Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Afisi Kuu ya Habari: Kongamano Kubwa "Kujiweka Mbali na Khiyana Kubwa"

Siku ya Jumanne 15/09/2020, Imarati na Bahrain zilitia saini katika mji mkuu mweusi Washington makubaliano ya khiyana kubwa kwa eneo la safari ya Isra na Miraj ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), bila ya kumhofu Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na waumini! Na nchi hizo mbili kwa jambo hilo wanafuata mwenendo wa mfano wa wao waliotangulia kabla: serikali ya Misri huko Camp David, ushirika huko Oslo, na serikali ya Jordan huko Wadi Araba! Watawala katika nchi za Waislamu, kabla na baada ya saini hizi, walikuwa wakiamiliana na serikali ya Kiyahudi, lakini nyuma ya pazia, wakichunga katika hilo kiasi kidogo cha haya, bali kutokana na aibu, hivyo walisawazisha mahusiano nyuma ya pazia. Pindi kitu hiki kilipoondoka hatimaye usawazishaji huu wa mahusiano ukawa dhahiri (kwa ufahari) kwao wanautangaza bila ya kuhisi udhalilifu au hata chembe ya aibu au soni! Na udhalilifu huu hapana budi utawafika wakubali au wakatae, kama njia ya kila mhalifu katika haki ya Dini yake na Ummah wake,

﴿سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُواْ صَغَارٌ عِندَ اللّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُواْ يَمْكُرُونَ﴾.

"Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya." [Al-An'am: 124]

Hakika ni katika haki ya moja ya mambo makuu kutokea haya ambayo yanayotokea ambapo ndani yake usawazishaji mahusiano unaendelea kwa haraka machoni na masikioni mwa Ummah na jeshi lake! Na bila ya majeshi ya Waislamu kusonga, ulimwengu unawageukia na kuwaondoa! Kisha wale ambao hawajatia saini makubaliano hayo yaliyotangazwa wao sio duni kidaraja kuliko waliotia saini, kwani Oman inashikilia na ikiongezewa na serikali ya Wayahudi, na Qatar nafasi ya mpatanishi (mwaminifu) kati ya Mayahudi na Gaza! Na serikali ya Saudia katika nchi ya Misikiti Mitakatifu Miwili anga zake zimefunguliwa kwa ajili ya ndege za kivita za dola yenye kuchukiza ambayo inaikalia kimabavu al-Qudsi sehemu takatifu ya Waislamu!! Halafu serikali ya Uturuki bado ingali inaitambua dola ya Mayahudi inayoikalia kimabavu Palestina! Hakika, ni moja ya mambo makuu kutokea haya ambayo yanatokea kana kwamba ni jambo la kawaida kati ya ndugu wa baba na mama na kwamba hamna la zaidi ila tofauti tu ya kimtazamo katika uchoraji wa mipaka!!

Katikati ya matukio haya maovu, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, ikishirikiana na Al-Waqiyah TV, inafanya kongamano kubwa kupitia mtandao juu ya khiyana kubwa iliyofanywa na Imarati na Bahrain kwa anwani:

"Kujiweka Mbali na Khiyana Kubwa"

Na hiyo ni baada ya Maghrib Jumamosi 02 Safar al-Khair 1442 H, sawia na Septemba 19, 2020 M, kuanzia saa mbili unusu jioni kwa saa za Madina Al-Munawwara na saa za Jerusalemu (Al-Quds Al-Sharif).

Link ya Kongamano Kutoka Katika Wavuti wa Runinga ya Al-Waqiyah:

Link ya Kongamano Kutoka Katika Ukurasa wa Facebook wa Runinga ya Al-Waqiyah: 


Link ya Kongamano Kutoka Katika Chaneli ya YouTube ya Runinga ya Al-Waqiyah: 

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Ijumaa, 01 Safar Al-Khair 1442 H sawia na 18 Septemba 2020 M


- Fuatilia Kongamano Hili kwa Lugha Nyenginezo -

Ili Kusoma Toleo Lililotolewa na Hizb ut Tahrir

Leo Hii Imarati Na Bahrain Zinatia Saini ya Mkataba Pamoja na Dola ya Kiyahudi, Mkataba wa Uhaini Mkuu kwa Palestina Ambayo Ndipo Alipofikia Mtume (saw) Katika Safari Ya Isra Na Miiraj Yake. … Wanafanya Hivyo Hata Bila ya Kumhofu Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini!

Jumanne, 27 Muharram Al-Haram 1442 H sawia na 15 Septemba 2020 M

Bonyeza Hapa

- Video za Amali ya Kongamano -

- Palestina Itakombolewa na Jeshi la Khilafah -

Kalima ya Dkt. Mosab Abu Arkoub

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

- Magharibi Imeshindwa Kuwakinaisha Waislamu kwa Umbile la Kiyahudi –

Kalima ya Ustadh Al-Qadir Ahmad Al-Qasas -

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon

- Ima ni Msimamo na Kujitokeza au ni Kuchukua na Kubadilisha -

Kalima ya Dkt. Ahmad Hassouna

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Jordan

- Tahadhari Msijemkatoa Jizya ya Usawazishaji Mahusiano Enyi Watu wa Sudan! -

Kalima ya Sheikh Nassir Ridha

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

- Palestina Sio Kadhia ya Kiarabu Bali ni Kadhia ya Uislamu -

Kalima ya Ustadh Abdullah Imam Oglo

Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki

- Umuhimu wa Misri Al-Kinanah katika Kadhia ya Palestina -

Kalima ya Ustadh Said Fadhl

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

- Wasifu wa Watawala Waovu -

Kalima ya Mwadhama Sheikh Yusuf Makharaza (Abu Hamam)

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

- Kulikataa Umbile la Kiyahudi ni Kukataa Sababu za Malezi Yake na Utunzaji Wake -

Kalima ya Mhandisi Usama Al-Thuwaini

Kitengo cha Vyombo vya Habari cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Kuwait

- Majibu Makali Dhidi ya Khiyana Kubwa kwa Ardhi ya Isra -

Kalima ya Dada Rana Mustafa

Mwanachama wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

- Watu wa Palestina Wako Imara Juu ya Amana -

Kalima ya Mwadhama Sheikh Usam Amira (Abu Abdullah)

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

- Kuzorota kwa utendaji wa kisiasa wa Magharibi -

Kalima ya Ustadh Mundhir Abdullah

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir Denmark

- Aminini Khiyana Yenu! -

Kalima ya Ustadh Ahmad bin Hussein

Mwanachama wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

- Risala ya Hizb ut Tahrir katika Hali Hii Uchungu -

Kalima ya Mhandisi Salahuddin Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

- Alama Ishara za Kongamano -

         ins tw           #براءة_من_الخيانة_العظمى

#InnocentofHighTreason  ins tw  

- Matangazo ya Moja kwa Moja ya Kongamano -

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumanne, 22 Septemba 2020 17:01

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu