Alhamisi, 05 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Fahali Wanapopigana, Zinazoumia ni Nyasi
“Sudan ni Mfano”

(Imetafsiriwa)

Sijapata katika historia msemo wenye ufasaha zaidi wa uovu wa ukoloni kuliko maneno ya Rabi ibn Amir, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, kwa kamanda wa Kifursi: “Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewatuma kuwatoa wanadamu kutoka katika ibada ya waja wengine hadi kwenye kumwabudu Mola wa waja wote.” Ijapokuwa kauli hii ilitolewa ili kubainisha lengo la ujumbe mtukufu wa Uislamu, unaowakirimu watu kutokana na kumwabudu kwao Mwenyezi Mungu, na kuhifadhi maisha yao, mali zao na heshima zao, hii wakati fulani hujidhihirisha kama kauli iliyo kinyume chake. Rehema ya Uislamu na uhuru unaowadhaminia watu unakinzana na utumwa wa watu na mataifa kwenye ukoloni, ambao unawaona kuwa ni mashini tu za kuzalisha dhahabu na pesa.

Baina ya Khosrau na Kaisari, Amerika na Ulaya, Urusi na China, kuna zama zilizopita na za sasa ambapo watu walifanywa watumwa, mali zao zikiporwa, na mifupa yao ikawekwa katika vita vilivyotumikia viti vya madhalimu tu. Mapambano haya ya viti vya utawala ulimwenguni sio kitu kipya. Ijapokuwa Uislamu ulikuja karne kumi na nne zilizopita na kuuokoa Ummah kutoka kwenye makucha ya Khosrau na Kaisari, ukiwaleta kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu na kuwatawala kwa wahyi, ili waishi katika raha na adhama, huku maisha yao, mali, hadhi, na heshima zao zikihifadhiwa, dola ya Kiislamu iliyakomeshwa zaidi ya karne moja iliyopita, na batili ikaanza upya kufanya watumwa mataifa na watu wake. Wanadamu waliunguzwa tena na moto wa Khosrau mpya. Ardhi za Waislamu zikawa ndio shabaha ya kudumu ya kudhulumiwa baada ya sisi kupoteza Khilafah yetu, dola hii tukufu iliyokuwa kiongozi asiye na shaka katika siasa za kimataifa, na hakuna nchi iliyosubutu kuvunja neno yake.

Sudan ni nchi yenye rasilimali nyingi. Hata kama Wamagharibi watadai kuwa ni masikini na wanahitaji msaada kutoka kwake na taasisi zake, hili ni dai la mwizi lenye malengo matatu: La kwanza ni kuwatoa Waislamu kutoka katika chanzo chao cha nguvu na kuendeleza udanganyifu wa udhaifu na upungufu wao. Pili ni kuhakikisha wanapora mali ya nchi bila kuvutia umakini na bila uwajibikaji au uangalizi. Muhimu zaidi, wanabakia kuwa mlinzi mkuu wa dola, kutekeleza sera zake na kutabikisha ajenda zake, kwa sababu, kwa urahisi kabisa, “hakuna jibini ya bure isipokuwa kwenye mtego wa panya.”

Kwa utatu huu: kupata mamlaka, kupora mali, na kuwaweka Waislamu nchini Sudan kuwa wanyonge na walio hatarini, nchi za dunia zinashindana kupata mgao nchini Sudan.

Yeyote anayeutazama mzozo wa Sudan kwa mtazamo wa kawaida atauona kama mzozo wa kijamii, rangi au kikabila, kama ambavyo vyombo vya habari vimekuwa vikitangaza. Anayetangaza angalu kwa ubora zaidi, ni mapigano kati ya wanajeshi na raia, mapambano ya kuwania madaraka. Hata hivyo, Muislamu mwenye ufahamu ambaye anaifanya itikadi ya Kiislamu (aqida) maregeo yake ya kisiasa, na ambaye anajua kwamba makafiri ni adui yake, na hivyo kuwachukulia hivyo, haruhusu kauli yoyote ya viongozi wa ukafiri impite bila kuitambua, wala hadanganyiki na urafiki wa uongo. Badala yake, anajua kwamba dola za ukafiri, huku zikijaribu kuzuia mwamko wa Ummah, zinafanya juhudi kubwa sana kufanya hivyo kila mahali. Hakuna kauli ya kisiasa ya Marekani au Ulaya kuhusu mzozo katika nchi kama Sudan, inayochukuliwa kuwa kikapu cha chakula duniani na inayoangazia njia muhimu za baharini, itakuwa ni maneno matupu au maoni tu. Badala yake, Muislamu lazima afahamu vyema kwamba kauli hizi za mfululizo kuhusu Sudan, madai ya usaidizi wa kibinadamu, na majaribio ya ujenzi upya, yote hayo ni majaribio ya kuhamasisha vibaraka na kuunda sera za mustakabali za nchi kwa mujibu wa maslahi ya mkoloni na kuimarisha ushawishi wake katika nchi hiyo.

Sudan imekuwa angazo la tahadhari ya Magharibi katika karne nzima iliyopita, tangu ushawishi wa Uingereza huko na uhusiano wake na Misri. Kisha, baada ya kutenganishwa na Misri, ushawishi wa Waingereza uliendelea kupungua na kutiririka hadi ushawishi wa Marekani ulipokaa huko wakati wa zama za Nimeiri na Bashir. Ulaya (Uingereza na Ufaransa) inaendelea kujaribu kuipenyeza kila fursa ilipotokea, kama walivyofanya katika kutumia suala la Darfur lakini wakashindwa, na wanaendelea kujaribu kuingia Sudan. Kwa hivyo, katika suala la umuhimu, Sudan ni muhimu na angazo makini kwa wahusika wakuu katika siasa za kimataifa. Umakini huu hauleti chochote kwa Sudan na watu wake isipokuwa vita kati ya watu wa wahusika wakuu hawa, wakiisaga ardhi na watu wake, huku wakiwa hawazingatii mamia ya maelfu ya watu waliokufa, mamilioni waliokimbia makaazi yao, au janga baya zaidi la njaa katika zama za kisasa.

Huu ni ubepari: mapambano ya wanasiasa kwa ajili ya vyeo na mali, kuendesha maisha na bahati za watu kwa bwana anayewafanya watumwa. Lakini kinaya ni kwamba, ili kudumisha udhibiti wake, inambidi kuachana na hadhi yake ya ukoloni na badala yake uingie kama mlinzi wa nchi dhidi ya adui uliyemtengeneza wenyewe. Hivi leo Marekani, ili kuwaondoa watu wa Ulaya kwenye mandhari na kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayevuruga harakati zake za kutafuta maslahi yake katika nchi hii na kwamba hakuna mshindani wa mali yake, inaendesha vita baina ya pande mbili ambazo kamba zake inazishikilia sambamba na maslahi yake. Watu wanafanywa kuamini kuwa Hemedti ni mtu wa upinzani na Burhan anawakilisha serikali. Kwa kweli, wote wawili wanatumiwa na vibaraka wa Marekani wenyewe: Misri, Saudi Arabia, na UAE. Wanacheza dori za ziada ambazo zinatimiza malengo yao kwa njia tofauti. Kuhu Burhan anatafuta kumakinisha mamlaka yake ndani kwa kuhamasisha uungwaji mkono wa watu na kubomoa ushawishi wa Ulaya kupitia hatua za kisheria, na nje, anafanya kazi ili kupata uhalali wa kimataifa. Hemedti, kwa upande mwingine, anafanya kazi ya kukamilisha kuondoa ushawishi wa Waingereza huko Darfur, haswa katika El Fasher, ambayo anajitahidi kuidhibiti, bila mafanikio licha ya majaribio yake mengi. Pia anafanya kazi ya kujijenga upya kama upinzani wenye silaha wenye uwezo wa kuwa na ushawishi uliobaki wa Ulaya katika harakati za mapambano ya silaha huko Darfur.

Hivyo, Amerika inahodhi eneo la Sudan kupitia watu wake wa pande zote mbili: serikali inayoongozwa na jeshi, linaloongozwa na Burhan, na upinzani unaoongozwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), vinavyoongozwa na Hemeti.

Serikali hizi mbalimbali, zikiongozwa na maadili yao ya kimada ya kibepari na njaa yao isiyoweza kushibishwa ya utajiri, hazina mashaka juu ya kuanzisha au kuchochea vita ili kupata faida, na hazijali idadi ya vifo vya kutisha, ukubwa wa mateso ya wanadamu, au maafa ya kibinadamu yanayotokea, mradi tu maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi yamepatikana.

Vita hivi vitaendelea kupamba moto nchini Sudan, na migogoro itaendelea, ikizidi kuwa mibaya kutokana na njaa, kuhama makaazi, na umwagaji damu, isipokuwa watu wa Sudan, hasa watiifu katika jeshi, wasimame dhidi ya malengo matatu ya Amerika: Kuigawanya nchi kwa kuitenganisha Darfur baada ya kuitenganisha kusini; kuhalalisha mahusiano na umbile la Kiyahudi lililonyakua Ardhi Iliyobarikiwa na kueneza ufisadi huko; na vita hivi vikali, viovu miongoni mwa Waislamu.

[إِنَّ فِي هَذَا لَبَلَاغاً لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ]

“Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.” [Al-Anbya 21:106]

#أزمة_السودان

#SudanCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Bayan Jamal

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu