Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jihad ni Nini? Sehemu ya 2

Je Ruhusa ya Jihad ni Lazima Itoke kwa Serikali?

Sheria za Jihad zimekatikiwa wala hazijafungwa na chochote, kama ilivyo bainishwa katika Qur’an:

كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ

 "Mmeandikiwa kupigana vita…" [Surah Al-Baqara 2:216]

Hivyo uwajibu wa Jihad hauna uhusiano wowote na kuwepo Khalifah au Serikali ya Kiislamu. Uwajibu wa Jihad utabakia ima Serikali ya Khilafah ipo ama la. Kwa muda, Wamagharibi wamejaribu kupandikiza mkanganyiko katika jambo hili kwa sababu wana hofu juu ya hisia za uungaji mkono Jihad walizonazo Waislamu. Hii ndio sababu Wamagharibi hawakutulia hata baada ya kuzikalia ardhi za Waislamu kwa ukamilifu, walikumbana na upinzani mkali, unaoendelea hadi leo. Hivyo wamagharibi wanajaribu kurudia kueneza propaganda kuwa Jihad hairuhusiwi bila mtawala na kuwa Jihad inahitaji ruhusa ya Khalifah au mtawala wa wakati huo. Baadhi ya Waislamu wameathiriwa na propaganda hizi na kukubali juu ya matokeo. Wengine hata kutamka kuwa kupigana Jihad pasi na ruhusa kutoka kwa Khalifah ni Haramu, japokuwa tabaka la watawala hukusanya vibaraka wa Amerika, kama Musharraf na Karzai. Kwa vipi watawala hawa waruhusu upinzani wowote dhidi ya Amerika? Hivi ndivyo Amerika ilivyotekeleza jaribio lililofeli kupunguza upinzani dhidi yao, kwa kuiunganisha Jihad na watawala hawa. Ifahamike wazi kuwa Ummah hauna mkataba wa kisheria na watawala hawa wa kutawala. Inapo kosekana Bay’ah ya kutawala kwa Uislamu, watawala hawa wa sasa sio viongozi halali kwa mujibu wa sheria, ili iwe utiifu kwao kuwa ni lazima. Hakika hawa ni waporaji tu wa madaraka. Katika Uislamu, Mtawala huwa wa halali pale tu atakapo pata ridhaa ya kutiiwa kwa sharti ya kuwa atatekeleza Uislamu juu yao. Hivyo, hakuna kati ya hawa watawala anayestahiki kutiiwa, au kuweza kutukataza kupigana dhidi ya Amerika au sisi kutaka ruhusa yao kwa kupigana Jihad ya kujilinda. Watawala wa Pakistan wameondoa Aya za surat At-Tauba katika mtaala wa elimu kwa maagizo ya Amerika ili kudhoofisha upinzani dhidi ya uvamizi kutoka nje katika akili za vizazi vipya. Katika historia, Uingereza ilivilea vikundi miongoni mwa Waislamu, ambavyo vilitangaza utiifu kwa Utawala wa Uingereza kwa kukataa Jihad. Vizazi vyao vya sasa bado vinaendeleza juhudi hizi, kwa Maqadiyani kufanya ubatilishaji wa Jihad kuwa ni fikra msingi, inayowafanya watoke nje ya kundi la Waislamu, pamoja na kukataa kwao Mwisho wa Utume.

Hivyo, uwajibu wa Jihad haufungwi na uwepo wa Khalifah wala kuunganishwa na ruhusa ya mtawala wa sasa kwa sababu hukumu za Jihad katika Quran na Sunnah ziko wazi na haziwezi kuwekewa kikomo au kubadilishwa. Hata hivyo, lazima iwekwe wazi hapa kwamba japokuwa uwajibu wa Jihad haukushurutishwa juu ya kuwepo kwa mamlaka ya Uislamu, kama Khalifah ametawazwa kwa mujibu wa Sharia, suala la Jihad huamuliwa na Khalifah, kama zilivyo wajibati nyengine za kijumuiya zinavyosimamiwa kupitia kwake. Khalifah atasimamia Jihad kulingana na Ijtihadi yake, hata kama atakuwa ni dhalimu au asiye muadilifu, lakini akiwa katika wadhifa wake, hubakia pekee juu ya majukumu yake. Ni wajibu kwa raia kufuata maoni yake. Abu Dawuud amepokea kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mtume (saw) amesema,

«اَلْجِھَادٌ وَاجِبٌ عَلَیْکُمْ مَعَ کُلِّ اَمِیْرٍ بَرًّا کَانَ اَوْ فَاجِراً»

“Jihad ni wajibu juu yenu pamoja na kila kiongozi (Amir), ima awe ni dhalimu au muovu.” Hii hata hivyo, haimaanishi kuwa uwajibu wa Jihad umeondoshwa panapo kosekana Serikali ya Khilafah. Ni lazima kwa Khalifah aongoze jeshi na moja kwa moja achukue udhibiti wa masuala yake. Hairuhusiki kwake kuwa ni kama alama tu ya Amiri jeshi Mkuu.

Jihad Ndogo na Jihad Kubwa

Imeenea sana miongoni mwa Waislamu kuwa kupigana dhidi ya maadui wasiokuwa Waislamu ni Jihad ndogo, na kupigana mtu dhidi ya nafsi yake ni Jihad kubwa. Hadith ya Mtume (saw) kwa kawaida hutolewa kama Ushahidi,

«رَجَعْنَا مِنَ الْجِھَادِ الْاَصْغَرِ اِلَی الْجِھَادِ الْاَکْبَرِ»

   “Tumeregea kutoka kwenye Jihad ndogo kuelekea kwenye Jihad kubwa” Wakauliza, “Ni ipi Jihad kubwa”? Mtume (saw) akasema, “Hii ni Jihad dhidi ya nafsi yake mtu” Hadith hii inayodhaniwa kuwa ni dalili ni yenye kukataliwa katika mapokezi na maana. Katika mapokezi, hadithi hii ni ya kuzushwa. Hafidh Al-Iraqi na Ibn Hajar Al-Asqalani, ambao ni mabingwa katika elimu ya Hadith, wamesema kuwa hii sio Hadith ya Mtume (saw), bali ni maneno ya mtu mmoja akiitwa Ibrahim Ibn Abi Eela. Imam Suyuti pia ameikataa “hadith” hii katika utungo wake maarufu Al-Ma’jam Al-Saghiir. Zaidi ya hivyo, katika maana, hii inagongana na sheria za Quran na Sunnah zenye kuzingatia Jihad dhidi ya maadui makafiri kuwa ni katika matendo bora zaidi. Muadh bin Jabal amepokea kuwa Mtume (saw) amesema,   ,

«رَأْسُ الْأَمْرِ الْإِسْلَامُ وَعَمُودُهُ الصَّلَاةُ وَذِرْوَةُ سَنَامِهِ الْجِهَادُ»

“Msingi wa jambo ni Uislamu, na nguzo yake ni swala, na kilele chake ni Jihad” (Tirmidhi).

Kwa hakika lengo la propaganda inayo husiana na Jihad kubwa na Jihad ndogo ni kuwafanya watu waridhike na kuwacha uwajibu wa Jihad. Inawapa matumaini ya urongo ya kuwa hawahitajii Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, ikiwa tu watajiweka mbali na kulewa, kuzini, kusema urongo na usaliti.

Kupigana Baina ya Waislamu sio Jihad

Kupigana baina ya Waislamu sio Jihad wala hakuna kifo cha shahid ndani yake, japokuwa malipo kama ya shahid huwezekana wakati kundi moja kama litaunga mkono haki na jengine likiwa linaunga mkono batil, kama mapigano baina ya Serikali ya Khilafah dhidi ya Waislamu waasi. Hata hivyo, mapigano haya sio Jihad na anaye kufa hapo hazingatiwi kuwa ni shahidi japokuwa kuna malipo yanayo lingana nayo. Hukumu zinazo husiana na mapigano haya ni tofauti na Jihad na hakuna ngawira wala yeyote kufanywa mtumwa. Hivyo hivyo, kupigana dhidi ya aliyetwaa utawala, akajitwalia uongozi kwa nguvu, kumuondosha kwa kutumia nguvu huitwa Khuruj. Khuruj pia haiingizwi ndani ya sheria za Jihad. Vile vile ikiwa Muislamu anadhuru maisha, mali au heshima ya Muislamu mwengine, basi Muislamu anaye dhuriwa ana haki ya kujilinda, lakini pia sio Jihad. Hivyo Jihad ni kupigana dhidi ya wasio kuwa Waislamu ili kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu (swt) liwe juu, wakati kupigana dhidi ya Waislamu sio Jihad, hata kama mapigano yatakuwa ni sahihi kwa mujibu wa Uislamu. Tafsiri za Jihad zilizotolewa na wanazuoni zimetaja wazi sharti la mapigano dhidi ya Makafiri. Hivyo, Khuruj na kuhifadhi maisha ya mtu, mali na heshima hayakutajwa na wanazuoni katika milango ya Jihad.

Mbali na masuala yaliovuliwa hapo juu, kupigana baina ya Waislamu ni Fitna na wanaokufa katika pande zote mbili ni watu wa motoni. Mtume (saw) amesema,

«إِذَا الْتَقَى الْمُسْلِمَانِ بِسَيْفَيْهِمَا فَالْقَاتِلُ وَالْمَقْتُولُ فِي النَّارِ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ هَذَا الْقَاتِلُ فَمَا بَالُ الْمَقْتُولِ قَالَ إِنَّهُ كَانَ حَرِيصًا عَلَى قَتْلِ صَاحِبِهِ»

“Watapopigana Waislamu wawili, muuwaji na anayeuliwa wote wataingia motoni, Sahaba akauliza: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Huyu muuwaji ni sawa, vipi kwa aliyeuliwa kuingia motoni? Akasema (saw): Kwa sababu naye alitaka kumuuwa ndugu yake MUislamu.” (Bukhari). Maisha, mali na heshima ya Waislamu wote sio halali kwa Muislamu mwengine, isipokuwa kwa dalili za kisheria, katika hali ya mivutano baina ya makundi mawili, jukumu la Waislamu ni kuwarejesha kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[وَإِن طَائِفَتَانِ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ اقْتَتَلُوا فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا فَإِن بَغَتْ إِحْدَاهُمَا عَلَى الْأُخْرَى فَقَاتِلُوا الَّتِي تَبْغِي حَتَّى تَفِيءَ إِلَى أَمْرِ اللَّهِ فَإِن فَاءتْ فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ]

Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenziwe, basi lipigeni linalodhulumu mpaka liregee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki. [Al-Hujrat: 9].

 Kwa hivyo Waislamu kupigana na Waislamu ni Fitna, kama ilivyokuwa vita vya Iran na Iraq au katika vita baina ya Jeshi la Pakistan na wapiganaji wa kikabila wanaovamia jeshi kote Pakistan.

Katika hali ya karibuni, wakati watawala wasaliti na vibaraka wa Pakistan, chini ya ushawishi wa Makafiri, walitumia vikosi vya Waislamu dhidi ya Waislamu Mujahidina na matokeo yake vikundi vya Jihad vikashambulia majeshi hayo, imeleta mazingira ya Fitnah kwa Waislamu. Ni wajibu juu ya Waislamu kuyaregesha makundi haya kwenye hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt). Na njia yake ni kuwan’goa watawala hawa kwa kufuata Njia ya Mtume (saw) na kusimamisha Khilafah na kisha kuwatoa Amerika kutoka eneo kwa kuwapa jukumu la Jihad kwa majeshi haya.

Katika Uislamu, kisasi ni dhidi ya mtu binafsi na sio dhidi ya taasisi. Hivyo yeyote anaye fanya uhalifu, kisasi kitachukuliwa kwake. Sheria imetoa hukumu za wazi na haikuwachwa kwa matashi ya watu. Kulipiza kisasi kwa Waislamu nje ya uwanja wa mapambano katika makao ya wanajeshi na taasisi mbali mbali, kwa sababu ya kuhusiana kwao kusikokuwa moja kwa moja katika mauwaji, pia sio dalili ya sawa. Ikiwa mantiki hii itachukuliwa kuwa ni sahihi, basi kila raia atatambuliwa kuwa ni muwezeshaji wa vita hivi kwa sababu analazimishwa kulipa kodi kwa serikali, ambazo zimetumika na watawala hawa wasaliti kwa kulipeleka jeshi la Pakistan hapo nyuma katika maeneo ya kikabila. Hata mujahidina wanachangia kwa njia isio ya moja kwa moja kwa wasaliti hawa, kwa kutumia huduma za simu na kulipa bili za huduma za ummah. Jeshi na Waislamu wa vikosi vya kikabila wote ni rasilimali za Ummah huu. Kuuwa maafisa na wapiganaji wengi zaidi sio suluhisho bali ni kazi ya makruseda makafiri.

Jihad Sio Njia ya Kusimamisha Khilafah:

Kama ilivyotajwa awali, Jihad ni utukufu na kilele cha Uislamu, na ni jukumu kubwa na ni lenye kubeba malipo makubwa. Hivyo hivyo, wajibu wa kusimamisha Khilafah ni wajibu wa kipaumbele. Ni msingi wa kusimamisha Uislamu. Itaregesha hukumu za adhabu, na Jihad itaregea katika uhalisia wake wa asili; uhai, mali, itikadi, heshima na ardhi za Waislamu zitahifadhika na Waislamu kwa mara nyengine watachukuwa uongozi wa Ulimwengu. Hata hivyo, ni muhimu kutia mkazo kuwa waajibat hizi mbili ni zenye kutofautiana. Kila moja ina mahitaji mbali, njia, nyenzo na mbinu. Kuhusiana na suala la kusimamisha Khilafah, njia yake huchukuliwa kutoka katika Maisha ya Mtume (saw) katika Makkah, wakati kizazi cha mwanzo kikiwa kinaharakati za kuhangaikia kusimamisha Serikali ya Kiislamu, ardhi ya kugura. Katika kipindi hichi, Mtume (saw) alikataza wazi wazi makabiliano ya kijeshi na alipoombwa kuyaruhusu alikazia njia yake kwa kusema,

«إِنَّا لَمْ نُؤْمَرْ بِذَلِكَ بعد»

“Hakika sisi hatujaamrishwa hayo bado” (At-Tabaqaat ya Ibn Saad). Hakika, Masahaba wote (ra) bila shaka ni wenye kuheshimika na kustahiki taadhima zaidi kuliko Waislamu wengine wote. Hata hivyo, Mtume (saw) alifanya mapambano ya kifikra na ya kisiasa tu. Yeye (saw) hakutumia mada (nguvu) kabisa katika kukabiliana na mateso, kutengwa, propaganda, vitisho, mauwaji na kashfa. Hatimaye alisimamisha serikali Madina kwa kuomba Nusrah, akiwashawishi watu wenye nguvu, kujenga rai jumla kupitia Mus’ab bin Umair (ra). Kinyume chake, Jihad kiasili hukusanya utumiaji wa vitu kama panga, farasi, upinde na mishale, pamoja na mbinu zitumikazo sasa zikiwemo ndege za kivita, mabomu, makombora, vifaru na silaha za kimbinu za nyuklia. Jihad haitekelezwi kupitia maandamano, mikutano ya wanahabari, semina, makongamano ya amani na mijadala. Jihad hutekelezwa katika uwanja wa mapambano kama Mtume (saw) alivyo tekeleza katika Badri, Uhud, Khandaq, Mu’tah, Tabuuk na vita vyengine. Kwa hivyo Waislamu hawawezi kufikia malengo yao kwa kuchanganya waajibat hizi mbili.

Hivi leo baadhi ya wanazuoni, wanaohusishwa na Jihad, wametangaza mapambano ya silaha dhidi ya watawala katika ardhi za Waislamu, kama ni njia ya kusimamisha Serikali ya Kiislamu. Wanatumia istilahi ya “Jihad” kwa mapambano haya ya kijeshi, na huhusisha watu wote kwenye utawala ambao ni sehemu ya muundo wa serikali. Fikra zao zimeegemea juu ya dhana zifuatazo:

1. Watawala wa sasa wameuasi Uislamu. Watawala hawa wamepandikizwa kwa mujibu wa mipango ya wakoloni, na Uislamu wao ni ishara tu, hata kama ni wenye kuonekana wanaswali na kufunga, lakini kwa kweli wameuasi Uislamu. Hivyo amani ni kwa Waislam tu na Jihad ni kwa Makafiri na Watawala waasi. Hivyo kuwapiga vita inajuzu.

2. Qaida, (ﻤﺎ ﻻ ﻴﺘم اﻟواﺠب إﻻ ﺒﻪ ﻓﻬو واﺠب)

“Kila chenye kuhitajika kukamilisha wajibu nacho ni wajibu”. Kwao wao, kwa kuwa kusimamisha Serikali ya Kiislamu ni wajibu; hivyo, kila chenye kuhitajika kukamilisha wajibu huu huwa vile vile ni wajibu, hata kama ni kupigana na watawala.

3. Dalili ya uvamizi. Mataifa ya kikoloni kwa hakika yamevamia nchi zetu na watawala hawa ni vibaraka wao. Hivyo, kama ilivyo kuwa Jihad ni wajibu juu ya uvamizi wa makafiri, hivyo hivyo, kuwapiga vita watawala hawa ni wajibu, kwa kuwa wanawakilisha nguvu ya wavamizi.

4. Dalili ya Ukafiri wa wazi; Wanaitaja kauli (Fatwa) ya Qadhi Iyad aliposema, “Ikiwa mtawala anashikilia kutekeleza Ukafiri, kubadilisha Sharia na kuzusha hadithi, basi utiifu kwake hautofaa na ni lazima kumuasi, kumuondosha na kumbadilisha kwa mtawala muadilifu, ikiwezekana.” Kwa kuwa watawala hawa wanayafanya haya na hawako tayari kuwachana na madaraka na wana majeshi makubwa kuhifadhi tawala zao; kwa hivyo, hakuna njia nyengine ya kusimamisha Serikali ya Kiislamu isipokuwa kwa kupigana nao.

Kutokana na dalili hizi, majibu yao ni kama ifuatavyo:

1. Dalili za uasi: Ushahidi juu ya uasi kwa kweli huchukuliwa kutoka aya 44, 45 na 47 za Surah Al-Maida zenye maana kuwa yeyote asiye hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu (swt) ni madhalimu, mafasiki na makafiri. Hakika hii ni hukumu ya wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa mujibu wa maelezo ya aya hizi kutoka kwa Ibn Abbas (ra), yeyote anaye kanusha hukumu ya Quran katika Sharia ni kafiri, na yeyote anaye sema kuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu (swt) isitekelezwe ni kafiri, na yeyote anaye sema kuwa sheria za wanaadamu ni nzuri zaidi ya sheria za Mwenyezi Mungu ni kafiri, na yeyote asiye kataa hukumu za Mwenyezi Mungu (swt), lakini anasema kuwa inaruhusiwa kutekeleza chochote kutoka kwa kisichokuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu (swt), huwa ni kafiri kwa sababu hakuziwekea kikomo sheria za Mwenyezi Mungu (swt), hata kama atasema kuwa hukumu za Mwenyezi Mungu ni nzuri zaidi. Hata hivyo, kama mtu atatawalisha na kuhukumu kinyume na hukumu za Mwenyezi Mungu (swt) lakini haziamini hukmu za kikafiri bali anazichukia, hii ni “Kufru isiyo Kufru” ikimaanisha hii ni kufru lakini ilio ya chini ya kufru. Hata hivyo, kwa hakika ni dhambi kubwa na bila shaka imekatazwa. Hivyo ataitwa dhalimu na fasiki lakini sio kafiri. Zaidi ya hivyo, dalili za wazi zinahitajika kuhakikisha uasi. Katika hadith iliyotolewa na Ubadah Ibn Samit (ra), Mtume (saw) amesema,

  «إِلَّا أَنْ تَرَوْا كُفْرًا بَوَاحًا عِنْدَكُمْ مِنَ اللَّهِ فِيهِ بُرْهَانٌ»

“…isipokuwa mkiona ukafiri wa wazi ambao mna dalili ya wazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu”. Dalili ya wazi maana yake ushahidi usio na shaka. Kwa hivyo, kutangaza uasi kwa watawala wote, mawaziri wao, washauri na maafisa wakuu kwa mchoro tu wa kalamu sio sahihi.

2. Qaida ya “Kila chenye kuhitajika kukamilisha wajibu…” ni qaida ya jumla na hutumika tu wakati hakuna dalili ya moja kwa moja kuhusu ukweli kwa kile ambacho hukumu huvuliwa. Hivyo qaida hii haiwezi kutumika wakati dalili ya moja kwa moja inapatikana. Kwa kuwa kuna patikana njia ya wazi katika Serah inayofungamana na usimamishaji wa Serikali ya Kiislamu, utumiaji wa qaida hii kwa ajili hiyo hiyo sio sahihi. Kwa hiyo kuwan’goa watawala wanaotekeleza Ukafiri na kuwabadilisha kwa kumuweka Khalifah mwenye mamlaka kwa mujibu wa Sharia, hukumu zinazopatikana kutoka kwenye Serah ni lazima zifuatwe. Haziruhusu mapambano ya kimada. Yeye (saw) hakuruhusu mapambano ya kimada katika jitihada za kusimamisha Serikali ya Kiislamu Madina. Kwa hivyo, hata leo, tunafungika kufuata hukumu za mapambano ya kifikra na kisiasa na kuomba Nusra kwa ajili ya kusimamisha Serikali ya Kiislamu. Kuzikiuka hukumu hizi ni sawa na kwenda kinyume na hukumu za Sharia.

3. Ushahidi wa uvamizi umejengwa juu ya ufahamu wa kuwa watawala hawa huwa ni kama vibaraka wa Makafiri na Makafiri wakoloni wamekita udhibiti wao juu ya nchi za Waislamu, ambapo kila Muislamu hulazimika kwenye Jihad ya kujihami. Kuna kosa katika ufahamu mbaya wa uhalisia yaani uhalisia wa udhibiti wa ukoloni. Kama udhibiti wao ni wa kijeshi, basi ni mapambano ya kijeshi dhidi ya jeshi. Hata hivyo kama uhalisia wa uvamizi sio wa kijeshi bali ni ukoloni mambo leo wa kisiasa na uchumi, basi matendo yanayo hitajika ni tofauti. Hivyo swali huzuka kuwa je, hali ya Pakistan ni sawa na hali ya Palestina na Afghanistan? Katika nchi kama Palestina na Afghanistan, majeshi ya nchi za kikafiri yameangamiza mamlaka ya Waislamu kwa kufanya uvamizi wa kijeshi, ambapo udhibiti wao juu ya nchi kama Pakistan, Uturuki na Misri ni kutokana na ushawishi wa kisiasa, na sio kutokana na uvamizi wa kijeshi. Usalama katika nchi hizi bado upo chini ya umiliki wa majeshi ya Waislamu, na Makafiri wana ushawishi wa kisiasa tu. Majeshi ya Waislamu yapo katika nchi hizi kiuhakika na ulinzi upo katika mamlaka yao.

Katika hali hii, badala ya kumaliza ushawishi wa kisiasa wa mataifa haya ya kikafiri na kuyashawishi majeshi haya ya Waislamu kutekeleza hukumu za Uislamu, kuuwa vikosi vyetu vya Waislamu na kuharibu miundo mbinu ya nchi ni madhambi na madhara. Uislamu umetatua tena tatizo hili kupitia Njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) inayo tufundisha kufichua mipango na hila za Ukoloni, pamoja na njama za vibaraka hawa wakiwa na Makafiri kupitia mivutano ya kisiasa katika mawanda ya ummah. Hii itapelekea kudhoofisha ushawishi wa wakoloni kupitia kudhoofika kwa vibaraka hawa mbele ya watu. Msumari wa mwisho katika jeneza la utawala wao muovu ni kuomba Nussrah kutoka kwa watu wa utawala, kama wale walio na mioyo safi katika watu wa mamlaka kuunga mkono katika kusimamisha Khilafah kwa kuun’goa mfumo. Hivyo, rasilimali kubwa ya nchi itatumika na mamlaka ya Khilafah, ikiwemo uwezo madhubuti wa majeshi ya Waislamu, ambayo yanatumiwa hivi sasa na wakoloni kupitia watawala hawa vibaraka.

4. Kuhusiana na suala la dalili ya Ukafiri wa wazi, dalili hizi zimetumiwa nje ya muktadha kwa sababu dalili zinazolazimisha utumiaji wa upanga dhidi ya mtawala ni kwenye dola ya Kiislamu, na sio kwenye dola ya Kikafiri. Hadith ziko wazi katika suala la Imam kuwa anafuatwa wakati hukumu ya kutomtii imetolewa kwa Ukafiri wa wazi. Utiifu ni kwa Imam ambaye ametawazwa kisheria tu. Zaidi ya hayo Hadithi hizi zimekataza kutumia panga muda wa kuwa “anatekeleza Salah (maana Sharia),”ambazo hupatikana tu chini ya Khalifah. Kwa hivyo, kutumia hukumu inayo husiana na Dar ul Islam kwenye ardhi za ukafiri ni makosa ya wazi.

Zaidi ya hayo, kutafiti “njia ya Jihad” inaonyesha kuwa “njia” hii ni kinyume na njia ya Mtume (saw) ambayo ni, kubadilisha nadharia za uongo, fikra na hisia za jamii na kuweza kuwashawishi kupitia Da’wah. Hivyo hivyo, wale wanaofuata “njia ya Jihad” wanashawishiwa juu ya kutumia nguvu, kulazimisha, kushurutisha na kuadhibisha katika kutekeleza mfumo. Hivyo “njia” hii sio ya sawa katika namna zote mbili kisharia na uhalisia. Inaelekea kuwa “njia” hii inafuatwa na baadhi ya Waislamu, kama ni lipizo kwa matendo maovu ya kutisha yanayo fanywa na Makafiri dhidi ya Waislamu, wanaotaka kulipiza kisasi kutokana na hisia za Kiislamu, lakini wanaisahihisha “njia” hii kupitia dalili za Kisharia baada ya kuichukuwa kwa kuitumia. Kuendesha Serikali yoyote, inatakiwa kuwa na uoni wa wazi wa nidhamu zake na watu wanaozielewa kwa upana. Kwa bahati mbaya, wale wenye shauku ya mabadiliko kupitia Jihad hawawakilishi mfumo wowote wa Kiislamu wala kundi la waliopevuka kisiasa na uoni wa kuweza kuendesha Serikali ya Khilafah. Waislamu hawa pia wamekosa utafiti wa ndani wa mazingira na matukio ambapo baadhi yao hutangaza “Imarah” katika mji mmoja na wakati mwengine hutangaza maafisa na viongozi wa “Imarah ya Kiislamu” katika kijiji chengine, kilicho chini ya majeshi ya uvamizi. Hakika, Jihad ni wajibu mkubwa na katika matendo bora zaidi. Hata hivyo, kuichanganya na waajibat nyengine hupelekea kutekelezwa kusiko sahihi kwa wajibu wowote kulingana na Sharia.

Ulinganizi kwa Uislamu ndio kitovu cha sera ya mambo ya nje ya Serikali ya Kiislamu na Jihad ni njia yake ya kivitendo

Msingi wa sera ya mambo ya nje ya Serikali ya Khilafah ni kuupeleka Uislamu Ulimwenguni kote. Hii ndio iliokuwa sera ya Serikali ya Khilafah ambayo ilidumu kwa kipindi cha miaka 1300 iliopita. Ni suala la wakati tu kabla ya kurudi tena katika medani ya kimataifa. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

 [وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَالَمِينَ]

“Na hayakuwa haya ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote” [Al-Qalam: 52].

Na amesema (swt),

[وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا كَافَّةً لِّلنَّاسِ بَشِيرًا وَنَذِيرًا وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na muonyaji. Lakini watu wengi hawajui” [Saba: 28].

Ni wazi kutokana na aya hizi kuwa Uislamu ni kwa walimwengu wote, sio kwa Waislamu pekee. Kwa hivyo, kupeleka neema hii kwenye mataifa mengine ni jukumu letu. Baada ya kusimamisha Khilafah, ni wajibu juu ya Khalifah kuondosha Serikali au mamlaka yoyote inayozuia Da’wah ya Kiislamu kuwafikia watu, hata kama itahitajia kutumia nguvu. Kwa hivyo kutekeleza Da’wah ya Kiislamu ni msingi wa mahusiano ya Serikali ya Khilafah na Serikali nyengine. Zaidi ya hivyo, utekelezaji wa kivitendo wa mfumo wa Uislamu juu ya wasiokuwa Waislamu ni njia bora zaidi ya kuudhihirisha kwao Uislamu. Hivyo, uandaaji wa Jihad ya kushambulia, kwa Ushahidi uliotajwa hapo juu, chini ya Khilafah ni njia ya kivitendo ya kueneza mfumo wa Uislamu na kuuonyesha Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu, kwa kuuweka mbele yao katika muundo wa kivitendo. Wajibu wa Serikali ya Khilafah ni kuutekeleza Uislamu kwa ndani na kuueneza ulimwenguni kupitia Da’wah na Jihad. Hili ndilo lengo na uhalali wa Serikali hii.

Jihad ni jukumu kubwa juu ya Ummah huu kuwakomboa walimwengu kutokana na ukatili. Leo Mhindu wa muonekano wa Shudar au Harijan India analazimishwa kuishi katika hali mbaya zaidi kuliko mnyama. Raia wa kawaida Ulaya anataabika kutokana na mfumo wa kirasilimali na asilimia 30 hadi 50 ya mali yake inakwenda kwa tabaka dogo la warasilimali kwa jina la kodi. Wanawake katika nchi za Magharibi wamefanywa lengo la soko la bidhaa kwa jina la uhuru. Katikati ya yote haya, nani atawakomboa watu wote hawa kutokana na ukandamizaji? Je, tuwaache katika madhila haya juu ya msingi wa kanuni ya uongo ya “mshikamano wa amani”? Haiwezekani! Uislamu unatuongoza kuwakomboa kutokana na udhalilifu huu, ambapo huwezekana tu wanapopewa haki zao kupitia Uislamu, mfumo uliomkomboa mwanaadamu kutokana na utumwa wa mwanaadamu miaka 1400 iliopita. Uislamu umewapa haki wanawake, watumwa na madhaifu na kuwaondoa madhaifu kutokana na ufukara. Hivi leo, kwa mara nyengine katika hali ya kuwa nyuma ya wakati wa sasa, Uislamu utawakomboa watu kutokana na maisha ya kinyama. Hii ndio sababu ya kuwa serikali ya Khilafah hutekeleza Jihad kuwatoa wanaadamu katika kiza hiki. Jihad sio kuwalazimisha Makafiri kuingia kwenye Uislamu; bali, ni kuumaliza huu mfumo wa Kikafiri unaomkandamiza mwanaadamu. Mwenyezi Mungu (swt) ametaja wazi kuwa sheria zisizo za Kiislamu ndio sababu ya dhulma. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

    [وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أنزَلَ اللّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Na wasiohukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu” [Al-Maida: 45]

Hivyo, kama kweli tuna wasi wasi kumhusu mwanaadamu, basi tuanze kupanga Jihad kupitia kuisimamisha Khilafah Rashida, ambayo itaeneza mfumo wa Kiislamu na kuwahifadhi wanaadamu kutokana na dhulma za mfumo wa Kikafiri.

Hivi leo, Jihad haitekelezwi kama inavyo takiwa na “Jihad ya mashambulizi” haiwezekani hata kufikiriwa, kwa kuwa hakuna Khalifah anaye tawala juu ya Ummah hivi leo. Khalifah atarudisha Jihad kutokea ilipo achwa wakati wa Khilafah Uthmaniyyah ili, wakati huu, Waislamu waifungue Ulaya na Amerika zikiwa chini ya Uislamu. Kwa mujibu wa bishara za Mtume (saw), hakutabakia kibanda au nyumba ambayo Uislamu hautoingia, kutoa heshima kwa wenye kustahiki heshima kupitia kuukubali Uislamu na kutoa udhalilifu kwa wenye kufedheheshwa kupitia kulipa Jizya. Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) utatawala Mashariki na Magharibi inshaallah. Bila shaka tendo hili ni bora kuliko dunia hii na kila kilichomo ndani yake. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Yeye ndie aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia. [At-Tawbah 33].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na

Muhammad Imran – Pakistan

 

Ili Kusoma Sehemu 1 Bonyeza Hapa

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 05 Mei 2020 10:41

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu