- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Kampeni ya Ramadhan 1444 H - 2023 M
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan imeandaa kampeni ya video fupi kwenye mitandao ya kijamii wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa mwaka huu wa 1444 H - 2023 M, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu azikubali Saumu, qiyaam, na ibada zote kutoka kwetu na kutoka kwenu.
Ewe Mwenyezi Mungu, turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume... Allahumma, Ameen.
#RamadhanDemandsAction
1 Ramadhan 1444 H |
Taqwa ni kuepuka Ghadhabu za Mwenyezi Mungu ﷻ. Taqwa inaamrisha kutekeleza maamrisho ya Mwenyezi Mungu ﷻ na Mtume wake ﷺ. Hebu tuzingatie Taqwah yetu Ramadhan hii, ili tuabudu kwa uthabiti, kwa kujitolea kamilifu kwa Mwenyezi Mungu ﷻ.
Alhamisi, 01 Ramadhan 1444 H - 23 Machi 2023 M
2 Ramadhan 1444 H |
Iman katika Mitume (as) sio Imani tu katika utakatifu wa viumbe fulani pekee. Iman katika Mitume (as) inathibitisha kwamba akili ya mwanadamu haina uwezo wa kupata tiba sahihi ya matatizo ya maisha. Ni Khilafah kwa Njia ya Utume, ndiyo itakayotutawala kwa Ujumbe wa Mtume wa Mwisho ﷺ.
Ijumaa, 02 Ramadhan 1444 H - 24 Machi 2023 M
3 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, إنَّ الإيمانَ لَيَخْلَقُ في جَوْفِ أحدِكُمْ كَما يَخلَقُ الثّوبُ “Hakika, Iman inachakaa kifuani mwa kila mmoja wenu, kama vile nguo zinavyochakaa.” [At-Tabarani]. Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni fursa kutoka kwa Mwenyezi Munguﷻ kujadidisha Iman yetu kupitia Kufunga, Qiyam ul Layl, kukumbuka Akhera na kutafakari juu ya Wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu ﷻ.
Jumamosi, 03 Ramadhan 1444 H - 25 Machi 2023 M
4 Ramadhan 1444 H |
Mwenyezi Mungu ﷻ ameamrisha kuamrisha mema na kukataza maovu katika dhurufu zote, bila ya kujali matokeo yake. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema,
[وَلْتَكُنْ مِّنْكُمْ اُمَّةٌ یَّدْعُوْنَ اِلَى الْخَیْرِ وَ یَاْمُرُوْنَ بِالْمَعْرُوْفِ وَ یَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِؕ وَ اُولٰٓىٕكَ هُمُ الْمُفْلِحُوْنَ]
“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Surah Aali Imran 3:104].
Jumapili, 04 Ramadhan 1444 H - 26 Machi 2023 M
5 Ramadhan 1444 H |
Uislamu sio tu falsafa ya kiroho, au kanuni ya maadili tu. Uislamu ni kanuni kamili ya maadili, inayotuongoza katika ibaadah zetu binafsi, pamoja na uchumi wetu, elimu, sera za kigeni na utawala wetu. Hiyo ndiyo maana kamili ya Dini.
Jumatatu, 05 Ramadhan 1444 H - 27 Machi 2023 M
6 Ramadhan 1444 H |
Nusra ya Mwenyezi Mungu ﷻ ndiyo siri ya mafanikio ya majeshi ya Kiislamu, dhidi ya maadui wakubwa, wenye nguvu zaidi. Huko nyuma, Khilafah ilizishinda dola kubwa za ulimwengu, kama vile Warumi, Wafursi, Wamongolia, Watartari na Makruseda. Katika siku zijazo, itafanya vivyo hivyo pia, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ﷻ.
Jumanne, 06 Ramadhan 1444 H - 28 Machi 2023 M
7 Ramadhan 1444 H |
Uislamu ni Dini ya Haki, iliyochaguliwa na Mwenyezi Mungu ﷻ. Hatugeukii chochote kingine kwa ajili ya mwongozo katika maisha yetu ya kibinafsi na ya pamoja. Mwenyezi Mungu ﷻ asema,
[وَمَنْ يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَنْ يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ]
“Na anaye tafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri.” [Surah Aali-Imran 3:85].
Jumatano, 07 Ramadhan 1444 H - 29 Machi 2023 M
8 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, نِعْمَتَانِ مَغْبُونٌ فِيهِمَا كَثِيرٌ مِنَ النَّاسِ الصِّحَّةُ وَالفَرَاغُ “Kuna neema mbili ambazo watu wengi huzifuja, afya na muda wa faragha.” [Bukhari]. Waumini huchunga afya yao, sio kwa ajili ya ubora wa maisha yenyewe, bali ili waweze kutimiza wajibu wa Uislamu kwa nguvu.
Alhamisi, 08 Ramadhan 1444 H - 30 Machi 2023 M
9 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, انْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ أَسْفَلَ مِنْكُمْ، وَلَا تَنْظُرُوا إِلَى مَنْ هُوَ فَوْقَكُمْ، فَهُوَ أَجْدَرُ أَنْ لَا تَزْدَرُوا نِعْمَةَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ “Watazameni wale ambao maisha yao yako duni kushinda nyinyi, wala msiwatazame wale ambao maisha yako juu kuliko yenu, ili musizidharau neema za Mwenyezi Mungu juu yenu.” [Muslim]. Tunazishukuru neema na tunajitolea kwazo katika kumtii Mwenyezi Mungu ﷻ
Ijumaa, 09 Ramadhan 1444 H - 31 Machi 2023 M
10 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, اغتنمْ خمسًا قبلَ خمسٍ: حياتَك قبلَ موتِك، وصحتَك قبلَ سقمِك، وفراغَك قبلَ شغلِك، وشبابَك قبلَ هرمِك، وغنَاك قبلَ فقرِك “Nufaika na mambo matano kabla ya mambo matano mengine, uhai wako kabla ya kifo chako, afya yako kabla ya maradhi yako, wakati wako wa faragha kabla ya kushughulika kwako, ujana wako kabla ya uzee wako, na utajiri wako kabla ya ufukara wako.” [Bayhaqi, Al-Haakim na Imam Sayuti katika Al-Jaam’a as-Saghir]. Wengi wa Maswahaba (ra) walikuwa wachanga waliposilimu, na waliinyanyua Haki ili kuubadilisha kwa ujasiri mwelekeo wa ulimwengu.
Jumamosi, 10 Ramadhan 1444 H - 01 Aprili 2023 M
11 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, الْكَيِّسُ مَنْ دَانَ نَفْسَهُ وَعَمِلَ لِمَا بَعْدَ الْمَوْتِ وَالْعَاجِزُ مَنْ أَتْبَعَ نَفْسَهُ هَوَاهَا وَتَمَنَّى عَلَى اللَّهِ "Mwenye hekima ni yule aliyeiadibu nafsi yake na akatenda kwa yale yatakayomfaa baada ya kufa, na mwenye ajizi ni yule aliyefuata matamanio ya nafsi yake, kisha akatarajia amani kwa Mwenyezi Mungu." [Tirmidhi]. Wenye busara hujitayarisha kwa ajili ya kifo ambacho hakitangazwi kuwasili kwake, huku wenye ajizi akikutana nacho kwa majuto.
Jumapili, 11 Ramadhan 1444 H - 02 Aprili 2023 M
12 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, وَاللَّهِ مَا الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ مِثْلُ مَا يَجْعَلُ أَحَدُكُمْ إِصْبَعَهُ هَذِهِ فِي الْيَمِّ فَلْيَنْظُرْ بِمَ يَرْجِعُ “Wallahi, haikuwa dunia isipokuwa ni kama mfano wa mmoja wenu kutumbukiza kidole ndani ya bahari kisha aangalie ataregea na nini.” [Muslim]. Sasa kwa nini tulegezee msimamo bahari, kwa kile ambacho hakiwezi hata kujaza mtondoo.
Jumatatu, 12 Ramadhan 1444 H - 03 Aprili 2023 M
13 Ramadhan 1444 H
Amesema Mwenyezi Mungu (swt): فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ "Tangaza uliyoamrishwa." [Surah Al- Hijr 15:94]. Hivyo, Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) aliufikisha Uislamu kwa uwazi na hadharani. Katika zama zetu hizi za kutawaliwa na usiokuwa Uislamu, ni juu ya kila mmoja wetu kuutangaza Uislamu kwa uwazi, mpaka tufanikiwe kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume.
Jumanne, 13 Ramadhan 1444 H - 04 Aprili 2023 M
14 Ramadhan 1444 H |
Katika mwaka wa 13 H, tarehe 14 Ramadhan, katika Vita vya Buwaib, Waislamu 8000 waliwashinda makafiri wa Kifursi 100,000. Ramadhan sio mwezi wa kufunga na Qiaym ul Layl peke yake. Ni mwezi wa kuwashinda maadui wa Dini hii, kuzikomboa Ardhi za Waislamu na kufungua ardhi mpya kwa ajili ya Uislamu.
Jumatano, 14 Ramadhan 1444 H - 5 Aprili 2023 M
15 Ramadhan 1444 H |
Mwenyezi Mungu ﷻ amesema,
[إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّ الَكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ]
“Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu.” [Surah Taghabun 64:14]. Ikiwa wale tunaowapenda na kuwajali, watatushinikiza kutomtii Mola wetu, tunapaswa kufanya nini? Hebu natujitahidi ili familia zetu ziwe tegemeo thabiti la kushikamana na Haki yetu, katika zama hizi za sasa za Batili.
Alhamisi, 15 Ramadhan 1444 H - 6 Aprili 2023 M
16 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliwakumbusha Maansaar (ra) wakati wa Hunayn, يَا أَلَمْ أَجِدْكُمْ ضُلَّالًا فَهَدَاكُمُ اللهُ بِي، وَكُنْتُمْ مُتَفَرِّقِينَ فَأَلَّفَكُمُ اللهُ بِي؟ “Je, sikukuteni mumepotea Mwenyezi Mungu akakuongozeni kupitia mimi, na mulikuwa mumegawanyika Mwenyezi Mungu akakuunganisheni kupitia mimi?” [Bukhari]. Wapiganaji wa Ansaar waliunganishwa kupitia kutoa Nusrah yao kwa ajili ya Dola moja ya Kiislamu kwa Waislamu wote. Majeshi ya Ulimwengu wa Waislamu wanahitaji hilo hilo leo.
Ijumaa, 16 Ramadhan 1444 H - 7 Aprili 2023 M
17 Ramadhan 1444 H |
Mnamo tarehe 17 Ramadhan, mwaka wa 2 H, siku ya Vita vya Badr, Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliomba, اللَّهُمَّ إِنْ تُهْلِكْ هَذِهِ الْعِصَابَةَ مِنْ أَهْلِ الْإِسْلَامِ لَا تُعْبَدْ فِي الْأَرْضِ “Ewe Mola, endapo kipote hiki cha Waislamu kitaangamia, hutaabudiwa tena katika ardhi.” [Muslim] Leo, vilevile, ni Mwenyezi Mungu ﷻ ndiye atakayewapa ushindi majeshi yetu dhidi ya jeshi kubwa na lenye nguvu la maadui.
Jumamosi, 17 Ramadhan 1444 H - 8 Aprili 2023 M
18 Ramadhan 1444 H |
Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema, إِنَّ اللَّهَ لاَ يَنْظُرُ إِلَى صُوَرِكُمْ وَأَمْوَالِكُمْ وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وَأَعْمَالِكُمْ “Hakika, Mwenyezi Mungu haangalii sura zenu na mali zenu, lakini anaangalia nyoyo zenu na amali zenu.” [Muslim]. Uislamu unaondoa maradhi ya kuipigania dunia. Unanyanyua matarajio ya muumini ya kukitafuta cheo cha juu Peponi.
Jumapili, 18 Ramadhan 1444 H - 9 Aprili 2023 M
19 Ramadhan 1444 H |
Abu Bakr As-Siddiq (ra) amesema, “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema, إِنَّ النَّاسَ إِذَا رَأَوْا الظَّالِمَ فَلَمْ يَأْخُذُوا عَلَى يَدَيْهِ أَوْشَكَ أَنْ يَعُمَّهُمْ اللَّهُ بِعِقَابٍ مِنْهُ “Pindi watu wanapomuona dhalimu kisha wasimkamate mikono yake (kutofanya maovu), Mwenyezi Mungu atakaribia kuwachanganya wote katika adhabu yake.”” [Abu Dawood, Tirmidhi na An-Nisaa'i]. Hivyo basi, Khalifa Rashid wa kwanza (ra) alikataa kuutenga na kuupuuzia uhalifu wa madhalimu.
Jumatatu, 19 Ramadhan 1444 H - 10 Aprili 2023 M
20 Ramadhan 1444 H |
Tarehe 20 Ramadhan, Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliifungua Makkah, huku akisoma ayah,
[وَقُلْ جَاۗءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ ۭ اِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوْقًا]
“Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke!” [Surah Al-Isra’a 17:81] Ni lazima sote tujitahidi kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ili Haki itawale katika zama zetu, juu ya batili ya Magharibi.
Jumanne, 20 Ramadhan 1444 H - 11 Aprili 2023 M
21 Ramadhan 1444 H |
Kuhukumu kwa yale Yote Yaliyoteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt)
Mwenyezi Mungu ﷻ amemwamrisha mtawala kuhukumu kwa yale yote ambayo Yeye ﷻ aliyateremsha. Mwenyezi Mungu ﷻ asema,
[وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ]
“Na wahukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu.” [Surah al-Ma’ida 5:49]. Khalifa ndiye atakayehakikisha kuwa Uislamu unatekelezwa katika utawala, uchumi, elimu na sera za kigeni, pamoja na kufunga na kuswali.
Jumatano, 21 Ramadhan 1444 H - 12 Aprili 2023 M
22 Ramadhan 1444 H |
Khalifa wa Waislamu Huchunga Mambo Yao
Mtume ﷺ asema, كَانَتْ بَنُو إِسْرَائِيلَ تَسُوسُهُمُ الأَنْبِيَاءُ، كُلَّمَا هَلَكَ نَبِيٌّ خَلَفَهُ نَبِيٌّ، وَإِنَّهُ لا نَبِيَّ بَعْدِي، وَسَيَكُونُ خُلَفَاءُ فَيَكْثُرُونَ “Walikuwa Banu Isra'il mambo yao yanachungwa na Mitume. Kila Mtume mmoja akifa, mtume mwengine anamrithi. Na kwa hakika yake hakuna mtume mwengine baada yangu na kutakuwepo na makhalifa na watakuwa wengi.” [Bukhari na Muslim] Ni wajibu kwetu kuhakikisha kwamba Khalifa ndiye mwenye kuchunga mambo yetu, kupitia Wahyi.
Alhamisi, 22 Ramadhan 1444 H - 13 Aprili 2023 M
23 Ramadhan 1444 AH |
Khalifa sio Dikteta wala Mwanademokrasia
Mwenyezi Mungu ﷻ amesema,
[فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ]
“Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho.” [Surah an-Nisa’a 4:59]. Khalifa hatawali kwa maoni yake binafsi wala maoni ya maafikiano ya mkusanyiko. Mizozo yote anairegesha kwenye Quran Tukufu na Sunnah za Mtume.
Ijumaa, 23 Ramadhan 1444 H - 14 Aprili 2023 M
24 Ramadhan 1444 H |
Kubeba Ulinganizi wa Kiislamu
Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) walizingatia sana Dawah ya Uislamu, kama walivyozingatia kufuata Dini ya Uislamu. Lau Waislamu wa zama za awali wasingefanya hivyo, basi Uislamu usingetufikia. Leo, kila Muislamu lazima asisite katika kubeba Dawah kwa Uislamu.
Jumamosi, 24 Ramadhan 1444 H - 15 Aprili 2023 M
25 Ramadhan 1444 H |
Wito kwa Uislamu
Uislamu unapokuwa hautabikishwi, ni lazima Dawah yetu iwe ya kuuwasilisha Uislamu kama mfumo mpana wa maisha, ili mambo yote ya watu yatawaliwe na Uislamu. Pindi Uislamu unapotabikishwa, Khilafah hutumia rasilimali ili kuondoa vikwazo, katika njia ya kubeba Dawah kwa ulimwengu mzima.
Jumapili, 25 Ramadhan 1444 H - 16 Aprili 2023 M
26 Ramadhan 1444 H |
Kuibadilisha Dar ul Kufr hadi Dar ul Islam
Pindi kunapokuwa hakuna dola ya Kiislamu katika Ardhi za Kiislamu inayotabikisha sheria ya Kiislamu, Ardhi za Waislamu zinakuwa ni Darul Kufr, hata kama wengi wao ni Waislamu. Kazi ya mageuzi ya kivipande haina athari, hata kama itaendelea kwa miongo kadhaa. Mabadiliko msingi yanahitajika, ambayo yanang'oa mfumo batili na kusimamisha Khilafah ya Kiislamu.
Jumatatu, 26 Ramadhan 1444 H - 17 Aprili 2023 M
27 Ramadhan 1444 H |
Uislamu Unaweza Tu Kulindwa Kupitia Fahamu zake
Amesema Mtume ﷺ katika mnasaba wa Hijja ya kuaga, اللَّهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ “Je, sikufikisha ewe Mwenyezi Mungu?” [Al-Bukhari]. Dawah kwa Dini ni urithi aliouacha Mtume ﷺ kwa Ummah. Ni lazima tuuhifadhi ujumbe wa Uislamu kwa usafi, sio kwa mchanganyiko wa fikra za Kimashariki na Kimagharibi.
Jumanne, 27 Ramadhan 1444 H - 18 Aprili 2023 M
28 Ramadhan 1444 H |
Kujumuishwa kwa Wanaharakati wa Kiislamu Hakuondoi Ukafiri kutoka katika Nidhamu
Wachungaji wa mfumo wa sasa wa batili hutumia jina la Uislamu kurefusha maisha yake. Khilafah ni Dola ya Kiislamu kiuhalisia. Kila sheria na kifungu cha katiba kinatokana na Quran Tukufu na Sunnah za Mtume. Pale ambapo kuna tofauti ya rai, Khalifah huamua ni rai ipi yenye nguvu zaidi, kwa ajili ya utekelezaji wa lazima.
Jumatano, 28 Ramadhan 1444 H - 19 Aprili 2023 M
29 Ramadhan 1444 H |
Kataeni Twaghut
Waislamu lazima wapambane dhidi ya utawala wa kitwaghut, ambayo ni mamlaka yoyote yasiyokuwa ya Mwenyezi Mungu ﷻ. Mwenyezi Mungu ﷻ amesema,
[يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ]
“Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo!” [Sura An-Nisa 4:60]. Ni katika Khilafah ambapo Mwenyezi Mungu ﷻ ni Mwenye Ubwana Pekee, kiasi kwamba hakuna sheria inayoweza kuwekwa katika kumuasi Yeye ﷻ.
Alhamisi, 29 Ramadhan 1444 H - 20 Aprili 2023 M
1 Shawwal 1444 H |
Idd chini ya kivuli cha Khilafah
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ مَثَلُ الْمُؤْمِنِينَ فِي تَوَادِّهِمْ وَتَرَاحُمِهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ مَثَلُ الْجَسَدَىٌ تَعَلُ الْجَسَدَى لَهُ سَائِرُ الْجَسَدِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى إِذَا اشْتَكَى مِنْهُ عُضْوٌ تَدَاعَى “Mfano wa Waumini katika kupendana, kuhurumiana na kuonea upole kwao ni kama mwili. Pindi kiungo kimoja kikiumia basi mwili mzima huitikia kwa kukosa usingizi na homa.” [Bukhari na Muslim]. Haipaswi kuwa sehemu moja ya mwili inaadhimisha, wakati sehemu nyingine ina maumivu. Tuombe kuregea kwa Khilafah, ngao ya Umma wa Kiislamu.
Ijumaa, 1 Shawwal 1444 H - 21 Aprili 2023 M