Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Srebrenica na Mustakbali wa Waislamu Barani Ulaya

Leo ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu wanamgambo wa Kiserbia kutekeleza mauwaji ya halaiki katika mji wa Bosnia wa Srebrenica. Mji uliokuwa rasmi chini ya ulinzi wa Batalioni ya Kiholanzi ya Umoja wa Mataifa. Zaidi ya wanaume na wavulana 8000 wa Kiislamu walitenganishwa na wanawake chini ya usimamizi wa kikosi cha Kiholanzi cha Dutctbat III, kupelekwa uhamishoni na kuuwawa kinyama na baadaye kuzikwa katika makaburi ya halaiki. Wanawake na watoto wa Kiislamu vilevile waliteseka wakati wa vita hivi vya miaka mitatu, vilivyo anza 1992 hadi 1995. Watoto wachanga na wadogo waliuwawa. Wanawake wa Kiislamu walidhulumiwa, kuchafuliwa heshima zao na kuuwawa kwa kiwango kikubwa vilevile.

Kwa miaka yote hii kumesemwa na kuandikwa mengi kuhusiana na mada hii, kwa vyovyote vile kuna umuhimu mkubwa wakati mwengine kuyaleta mauwaji haya ya halaiki ya Waislamu barani Ulaya katika mazingatio ya vizazi vichanga. Lengo la hili, ni kitovisahau vifo vingi vilivyokuwa havina hatia, lakini pia ni kujifunza kutokana na hatma ya wale Waislamu ambao walijichukulia kuwa salama barani Ulaya. Hivyo basi ni muhimu kufahamu malengo msingi ya mauwaji haya ya halaiki. Juu ya hayo, ni muhimu kumulika juu ya namna walivyo amiliana nayo. Ili kuutambua ukweli na uhalisia zaidi wa mtazamo wa mustakbali wa vizazi vya Waislamu.

Srebrenica: “Eneo-Salama”

Kabla ya mauwaji ya halaiki kutokea maelfu ya Waislamu walikimbia unyama wa wanamgambo wa Kiserbia na kutafuta hifadhi katika eneo la Waislamu la Srebrenica, ambalo awali lilitangazwa kuwa "eneo salama" na Umoja wa Mataifa. Kikosi cha Dutchbat, chini ya amri ya Umoja wa Mataifa, kingedhamini usalama wao. Lakini, hili liligeuka kuwa uongo kwani Waislamu walikabidhiwa wanamgambo wa Kiserbia wenye kiu ya damu pasi na upinzani wowote. Dutchbat hata ilichangia kuwaondoa wanaume wa Kiislamu hata baada ya kutangulia kujua kwamba wangeteswa au kuuwawa. Chuki dhahiri ya wanamgambo hao iliyo tekelezwa dhidi ya Uislamu na Waislamu ilijulikana vizuri sana.

Chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu

Chuki nzito na hasira ambazo sehemu kubwa ya Waserbia wanabeba dhidi ya Waislamu iliangazwa kwa sauti ya jenerali wa Kiserbia Ratko Mladic katika ujumbe mfupi wa video. Ujumbe huo wa video ulichapishwa kabla ya kutoa amri ya kuwachinja Waislamu. Alisema: "Sisi ndio hawa hapa tumesimama, Julai 11, 1995 katika mji wa Srebrenica, nchini Serbia. Katika mkesha wa siku tukufu ya Kiserbia tunaupa tena mji huu taifa la Serbia. Kwa kukumbuka mapinduzi dhidi ya Waturuki (yaani Khilafah Uthmani) siku imewadia ya kulipiza kisasi dhidi ya Waislamu." Zaidi ya hayo, kanda ya video ilionekana ambamo anatoa wito kwa watoto wa Kiislamu akisema, "Allah wenu yuko wapi? Mladic ndiye atakaye waokoa." Chuki kwa Waislamu haiwezi kuelezewa kwa ufasaha zaidi ya hivi.

Hili pia lilijulikana vyema na Kofia za Samawati za Kiholanzi (majeshi ya kuweka amani). Licha ya jukumu lao la kulinda eneo la Waislamu kulikuweko na mapendeleo fulani kwa Waserbia na chuki ya pamoja dhidi ya Waislamu. Kuna ripoti nyingi ambazo ni ushahidi unao thibitisha na kwa ufafanuzi kutokea kwa vitisho vya kihakika. Kama kuwaelekezea bunduki Waislamu wa Bosnia wasio na hatia na kutoa matamshi ya kutamani kuwasagasaga kwa vifaru Waislamu, pamoja na kuwadhulumu na kuwabaka wanawake wa Kiislamu! Hata michoro juu ya kuta za kiwanja cha wanajeshi wa Kiholanzi ilielezea chuki za wanajeshi wa Kiholanzi kwa Waislamu wa Bosnia.  

Dharau iliyo elekezwa kwa wakimbizi wa Kiislamu mjini Srebrenica ilikuwa kubwa mno. Walirusha vipande vya mkate katikati ya mamia ya Wabosnia waliokuwa na njaa, waliovipigania huku wao wakicheka. Suluki ya watesaji wa Kiholanzi iliyo dhihirika baada ya kutokea mauwaji ya halaiki juu ya Waislamu ilikuwa ni ya kuchukiza na inakwenda sambamba na kufikiri kwao. Katika video maarufu iliyo vujishwa, watesaji walevi wa Kiholanzi walikuwa wakicheza densi siku chache tu baada ya mauwaji ya halaiki kutokea kana kwamba hakuna lolote lililotokea. Je, ni ukweli gani basi ulioko katika matarajio ya watesaji hao wa Kiholanzi ya kujitolea mhanga maisha yao ili kuwalinda Waislamu?     

Vilevile, kujificha nyuma ya "nguvu kuu" ya Kiserbia ili kuhalalisha kujisalimisha kijeshi kwa Waserbia pasi na kuwepo kiasi fulani cha upinzani ni udhaifu. Ni ipi basi kazi ya wanajeshi waliopewa mafunzo ikiwa hawatajitolea vilivyo kulinda raia wasiokuwa na silaha? Je, kujibu mashambulizi hadi mwisho wa kiheshima haizingatiwi sehemu ya kazi hizi? Juu ya hayo, wiki mbili baadaye wakati wa kutekwa tena kwa Krajina na Croatia, Waingereza waliwachukua maelfu ya raia wa Serbia ndani ya makao makuu yao, wakajibu mashambulizi na kuwalinda raia. Vyovyote hali ilivyo kuwa, jambo halisi lililotokea ni kwamba Waislamu walikabidhiwa kwa urahisi mhalifu.  

Mtazamo wa Waholanzi na matokeo baada ya mauwaji ya halaiki

Mpaka sasa, vitendo hivi viovu vya Dutchbat, ambao hawakufeli tu kuchukua jukumu lao lakini pia walimsaidia mhalifu. Doa kamili na aibu ambapo kwa uchache inapaswa kutambuliwa ili kupunguza uchungu uliohisiwa, waweza kusema pengine. Lakini mamlaka za Kiholanzi zimeonyesha tabia isiokuwa tofauti na ya mwanzo na hadi leo hupinga madai yoyote.

Ripoti ya kwanza ya Srebrenica ya NIOD ilichapishwa sio zaidi ya mwaka 2002, miaka 7 baada ya mauwaji ya halaiki. Hitimisho lilikuwa kwamba misheni haikutayarishwa vya kutosha, kiasi cha kuwa Dutchbat haingeweza kuhesabiwa kwa sokomoko iliyotokea mjini Srebrenica. Nyuma mnamo 1999, Umoja wa Mataifa pia ulihitimisha kuwa Kofia za Samawati za Kiholanzi hazingeweza kulaumiwa kutokana na mauwaji hayo ya halaiki.

Jamaa za wahanga: "Kina mama wa Srebrenica", hawaoni maendeleo yoyote kuelekea mwisho wenye haki baada ya miaka 15 na kuamua kuripoti mauwaji ya halaiki na uhalifu wa kivita. Akiwemo Kamanda Thom Kerramans, aliyeiongoza batalioni ya Kiholanzi ya Umoja wa Mataifa ya Dutchbat. Lakini, miaka mitatu baadaye Mwanasheria wa Umma akaamua kutomshitaki Karremans.

Mnamo 2014 mahakama jijini Hague iliamua kwamba Waholanzi hawawajibiki kwa wanaume 8000 wa Kiislamu lakini wanawajibika nusu kutokana na uhamishaji wa zaidi ya wanaume mia tatu. Kwa maana nyengine: Dutchbat haiwajibiki kwa hatma ya wahanga 7500.

Mnamo 2017 mahakama jijini Hague ilithibitisha hukmu iliyo tangulia ambayo kwayo dola hiyo ilipatikana kuwajibika kutokana na vifo vya wanaume 350, lakini kwa hilo ni asilimia 30 pekee ya uharibifu ndio ambao utalipwa. Wanajeshi hao wa Kiholanzi wa Dutchbat, waliopewa kazi ya kulinda eneo la Waislamu pia walihesabiwa kutokana na kukimbia. Kwa mujibu wa mahakama hiyo, serikali ya Uholanzi inawajibishwa kwa asilimia 30, ni wahanga 350 pekee ndio waliokuwemo ndani ya uwanja wa Kiholanzi. Hivyo hata katika kutoa uamuzi wa fidia kwa kesi zilizotambuliwa na kuthibitishwa (kutokana na mapuuza katika upande wa serikali ya Uholanzi) ni asilimia 30 pekee ndio inayolipwa.

Mnamo 2019 Baraza Kuu lilihukumu kwamba dola hiyo inawajibika nusu pekee kwa vifo vya zaidi ya Waislamu 300 na kuhukumu kwamba sio asilimia 30 bali ni asilimia 10 pekee ya fidia ndio inapaswa kulipwa jamaa za waathiriwa.

Ni hukmu gani itakayo kuja baada ya hii? Hakuna fidia na/au kuondolewa mashtaka?

Yote haya yanaziangukia Uholanzi, Ulaya na Umoja wa Mataifa mzima kwa kushindwa kuwalinda Waislamu Magharibi kutokana na chuki dhidi ya Waislamu. Zaidi ya hayo, wameshindwa kuchukua jukumu lao kuhusiana na mauwaji ya halaiki na uangalizi baada yake kwa jamaa za waarithiwa. 

Sisi pia tunaiona suluki hii katika uhalifu wa serikali ya Uholanzi dhidi ya koloni zake za zamani kama Indonesia, lakini pia kwa mfano mashambulizi ya angani ya Uholanzi nchini Iraq, ambayo kwayo mtaa mzima uliangamizwa na ndege za kivita za Uholanzi aina ya F-16. Zaidi ya raia 70 walipoteza maisha yao kwa sababu ya hili. Wakati huo pia, serikali ya Uholanzi ilikataa madai yoyote ya kuwa na hatia. Swali ni vipi Uholanzi na Ulaya nzima itazilinda jamii za Waislamu siku za usoni kutokana na hisia zinazo zidi kukua kila uchao dhidi ya Uislamu. Kwa kuzingatia msururu wa matukio ya sasa mustakbali una kiza.

#Srebrenica25YearsOn   سربرنيتشا_جرح_لم_يندمل#   #Srebrenitsa25Yıl

     #SrebrenicaMiaka25Baadaye

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Okay Pala

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uholanzi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu