- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Pakistan: Utekaji nyara wa Naveed Butt Unathibitisha kwamba Watawala wa Waislamu Wanazuia Kuhisabiwa Kwao!
Kesi 379 za upotezwaji wa lazima ziliwasilishwa kwa Tume ya Uchunguzi juu ya Kupotezwa kwa Kulazimishwa (COIOED) mnamo 2024. Watawala wa Waislamu huwateka nyara wale wanaowawajibisha, ni wakali kwa Waislamu na wana huruma na maadui. Hawakumnyonga jasusi na muuaji wa Kihindi Kulbhushan Yadav. Walimwachilia huru jasusi na muuaji wa Kimarekani Raymond Davis. Hata hivyo, walimteka nyara Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, mnamo Mei 11, 2012. Naveed Butt alitoa wito wa ukombozi kutokana na ukoloni wa Marekani na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida. Baada ya zaidi ya miaka kumi na mbili, watawala wangali hawajamwachilia huru. Ni lazima kwa umma na majeshi yake kuwang’oa madhalimu miongoni mwa watawala na kusimamisha Khilafah Rashida.
Imetolewa na: Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan
Alhamisi, 09 Rajab Tukufu 1446 H sawia na 09 Januari 2025 M
Kwa Maelezo zaidi, Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan