Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ

“Na wale waliokufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe.”

Vita vya Bosnia ni Mfano

Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaelezea makafiri kuwa ni marafiki wao kwa wao

وَالَّذِينَ كَفَرُوا بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ

“Na wale waliokufuru ni marafiki wenyewe kwa wenyewe.” [Al-Anfal: 73]. Na Quran inataja kuhusu uadui wao kwa Uislamu na Waislamu; Mwenyezi   Mungu Mtukufu amesema:

قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ ‏مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Al-Imran: 118]. Ibn Kathir ameeleza katika tafsiri yake ya aya, maana, chuki imedhihiri kwenye nyuso zao, na katika yale wanayoyatamka baadhi ya wakati, pamoja na, uadui walio nao dhidi ya Uislamu na watu wake katika vifua vyao. Kwa kuwa hali hii iko wazi kwa kila mtu aliye na ufahamu makini, hivyo Mwenyezi Mungu akasema:

قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الآيَاتِ إِنْ كُنْتُمْ تَعْقِلُونَ

“Tumekwisha kubainishieni ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Al-Imran: 118].

Hii ndio hali ya makafiri wakati wote na mahala popote, chuki na uadui wa wazi kwa Uislamu na Waislamu, hawazingatii mkataba wowote au heshima kwa waumini, na licha ya tofauti zao miongoni mwao juu ya maslahi ya kisiasa na kiuchumi, wanakubaliana katika vita vyao dhidi ya Uislamu na Waislamu. Hakuna vita au mauwaji yanayotekelezwa dhidi ya Waislamu zamani na sasa isipokuwa nchi za Magharibi zimeshiriki, moja kwa moja au kupitia wawakilishi, au angalau kunyamazishwa na kula njama na madhalimu, na vita vya Bosnia vilivyotokea baina ya 1992 na 1995 vimeonyesha haya. Vita hivi vilianzishwa kwa chuki iliojificha dhidi ya Uislamu na Waislamu, na njama kubwa ya Ulaya na Amerika na matumaini ya Waserbia kutekeleza uovu wa kishenzi na mauwaji katika vita, kwa kuwa nchi hizi zinahofia Wabosnia kusimamisha dola ya Kiislamu katika Ulaya ya Kati, ambacho pia ni kisingizio cha Waislamu kupigwa na kukandamizwa katika jamii za Wamagharibi, kuhofia jamii hizi kugeuzwa kuwa za Kiislamu, na ambapo vita vya kikoloni vilitekelezwa – na kuendelea kutekelezwa – katika nchi za Waislamu kuzuia kugejea kwa Khilafah. Mkuu wa Kiserbia wa Bosnia Milorad Dodik, ametaja mbele ya Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, sababu ya mzozo ulioivuruga Bosnia kuwa vipande vipande kwa miaka kadhaa ni “hamu ya Waislamu kutaka kusimamisha dola ya Kiislamu.” Kauli ya Dodik imekuja katika mazingira ya Ushahidi wake kwenye kesi ya Radovan Karadzic, aliyetuhumiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu, kwa amri ya Dodik. (Agence France-Presse (AFP), 09/04/2013).

Nchi za Magharibi na washirika wao wa NATO waliupendelea upande wa Waserbia katika vita vyao dhidi ya Waislamu wa Bosnia, na damu safi ya Waislamu ilimwagwa kwa msaada wa nchi za muungano huu kama ilivyomwagwa Iraq, Afghanistan, Syria na nchi nyengine za Waislamu. Nchi za NATO zilitoa msaada wa vifaa na kijeshi kwa waovu wa Kiserbia, wakati Magharibi ikiweka vikwazo vikali vya silaha, hali iliyowafanya Waislamu wa Bosnia washindwe kupata silaha. Aliyekuwa raisi wa Baraza la Uraisi katika Bosnia na Herzegovina, Dkt. Harith Siladic, alizungumza katika Ushahidi wake wa saba katika kipindi cha idhaa ya Al-Jaeera “Witness to the Times” tarehe 12/12/2015, kuhusiana na jukumu chafu lililotekelezwa na nchi hizi katika vita na kuhusu mfungamano wa UN kwa upande wa Serbia, alisema Waserbia walikuwa na msaada wa kijeshi na kisaikolojia wa vikosi vya Urusi, na kuwa mauwaji yalifanyika chini ya macho ya Umoja wa Mataifa na NATO. Na alisema kuwa Waserbia walikuwa wakipata msaada kutoka nchi zenye nguvu kama Ufaransa na Uingereza. Bila shaka, idara za kijasusi za Amerika, kiongozi wakiongozi wa muungano huu muovu, zilielewa juu ya mauwaji yaliotekelezwa dhidi ya Waislamu, lakini utawala wa Amerika ulizuia taarifa hizi na kuziweka siri, kama lilivyo chapisha gazeti la Guardian la Uingereza (Al-Awai’ Magazine Issue 66 – Sixth Year, Rabi’I al-Akhir 1413Aah, June 1992)

Maovu yaliotendeka chini ya macho ya jumuiya ya kimataifa na vitengo vyake, vilivyo wakilishwa katika Umoja wa Mataifa, dhidi ya Waislamu wa Bosnia hayawezi kufikirika na unyama wao usiokadirika, kwa kusababisha uangamizaji wa zaidi ya watu alfu 300 kwa utambuzi wa Umoja wa Mataifa, yametambuliwa na Umoja wa Mataifa na makaburi ya pamoja kuwa ni ushuhuda kwa kiwango na kitisho cha mauwaji haya, uhamishwaji wa kiasi cha wengine wapatao milioni 2.2, na ukiukwaji wa heshima kwa wanawake wanaozidi 50,000. Zaidi ya misikiti 800 ilibomolewa, baadhi yao ilijengwa katika karne ya 16, na Maktaba ya Kihistoria ya Sarajevo ilichomwa moto, maelfu walinyiwa chakula hadi kuwa kama mifupa tu. Kulifanyika mauwaji makubwa zaidi humo tokea vilipomalizika Vita Vikuu vya pili vya Dunia (mauwaji ya Srebrenica) ambapo zaidi ya Waislamu 8,000 waliuliwa mbele ya macho ya vikosi vya Umoja wa Mataifa, bali hayo yakiwa ni njama zao baada ya kutangaza kuwa ni mji salama ukiwa chini ya ulinzi wa vikosi vya UN. Bataliano ya Wadachi ya askari 400 ilipelekwa kuulinda mji, na kwa bahati mbaya, Waislamu waliamini uongo wa UN, na wanamapinduzi wa mji walioapa kulinda maisha na heshima ya wakaazi walisalimisha silaha zao kwa bataliano ya Wadachi. Julai 1995, vikosi viovu vya Kiserbia viliingia kwenye mji chini ya macho ya vikosi vya Umoja wa Mataifa, na wanaume walitenganishwa na wanawake, na mauwaji ya kikatili yalianza Julai 6 hadi 25. Umoja wa Mataifa na wanachama wa bataliano ya Wadachi hawakufanya kitu kuwalinda Waislamu, bali, waliwasalimisha kwa kila aliyetaka msaada wao kwa vikosi vya Serbia ambao waliwauwa mara moja. 

Umoja wa Mataifa ulitekeleza mazingira kama hayo Syria eneo la Aleppo, Idlib na maeneo mengine, kuyatangaza ni maeneo salama, kuwanyanganya silaha waasi, na kuwakusanya raia katika maeneo maalum, na kuuwezesha utawala muovu na washirika wake kuwapiga mabomu raia na kuregesha maeneo yaliokombolewa kwa utawala.

Waislamu wameng'atwa kwenye tundu la nchi za Wamagharibi na vyombo vyao kutoka taasisi za kimataifa, kwa makumi bali kwa mamia katika Bosnia, Iraq, Palestina, Afghanistan, Syria na nchi nyengine za Waislamu, japokuwa Mtume wetu (saw) ametuonya kuwa

 «لَا يُلْدَغُ الْمُؤْمِنُ مِنْ جُحْرٍ وَاحِدٍ مَرَّتَيْنِ»

“Muumini hang'atwi katika tundu moja mara mbili” Matokeo yake ni maafa kila mara, na utatuzi wanaouweka kukabili mizozo na kumaliza vita yalikuwa ni uharibifu, na yalikuwa ni kutekeleza tu maslahi yao, na kwa kawaida hayatengani na utumaji wa vikosi vya kimataifa ambavyo vinaunda uvamizi mpya wa nchi chini ya dhana ya uwekaji amani, na sio kabisa kuwalinda Waislamu na kuhifadhi amani yao. Badala yake, wanachama wake wamekuwa kama mbwa mwitu wanaowalinda kondoo, na kushambulia na unyanyasaji wa ngono, na ukiukaji wa heshima ya wanawake katika Sudan na Afrika ya Kati na kwengineko, ni ushahidi kwa hili. Au, kutia saini kinachoitwa mikataba na makubaliano ya amani yanayowezesha mawakala wake kudhibiti nchi na uwezo wake, na kuzigawa na kuzitawanya nchi za Waislamu, kama ulivyokuwa Mkataba wa Amani wa Bosnia (Dayton Accords) uliotiwa saini kumaliza vita vya Bosnia.

Hakuna mazuri yanayotegemewa kutoka kwa makafiri na vitengo vyao kwa Waislamu na masuala yao, na hii imeelezewa na aya na hadith, na kuhakikishwa na uhalisia, na Mola wetu Mtukufu ametuonya tusiwategemea madhalimu na kuwa Yeye (swt) atatutoa kutoka kwenye ushindi Wake, na atawapa nguvu maadui dhidi yetu kama tutafanya hivyo,

وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ

“Wala msiwategemee wanaodhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Bara’ah Manasrah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu