Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wilaya Pakistan: Kampeni ya Mtandaoni ya Ombi "Mwacheni Huru Naveed Butt"

Hizb ut Tahrir / Wilaya Pakistan ya andaa kampeni pana ya mtandaoni ya kutaka kuachiliwa huru kwa Naveed Butt, Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.

Mnamo siku ya Ijumaa 11 Mei 2012 M Naveed Butt alitekwa nyara mikononi mwa majasusi wa Pakistan, alipo kuwa akiwachukua watoto wake wadogo kutoka shuleni, na huu sasa ni mwaka wa tisa tangu mara ya mwisho familia ya Naveed Butt ilipo sikia lolote kutoka kwake.

Na kwa sifa yake kama Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan, Naveed Butt alisimamisha harakati ya amani ya kisiasa, ya ulinganizi wa Khilafah. Naveed butt anaitakidi kwamba maendeleo ya Pakistan yamelemaa kwa sababu ya utiifu wake kwa Amerika na kutabikishwa kwa nidhamu ya kidemokrasia (ya kikafiri) nchini Pakistan.

Na kihakika, Naveed Butt alitekwa nyara baada ya kuwakosoa vikali watawala wa Pakistan kwa kumwachilia huru jasusi wa Kiamerika (Raymond Davis) na kushindwa kwao kuihami Pakistan kutokana na shambulizi la Amerika la Abbottabad.

Kwa upande wa taaluma, Naveed Butt ni mhandisi wa umeme na baba wa watoto watatu wa kiume na binti mmoja, nao wanasubiri kurudi kwake.

Na licha ya kuonyesha kwake kuvutiwa na muundo wa utawala wa Kiislamu, serikali ya Imran Khan iliendelea kuwafunga gerezani watetezi wengi wa Khilafah nchini Pakistan.

Sisi tunailaani serikali ya Imran Khan kwa muamala wake wa kikatili kwa Naveed Butt, tunatoa wito wa kuachiliwa kwake mara moja na kuregea kwa familia yake salama salmin.       

Tafadhali tia saini ombi letu la mtandaoni la kuachiliwa huru kwa Naveed Butt:

https://secure.avaaz.org/en/community_petitions/prime_minister_pakistan_imran_khan_free_naveed_butt_1

Ewe Mola turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume… Ameen

Jumanne 19 Ramadhan Iliyo Barikiwa 1441 H sawia na 12 Mei 2020 M

#FreeNaveedButt    #KnowNaveedButt    #MwacheniHuruNaveedButt    #MjueNaveedButt

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 22 Mei 2020 07:34

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu