Jumamosi, 26 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 03/05/2023

Maoni ya Habari ya Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan.

Kwa Mabadiliko ya Kweli... Kataeni Demokrasia... Simamisheni Khilafah.

Ewe Mwenyezi Mungu, turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida... Allahuma Ameen.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 13 Shawwal 1444 H sawia na 03 Mei 2023 M

Sudan ni Ardhi ya Waislamu na Waislamu Wake Wanahitaji Kuwatia Maanani Kwetu

Mnamo 24 Aprili 2023, Afisi ya Mambo ya Nje (FO) ilithibitisha juhudi za kuwahamisha Wapakistani kutoka Sudan. Hata hivyo, wajibu ambao Pakistan lazima itekeleze ni kuwalinda Waislamu wote nchini Sudan dhidi ya wale wanaopigania mamlaka, wanaosimamiwa na Marekani. Ni Khilafah ndiyo inayokusanya jeshi kuziunganisha nchi za Kiislamu. Ni Khilafah ndiyo inayoangamiza ushawishi wote wa Magharibi katika nchi za Kiislamu. Ni Khalifa ndiye anayewazima makamanda wa jeshi, wanaomwaga damu za Waislamu nchini Sudan, Syria na sehemu nyinginezo.

07 Shawwal 1444 H sawia na 27 Aprili 2023 M

Uongozi wa Pakistan ulifanya Makubaliano ya Siri ya Kuisalimisha Kashmir kwa Modi

Uongozi wa Pakistan ulikataa kujibu kijeshi kwa India kuiunganisha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu mnamo Agosti 2019. Uongozi huu uliwezesha ukaliaji kimabavu wa India. Ulitangaza Jihad kuwa ni khiyana. Ulitangaza kusitisha mapigano kwenye Mstari wa Udhibiti. Ulizuia vikosi vyetu vilivyo tayari na vyenye uwezo. Unafuata fundisho la Bajwa la kujisalimisha kwa India hadi sasa. Ni Khilafah ndiyo itakayotumia nguvu za kijeshi kukomboa Kashmir na ardhi nyinginezo za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu.

08 Shawwal 1444 H sawia na 28 Aprili 2023 M

Kumiliki Silaha za Nyuklia Hakuzuii Ukombozi wa Kashmir

Licha ya Urusi kumiliki silaha za nyuklia, Ukraine imekuwa ikipigana kwa zaidi ya mwaka mmoja kulinda ardhi zake. Ni kipi kinachozuia uongozi wa Pakistan kuhamasisha Jeshi la Pakistan, lililo na silaha za nyuklia, kuikomboa Kashmir, wakati India inashughulika na China katika mivutano ya uhasama huko Ladakh? Ni Khilafah ndiyo itakayoyatia Mafundisho ya Bajwa, na kizuizi chake cha kimkakati dhidi ya India, katika jaa la historia. Itatangaza jihad iliyopangiliwa chini ya mzingiro wa nyuklia, ili kuikomboa Kashmir.

09 Shawwal 1444 H sawia na 29 Aprili 2023 M

Khilafah Itajitosheleza na Kawi, Bila Kuhitaji Dola za Kikoloni

Baadhi ya viongozi wa Pakistan wanaweza kudai kwamba kununua mafuta ya Urusi, huku wakisambaza makombora ya mizinga ya Ukraine, ni mchezo wa ujanja wa unafiki. Hata hivyo, msimamo huu unathibitisha kwamba uongozi wa sasa hauwezi kufikiria zaidi ya kutegemea dola za kikoloni. Ni Khilafah ndiyo itakayokusanya rasilimali kubwa za kawi, madini na kilimo za Ummah kupitia kuunganisha ardhi za Waislamu, kuhakikisha dola imara huru.

10 Shawwal 1444 H sawia na 30 Aprili 2023 M

Khilafah Itakabiliana na China kama Adui wa Uislamu na Waislamu

Akiangazia ushirikiano wa kijeshi, mkuu wa jeshi la Pakistan alizuru China kuanzia tarehe 26 Aprili 2023. Hata hivyo, China imeikalia kwa mabavu Turkestan Mashariki, ambako inapigana vita dhidi ya Uislamu, Swala na Saumu. Kama sehemu ya mpango wake wa "Umoja wa Kitaifa, Familia Moja", China hata inahakikisha ndoa kati ya wanawake waumini Waislamu wa Uyghur na wanaume makafiri wa Kichina wa Kihan. Ni Khilafah ndiyo itakayokabiliana na dola zenye uadui kwa misingi ya vita. Ni Khilafah ndiyo itakayojenga kwa ghera sekta ya kijeshi ili kukomesha utegemezi kwa maadui.

11 Shawwal 1444 H sawia na 01 Mei 2023 M

Kuiegemeza Sarafu na Maduhuli kwa Dolari Kunawanyima Watu Tiba

Kamati ya Uratibu wa Uchumi ya Baraza la Mawaziri imeidhinisha ongezeko la bei ya dawa kwa asilimia 20, kutokana na kuthaminiwa kwa dolari na utegemezi wa dolari kwa malighafi zinazoagizwa kutoka nje. Huu ni mshtuko unaofuata kwa watu kufa kwenye foleni za unga. Multivitamini, antibiotics na dawa za kukata maumivu sasa hazipatikani. Khilafah itaondoa mfumko huo wa bei kwa kujenga uchumi unaojitosheleza na sarafu inayoegemezwa juu ya dhahabu na fedha, huku ikihakikisha huduma ya afya kwa watu wote.

12 Shawwal 1444 H sawia na 02 Mei 2023 M

Komesha Mafunzo ya Kijeshi ya Kigeni na Jeshi la Wahalifu la Marekani Lisilostahili

Ripoti ya Mwaka ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani (DOD) kuhusu Unyanyasaji wa Kimapenzi katika Jeshi iliyotolewa mnamo 27 Aprili 2023. Ilifichua ongezeko la idadi kubwa ya ubakaji ndani ya jeshi la Marekani. Hii ni kando ya uoga, magonjwa ya akili na kujiua ambayo yanalikumba jeshi la Marekani. Jeshi hilo sio bora kwa afisa wa kijeshi wa Kiislamu. Jeshi la waumini la Khilafah ni bora kuliko jeshi lolote la kikafiri. Vikosi vyake vinamuogopa Mwenyezi Mungu ﷻ katika kuamiliana na watu, huku wakipigania kufa kishahidi na ushindi.

13 Shawwal 1444 H sawia na 03 Mei 2023 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu