Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mazingatio ya Korona: Janga Hili Linatoa Wito kwa Mfumo Mpya wa Ulimwengu

Kila siku ikipita, inakuwa wazi kwamba mgogoro wa virusi vya Korona kihakika unawakilisha mgogoro wa kiulimwengu, urasilimali wa sekula. Mgogoro wa virusi vya Korona, kama ilivyo migogoro mengine, umefichua mtazamo wa dunia na mfumo wa urasilimali.

Virusi vya Korona vinauwa watu, lakini haijafikia kiwango cha mgogoro, ukosefu wa rasilimali kutoka mfumo wa huduma za afya, hisia jumla za wasiwasi na mfadhaiko, au mgogoro mkubwa wa kiuchumi unaofuatia usioepukika.

Haya kinyume chake husababishwa na dosari ya kimsingi, mazingira yasio ya haki, na msingi wenye ufa wa mfumo wa kirasilimali, uliokosa uhalisia, maadili ya ubinaadamu.

Wajibu wa ubinaadamu kwa ajili ya mfumo mbadala umefafanuliwa sambamba na kutokea kwa migogoro, pamoja na hitajio la haraka la nidhamu ya kisiasa, inayo simamia mambo ya watu kwa namna ya uadilifu. Nidhamu inayo weka maisha ya mwanaadamu, katika umri au hali yoyote, kuwa ni kipaumbele cha juu zaidi, katika masuala ya afya, madawa, na utafiti, kinyume na hatua za kiuchumi na maslahi.

Kwa msingi huu, ni muhimu kutilia mkazo yafuatayo:

1] Ubepari kwa mara nyengine tena, unao dhihirishwa na baadhi ya mataifa ya Kimagharibi katika ushughulikiaji wao wa mgogoro huu, umefichua ukweli wake, wa sura yake mbaya kwa kutanguliza uchumi zaidi ya maisha ya mwanaadamu.

Kiongozi wa inayoitwa dunia huru, Amerika, inakumbwa na janga la huduma za afya, linalosababishwa na kuegemezwa kwake na mfumo wa bima ya afya ya Kiamerika, ambao tayari umo matatizoni, ikijumuishwa na kutoa kipaumbele cha wazi kwa maslahi ya kiuchumi, hasa kwa ajili ya hali nzuri ya tabaka la wachache dhidi ya afya ya ummah inayo tolewa na serikali ya Amerika.

Nchini Denmark, ukataji na kubana matumizi yamefanyika katika huduma za afya, na matokeo yanadhihirika kwa kutokea janga hili la sasa.

Katika kipindi cha mwaka mmoja tu uliopita, serikali ya Denmark ilikashifiwa na wanauchumi kwa kutumia kiwango cha chini ya dola bilioni 1 katika huduma za afya, ambacho ni takriban nusu ya kiasi kinachohitajiwa na Wizara ya Fedha kwa matumizi yote yanayo tarajiwa katika idara ya huduma za afya.

2] Mfumo wa sasa umeonyesha kushindwa kwake katika kudhibiti mgogoro.

Shirika la Afya Ulimwenguni WHO limeonya mapema juu ya kuenea kwa virusi hivi kwa maeneo yote duniani, na uwezo wa kuzuka janga la maambukizi. Pindi ueneaji uliposhitadi, WHO ilizishauri serikali kuhusu umuhimu wa kumpima kila mtu anaeshukiwa kuwa na dalili. Hili lilichukuliwa kwa wepesi na serikali za Ulaya, ambapo imepelekea mzunguko mwengine wa shutuma za mshauri mkuu wa WHO kwa serikali za Magharibi kwa kutotia msukumo wa kulishughulikia janga la Korona.

3] Uislam umeweka tahadhari kwa Waislamu kutekeleza wakati wa maambukizi, kama usafi na karantini, ambayo yanajulikana katika maandiko ya Kiislamu. Pamoja na haya, Itikadi ya Kiislamu inakuuza fahamu ndani ya Waislamu, kama Ajal (kumalizika kusiko epukika kwa uhai), tawakkul (kumtegemea Mwenyezi Mungu pekee), na kukubali qadhaa ambayo yanamhakikishia Muislamu umiliki na udhibiti kamili wa uhai na kifo kwa Mwenyezi Mungu, pamoja na maradhi na kupona kutokana nayo.

Allah (swt) amesema:

قُل لَّن يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ

Sema: Halitusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu! [At-Tawbah 9:51]                                                                         

4] Ni mfumo huruma, na wa kibinaadamu pekee utakaotekelezwa na Dola ya Khilafah inayokuja ndio utakaoweza kuchunga mambo ya wanaadamu kwa njia sahihi na adilifu. Sharia ya Kiislamu daima itayapa kipaumbele maisha ya mwanaadamu juu ya mazingatio ya kimada, na kiuchumi. Pindi maradhi yanapo ripuka, rasilimali za jamii na ziada ya kiuchumi ya matajiri zitaingizwa hudumia kuhifadhi ya maisha ya wanaadamu na kutoa uangalizi maalum kwa walio hatarini zaidi.

Virusi vya Korona vimejitokeza katika ulimwengu, ambao watu 8 ni wenye utajiri wa nusu ya watu duniani. Muda sasa umewadia kwa ubinaadamu kufungua macho yake kwa badali ya kweli ya uovu na vitisho vya Urasilimali. Maadamu Urasilimali unatawala mambo ya dunia, wengi wa wanaadamu hawatoona utulivu, usalama na amani.

Kama Waislamu, tuna utulivu na kishajiisho kwa kule kwamba Mwenyezi Mungu (swt) bila shaka anaitayarisha dunia kwa kuibuka tena kwa Uislamu kupitia kusimama dola ya Khilafah, huku Ummah wa Muhammad (saw) ukitayarishwa kwa fahari na kwa kuregesha nafasi yake kama kiongozi wa Ulimwengu, kama mwenge unao ng'aa unao ongoza na kusimamia wanaadamu kwa Dini nzuri ya Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdelrahman Muhammad

 #كورونا | #Covid19 | #Korona

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu