga mkono Dini. Ushabiki wa kikabila ni kusaidia taifa lake katika dhulma.” Neno asabiyah linamaanisha ukabila na fikra zake zote zinazohusiana kama vile utaifa. Kuna hadith nyingi zinazojadili ni kwa kiasi gani ukabila unachukiwa katika Uislamu. Kama Waislamu, tunaunganishwa kupitia Uislamu, kitambulisho chetu cha Kiislamu kinatawala juu ya kila kitu chengine. Vyenginevyo, kifo chetu kinafananishwa na kifo cha ‘Jahiliyyah,’ kana kwamba sisi si Waislamu. Tunakufa tukiwa na dhambi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Khalil Musab – Wilayah Pakistan

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Ni ipi Hatua Inayofuata?

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu