Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 COVID-19 na Idadi Isiowiana ya Watu Weusi Walioathiriwa na Virusi Hivi

Maafisa wa afya wameshughulishwa na matokeo ya kutowiana juu ya Waamerika weusi. Tofauti imeshtadi zaidi katika miji kama New Orleans, Chicago na Detroit, ambako kunaishi mkusanyiko mkubwa zaidi wa Waamerika weusi. Katika Chicago, ambako asilimia 30 ni weusi, Waamerika weusi wamechukua asilimia 70 ya kesi zote za maambukizi ya virusi na zaidi ya nusu ya vifo. “Tunajua sote kuwa kuna tofauti jumla katika matokeo ya kiafya zilizo katika upande wa safu za rangi ya ngozi na hilo huweza pia lakawa ni kweli kwa hivi virusi,” amesema Ngozi Esike, mkurugenzi wa idara ya afya ya ummah ya Illinois. (Chanzo: The Guardian, 8 Aprili 2020)

Daktari Keith Ferdinand, profesa wa tiba katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Tulane jijini New Orleans, amesema kuna mambo mengi yanayoweza kuwafanya Waamerika weusi kuwa hatarini zaidi kuathiriwa na COVID-19. Yanajumuisha kufanya kazi katika sekta za utoaji huduma au “kazi muhimu” zinazohitaji kuwakabili wengine ambao huenda wameathirika; utumiaji wa usafiri wa ummah kuwafikisha kazini; kukosa fursa ya kupimwa mapema; na shaka ya kihistoria ya mfumo wa huduma ya afya kwa sababu ya upendeleo tulioutaja kabla. Hii inapelekea “mchanganyiko wa matatizo mengi yanayowafika Waamerika weusi ambayo huongezeka au hata kuongeza mzigo wa visababishi vya virusi vya korona,” amesema Ferdinand. (Chanzo: National Geographic, Aprili 24, 2020)

Watu weusi takriban katika kila jimbo ikiambatana na takwimu za kimakundi wana kasi kubwa zaidi ya maambukizi na vifo vya COVID-19. (Chanzo: Brookings Institute, April 9, 2020)

COVID-19 imefichua tofauti nyengine ambayo imechorwa muda mrefu katika historia ya Amerika, mgawanyiko mkubwa wa tofauti ya rangi ya ngozi uliokuwepo na unaoendelea kuwepo katika jamii ya Waamerika, watu weusi wakiwa katika hali ngumu zaidi ikilinganishwa na watu weupe. Hoja hutolewa pamoja na takwimu za kuunga mkono kuwa Waamerika weusi kwa kawaida ni wafanyakazi muhimu kuanzia wafanya kazi katika bohari hadi kukusanyika kwenye mitaa isiyo bahatika ambao kwa kawaida huwa wamo ndani ya nyumba zilizo songamana zisizo au zenye uchache wa fursa za manufaa kiafya na kijamii. Hisia zilizo enea kote katika majimbo ya Amerika ni, “kuisifia jamii yangu (ya weusi)”. Hivyo watu wenye ngozi ya rangi (wasio wazungu) wako hatarini zaidi ya virusi vya korona na hawawezi kupewa “bahati” ya kuepuka kudumisha masafa ya kijamii baina ya mtu kwa mtu na kujiweka karantini ya kibinafsi kama wanavyo pata wale wanao weza kuhifadhi mafao bora ya kazi (ambao idadi kubwa ni watu weupe). “Takwimu zilizo tolewa hadi sasa zinaonyesha asilimia 68 ya vifo vya virusi vya korona jijini [Chicago] ni vya Waamerika weusi, wanao jumuisha idadi ya asilimia 30 ya watu wote.” (Chanzo: BBC) “Lousiana ina kiwango cha juu zaidi cha vifo vinavyo tokana na COVID-19 katika taifa na, kwa mujibu wa Gavana John Bel Edwards, zaidi ya asilimia 70 ya watu wanaokufa hadi sasa ni weusi. Watu weusi wanajumuisha asilimia 32 tu ya watu wote katika jimbo hili,” (Chanzo: WWNO.org)

Taarifa mbali mbali za afya ya ummah zinawasihi wananchi wa Amerika kufuata tahadhari za afya za CDC na WHO lakini bila ya usalama wa kutosha wa ustawi wa kiuchumi kutosheleza mahitaji ya watu, tumeshasikia matukio ya uchache wa fedha kutoka kwa mfuko wa Trump wa kuchangamsha uchumi na tayari umesharambwa na mashirika makubwa ukiwacha biashara ndogo ndogo kujihami zenyewe. Pia misaada mbali mbali huwa ni kwa raia wa Amerika wanaoweza kuzifikia fedha hizi, ambapo kwa mara nyengine hupatikana suala la tofauti ya kitabaka. Watu wasio na makaazi wasio na anwani ya makaazi ya kudumu au akaunti ya benki pia huangukia ndani ya ufa wa tundu la waliosahauliwa isipokuwa kwa huruma ya watu wa kawaida wanaotoa msaada wa chakula na nguo kwa kiwango chao kichache lakini wakishindwa kuwapatia huduma za hospitali au dawa kutokana na mfumo wa huduma za afya wa Amerika uliochoka.

Wataalamu wengi wa afya ya ummah, wanasiasa na wataalamu wa uchumi wanahangaika kujadili suala hili sio tu kutokana na janga la shambulizi la COVID-19 bali kwa miongo kadhaa kwani Amerika imeshuhudia majanga mengi yatokanayo na maumbile hadi mdororo wa kiuchumi lakini tatizo msingi linaendelea kuwepo na kutanuka. Huku kizungumkuti kikiwa bado kimeegemea na kushughulikiwa kwa msingi wa tofauti ya rangi ya ngozi, tatizo litaendelea kuwepo na si tu kutanuka bali kuwa baya zaidi. Haya yanaonekana katika mujtamaa wa Amerika. Muelekeo wa kizungumkuti hiki unahitaji kuchunguzwa kabla ya tatizo kujadiliwa kwenye meza. Mujtamaa wa Amerika unasifika vibaya mno kwa ubaguzi wake mkubwa wa rangi uliorithi kutoka zama ovu za utumwa ambapo (ubaguzi wa rangi) umekuwa ukifanywa waziwazi au kuchochewa na wanasiasa mbali mbali ili kuvuna kura za walio wengi lakini hiyo ni mada nyengine.

Mfumo wa afya ya ummah umejaa dosari usio dhamini mara moja ubora wa hali ya juu na umakinifu wa tiba na dawa kwa wote wanaohitaji bila kuzingatia rangi au tabaka. Hivi hapa Amerika ina uwezo wa kumudu huduma za afya lakini haitowi fedha za kutosha kwa sekta hii kutokana na kujitenga na kinachoitwa mtindo wa serikali ya kijamaa ambayo ni dosari nyengine ya mfumo wa Kirasilimali, hivyo ina watu wanaokufa na kutaabika katika kiwango cha mripuko ikiwa takwimu zinathibitisha wazi (lakini pia wengi wakipinga kuwa takwimu hizo zinaelekea upande mmoja kutokana na vitu mbali mbali au kukosekana kwake) lakini bado idadi ikionyesha wengi walio hatarini ni watu weusi nchini Amerika.

Badala ya hospitali kufungua milango yake na vyumba vyake kwa haraka kwa wale wanaohitaji uangalifu, wanaitishwa kadi za bima ya afya ambapo kwa mara nyengine tena wafanyakazi wa kipato cha chini hawatoweza kulipa makato au kuweza kulipia gharama za kukaa hospitali kutokana na bei inayopaa kwa kasi mno hivyo hubakia majumbani mwao au kulazimishwa kufanya kazi sehemu ambazo maambukizi huenea kwa watu wa aina moja (weusi) au watu wengine (wasiokuwa weupe).

COVID-19 sio tu imefichua udhaifu wa binadamu wa kushindwa na virusi hivi lakini pia imefumua guo ambalo Amerika ililivaa kwa majivuno mbele ya ulimwengu kufichua mianya ya mashimo; kwa upande wa serikali na kufeli kwake kushughulikia kikamilifu virusi hivi vilivyo pelekea maambukizi; kwa upande wa sekta ya afya kutomudu kushughulikia virusi kikamilifu katika upande wa afya ya ummah na kisha kusababisha utoaji matibabu ya kibaguzi kwa wale walio na uwezo wa kumudu ile iitwayo bahati ambapo inapelekea hatari kubwa ya kuenea katika tabaka la wasio bahatika wengi wao wakiwa ni watu weusi; na kufeli kiuchumi katika kuwasaidia wale wanao ng'ang'ana kukidhi mahitaji yao na kuwasaidia wale walioathiriwa na virusi, kimsingi kuwapatia afueni wale wachumaji katika familia na wanaowategemea.

Hivyo badala ya kujaribu kushughulikia matatizo ya janga hili, vipi kuhusu kushughulikia mtazamo mkuu kwa janga hili linaloendelea ili kuzuia kufeli kukubwa zaidi. Urasilimali umeraruka katika miongo yote hii, ni wakati sasa wa kuuvua guo lake na kulichoma… Uislamu, pamoja na sheria zake maalumu kutoka kwa Muumba, umeweza kuthibitisha katika kipindi chake chote (cha utawala) namna gani uliweza kukidhi mahitaji ya watu wake katika muundo wa kiwango cha juu na kiwango cha juu kisio na mgawanyo wa kikabila au rangi ukitoa huduma za afya ya hali ya juu na kwa namna bora zaidi na ya heshima kwa watu wake wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu, masuala ya kiuchumi hushughulikiwa kwa lengo la kusaidia watu kama katika umbile lao kama watu na sio kufuata njia za kifedha kama ilivyo katika mfumo wa leo. Mara tu hili linapokuwa ndicho kiini cha mfumo, basi maendeleo yataweza kuhisiwa na kuonekana na watu. Kwa wakati huu, watu weusi wataendelea kuteseka kutokana na hisia za kubaguliwa nchini Amerika huku wengi wakilipia gharama kubwa kwa maisha yao kwani Urasilimali haubebi thamani yoyote ya maisha ya mwanadamu. 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na

Manal Bader

#كورونا   #Covid19         #Korona

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 08 Mei 2020 16:39

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu