Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Gaza: Mwaka Mmoja ndani ya Mauaji ya Halaiki, Na Hakuna Msaada kutoka kwa Vikaragosi vya Magharibi

(Imetafsiriwa)

Tafadhali usiiruke video hii ili usaidie familia mjini Gaza!”

Tafadhali sambaza video hii ili uokoe familia yangu na mimi!”

Tafadhali toa mchango ili tuweze kumudu dawa hii ya babangu mgonjwa!”

Video hizi zimekuwa ada kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii. Maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wanaomba kwa kutapatapa watu wachangie kukusanya fedha zao ili kuwawezesha kununua mahema, vipumulio, dawa, chakula, au nafasi ya kutoroka kwao pekee walikowahi kukujua.

Wengi wa watu hawa hawakuzungumza Kiingereza mwaka mmoja uliopita. Wengi wao hawakutumia mitandao ya kijamii au kuchukua video zao mwaka mmoja uliopita. Walakini, hii imekuwa kawaida yao mpya. Kina baba ambao walifanya kazi kama madaktari, wahasibu, wanasheria, wamiliki wa biashara, walianza kujifunza Kiingereza ili kuja mtandaoni ili kuwaomba watu kusaidia. Haya yanajiri baada ya kuwasihi viongozi wa Waislamu kwa miezi kadhaa, baada ya kuwaomba usalama kwa miezi kadhaa na hawakupokea chochote isipokuwa ahadi tupu.

Umma umewaangusha watu hawa, viongozi wetu Waislamu wafisadi wamewaangusha watu hawa, na matokeo yake wametafuta njia tofauti za kuishi. Wameacha kuwasihi viongozi, na badala yake wamegeukia kizazi kipya, na wamesikiliza. Kizazi kipya, ambacho wengi wao bado wako shuleni, wanaishi na wazazi wao, wanafanya kazi ya mshahara wa chini, wamechukua muda, jitihada za kusambaza jumbe za watu wa Palestina. Wameshiriki katika kususia, maandamano, kupiga kambi. Wameandaa makongamano, wametaka haki na wao pia wamekutana na kimya kutoka kwa “viongozi” wetu.

Wengi katika Ummah wamekataa kuzungumza kuhusu Palestina, wakiogopa matokeo. Wengine wameeleza kuwa ilikuwa ni faradhi kumsikiliza kiongozi akinukuu ayah ambayo Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَطِيعُواْ اللّهَ وَأَطِيعُواْ الرَّسُولَ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللّهِ وَالْيَوْمِ الآخِرِ ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً]

“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [An-Nisa:59].

Hata hivyo, wanasahau Hadith ambayo kwayo Mtume (saw) amesema: Amepokea Ali: Mtume (saw) amesema, «لَا طَاعَةَ فِي مَعْصِيَةِ اللَّهِ، إِنَّمَا الطَّاعَةُ فِي الْمَعْرُوف فِي الْمَعْرُوف فِي الْمَعْرُوفِ» “Hakuna utiifu kwa yeyote katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Hakika utiifu ni katika mambo mema tu.” ( Ṣaḥīḥ al-Bukharī 7257, Ṣaḥīḥ Muslim 1840) Na Mwenyezi Mungu (swt) pia anasema:

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا * الَّذِينَ آمَنُواْ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالَّذِينَ كَفَرُواْ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ الطَّاغُوتِ فَقَاتِلُواْ أَوْلِيَاء الشَّيْطَانِ إِنَّ كَيْدَ الشَّيْطَانِ كَانَ ضَعِيفًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako. Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu.” [An-Nisa: 75-76].

Hawa vikaragosi mafisadi wa Magharibi hawapaswi, na hawatakiwi kuchukuliwa kuwa viongozi waaongofu wa Kiislamu. Ni vikaragosi katika udhibiti wa mikono ya viongozi wa Magharibi. Hili linathibitishwa zaidi na Ariel Sharon, waziri mkuu wa zamani wa uvamizi ambaye alisema: “Majeshi ya Misri hayatasonga bila idhini yetu.”

Ni dhahiri kwamba mwaka mmoja baada ya kuanza kwa mauaji ya halaiki, viongozi wa Waislamu hawajaweza kukata kamba wanazoshikilia mabwana zao. Kwa kufanya hivyo wanauthibitishia Ummah kwamba wao hawasimami pamoja na Waislamu. Wanasimama na pamoja uvamizi, na dola za Magharibi. Kwa hiyo ni wakati wa Ummah kuamka kama kizazi kipya. Ni wakati wa Umma kuungana chini ya Dini moja, bendera moja, kiongozi mmoja. Ni wakati wa sisi kuacha kuomba amani na usitishaji vita na kuanza kuitisha suluhisho halisi.

Kama mmoja wa waandamanaji alivyosema, baada ya Mgombea Urais Kamala Harris, kudai kifo cha kiongozi wa Hamas kitaleta amani: “kuomba amani, ni kumtaka Mpalestina arudi kufa kimya kimya.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Amatullah Hechmi

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Kufahamu Uke na Uume katika Uislamu

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu