Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Kenya:
Msururu wa Amali za Kukumbuka Miaka 98 Tangu Kuangushwa kwa Khilafah

Hizb ut Tahrir ndani ya Kenya ilizindua msururu wa amali katika misikiti baada ya Swalatul Juma’ katika kuikumbuka miaka 98 tangu kuvunjwa kwa Khilafah.


Imewakumbusha Waislamu tukio chungu la kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu mnamo 3 Machi 1924. Ummah wa Kiislamu unaendelea kutaabika kutokana na kukosekana kwake na kuwasisitizia Waislamu kufanyakazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kurudisha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

Ijumaa, 24 Jumada al Akhr 1440 AH - 01 Machi 2019 M

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir /Kenya Ilifanya Maandamano Baridi Kulikumbuka Tukio la Kiza la Kuanguka kwa Khilafah yetu

28 Rajab 1440 H - 04 Aprili 2019 M

Mnamo Jumatatu, 25 Rajab 1440 H sawia na 1 Aprili 2019, Hizb ut Tahrir / Kenya iliandaa mizunguko katika mitaa kukutana na watu katika mabaraza na masoko ili kunyanyua ufahamu kuhusu kutamatisha kwa kampeni ya kiuchumi ambayo chama ilizindua ndani ya Kenya kwa kichwa “Kuzidi kwa Gharama za Maisha: Uislamu ndio Suluhisho.” Mizunguko ilijumuisha ziara katika misikiti na kusoma mwa taarifa kwa vyombo vya habari kwa kichwa: Hizb ut Tahrir / Kenya Imefaulu Kukamilisha Kampeni Maalum kwa Mwito – Kuzidi Kwa Gharama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba

Mnamo Jumanne, 26 Rajab 1440 H sawia na 2 Aprili 2019 M – Tuliandaa usambazaji mkubwa wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kwa kichwa, Hizb ut Tahrir / Kenya Imefaulu Kukamilisha Kampeni Maalum kwa Mwito – Kuzidi Kwa Gharama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba katika mabarabara, masoko n.k. Kwa kuongezea, tulitumana ujumbe kwa Ubalozi wa Uchina nchini Kenya. Ujumbe uliongozwa na Mkuu wa Kamati ya Mawasiliano wa Hizb ut Tahrir / Kenya Arkanuddin Yassin akiwa pamoja na Shabani Mwalimu – Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya. Waliwasili katika ubalozi ulioko Nairobi saa 2:56 asubuhi E.A.T. Ubalozi wa Uchina ulikataa kupokea wala kutambua upokeaji wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kichwa: Khilafah Itakomboa Turkestan Mashariki Na kuwanusuru Uyghur kutoka kwa Ukandamizaji wa Kihalifu wa Uchina. Kwa kuongezea, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Kenya ilitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kwa kichwa: Dola ya Uchina na Utawala wake Unaogopa Mwito wa La ilaha illa Allah

 

Mnamo Jumatano, 27 Rajab Muharram 1440 H sawia na 3 Aprili 2019 – tuliandaa maandamano baridi katika miji mikuu ya Kenya kwa maana Mombasa na Nairobi. Wazungumzaji waliongozwa na Shabani Mwalimu – Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahri Kenya; waliangazia matatizo yanayowakumba Ummah wa Waislamu duniani kote kama natija ya kuvunjwa kwa Khilafah mnamo 28 Rajab 1342 H (3 Machi 1924 M). Kwa kuongezea, waliwasilisha suluhisho la Kiislamu ambalo limo katika kurudisha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume.

 

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 05 Aprili 2020 18:21

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu