Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan Kampeni:

Pingeni Hadhara ya Kimagharibi na Linganieni Uislamu

[ٱدْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلْحِكْمَةِ وَٱلْمَوْعِظَةِ ٱلْحَسَنَةِ ۖ وَجَٰادِلْهُم بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ]

“Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora.” [Surah an-Nahl 16:125]

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan inaandaa kampeni kwa anwani “Pingeni Hadhara ya Kimagharibi na Linganieni Uislamu” katika mitandao ya kijamii.

Ewe Mwenyezi Mungu turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume… Ewe Mwenyezi Mungu, Amin.

#RefuteWesternCivilization

Dhul Qa’adah 1443 H - Juni 2022 M

1. Urazini wa Kimagharibi

Urazini wa Kimagharibi hutelekeza dini na kutegemea akili ya mwanadamu, na akili pekee, kama mtunzi wa sheria, hakimu na kiongozi. Urazini huifanya akili yenye kikomo ya mwanadamu, iliyo na dosari, upendeleo na migongano, kama maregeleo ya kuhukumu juu ya mambo na vitendo. Hata hivyo, akili ya mwanadamu inaweza kuamua jambo fulani kuwa jema, ilhali ni baya. Kinyume chake, akili inaweza kuhukumu kitu kuwa kibaya, ilhali ni kizuri. Uislamu unaacha hukumu ya yale yaliyoruhusiwa na yaliyoharamishwa kwa Mwenyezi Mungu ﷻ ambaye elimu yake haina mipaka. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema, [وَعَسَى أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَكُمْ وَعَسَى أَنْ تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَكُمْ وَاللَّهُ يَعْلَمُ وَأَنْتُمْ لَا تَعْلَمُونَ  ] “Lakini huenda mkachukia kitu nacho ni kheri kwenu. Na huenda mkapenda kitu nacho ni shari kwenu. Na Mwenyezi Mungu anajua na nyinyi hamjui.” [Surah Al-Baqarah 2: 216]. Hivyo basi, jamii na mujtamaa wa Kiislamu hushikamana na maamrisho na makatazo Mwenyezi Mungu ﷻ na Mtume Wake ﷺ.

11 Dhul Qa’adah 1443 H - 10 Juni 2022 M

2. Tafakari ya Kisayansi

Tafakari ya kisayansi ina mapungufu. Ni ina faida kwa maendeleo ya kimada, lakini haiwezi kuelezea madhumuni ya kuwepo kwa mwanadamu. Haiwezi kuhitimisha mambo kwa yakini, kwa kuwa na uwezekano wa makosa. Maono yake yamefungika na mada na sio zaidi yake. Inaelezea kile kinachoonekana, jinsi, lakini haielezi kwa nini. Mwenyezi Mungu ﷻ asema, يَعْلَمُونَ ظَاهِرًا مِّنَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ عَنِ الْآخِرَةِ هُمْ غَافِلُونَ ] ] “Wanajua hali ya dhaahiri ya maisha ya dunia, na wameghafilika na Akhera.” [Surah Ar-Rum 30:7]. Hadhara ya Kiislamu hufanya kufikiri kiakili kuwa ndio msingi wa tafakari ya mwanadamu. Hivyo basi, mujtamaa wa Kiislamu umejengwa juu ya hitimisho la yakini kwamba ulimwengu una Muumba, Mwenyezi Mungu ﷻ Ambaye kwake wanadamu wataregea kwa ajili ya kuhesabiwa kuhusu mwenendo wao katika maisha. Hivyo basi, zama za Khilafah zilishuhudia maendeleo makubwa ya kisayansi, sambamba na utulivu, ufanisi, uadilifu na ustawi kwa raia wake wote, bila kujali rangi zao, jinsia au dini.

12 Dhul Qa’adah 1443 H - 11 Juni 2022 M

3. Haki na Batili

Hadhara ya Kimagharibi hudai kwamba, "Hakuna kitu kama haki tupu na batili tupu" (Henry Augustus Rowland). Fahamu ya haki ni ya moja kwa moja kwa mtu yeyote, tofauti na miongozo iliyotungwa na nadharia za kisasa za Kimagharibi, kama vile qaida kuwa vitendo huwa ni sahihi ikiwa vina manufaa au maslahi kwa idadi ya wengi wa watu (utilitarianism), uwiano, uwili na qaida kuwa elimu, haki na maadili yanakuwepo kwa mujibu wa muktadha wa utamaduni, jamii au wa kijamii na sio ya kijumla (relativism). Ikiwa hukumu ya kimantiki inahusiana na kuwepo kwa kitu, basi hakuna shaka kuwa ni yakini. Ama hukumu inayohusiana na dhati au sifa ya kitu, hukumu hii sio ya kukatikiwa, yaani inaweza kuathiriwa na dosari. Hata hivyo, kuwepo kwa uwezekano wa kutokuwa na kukatikiwa, katika baadhi ya hukumu, hakupingi kuwepo kwa haki yoyote ya kukatikiwa. Ama kuhusu ‘Aqidah ya Kiislamu, kuwepo kwa Mwenyezi Mungu ﷻ ni haki, kama vile Muujiza usio na kifani wa Quran. Ama kuhusu mambo yasiyo ya kukatikiwa, kama vile rai ndani ya Fiqh, qaida yake ni, رأيي صواب يحتمل الخطأ، ورأيك خطأ يحتمل الصواب  “rai yangu ndio sahihi yenye uwezekano wa makosa, na rai yako ni ya makosa yenye uwezekano wa kuwa sahihi.”

13 Dhul Qa’adah 1443 H - 12 Juni 2022 M

4. Usekula

Itikadi ya Kimagharibi ya usekula iliibuka kutokana na mzozo kati ya Kanisa na wanafikra. Ilikuwa ni mwitikio kwa ukandamizaji mkali wa Kanisa, kwa jina la dini. Usekula unanadai, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, na Mungu kilicho cha Mungu (kwa Kigiriki: Ἀπόδοτε οὖν τὰ Καίσαρος Καίσαρι καὶ εῦ τὰ τὰ τὰ τὰ τἦ). Hata hivyo, uzoefu wa Magharibi wa dini hauhalalishi kutenganisha dini na maisha ya umma kwa Waislamu. Uislamu unamsalimisha mtawala, nafsi yake, mali na heshima, mbele ya Mwenyezi Mungu ﷻ, usalimishaji wa kikamilifu. Ikiwa Khalifa hatatawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ﷻ, basi idara ya mahakama ya Kiislamu inawajibika kumuondoa katika utawala. Pia, mbali na dhulma, Khilafah ilihakikisha uadilifu, usalama, maendeleo ya kimada na ustawi kwa raia Waislamu na wasiokuwa Waislamu, kwa karne nyingi. Kwa hivyo, usekula sio itikadi inayofaa kwa Waislamu kuifuata, sio kutoka kwa msimamo wa Shariah, wala kutoka kwa uzoefu wa kivitendo, wa kihistoria.

14 Dhul Qa’adah 1443 H - 13 Juni 2022 M

5. Kutenganisha Dini na Maisha

Usekula, kutenganisha dini na maisha, una migongano ndani yake. Usekula unathibitisha dini, lakini unahusisha dini kwa ibada ya kibinafsi pekee. Usekula unathibitisha Muumba, lakini unayafunga  mahusiano yake na mambo ya kibinafsi pekee. Usekula unathibitisha kuhesabiwa mbele ya Muumba, lakini unayazuia matendo ya umma yanayohitajika kwa ajili yake. Usekula unathibitisha kwamba mwanadamu ni kiumbe mwenye kikomo na dhaifu, lakini bado anamfanya mtunzi wa sheria kwa watu wengine, kama mungu duniani. Usekula unakubali maumbile ya muda ya maisha haya ya kidunia, lakini unakuuza kushikamana imara na maisha haya ya dunia, karibu kana kwamba hayataisha. Haishangazi kwamba Magharibi inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiroho, unaojikwaa juu ya mipaka ya dini katika maisha ya umma. Katika Uislamu, maisha ya faragha na ya umma ni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu ﷻ. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema: وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ “Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.” [Surah ad-Dhaariyat 51:56]

15 Dhul Qa’adah 1443 H - 14 Juni 2022 M

6. Maadili Yenye Kupigia Debe Vitendo yenye Kuleta Furaha (Utilitarianism)

 Usekula huleta utilitarianism, kutafuta raha za kimwili, kuona furaha tu katika maisha haya mafupi, na sio Akhera ya milele. Bila ya maadili ya kiroho, ya kiakhlaqi au ya kiutu, usekula umewazamisha wanadamu katika kupenda mali na raha za kimwili. Chini ya usekula, kumekuwa na vita vya ulimwengu vyenye uharibifu, kambi za mateso, uhalifu wa kupangwa, umaskini mkubwa na njaa. Ponografia imesababisha kuvunjika kwa mahusiano ya familia, na kuzalisha utamaduni wa ubakaji na unyanyasaji dhidi ya wanawake. Usekula umesababisha kuongezeka kwa magonjwa ya kisaikolojia, ikiwemo na msongo wa mawazo na wasiwasi, pamoja na kujiua na uuwaji wa wagonjwa wasiotarajiwa kupona (euthanasia). Umefika wakati sasa kwa Uislamu kuibuka kama dola na hadhara ya kimataifa, ambao utaelekeza wanadamu katika kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu ﷻ, huku ukiyapa maadili ya kiutu, kiakhlaqi na kiroho, uzito unaostahiki. Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ: وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ  “Na maisha ya dunia si chochote ila ni starehe ya udanganyifu.” [Surah al-Hadid 57:20]

16 Dhul Qa’adah 1443 H - 15 Juni 2022 M

7. Dola ya Kitaifa

Madai ya Magharibi kwamba mfumo wa dola ya kitaifa unahakikisha amani ya ulimwengu ni ya uongo. Kwa hakika, ulizua aina mpya ya ukandamizaji, ukoloni. Dola za Kimagharibi hapo awali zilitumia nguvu za kijeshi kuvamia kila bara lisilo la Ulaya. Hata baada ya uhuru jina, dola za Kimagharibi zilidumisha udhibiti kupitia mikataba ya kiuchumi, ushirikiano wa kijeshi na ufadhili wa vikundi tawala fisadi vya ndani. Mataifa yaliyokoloniwa yanahuruji malighafi na nguvukazi zao kwa gharama ya chini isivyo haki, huku yakiagiza bidhaa na huduma za Magharibi kwa bei ya juu kupita kiasi. Kuhusu vita, dola za Magharibi huandaa kwa urahisi kampeni za kijeshi zenye uharibifu, na kusaidia wengine kufanya hivyo, ili kupata mapato ya mali. Hakika dunia inauhitajia Ummah kusimamisha dola ya Uislamu, Khilafah, ambayo kwa karne nyingi ilihakikisha amani na ustawi kwa sehemu kubwa ya Afrika, Mashariki ya Kati, Asia ya Kusini, Asia ya Kati na Kusini-Mashariki mwa Asia.

17 Dhul Qa’adah 1443 H - 16 Juni 2022 M

8. Mali ya Umma

Pengo kubwa kati ya matajiri na maskini linashuhudiwa katika uchumi wa kibepari wa nchi zote. Kwa makosa, ubepari unadai kwamba kila rasilimali ya kiuchumi, zikiwemo huduma za umma, lazima ibinafsishwe. Hata hivyo, usawa wa kiuchumi unahitaji kutofautishwa kwa aina za umiliki, ili kugawanya mali na kuzuia mrundiko wake. Usimamizi wa umma, kama jamii yenye kushirikiana, unaamuru aina maalum ya umiliki wa huduma za umma, kama vile madini, maji, malisho na nishati. Uislamu ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu pekee ndio ulio na hukmu ya kisheria ya ‘mali ya umma,’ inayotekelezwa kipekee juu ya huduma za umma. Khilafah lazima itumie mali na mapato ya huduma za umma kwa mahitaji ya umma pekee, huku ikizuia ubinafsishaji wake. Mtume wa Mwenyezi Mungu

ﷺ said, الْمُسْلِمُونَ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ الْمَاءِ وَالْكَلَإِ وَالنَّارِ  “Waislamu ni washirika katika vitu vitatu, maji, malisho na moto.” (Ahmad)

18 Dhul Qa’adah 1443 H - 17 Juni 2022 M

9. Uzalishaji

Kwa mujibu wa Urasilimali, uzalishaji ni uundaji wa manufaa (matumizi) pekee, yaliyofungwa kimada na kibiashara. Kwa hivyo, kazi ya mwanamke kwa familia inachukuliwa kuwa yenye manufaa ikiwa tu ataiuza kama huduma kwa wengine. Kwa mtazamo wa kiuchumi wa kirasilimali, kuhusiana na 'gharama ya fursa,' mke nyumbani anachukuliwa kuwa ni hasara kwa soko la ajira. Urasilimali hivyo basi umedunisha pakubwa dori ya kiasili ya kuwa mama. Kwa hivyo, mwanamke akahisi kulazimika kuingia katika soko la ajira kwa kujitolea kikamilifu, na kushindwa kujitolea kikamilifu kwa familia yake, na kusababisha hasara kubwa za kijamii na kisaikolojia. Uislamu hautathmini mambo kwa manufaa ya kiuchumi pekee. Hadhara ya Kiislamu ulitoa thamani kubwa kwa mke pamoja na mama, iliyoakisiwa katika hukmu zake za Shariah. Kwa hakika, familia ya Kiislamu yenye utulivu ndio msingi wa jamii ya Kiislamu na ngome ya mujtamaa wa Kiislamu.

10. Ugavi wa Mali

Urasilimali unadai kirongo kwamba tatizo la kiuchumi ni lile la uhaba, na rasilimali kidogo, ilhali mahitaji hayana kikomo. Kwa hakika, kuna bidhaa na huduma za kutosha kukidhi kikamilifu mahitaji ya kimsingi ya kila mtu, kama vile chakula, mavazi na malazi, kwani mahitaji haya ya kimsingi ni machache, na sio kuwa hayana kikomo. Kinyume chake, mahitaji ya ziada yanayotokana na maendeleo ya kimada kwa hakika daima yanaongezeka. Wanadamu kimaumbile hujitahidi kupata mahitaji kama haya ya ziada, lakini ikiwa hayakidhiwi, hatakuwa na njaa, ukosefu wa makazi na malazi. Kwa hiyo, tatizo la kiuchumi kwa kweli ni ugavi wa mali na juhudi, ili mahitaji yote ya kimsingi yashibishwe, huku watu wakisaidiwa kujitahidi kupata mahitaji ya ziada. Khilafah itamaliza mrundiko wa mali uliokithiri mikononi mwa wachache, na kutoa afueni kwa wanadamu. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema, كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْأَغْنِيَاءِ مِنكُمْ  “ili (mali) isiwe ikizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Surah Al-Hashr 59:7].

20 Dhul Qa’adah 1443 H - 19 Juni 2022 M

11. Fikra ya Uwingi

Demokrasia inadai kuwepo kwa uwingi kwa yenyewe pekee, kwa njia kamilifu. Hata hivyo, uwingi wa Magharibi umejikita kwenye mfumo wake wa kiliberali. Kwa hivyo, Magharibi ilipambana na Ukomunisti hapo awali, huku sasa inapambana na kile kinachoitwa Uislamu wa kisiasa, ikiwadhibiti Waislamu, kifikra na tabia. Ama uwingi kwa maana ya mitazamo tofauti ndani ya mfumo mmoja, sio kwa Demokrasia pekee. Uwingi huo unapatikana pia katika Uislamu. Tofauti za rai juu ya hukmu za kisheria na misimamo ya kisiasa imethibitishwa vyema, ambapo Khalifah ana haki ya kufanya tabanni yenye kuwafunga watu wote, inapohitajika. Katika Uislamu, kuna raia wasiokuwa Waislamu wanaolindwa, ambayo ni bora zaidi kuliko fahamu ya Demokrasia ya jamii ya wachache. Katika Demokrasia, utungaji wa sheria hufanywa na kura za walio wengi, jambo ambalo linawanyima haki wachache. Hata hivyo, katika Uislamu haki ambayo Mwenyezi Mungu ﷻ amempa raia asiye Muislamu haiwezi kamwe kuondolewa, hata kwa kura za Ummah mzima.

21 Dhul Qa’adah 1443 H - 20 Juni 2022 M

12. Mamlaka na Ubwana

Magharibi inadai Demokrasia inatoa mamlaka na ubwana kwa watu. Lakini, zote mbili ni za kipote cha wachache wenye nguvu pekee. Wamiliki wa mali nyingi huunda rai jumla wakati wa uchaguzi. Wao pekee ndio wenye uwezo wa kufadhili kampeni za gharama kubwa za uchaguzi. Kipote cha wachache wenye nguvu huwafanya watu kuwa watumwa, na kutunga sheria za kuongeza utajiri wao. Katika Uislamu, mamlaka ni ya watu, wanaowachagua wawakilishi wa Baraza la Umma. Khalifah huchaguliwa na Baraza la Ummah na huteuliwa kupitia Bay’ah ya chaguo na ridhaa. Akiingia madarakani kwa njia nyingine isiyokuwa ya Bay’ah ya kisheria, anachukuliwa kuwa ni mnyakuzi haramu wa mamlaka. Ama ubwana hauko kwa Khalifah wala Baraza la Ummah wala Ummah wenyewe. Ni kwa Shariah ya Mwenyezi Mungu ﷻ pekee. Kwa hakika, endapo Khalifah atatawala kinyume na yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi ataondolewa na idara ya mahakama.

22 Dhul Qa’adah 1443 H - 21 Juni 2022 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu