Ijumaa, 25 Jumada al-awwal 1445 | 2023/12/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa:

Wito kwa Majeshi kutoka Katikati mwa Msikiti wa Al-Aqsa Kuihami Al-Aqsa na Matukufu ya Mtume (saw)

Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) iliandaa kisimamo cha halaiki katikati mwa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, ambapo kupitia kwacho ilitoa wito kwa majeshi ya Umma wa Kiislamu kujibu hujma ya Mayahudi dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa na kuchafuliwa kwake, na kupandisha bendera ya umbile lao liliopotoka katika viwanja vyake na matusi yao kwa Mtume (saw).

Na Hizb ikasema katika hotuba yake: "Je, hamuyaoni makundi ya walowezi yakiichafua Al-Aqsa, masra ya Mtume wenu (saw)? Je, haujakufikieni ujumbe kwamba makundi ya walowezi yanamtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu katika nyua za Al-Aqsa?! Je, ujumbe haujakufikieni kwamba wanazuia adhana ya swala katika Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa katika mchakato wao wa kuuvunjia heshima?! Je, hamjaziona bendera za wale waliokasirikiwa juu yao zikipandishwa katika Msikiti wa Al-Aqsa?! Basi ni lini mlo wa Kiislamu unazuka katika nafsi zenu?! Ni lini mnaasi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake? Basi ni lini shauku ya Uislamu itachemka katika nafsi zenu?!

Ni lini mtachangamka kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake?

Na Hizb ikayataka majeshi ya Misri, Ash-Sham, Jordan, Pakistan na Uturuki kufanya uasi dhidi ya tawala saliti na kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume na kuelekea Bait ul-Maqdis ili kuikomboa na kulipiza kisasi kwa ajili ya matukufu ya Mtume (saw), na ikasisitiza kwamba nusra kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na nusra kwa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa ni heshima kubwa ambayo inaweza kupatikana tu kwa kubeba roho yake juu ya kiganja chake na ni kheri kwake kujitoa mhanga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw). Hakika nusra kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, rehema na amani ziwe juu yake, na kukombolewa kwa Msikiti wa Al-Aqswa ni heshima kubwa ambayo wale wanaopuuza au kujidhalilisha kwa tawala hizi hawawezi kuipata. Hakika ni heshima kubwa inayoweza kupatikana tu kwa wenye izza, wachamungu, wasioogopa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumiwa.

Ijumaa, 29 Shawwal 1444 H, sawia na 19 Mei 2023 M

Kwa Maelezo Zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina:

Tovuti Rasmi: Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Facebook: Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Twitter: Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

YouTube: Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu